JINI WA DARAJA LA SALENDA.......EP.1 
 JINI WA DARAJA LA SALENDA.......EP.1


Majira ya saa nane za usiku msichana Suzana alikuwa akitoka kujirusha katika ukumbi wa Bilicanas. Kilichomshtua kilikuwa kutoweka kwa mpenzi wake Sammy ambaye aliondoka bila kumuaga. Wazo lake la kwanza lilikuwa Sammy kaondoka na msichana mwingine akijua kabisa yeye ndiye mchumba wake.

Akiwa amekasirika kwa kitendo cha Sammy kuondoka na kumuacha peke yake, kila alipopiga simu yake iliita bila kupokelewa kitu kilichoonesha dharau. Aliamua kurudi nyumbani kwake japo alipanga siku ile kwenda kulala kwa Sammy. Aliendesha gari akiwa amefura kwa hasira huku machozi yakimtoka kutokana kitendo alichotendewa na mpenzi wake ambaye ndiye aliyemtoa kitandani alipokuwa amekwisha kulala. Suzana awaliza mengi juu ya kitendo cha mpenzi wake kumwita klabu na kumkimbia.

Wakati akitoka Bilicanas mvua ilianza kunyesha, hakutaka kuisubiri aliamua kwenda nayo ili awahi kunyumba angalau alale kwa muda mchache ili asubuhi awahi kanisani misa ya kwanza.

Mvua ilikuwa kubwa iliyoambatana na upepo mkali kitu kilichomfanya ashindwe kuona mbele ilimbidi alisimamishe gari pembeni ya daraja ya Salenda ili kusubiri upepo upungue ndipo aendelee na safari yake. Upepo ule haukuchukua ulitulia na mvua ilikuwa imekatika.

Alipowasha gari liligoma kuwaka, alirudia zaidi ya mara tano kuzungusha funguo lakini liligoma kuwaka. Kuteremka kwenye gari alishindwa kutokana na hali ya kiza cha kutisha nje. Wasi wasi ulimtawala na kujiuliza atatokaje pale au ndio atalala mpaka asubuhi.

Hasira zilizidi kumpanda Suzana kutokana na kukimbiwa na mpenzi wake na kuharibikiwa na gari. Kutokana na hofu aliyokuwa nayo alihakikisha milango na vioo vyote vimefungwa vizuri. Alijikuta akipiga dua kumuomba Mungu amuokoe la janga lile kwa kupata msaada wa watu wenye gari kumsaidia kuwasha gari lake. Lakini kwa muda ule hakukuwa na dalili ya gari lolote kupita.

Akiwa ameinama mikono ameikutanisha kifuani kwake alishtushwa na upepo makali uliovuka toka baharini na kulifanya gari lake kuyumba na kusogea kidogo. Kwa woga uliompata Suzana alijikuta akitokwa na haja ndogo bila kuelewa. Alitamani kulia lakini aliamini sauti yake haitasaidia lolote kwa vile hakukuwa na wakumsaidia.

Aliinama kwa woga hakutaka kuangalia popote zaidi ya kusubiri chochote kitakachomtokea. Baada ya muda hali ile ilitulia, Suzana alinyanyua kichwa taratibu ili achukue simu ampigie baba yake amfuate eneo lile ambalo lilikuwa limemuweka katika hali ya hatari.

Aliponyanyua uso achukue simu iliyokuwa kwenye kwenye dash board, alishtushwa na mwanga mkali kama jua la saa saba mchana. Aliangalia katikati ya bahari palipokuwa kunatoka mwanga ule. Alituliza macho baada ya kumuona mwanamke aliyekuwa amevaa gauni jeupe lilikuwa liking’aa kutokana na mapambo yake.

Hali ile ilimfanya asahau yalitomtokea muda mfupi na kutuliza macho kumuangalia yule mwanamke aliyekuwa akitembea juu ya maji huku nyuma akisindikizwa na wasichana walikuwa wamebeba vikapu vidogo vilivyokuwa na maua ambayo walimwagia kila hatua ilivyopigwa huku wakiimba nyimbo nzuri.

Suzana alijikuta akipata ujasiri wa ajabu kwa kufungua dirisha kidogo ili aweze kusikia watu wale walikuwa wakiimba kitu gani. Zilikuwa sauti nzuri kama za kaswida zilizoibwa kwa lugha ya kiarabu. Nyimbo zile zilimvutia na kujikuta akiwa na hamu ya kuwaona watu wale waliokuwa wakitembea juu ya maji huku kwa mstari mbele akitangulia yule mwanamke ambaye usoni kwake kulikuwa kunawaka kama taa na kushindwa kuiona sura yake vizuri.

Suzana alijikuta akisahau kama wale watu walikuwa wakitembea juu ya maji zaidi ya kushangazwa na sherehe ile ambayo toka azaliwe hajawahi kuona sherehe ya aina ile ya mtu mmoja kutangulia mbele wengine kumfuata nyuma huku wakimuwagia maua na kumwimbia nyimbo nzuri.

Baada ya muda watu wote walikaa mstari mmoja, kisha yule mwanamke aliyekuwa amepeneza kuliko wote alipita katikati yao na kupigiwa vilegele huku akitupiwa maua. Manukato ya maua yalisambaa mpaka ndani ya gari la Suzana alilokuwa amefungua kioo kidogo kusikia nyimbo alizokuwa anaimbiwa yule mwanamke ambaye alionekana kama bibi harusi lakini muda wote hakumuona bwana harusi wala mwanaume kwenye kundi lile.

Yule mwanamke alipita kwenye mstari mpaka mwisho alitembea peke yake bila kufuatwa na mtu kisha aligeuka na kuwapungia mkono wenzake ambao nao walimpungia huku wakimrushia maua. Baada ya kutembea kidogo Suzana alimshuhudia yule mwanamke alikunja gauni lake usawa na kifua na kushangaa kumuona akitembea ndani ya maji yaliyokuwa yamemfika tumboni.

Suzana alijikuta akishtuka na kujiuliza yupo ndotoni au anaona kweli, kilichomshangaza ni umbali aliotoka yule mwanamke akitembea juu ya maji. Lakini cha kushangaza alipokaribia ufukweni alionekana yupo ndani ya maji yaliyomfikia tumboni.

Aliendelea kumtazama amuone anakwenda wapi, yule mwanamke baada ya kutoka ndani ya maji alitembea juu ya mchanga kulifuata lile gari. Kila hatua ilivyokuwa akipiga ilizidi kumtisha Suzana, alijikuta akimshangaa kutaka kuijua sura yake. Alituliza macho yake kwenye uso wa yule mwanamke aliyekuwa akiisogelea gari huku manukato makali yakizidi kujaa ndani ya gari.

Kilichomshangaza zaidi ni sura ya yule mwanamke alikuwa akifanana naye kwa kila kitu umbile na sura. Suzana alishtuka na kufunga kioo haraka ili mtu yule ambaye yeye alimuona wa muujiza asiingie kwenye gari. Yule mwanamke alisogea kwenye gari na kuligusa, ajabu baada ya kuligusa lile gari alitoweka ghafla.

Suzana akiwa anatetemeka alijaribu kuwasha gari kwa mara nyingine, ajabu ya Mungu gari liliwaka aliondoka eneo lile kwa mwendo wa kasi. Alipofika nyumbani kulikuwa kumekucha, alikwenda kuoga haraka ili awahi kanisani kwani muda ulikuwa umekwenda.

Baada ya kuoga alirudi ndani, lakini alishtushwa na harufu ya manukato ambayo aliyasikia muda mfupi darajani gari lake lilipozima na kuenea hadi ndani ya gari lake. Hakutaka kulifikiria sana lile kwa muda ulikuwa umekwenda, alikwenda kwenye kabati kubadili nguo ili awahi kanisani.

Baada ya kumaliza kubadili nguo alijikuta akiingiwa na uvivu na kwenda kukaa kwenye kitanda haikupita muda. Usingizi mzito ulimshika na kulala bila kujielewa, aliposhtuka usingizini alishtuka kuiona familia yake yote imesimama mbele yake. Alijiuliza kuna nini, alipojiangalia alijiona alikuwa amevaa nguo za kuendea kanisani.

“Suzana upo sawa?” Mama yake alimuuliza.
“Mbona unaniuliza hivyo? Halafu mbona kama wote mlikuwa mnalia kuna nini mbona mnanitisha?

Nini kimemtokea Suzana mpaka familia yake ikusanyike mbele yake huku wakitokwa na machozi. Kuyajua yote fuatana nami katika simulizi hii mpya ya kusisimua..
 
 
 
 
 JINI WA DARAJA LA SALENDA.........EP.2.

LIPOISHIA;
Yule mwanamke alipita kwenye mstari mpaka mwisho, alitembea peke yake bila kufuatwa na mtu kisha aligeuka na kuwapungia mkono wenzake ambao nao walimpungia huku wakiendelea na zoezi la kumrushia maua. Baada ya kutembea kidogo Suzana alimshuhudia yule mwanamke akikunja gauni lake usawa wa kifua na kushangaa kumuona akitembea ndani ya maji yaliyokuwa yamemfika tumboni.

Suzana alijikuta akishtuka na kujiuliza yupo ndotoni au anaona kweli, kilichomshangaza ni umbali aliotoka yule mwanamke akitembea juu ya maji. Lakini cha kushangaza alipokaribia ufukweni alionekana yupo ndani ya maji yaliyomfikia tumboni.

Aliendelea kumtazama amuone anakwenda wapi, yule mwanamke baada ya kutoka ndani ya maji alitembea juu ya mchanga kulifuata gari lake. Kila alivyopiga hatua Suzana alizidi kutishika, alijikuta akimshangaa na kutamani kuijua sura yake. SASA ENDELEA...

Alituliza macho yake kwenye uso wa yule mwanamke aliyekuwa akiisogelea gari huku manukato makali yakizidi kujaa ndani ya gari.

Kilichomshangaza zaidi umbile la yule mwanamke ambaye mwanzo alionekana kama mrefu tena mweupe lakini kila alivyomsogelea sura na umbile la yule mwanamke lilibadilika na kufanana naye kwa kila kitu. Suzana alishtuka na kufunga kioo haraka ili mtu yule ambaye yeye alimuona wa muujiza asiingie ndani ya gari.

Yule mwanamke alisogea kwenye gari na kuligusa, ajabu baada ya kuligusa, alitoweka ghafla. Suzana akiwa anatetemeka alijaribu kuwasha gari kwa mara nyingine, ajabu ya Mungu gari liliwaka aliondoka eneo lile kwa mwendo wa kasi. Alipofika nyumbani kulikuwa kumekwisha pambazuka, alikwenda kuoga haraka ili awahi kanisani kwani muda ulikuwa umekwenda sana.

Baada ya kuoga alirudi ndani, lakini alishtushwa na harufu ya manukato ambayo aliyasikia muda mfupi darajani gari lake lilipozima na kuenea hadi ndani ya gari lake. Hakutaka kulifikiria sana lile kwa sababu muda ulikuwa umekwenda, alikwenda kwenye kabati kubadili nguo ili awahi kanisani.

Baada ya kumaliza kubadili, alijikuta akiingiwa na uvivu na kwenda kukaa kwenye kitanda haukupita muda usingizi mzito ulimshika na kulala bila kujielewa, aliposhtuka usingizini alishtuka kuiona familia yake yote imesimama mbele yake. Alijiuliza kuna nini, alipojiangalia alijiona alikuwa amevaa nguo za kuendea kanisani.
“Suzana upo sawa?” Mama yake alimuuliza huku akifuta machozi.

“Mbona unaniuliza hivyo? Halafu mbona kama wote mlikuwa mnalia kuna nini mbona mnanitisha?
“Suzana,” mama yake alimwita tena akiwa bado anamshangaa..
“Abee mama.”
“Upo sawa?” Mama yake alimuuliza huku akimkagua mwanaye kwa kumshika kila kona ya mwili.

“Nipo sawa mama, kwani vipi?”
“Siamini kweli Mungu wa ajabu.”
“Mama mbona sikuelewi nilitokewa na nini?” Suzana alizidi kushangaa.

“Hebu nyanyuka kwanza.”
Suzana alinyanyuka kitandani kuonesha yupo sawa, wote waliokuwa mule ndani walishukuru Mungu.
“Kwani muda huu ni saa ngapi?”

“Saa kumi na moja.”
“Jamani ina maana sikwenda kanisani?” Suzana alizidi kujishangaa.
“Kwani ilikuwaje?” Mdogo wake wa kike alimuuliza huku akionesha kumshangaa dada yake.

“Hata najua, nashangaa kuwaona mpo mbele yangu mkitokwa na machozi kwani nilikuwa kwenye hali gani?”
“Mmh, haielezeki.”
“Mbona mnanitisha.”
“Ulitaka kwenda kanisani misa ya ngapi?”

“Ya kwanza, ooh, nimekumbuka nilihisi uchovu na kuja kujilaza kilichoendelea sikujua, kwani mama nini kimenitokea?”
“Tumepigiwa simu na shoga yako kuwa upo katika hali isiyoeleweka, ndipo tulipozoana na wadogo zako kuja hapa. Tulipofika tumekukuta umepoteza fahamu hujitambui hata mapigo yako ya moyo yalionesha kusimama.”
“Mungu wangu!” Suzana alishtuka sana.

“Basi tulichanganyikiwa, lakini sikutaka kuamini kama kweli utakuwa umekufa, ndipo tulifanya maombi ambayo yamekufanya unyanyuke na kuonesha kama ulikuwa katika usingizi mzito. Hatuamini kama huna tatizo lolote.”
“Ni ajabu kulala muda mrefu kiasi hicho sijawahi kutokewa na kitu kama hicho, lakini nipo sawa kama uchovu ni wa kawaida tu.”

“Mmh, haya ni maajabu makubwa sana, kuna umuhimu wa kwenda kwanza hospitali kuichunguza afya yako.”
Suzana hakutaka kubishana na familia yake, walimchukua na kumpeleka hospitali ya TMJ. Walipofika walimueleza daktari hali waliyomkutana nayo na baada ya maombi kuamka kama alikuwa usingizini.

Alichukuliwa vipimo vyote ambayo havikuonesha ugonjwa wowote, waliruhusiwa kurudi nyumbani. Siku ile alichukuliwa kwenda kulala kwa wazazi wake, usiku kwake ulikuwa mrefu kuwaza yote aliyokutana nayo na hali iliyomtokea. Mpaka siku ya pili inaingia hali ya Suzana ilikuwa nzuri hakuonesha mabadiliko yoyote.

Siku hiyo aliondokea kwa wazazi wake kwenda kazini, alipofika kazini alikuwa mtu mwenye mawazo mengi juu ya matukio yaliyomtokea toka alipokimbiwa na mpenzi wake kwenye ukumbi wa Club Bilicanas, matukio ya ajabu aliyoyaona baharini kwenye sherehe ya ajabu.
Kingine hali waliyomkutanayo kama mtu aliyekuwa amefariki, na kushangazwa na jinsi alivyoamka na kukutwa hana ugonjwa wowote zaidi ya uchovu wa usingizi. Alijiuliza hali ile imemtokea kwa sababu gani, akiwa katika dimbwi la mawazo shoga yake kipenzi Sharifa aliingia.

“Vipi shoga mbona leo sikusomi?”
“Mmh, shoga wee acha tu kuna mambo yamenitokea yananichanganya.”
“Yapi? Hebu kaa chini nikueleze yaliyonisibu najuta kwenda club usiku.”
“Yepi tena hayo shoga?”

Suzana alimueleza yote aliyokutatana nayo usiku na hali iliyomkuta baada ya kumaliza kuoga ili aende kanisani na alipoamka na kukukuta watu wamemzunguka na kumueleza walimkuta akiwa kama amekufa.
“Haa! Shoga unayosema ni kweli?”
“Kweli kabisa.”

“Huyo mtu unasema umemuona wapi?”
“Daraja la Salenda”
“Mmh!” Sharifa aliguna.
“Mbona unaguna?”
“Mbona tukio linafanana kama langu.”
Sharifa naye alikutana na tukio gani linalo fanana na Suzana?
 
 
 
 
 
 
JINI WA DARAJA LA SALENDA......EP.3


ILIPOISHIA;
Kingine, hali waliyomkutanayo kama mtu aliyekuwa amefariki dunia na kushangazwa na jinsi alivyoamka na kukutwa hana ugonjwa wowote zaidi ya uchovu wa usingizi. Alijiuliza hali ile imemtokea kwa sababu gani. Akiwa katika dimbwi la mawazo shoga yake kipenzi, Sharifa aliingia.
“Vipi shoga mbona leo sikusomi?”

“Mmh, shoga wee acha tu kuna mambo yamenitokea yananichanganya.”
“Yapi? Hebu kaa chini nikueleze yaliyonisibu najuta kwenda klabu usiku.”
“Yapi tena hayo shoga?”

Suzana alimueleza yote aliyokutana nayo usiku na hali iliyomkuta baada ya kumaliza kuoga ili aende kanisani na alipoamka na kukukuta watu wamemzunguka na kumueleza walimkuta akiwa kama amekufa.
“Haa! Shoga unayosema ni kweli?”
“Kweli kabisa.”

“Huyo mtu unasema umemuona wapi?”
“Daraja la Salenda”
“Mmh!” Sharifa aliguna.
“Mbona unaguna?”
“Mbona tukio linafanana na kama langu.” SASA ENDELEA...

“Lako?”
“Eeeh.”
“Tukio gani?”
“Unajua kuna mtu nilimueleza akasema eti ni uongo na uzushi, si unakumbuka kuna tukio moja lilitamba katika vyombo vya habari?”
“Tukio gani?”

“Lile la msichana kuota manyoya baada ya kumpa msaada ombaomba kwenye Daraja la Salenda?”
“Ndiyo.”

“Mimi nilikuwa mmoja ya watu walio kataa katakata kuwa ni uzushi, Suzana mimi ni mbishi sana kukubaliana na jambo linaloonekana ni la kusadikika.”
“Mh.”

“Basi wiki iliyopita katika majira ya saa kumi na mbili jioni nikiwa narudi nyumbani, si unajua foleni za Dar. Toka pale Palm Beach magari yalikuwa yakienda taratibu sana, tulipofika katika Daraja la Salenda magari yalisimama. Niliendelea kusubiri huku nikisikiliza nyimbo za Injili.

“Nje ya magari kulikuwa na ombaomba wachache, sikushughulika nao, niliendelea kusikiliza muziki nikisubiri foleni isogee. Nilishtushwa na dirisha kugongwa kwa nje, niliponyanyua macho nilimuona ombaomba wa kike akitaka msaada kwangu.

“Huruma iliniigia, nilifungua dirisha kidogo na kumpa noti ya elfu moja, halafu nilifunga dirisha na kuendelea kusikiliza muziki. Nilishtushwa tena dirisha kugongwa, nilipoangalia nilimuona yule yule ombaomba wa kike. Nilijiuliza ana shida gani ya kugonga tena, safari hii nilijikuta nimefungua kioo mpaka chini na kumuuliza:

“Una shida gani tena?”
Yule ombaomba aliyekuwa ameinama na uso wake kuzibwa na nywele nyingi alinyanyua uso wake na kunitazama, alionesha kama kunishangaa. Nilijiuliza mbona amenishangaa huenda kanifananisha na mimi nilikaza macho kumwangalia.

Kilichonishangaza zaidi ilikuwa sura yake iliyofanana sana na yangu kama pacha. Moyo ulinilipuka ajabu, kuna kitu nilikiona kikitoka kwenye macho yake na kupiga kwenye macho yangu na ghafla alitoweka.”
“Weee!” Suzana alishtuka.

“Ndiyo maana nikasema tukio kama langu japo tofauti yake ni ndogo sana. Baada ya foleni kuanza kutembea, niliondoa gari na kwenda moja kwa moja nyumbani. Amini Suzana tukio lile wala sikulitilia maanani kwa vile sikulielewa na pia sikuwa muumini wa mambo ya kishirikina.”
“Mh!”

“Basi shoga, siku ile nyumbani nilikutana kimwili na mume wangu. Kama kawaida mzunguko wa kwanza ulikwenda vizuri, ajabu wa pili hakuwa na nguvu. Kila alivyojitahidi nguvu zake za kiume ziligoma.”
“Mmh!” Suzana aliguna na kujitengeneza vizuri kwenye kiti chake.
“Tokea siku ile mpaka leo mume wangu hana nguvu za kiume.”
“Usiniambie!”

“Kweli kabisa.”
“Sharifa unataka kuniambia ombaomba yule ndiye aliyesababisha yote hayo?”
“Sasa napata picha kuwa sehemu ile kweli kuna kitu kinafanyika.”
“Kwa hiyo unataka kusema ni kweli pale kuna jini kama watu wanavyoamini?”

“Sina uhakika kama ni jini lakini kuna kitu kibaya.”
“Kwa hiyo hata ya mwanamke kuota manyonya ni kweli?”
“Inawezekana.”
“Mmh! Kama ni kweli basi tuna hatari, kwani yule mwanamke alipatikana?”
“Nilisikia alionekana ufukweni akiwa uchi na akili zake kama chizi.”
“Unataka kuniambia ndiye aliyetutokea?”

“Huenda.”
“Basi kuna umuhimu wa kulifanyia kazi jambo hili.”
“Ngoja tutafute ushauri wa watu wazima.”
“Kwani mumeo ulimueleza uliyokutana nayo?”
“Sikumueleza kwa kuamini hali ile imetokana na yeye kutoka nje ya ndoa.”
“Una uhakika gani?”

“Suzana, sasa naingiwa na imani hiyo kutokana na tukio lililokutokea wewe.”
“Sharifa kabla ya kutafuta ufumbuzi mbadala kwa nini usikae chini na mumeo kutafuta sababu ya yeye kuwa vile?”
“Suzana mume wangu namfahamu vizuri, hata kama anatembea nje haijawahi kutokea, ninaye mwaka wa kumi sasa.”

“Mmh! Bado haijawa sababu, kwani yeye anasemaje?”
“Kwa kweli nyumba yetu imeingia matatizo ya kulaumiana huku nikimlaumu mume wangu na yeye kusema haelewi sababu ile inatokana na nini.”
“Mmekwenda hospitali?”
“Suzana wazo hilo sikuwa nalo, akili yangu yote niliielekeza kwenye lawama.”

“Sharifa hasira siku zote haijengi ulitakiwa kumsikiliza mwenzako.”
Wakiwa tukiwa katikati ya mazungumzo Brighton mpenzi wa Suzana aliingia. Baada ya kusalimiana Sharifa aliwaaga na kuwaacha wapendanao wazungumze. Baada ya kuondoka Sharifa alimuangalia Brighton kwa jicho la hasira.
“Vipi sweet, mbona unaniangalia hivyo?”

“Brighton wewe wa kunifanya hivyo, nimepungukiwa nini mwilini mwangu kufikia hatua ya kunidhalilisha kiasi hicho,” Suzana alimlalamikia mpenzi wake.
 
 
 
 
 
 
 

JINI WA DARAJA LA SALENDA.......EP.4.


ILIPOISHIA;
“Sikumueleza kwa kuamini hali ile imetokana na yeye kutoka nje ya ndoa.”
“Una uhakika gani sababu ya mumeo kuwa hivyo ni kutokana tukio lile?”
“Suzana sasa naingiwa na imani hiyo kutokana na tukio lililokutokea.”

“Sharifa kabla ya kutafuta ufumbuzi mbadala kwa nini usikae chini na mumeo kutafuta sababu ya yeye kuwa vile?”
“Suzana mume wangu namfahamu vizuri, hata kama anatembea nje haijawahi kutokea ninaye mwaka wa kumi sasa.”

“Mmh! Bado haijawa sababu, kwani yeye anasemaje?”
“Kwa kweli nyumba yetu imeingia matatizo ya kulaumiana huku nikimlaumu mume wangu na yeye kusema haelewi sababu ile inatokana na nini.”

“Mmekwenda hospitali?”
“Suzana wazo hilo sikuwa nalo, akili yangu yote niliielekeza kwenye lawama.”
“Sharifa hasira siku zote haijengi ulitakiwa kumsikiliza mwenzako.”

Wakiwa katikati ya mazungumzo Brighton mpenzi wa Suzana aliingia, baada ya kusalimiana Sharifa aliwaaga na kuwaacha wapendanao hao wazungumze. Baada ya kuondoka Sharifa alimuangalia Brighton kwa jicho la hasira.

“Vipi Sweet mbona unaniangalia hivyo?”
“Brighton wewe wa kunifanya hivyo, nimepungukiwa nini mwilini mwangu kufikia hatua ya kunidhalilisha kiasi hicho?” Suzana alimlalamikia mpenzi wake. SASA ENDELEA...

“Suzana nimekufanya nini tena mpenzi wangu?”
“Hujui...hujui eeh, juzi umenifanya nini Bilicanas?”
“Sasa Suzana nani wa kulaumiwa kati yangu na wewe?”
“Brighton unachukua mwanamke unaniacha club peke yangu, nilikulazimisha kuwa na wewe siku hiyo, si ni wewe ndiye uliyenipigia simu nije tujumuike wote kisha nikalale kwako.

Kama ulijua una miadi na mwanamke mwingine kwa nini uliniita?” Suzana alijisahau kama yupo ofisini na kujikuta akitokwa na machozi ya uchungu.
“Mimi?”
“Kwani nazungumza na ukuta?”

“Suzana juzi si nilikuacha unakunywa mimi nikapanda juu kuzungumza na Shakoor, nilipoteremka nilishangaa kukuta meza nyeupe na vinywaji vipo kama nilivyoviacha. Nilijua umekwenda msalani lakini muda ulipokwenda sana ilibidi nitoke nje kukutafuta. Kilichonishangaza sikukuta gari lako ilibidi nikodi teksi hadi nyumbani kwa kuamini umekwenda huko.

“Kila nilipopiga simu yako iliita bila kupokelewa, nilipofika nyumbani kwangu sikukuta, nilisubiri kwa saa moja mpaka saa tisa na nusu. Baada ya kutokukuona niliamua kukufuata kwako, nilikuta mlango umefungwa. Nilipomuuliza mlinzi aliniambia hujarudi.

“Hapo nilichanganyikiwa, nilijiuliza utakuwa wapi? Huwezi kuamini mpaka kunakucha nilikuwa sijapata jibu. Simu yako kila nilipopiga iliita bila kupokelewa, nilirudi nyumbani na kuamua kujilaza kidogo niende kanisani misa ya pili kutokana na uchovu wa kutopumzika.

“Amini usiamini nimeamka saa tatu usiku toka saa moja asubuhi nilipoweka ubavu, toka nizaliwe na kuwa na akili zangu timamu sijawahi kutokewa na usingizi wa ajabu kama ule. Hata nilipoamka nilikuwa kamsa mlevi niliyekunywa pombe nyingi, sikunyanyuka kitandani niliendelea kulala, huwezi kuamini nililala bila kula kwa saa 24 na nilipoamka leo asubuhi nilikuwa na nguvu kama sijatokewa na kitu chochote.

“Nilipitia kwako mlinzi alinieleza kama ulirudi, lakini kuna kitu kilitokea kilichoonesha kuna jambo limekupata na kuchukuliwa na familia yako. Mimi kiguu na njia mpaka kwenu, nilipofika niliambiwa umekuja kazini na afya yako ni salama. Kwani ulitokewa na nini?”
“Yangenitokea bila wewe?”

“Bila mimi kivipi Suzana?”
“Eeh, kama ningekwenda kwako unafikiri ningekutana na mauzauza, Brighton uliondoka na mwanamke unajitetea tu,” Suzana alizidi kulakamika.
“Suzana mpenzi wangu tuna muda gani juzi nifanye hivyo?”
“Si umenichoka.”

“Suzana naapa kwa jina la Yesu Kiristo uliniacha juu sikutoka na mwanamke muulize hata Shakoor kama nilitoka na mwanamke au muulize mlinzi wako nimefika kwako saa ngapi?”
“Itanibidi nikubali kwa vile nakupenda.”

“Suzana mpenzi wangu niamini siwezi kwenda kunyume na ahadi yetu, nakupenda na sitakusaliti hata siku moja.”
“Basi yamekwisha lakini uliniumiza sana.”
“Mh, eti ulipatwa na nini?”

“Samahani Brighton toka niingie ofisini sijafanya kazi yoyote, naomba unipe muda baada ya kazi nikitoka hapa nikakuja kwako moja kwa moja tuzungumze, ni mazungungumzo marefu.”
“Nigusie hata kidogo”
“Ni kuhusu nilipotoka Bilicanas na mambo niliyokutata nayo njiani.”
“Mambo gani?”

“Nimekueleza nitakueleza au unataka nifukuzwe kazi?”
“Basi mpenzi wangu nimekuelewa.”
Waliagana Brighton na mpenzi wake Suzana na kumuacha akifanya kazi. Baada ya kuondoka Brighton, Suzana alijikuta akihamia kwenye maelezo ya Brighton juu ya hali iliyomtokea ya kulala zaidi ya saa kumi na nne. Alijiuliza kama yeye alikutana na maajabu yale, Brighton alikutana na kitu gani.

Kazi kwake ilikuwa nzito siku ile, aliomba ruhusa na kurudi nyumbani kupumzika, kabla ya kutoka alimjulisha mpenzi wake kuwa anatangulia nyumbani kwake.

Baada ya kutoka kazini alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa mpenzi wake, kwa vile alikuwa na funguo za nyumba alifungua na kuingia ndani. Alipoingia alishangaa kukuta chumbani kumesafishwa tofauti na siku zote, mara nyingi usafi wa nyumba ile alikuwa akifanya yeye.

Ile haikumsumbua akili yake aliamini kutokana na msongo wa mawazo hali ya usafi ya nyumba ingemfanya asisumbue mwili wake zaidi ya kwenda moja kwa moja chumbani kujilaza. Hali ya hewa ndani ilikuwa nzuri tofauti na siku zote huku harufu ya manukato aliyowahi kuyasikia alipokutana na maajabu ya dalaja la Salenda.

Upepo mwanana uliompuliza ulimfanya apitiwe na usingizi bila kujijua, katikati ya usingizi alishtushwa na Brighton akimpapasa.
“Aah, mpenzi umerudi zamani?”
“Kama robo saa.”

Kwa vile Brighton alikuwa amekwishaoga Suzana naye alikwenda kuoga na kujumuika wote kitandani. Kama kawaida walisafiri katika meli ya wapendanao, safari ya kwanza ilianza vizuri kila mmoja aliifurahia. Baada ya safari ya kwanza kwisha Suzana hamu ilikuwa bado haijamuisha alitaka asafiri safari moja zaidi ndipo wapumzike.

Ajabu kila alipomgusa mwenzake jogoo alikataa kuwika kitu kilichomshtua Suzana.
“Vipi mpenzi mbona hivi?”
“Hata mimi nashangaa.”
Nini kimempata Brighton? Au ndiyo yaliyompata mume wa Sharifa?
 
 
 
 
 
 
JINI WA DARAJA LA SALENDA.......EP.5.


ILIPOISHIA:
Kwa vile Brighton alikuwa amekwishaoga, Suzana naye alikwenda kuoga na kujumuika wote kitandani. Kama kawaida walisafiri katika meli ya wapendanao, safari ya kwanza ilianza vizuri kila mmoja alifurahia safari ile.
Baada ya safari ya kwanza kwisha, Suzana hamu ilikuwa bado haijamuisha, alitaka asafiri safari moja zaidi ndipo wapumzike.
Ajabu kila alipomgusa mwenzake, jogoo alikataa kuwika kitu kilichomshtua Suzana.
“Vipi mpenzi mbona hivi?”
“Hata mimi nashangaa.”
SASA ENDELEA...

“Au umeanzia kwa mwingine?”
“Lakini kwa nini kila linapotokea tatizo unanifikiria vibaya kuwa nilikuwa na wanawake? Siku hizi sina kazi, kazi yangu kutembea na wanawake,” Brighton alilalamika.
“Mbona leo imekuwa hivi?”

“Hata mimi nashangaa.”
Suzana alijitahidi kumkanda mpenzi wake kumrudisha kwenye hali ya kawaida lakini hakukuwa na mabadiliko, jogoo alikataa kuwika. Aliamua kumwacha ajipumzishe waendelee baadaye. Alijilaza pembeni ya Brighton aliyeonekana mwingi wa mawazo.

Suzana akiwa amejilaza alikuwa na yake aliyokuwa akiwaza, ghafla mazungumzo yake na Sharifa yalijaa kichwani na kuyakumbuka maneno aliyoelezwa juu ya tatizo la mume wake.

“Basi shoga, siku ile niliporudi nyumbani nilikutana kimwili na mume wangu kama kawaida mzunguko wa kwanza ulikwenda vizuri, ajabu wa pili hakuwa na nguvu kila alivyojitahidi, nguvu za kiume ziligoma.”

Sauti ile ilijirudia kichwani mwake na kumfanya atishike na kuamini huenda tatizo la Sharifa limempata na yeye. Bila kujielewa, alijikuta akikaa kitako na kumshtua Brighton aliyekuwa katika dimbwi la mawazo.
“Brighton,” alimwita kwa sauti ya juu japo alikuwa pembeni yake.
“Unasemaje?”

“Hali hii imekutokea mara ngapi?”
“Suzana swali gani hilo, toka niwe na wewe hali hii imeshanitokea?”
“Hapana, basi utakuwa na tatizo la muda mrefu.”

“Lakini siamini huenda ni uchovu ngoja nipumzike kidogo tutaendelea,” Brighton alimtoa hofu Suzana.
“Mmh! Sawa,” Suzana aliguna akiwa na wasiwasi na maneno aliyoelezwa na Sharifa ya mpenziwe kuwa amekufa nguvu za kiume.

Kila mmoja alilala upande wake, mchana waliamka na kwenda kupata chakula cha mchana. Wakiwa wamekaa wanakula, Brighton akamsifia Suzana kwa usafi aliofanya na kuifanya nyumba ipendeze.
“Mpenzi umetumia muda gani kufanya usafi ule?”
“Usafi gani?”

“Wa nyumba,” kauli ile ilimshtua Suzana na kuamini kabisa tayari nyumba yao imeingia kwenye tatizo lakini hakutaka kulikubali mara moja ili kuficha kila anachokiwaza, alijikuta akikubali pongezi zisizo zake.

Baada ya kupata chakula walirudi nyumbani kupumzika, kwa vile kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzake baada ya kuoga walipanda kitandani kujiachia kwa raha zao. Lakini hali ilikuwa mbaya zaidi Brighton hakuwa na nguvu za kiume.
Hali ile ilizidi kumweka Suzana kwenye hali mbaya, hakukubaliana nayo, aliendelea kumsaidia mpenzi wake lakini hali ilikuwa ile ile.
Suzana alijikuta akiangua kilio kitu kilichomshtua Brighton na kuhoji:

“Suzana mbona unalia?”
“Brighton unajiona upo sawa?”
“Sijajua nikujibu nini?”
“Hujioni haupo sawa?”
“Hali ya leo inanishangaza hata mimi si kawaida yangu.”
“Inawezekana kuwa ndiyo yenyewe,” Suzana aliropoka.
“Yenyewe nini?”

“We acha tu, kesho nitakwenda kumweleza Sharifa.”
“Kumweleza nini?” Brighton alizidi kuyashangaa maneno ya mpenzi wake.

“Naomba leo tuachane na hilo.”
“Kwani umegundua nini kuhusu tatizo langu?”
“Brighton sijagundua lolote.”
“Mbona unasema utanijibu kesho?”
“Sijajua nini tatizo, linafanana na la Sharifa.”
“Sharifa ana tatizo gani?”
“Brighton tutazungumza kesho, naomba niondoke.”
“Si ulisema utalala?”

“Kwa hali hii siwezi kulala niache tu niwahi nyumbani.”
Brighton hakuwa na la kusema zaidi ya kumruhusu Suzana akalale kwao. Suzana akionekana amechanganyikiwa, aliwasha gari na kurejea kwake. Alijikuta akilia njia nzima juu ya hali ya mpenzi wake huku akijiuliza kama itakuwa hivyo mpenzi wake amekufa nguvu za kiume atafanya nini? Alipoingia ndani kwake alijitupa kitandani hata usingizi ulivyomchukua hakujua.

Suzana alishtuka siku ya pili, alijiandaa kwenda kazini huku akiwa na shauku ya kuonana na Sharifa kumwelezea yaliyomsibu kama yake. Alipofika kazini kiti alikiona cha moto, hakukaa, alikwenda moja kwa moja ofisini kwa Sharifa. Sharifa alipomuona alishtuka na kumkaribisha:

“Mmh! Dada mbona asubuhi asubuhi?”
“Wee acha tu, ukiona hivyo ujue kuna jambo.”
“Karibu, mi ndo naingia sasa hivi hata vumbi sijafuta kwenye kompyuta.”
“Yaani wee acha tu,” Suzana alisema huku akiketi kwenye kiti.
“Mh, kuna kipi kipya?”

“Kuna mapya! Yale yaliyokutokea yamefika na kwangu.”
“Yapi hayo tena?”
“Si yaliyomtokea mume wako.”
“Unamaanisha jogoo kushindwa kuwika?”
“Ndiyo.”
“Ehe!”

Suzana alimwelezea Sharifa yaliyomkuta, baada ya kumsikiliza alishusha pumzi na kusema:
“Unajua unaweza kuona nakutania .”
“Kwa kipi?”
“Jana usiku nilipokutana na mume wangu huwezi kuamini, nimefurahia tendo kama kawaida.”

“Wewee! Mara zote?”
“Tena ajabu lilikuwa penzi tamu ajabu hata asubuhi nimeamka nilihisi kama siku ya kwanza kuonana na mume wangu.”
 
 
 
 
 
 
 
 
JINI WA DARAJA LA SALENDA.......EP.6.


ILIPOISHIA;
Suzana alimuelezea Sharifa yaliyomkuta, baada ya kumsikiliza alishusha pumzi na kusema:
“Unajua unaweza kuona nakutania!”
“Kwa kipi?”

“Jana usiku nilipokutana na mpenzi wangu huwezi kuamini nimefurahia tendo kama kawaida.”
“Wewee! Mara zote?”
“Tena ajabu lilikuwa penzi tamu ajabu hata asubuhi nimeamka nilihisi kama siku ya kwanza kuonana na mume wangu.”
“Usiniambie,” Suzana alishika mkono kwa mshtuko. SASA ENDELEA...

“Hata nashindwa kuelewa hali ya jana inatokana na nini?”?”Au alikwenda hospitali?”
“Walaa, hata yeye anashangaa.”
“Sasa kwangu imetokana na nini?”
“Hapo ndipo nashindwa kujua hali hii inatokana na nini.”

“Yaani nashindwa kuelewa na kubakia njia panda, niliamini lililonitokea jana ndilo lililokutokea wewe wiki moja iliyopita. Leo imekuwa tofauti kabisa uliponieleza hali imebadilika.”
“Suzana hebu nawe angalia kwa wiki tuone mabadiliko, huenda vyakula tunayokula vimesababisha upungufu wa nguvu za kiume.”

“Lakini Sharifa upungufu gani hata kunyanyuka kidogo.”
“Suzana hata kwangu ilikuwa hivyo hivyo, jana sikuamini, tena mume wangu ndiye aliyeniamsha usingizini.”
“Basi inawezekana tatizo hili limeingia, kwani hujawahi kusikia mwingine zaidi yetu mwenye tatizo kama hili?”?”Mmh! Sijawahi.”

“Kama lako limekwisha huenda langu bado nalo litakwisha.”
“Ondoa wasiwasi nina imani litakwisha.”
“Mmh! Sawa.”

Suzana alimuaga Sharifa na kurudi ofisini kwake, alipofika alijikuta akicheka peke yake na kuamini huenda tatizo lile huondoka bila dawa.
Siku hiyo Suzana alishinda akiwa bado yupo njia panda, baada ya kuamini alichokiona Daraja la Salenda ndicho kilichosababisha hali ile.

Lakini ilikuwa tofauti baada ya kukutana na Sharifa na kumueleza kuwa hali ya mumewe kukosa nguvu za kiume imekwisha. Pamoja na kusikia nguvu za mume wa Sharifa zimerudi katika hali yake bado alikuwa na maswali juu ya hali ile kuwatokea wanaume wawili tofauti ilitokana na nini?

Suzana naye alijipa moyo kuwepo na mabadiliko kwa mpenzi wake, lakini walipokutana zaidi ya mara tatu hakukuwa na mabadiliko yoyote. Bado alijipa moyo kwa vile wiki ilikuwa bado haijakatika. Akiwa ofisini kwake akiendelea na kazi alimuona Sharifa akiingia kwa mwendo wa kujivuta.

Alipomuona alishtuka na kumuuliza:
“Vipi shoga mbona hivyo?”
“Wee acha tu, hata sijui hili ni balaa gani?”
“Kwa nini? Hebu kaa kwanza.”

Baada ya kuketi Sharifa alishusha pumzi huku akiuma meno kuonesha kuna kitu kilimuuma sana.
“Vipi shoga kulikoni?”
“Mmh! Hata nashindwa nianzie wapi.”
“Kivipi tena Sharifa mbona unanitisha.”

“Hebu ngoja,” alisema huku akijiweka vizuri kwenye kiti.
Suzana alimuangalia Sharifa kwa huruma alivyokuwa akiugulia maumivu.
“Jamani Sharifa si uende hospitali?”
“Hata sielewi ugonjwa huu ni wa hospitali au vipi.”
“Kwa nini?”

“Hadithi bado inaendelea?”
“Hadithi gani tena Sharifa?”
“Si ile niliyokueleza.”
“Ya?”

“Kuhusu mume wangu na matatizo yake.”
“He! Yamerudi tena?”
“Tena sasa hivi hata kuielezea siwezi.”
“Sharifa mbona unanitisha au bado ni yale yale ya Daraja la Salenda?”

“Inaweza kuwa hivyo.”
“Mmh! Ehe, kwa hiyo tatizo limejirudia?”
“Hapana, ila limezuka lingine.”
“Lipi hilo?”

“Basi shoga siku ile baada ya kukueleza raha nilizipata kwa mume wangu usiku wake vilitokea vitu vya ajabu. Nilipokutana na mume wangu nilishangaa kuhisi maumivu makali kama vile maumbile yake yameongezeka hata kuingia ilikuwa shida.”
“Weweee!”

“Basi shoga wacha nipige kelele za maumivu ambazo zilimshtua mume wangu na kuniuliza hali ile imeanza lini la kuyaona maumbile yake yananiumiza. Nilivumilia lakini sikuona raha yoyote zaidi ya maumivu. Mpaka tunamaliza sikuwa na hamu tena sehemu za siri zilikuwa zikiniuma sana.

“Siku ya pili sikuwa tayari kuendelea kuumizwa, lakini mume wangu alikuwa akinishangaa na kusema mbona yupo kawaida. Siku ile tulifanya gizani, lakini jana tuliwasha taa na kuyaona ya kawaida. Hata tulipokuwa kwenye zoezi sikuhisi maumivu yoyote.

“Baada ya kufanya mapenzi na mume wangu kila mmoja aligeuka upande wake kulala, katikati ya usingizi niliota kuna mtu kaingiza mkono sehemu zangu za siri na kuanza kukoroga, kitu kile kilifanya nihisi maumivu makali sana chini ya tumboni.

Niliposhtuka usingizini nilishtuka kumuona mume wangu akiwa juu yangu, kutokana na maumivu niliyokuwa nikisikia nilimsukuma kwa miguu. Baada ya kumsukuma tumbo lilinikata kwa muda kisha lilitulia.”

“Jamani kama angekuwa na shida na wewe kwa nini usikuambie kuliko kukuingilia bila taarifa?” Suzana alichangia.
“Hata mimi nashangaa mume wangu toka anioe hajawahi kufanya vile.”
“Wewee!’” Suzana alishtuka kusikia vile.

“Hebu ona ajabu nyingine baada ya kumsukuma mume wangu na miguu na kuanguka upande wa pili, aliendelea na usingizi mzito na asubuhi nilipomuuliza alishangaa huku akiapa kwa miungu yote hakuniingilia usiku.”

“Weweee!”
“Yaani nilimueleza yote lakini alibisha na kusema labda nilikuwa naota.
Nilimueleza kuwa alikuwa juu yangu na hali niliyosikia, bado alikataa.

Basi shoga yangu tokea hapo nilishangaa kuiona damu yangu ya hedhi, ilikuwa ajabu kuingia hedhi mara mbili kwa mwezi. Hata kutembea sitakiwi kuharakisha, nikiharakisha chini ya kitovu pananivuta sana.”

“Sharifa unajua tunafanya uzembe, tukija shituka tumekwisha umia.”
“Na kweli hili jambo siwezi kuliacha lipite hivi hivi, sasa hivi mapenzi nayaogopa kwani yamekuwa mateso.”

“Si ulinieleza kuna mtu unayemfahamu tulifanyie kazi, nipo tayari kukusaidia
Mpaka hatua ya mwisho.”
“Nimekuelewa acha nikapumzike, kiuno chote kimenishika na mama amesema anikute nyumbani.”

Suzana na Sharifa waliagana, baada ya kutoka shoga yake Suzana alizidi kuchanganyikiwa. Alijiuliza ni kitu gani tena kilichomtokea Sharifa, alipanga amtafute mtu amuelezee matatizo ya mpenzi wake.
 
 
 
 
 
 
 
JINI WA DARAJA LA SALENDA.......EP.7.

ILIPOISHIA;
“Nimekuelewa, acha nikapumzike nyumbani kwani kiuno chote kimenishika na mama amesema anikute.”
Suzana na Sharifa waliagana, baada ya kutoka, Suzana alizidi kuchanganyikiwa juu ya hali ya shoga yake. Alijiuliza ni kitu gani kilichomtokea Sharifa, alipanga amtafute mtu amwelezee matatizo ya mpenzi wake.
SASA ENDELEA...

Sharifa akiwa na maumivu makali ya chini ya tumbo, alitembea taratibu kurudi nyumbani. Suzana alipata wazo la kumsindikiza shoga yake ambaye aliamini kabisa alihitaji msaada wake. Alitoka haraka nje na kumkuta akimtafuta dereva wa kampuni ampeleke nyumbani.

“Sharifa acha nikupeleke mimi.”
“Suzana endelea na kazi, acha tu nitafika.”
“Haiwezekani, lazima nikusindikize.”
“Mmh! Sawa.”

Suzana alikimbilia kwenye gari lake na kuligeuza haraka kisha akasimamisha pembeni ya Sharifa na kumfungulia mlango. Sharifa aliingia na kufunga mlango. Alimpeleka kwake kupitia Barabara ya Ali Hassani Mwinyi. Ajabu walipokaribia Daraja la Salenda, Suzana alipunguza mwendo na kumfanya Sharifa aliyekuwa amejilaza kukaa kitako.

Wote walijikuta wakitupia macho maeneo ya baharini labda wataona kitu chochote lakini hawakuona kitu walichokikusudia zaidi ya kuwaona watu wakitembea juu ya mchanga baada ya bahari kupwa. Baada ya kila mmoja kuwa na uhakika hakuna kitu, Suzana aligeuza uso wake na kubadili gia ili waendelee na safari yao.

Sharifa alikuwa wa kwanza kushtuka na kupaza sauti yake...
“Suzana umemuona yule mwanamke pale pembeni ya barabara?”
Suzana aligeuza shingo tena kuangalia sehemu aliyooneshwa na rafiki yake, kweli alimuona mwanamke mmoja mrefu aliyekuwa amevalia gauni la rangi nyekundu na mtandio wake mwepesi ulioziacha nywele zake nje. Ajabu wakati huo gari lao lilizimika ghafla.

“Suzana vipi, mbona hivyo?”
“Hata mimi nashangaa gari limezimika ghafla.”
“Makubwa, sasa yule dada ni nani?”
“Hata najua, muone jinsi alivyo mzuri, tena anatuchekea labda anatujua.”

“Mmh! Lakini mbona sielewi, nausikia mwili wote ukinisisimka.”
“Siyo wewe tu, hata mimi nasikia nywele zikinisisimka.”
“Mmh! Inawezekana mtu yule si mzuri?”
“Na kweli Suzana, hebu yaone macho yake! Mbona siyaelewi... Mungu wangu! Ona miale inatoka machoni kwake, Suzana washa gari tuondoke.”

Suzana alijaribu kuwasha gari lake lakini liligoma kuwaka, walijikuta wakizidi kupagawa na kutamani kupiga kelele. Sharifa alishtuka kuona mabadiliko kwa yule mwanamke aliyekuwa bado amesimama sehemu ile ile chini ya mti.
“Suzana haya ni maajabu!”
“Ya nini?”

“Muone yule mwanamke, si alikuwa amevaa gauni jekundu na mtandio?”
Suzana alinyanyua uso kumuangalia yule mwanamke na kumuona akiwa na gauni lingine la rangi pinki lililokuwa limempendeza zaidi ya mwanzo, nywele zake zikiwa zimetengenezwa vizuri na kuongeza urembo wake.

“Mmh! Kweli! Kama sikosei alikuwa na gauni jekundu.”
“Unajua yule si kiumbe wa kawaida, huenda ni jini.”
“Jini?”

Kauli ile ilifanya wasikie msonyo mkali ambao ulifanya tumbo la Sharifa livurugike ghafla, baada ya muda lilitulia na kurudi katika hali ya kawaida. Yule mwanamke waliyekuwa wanamshangaa aliwapungia mkono kama anawafahamu, wakajikuta wote wakimpungia mkono, aligeuka na kuondoka kuelekea baharini.

Walijikuta wakimsindikiza kwa macho yule mwanamke aliyeanza kuelekea katikati ya bahari na kupotea machoni mwao.
“Mmh! Suzana hii nini?”
“Hata sijui.”

“Sasa yule atakuwa nani?”
“Yaani nazidi kuchanganyikiwa, ulisikia ule msonyo?”
“Nisiusikie vipi wakati umelifanya tumbo langu lingurume na kutulia.”

Ajabu nyingine, Suzana alipojaribu kuwasha gari liliwaka, wakaamua kuendelea na safari yao huku kila mmoja akijiuliza yule mwanamke mzuri aliyevalia gauni lenye mshono mzuri ambao hawakuwahi kuuona.
“Jamani haya ni maajabu, sasa yule mwanamke ni jini?”

“Lakini jini gani anavaa nguo nzuri kama zile tena za gharama?”
“Mmh! Makubwa, hata sielewi eneo hili lina nini. Kuna umuhimu wa kuulizia zaidi kwa watu ili tupate ufumbuzi.”

Suzana aliendesha gari mpaka nyumbani kwa Sharifa, bahati nzuri walimkuta mama yake ameshafika nyumbani kwake. Hali ya Sharifa ilikuwa tofauti na muda mfupi uliopita akiwa ofisini. Alishangaa kujiona akiwa mzima kabisa, wala hakutembea kwa kupinda mgongo kwa maumivu ya tumbo tena.

Hali ile ilimshangaza hata Suzana kumuona shoga yake yupo katika hali nzuri.
“Sharifa vipi maumivu yamekwisha?”
“Huwezi kuamini sasa hivi sijambo kabisa, siumwi chochote mwilini.”

“Mmh! Mbona mwaka huu wa maajabu, kila dakika kinazuka kitu kipya machoni mwangu.”

“Shoga karibu ndani umsalimie mama uwahi kazini.”
Suzana aliingia ndani kwa Sharifa kumsalimia mama yake. Alipoingia nusura akimbie kwa mshtuko, aliyeambiwa ni mama yake Sharifa alikuwa ni yule mwanamke mrembo waliyemuona maeneo ya Daraja la Salenda.

“Karibu mwanangu.”
“A..a..sante.”
Alishangaa kumuona akitabasamu lakini ajabu Sharifa hakuonesha mabadiliko yoyote zaidi ya kuendelea kumtambulisha kwa mama yake.
“Sharifa huyu ndiye mama yangu.”

Suzana alijiuliza iweje amshangae baharini lakini nyumbani amtambulishe kuwa ni mama yake. Tofauti yake ilikuwa vazi alilovaa, muda ule alivaa hijabu nyeusi na mtandio mwepesi.

Suzana aliaga na kutaka kuondoka baada ya kushindwa kumuelewa mama. Ghafla yule mama alibadilika na kuwa mtu wa makamo tofauti na mwanzo. Suzana aliaga ili aondoke baada ya kushindwa kuelewa alichokiona mbele yake.

Kila dakika imekuwa ikimshangaza Suzana, ni kweli aliyemuona mbele yake ni yule waliyemuona baharini na aligeuka na kuwa mtu mwingine?
 
 
 
 
 
 
 

JINI WA DARAJA LA SALENDA.......EP.8.


ILIPOISHIA;
Alishangaa kumuona akitabasamu, lakini ajabu Sharifa hakuonesha mabadiliko yoyote zaidi ya kuendelea kumtambulisha kwa mama yake.
“Sharifa huyu ndiye mama yangu.”

Suzana alijiuliza iweje amshangae baharini lakini nyumbani amfahamishe ni mama yake. Tofauti yake ilikuwa vazi alilovaa muda ule lilikuwa hijabu nyeusi na mtandio mwepesi. Suzana aliaga ili aondoke baada ya kushindwa kumuelewa mama, lakini ghafla yule mama alibadilika na kuwa mtu wa makamo tofauti na mwanzo. Suzana alishindwa kuelewa alichokiona mbele yake. SASA ENDELEA...

Akiwa njiani alijiuliza maswali yasiyo na majibu juu ya mambo aliyokutana nayo ya kumuona mwanamke mzuri aliyebadilika nguo, pia kutambulishwa tena kuwa ndiye mama yake Sharifa. Alijikuta akijiuliza Sharifa huenda naye ni jini lakini wasiwasi wake mkubwa ulikuwa kwa Sharifa, mtu aliyemfahamu muda mrefu hakuonesha kitu chochote cha kumfanya amdhanie kuwa si mtu wa kawaida.

Alijiuliza ilikuwaje amuone akifanana na mwanamke waliyemuona pembeni mwa Barabara ya Ali Hasani Mwinyi karibu na Daraja la Salenda na baadaye kumuona mtu tofauti. Aliamua kurudi ofisini kuendelea na kazi.

******
Jioni akiwa nyumbani alipigiwa simu na Sharifa, aliipokea na kuzungumza.
“Vipi shoga za muda?’
“Nzuri tu, vipi unaendeleaje?”
“Huwezi kuamini sijambo kabisa kama siyo mimi niliyekuja ofisini nikitembea kwa shida, kingine kilichonishangaza ni kukatika ghafla kwa damu yangu ya hedhi.”

“Wewee!”
“Yaani Suzy siamini kila dakika kwangu ni miujiza.”
“Mmh! Makubwa.”
“Halafu Suzy eti kuna kitu gani kisicho cha kawaida ulikiona tulipofika nyumbani?”
“Kitu gani?”
“Kisicho cha kawaida ambacho kilikutisha,” swali lile lilimshtua Suzy na kujiuliza kwa nini ameulizwa.

“Kwa nini umeniuliza swali hilo?”
“We nijibu kuna kitu nataka kukuambia.”
“Ni kweli, we umejuaje?”
“Hivi nd’o nimeingia toka kwa mtaalamu mama alinipeleka.”
“He ! Amesemaje?”
“Mmh! Shoga mazito si ya kuyazungumza kwenye simu.”
“Kwa hiyo?”

“Kama unaweza kuja nyumbani njoo, maana hapa nilipo niliyoelekezwa yamenichosha.”
“Mmh! Lazima nije?”
“Basi shoga njoo usikie mambo ya dunia.”
Taarifa zile zilimfanya Suzana ajiandae haraka haraka na kuingia ndani ya gari lake, tayari kwenda kwa Sharifa akiwa na shauku ya kutaka kujua kitu gani kilichomfanya aseme vile. Alimkuta Sharifa akimsubiri kwa hamu.

“Karibu shoga yangu.”
“Asante.”
“Naona ndiyo unatoka kuoga?’
“Wee acha mwili ulikuwa umechoka kila kona, karibu.”
“Asante,” Suzana alijibu huku akikaa kwenye kochi.
“Mh! Shoga lete habari,” Suzana alianzisha mazungumzo.

“Basi shoga baada ya kuondoka nilibakia na mama na kumueleza yote yaliyonitokea hata tukio la kuonana na yule mwanamke leo.”
“Ehe.”
“Mama alinieleza lazima yule atakuwa jini.”
“Ehe.”

“Basi alinichukua na kunipeleka kwa mzee mmoja mtaalam wa majini, tulipofika tulikaribishwa kwenye chumba kilichokuwa na mkeka na nyuma yake kulikuwa shuka nyekundu, pia kulikuwa na picha za kuchora za simba na viumbe visivyoeleweka.”
“Mmh.”

“Basi mganga huyo kijana akachukua kioo kidogo na kunitaka niweke mkono juu yake na kuniuliza matatizo yangu. Baada ya muda akatanitaka nitoe mkono na kunitaka nikitazame kile kioo kwa muda kisha alishusha pumzi.

“Huwezi kuamini wakati akikitazama kile kioo jasho lilianza kumvuja yule mganga kama kamwagiwa maji, kitu kilichonishtua sana. Baada ya kushusha pumzi alichukua kitambaa na kukifuta na kutuuliza.”

“Mnataka mtatuliwe matatizo yenu au unataka kujua sababu ya yote yaliyotokea?”
“Wewe utakavyoona inafaa,” Mama alijibu.
“Mama si huwa nasikia eti waganga wanajua kila kitu kilichotokea kabla ya kutibu?” Niliuliza.

“Ni kweli tunajua na yote nimeyaona hapa,” mganga alinijibu.
“Sasa si ungeniambia ili nijue natibiwa kitu gani?”
“Hakuna tatizo, kwa hiyo upo tayari kuyasikia yaliyokusibu?”
“Nipo tayari,” nilimjibu.

“Haya vizuri,” Baada ya kusema vile alichukua unga na kuumwaga mbele yake huku akisema maneno kwa sauti ya chini. Baada ya kusema vile alikichukua kioo na kuangalia tena kwa muda wa kama dakika kumi kisha alitugeukia na kusema:
“Kama nitakuwa nasema uongo naomba ukatae, sitaki nionekane nazungumza tofautina ukweli.”
“Sawa.”

“Unaitwa Sharifa, sawa?”
“Ndiyo”
“Umeolewa?”
“Ndiyo.”
“Ndani ya wiki tatu kumetokea matatizo ndani ya ndoa yako?’
“Ndiyo.”

“Wasiwasi wako ni tukio lililokutokea katika Daraja la Salenda?”
“Kweli.”
“Basi ni kweli tatizo lako lilitokana na tukio la darajani ambalo lilipelekea kukuingizia mgogoro ndani ya ndoa yako. Yule uliyekutana naye ni Jini Balikis, kazi yake kubwa ni kuvuruga ndoa za watu. Si wewe tu kuna watu wengi wamekumbwa na mgogoro huu hata kufikia hatua ya kuachana.

“Hata rafiki yako kipenzi ana tatizo hilo, tena yule ndiye chaguo la Jini Balkis kwa vile ni mwanadamu pekee aliyeshuhudia sherehe ya kuagwa kwake kuja duniani.

“ Tuachane na hayo ya shoga yako najua naye ana yake, ila tatizo la mumeo kukosa nguvu za kiume linatokana na kufanya mapenzi na Jini Balkis.
“Kila mnapofanya mapenzi, jini huyo hufika katika eneo la tukio hilo na kuziondoa nguvu za mumeo ili asiweze kukuridhisha vyema.

“Anafanya hivyo makusudi ili aweze kufanya naye mapenzi yeye wakati wa usiku mkiwa mmelala.
“Kama nasema uongo muulize mumeo kama huwa hafanyi mapenzi na mwanamke mzuri kiasi cha kufikia kukuona wewe hufai tena kwake.”

Huu ni mwanzo wa siri ya Jini la Daraja la Salenda. Nini kiliendelea?
 
 
 
 
 
 
 
JINI WA DARAJA LA SALENDA.......EP.9.


ILIPOISHIA:
Kama nasema uongo muulize mumeo kama huwa hafanyi mapenzi na mwanamke mzuri usingizini hadi kufikia hatua ya kukuona hufai tena kwake.”
SASA ENDELEA...

Kauli ile kwa kweli ilinishtua sana, basi mganga akaendelea kuchimbua mambo na kusema:

“Baada ya kufanya vile kitu kile kilikutia wasiwasi kiasi cha kufikiria kutafuta ufumbuzi baada ya kupata tatizo kama hilo kumtokea shoga yako. Kumbuka mwanzo uliamini kabisa tatizo lile linatokana na mwenzako kutokuwa mwaminifu ndani ya ndoa yako kweli?”
“Kweli.”

“Baada ya kupanga mipango ya kutafuta ufumbuzi wa mumeo kupoteza nguvu za kiume na shoga’ako kukutwa kama mtu aliyekufa, pale shoga’ako kama wangechelewa alikuwa anabadilishwa kwa kuchukuliwa maiti yake ambayo ingepelekwa chini ya bahari na yeye Jini kukaa na mchumba wake.”

Kauli ile ilimshutua sana Suzana na kujikuta akishika mdomo kwa mshtuko.
“Mungu wangu, ina maana pale nilikuwa nakufa?” Suzana alimuuliza Sharifa.

“Shoga hebu tulia kwanza unisikilize utaniuliza maswali mwisho japo nina imani maelezo nitakayokupa hutahitaji kuniuliza swali.”
“Mmh! Inatisha sana, haya endelea.”
Basi mganga akaendelea kunieleza:

“Kilichomrudisha shoga yako duniani ni maombi yaliyofanywa na familia yake bila hivyo maisha yake yote yangekuwa chini ya bahari na jini yule kuishi na mpenzi wake kwa kuwa shida yake ilikuwa kusambaratisha ndoa za wanadamu au uhusiano wa watu waliopendana. Baada ya shoga yako kurudi katika hali yake ya kawaida na wewe mumeo akapoteza nguvu za kiume.

“Mlipokutana na kuhadithiana juu ya kilichotokea Daraja la Salenda na matukio yaliyowatokea. Alihamia kwa shoga yako kumtoa nguvu za kiume mpenzi wake. Mwanzo shoga yako hakuwa na imani kuwa kuna vitu kama hivyo vinatokea, vilipomtokea kama ulivyomuhadithia mumeo kutokewa na hali ile, hapo ndipo akaamini kabisa ni kweli tatizo lipo katika Daraja la Salenda.

“Jini Balkis aliwachezea akili kwa kumrudishia mumeo nguvu za kiume ili taarifa za shoga zako zipingane na ukweli ambao ungepata picha ya tukio la Daraja la Salenda.

Kumbuka usiku wa siku ile ulipokutana kimwili na mumeo kulikuwa na tofauti kubwa na siku zote tangu muoane, kweli au uongo?” Mganga aliniuliza.
“Kweli,” nilijibu huku nikiona aibu kutamka maneno yale mbele ya mama.
“Unajua ni kwa nini?” Aliniuliza.
“Hata sijui.”

“Majini wanapotaka kufanya mapenzi na wanadamu huwapaka mafuta sehemu za siri ili asipungukiwe nguvu za kiume ili waweze kumpa raha kwa muda mrefu. Hawapendi kukatishwa raha, huchukia sana. Mwanzo walikuwa wakifanya mapenzi na wanadamu bila kutumia kitu chochote.

“Lakini tatizo la nguvu za kiume ndilo lililowakasirisha na kutafuta njia ya kustarehe na mwanadamu kwa muda mrefu. Njia ilikuwa ni kutafuta dawa ya kumwezesha mwanaume awe na nguvu muda wote wa kufanya mapenzi chombo kisilale, nina imani umenielewa kusema chombo?” Mganga aliniuliza.

“Ndiyo nakuelewa endelea mzee wangu,” nilimjibu huku nikihisi mwili ukinisisimka kwa yale niliyoyasikia. Basi mzee akaendelea huku akiangalia kioo kama anasoma kitu.

“Basi baada ya kujua kesho yake shoga yako naye yamemtokea kama yako na kuamini kabisa mtaamini kilichotokea kinatokana na tukio la Darajani Salenda. Usiku mkiwa mmelala, Jini Balkis alikuja na kumpaka mafuta yale mumeo sehemu za siri ambayo yalizifanya sehemu zake zinyanyuke. Mumeo alikuamsha usingizini kutaka haki yake, kweli au si kweli?” Mganga aliniuliza.

“Kweli,” nilimjibu kwa aibu mbele ya mama aliyekuwa ametulia akisikiliza kwa makini.
“Najua hukuamini kuikuta hali yake tofauti na siku zilizopita za kukosa nguvu za kiume, ulishtuka, hukushtuka?”
“Nilishtuka.”

“Hata ulipokubali kufanya naye mapenzi bado hukumuamini, ulijua ni yale yale ya siku zote, lakini ilikuwa tofauti na siku zote. Pia kulikuwa na tofauti kubwa siku za nyuma ulipofanya mapenzi kwa muda mrefu ulikuwa unachoka sana lakini siku ile ilikuwa tofauti, kweli au si kweli?”

“Kweli.”
“Usijibu kwa kuniogopa, nijibu kwa uhakika siyo ukubali hata la uongo.”
“La uongo nitakuambia lakini yote unayosema ni kweli.”
“Najua asubuhi ulipoamka ulijishangaa kuwa na nguvu za ajabu huku ukikumbuka penzi tamu la mumeo ambalo hakuwahi kukupa tangu akuoe.”
“Ni kweli.”

“Ni kwa nini hukuchoka kama siku zote?”
“Hata sijui, nilifikiri labda kutokana na kukaa muda mrefu bila kukutana na mume wangu.”
“Unataka kuniambia kipindi hiki ndicho kirefu kuchelewa kukutana na mumeo?”
“Hapana.”

“Unajua sababu ya kufurahia penzi la siku hiyo na asubuhi kuamka na nguvu za ajabu hata kazi siku hiyo ulifanya ukiwa na furaha tele moyoni?”
“Hata sijui.”
“Nawe ulipakwa mafuta yale ambayo hutumia majini wa kike, kujipaka sehemu za siri ambayo huongeza raha ya mapenzi kiasi cha kumfanya mwanaume asikuchoke na yeye kusikia raha ya mapenzi.

Hata wewe hukuchoka na kusikia raha muda wote wa kufanya mapenzi na ulipoamka hukusikia uchovu wa mwili. Kwa kutumia mafuta yale unaweza kufanya mapenzi ya nguvu kila siku.”
“Mmh! Kumbe.”

“Wakati wewe unakula raha ndiyo siku hiyo shoga yako yalimtokea kama yaliyokutokea wewe siku za nyuma za mumeo kupoteza nguvu za kiume. Shoga yako alikuja kazini akiamini ungeungana naye kwenye tatizo lake lakini ilikuwa kinyume kitu kilichomchanganya mwenzako na kuwa njia panda tatizo la nguvu za kiume za mpenzi wake lilitokana na nini.

“Baada ya Jini Balkis kuwachanganya, wazo la kutafuta ufumbuzi wa tatizo lenu lilifutika. Hali ile mwenzako aliamini huenda itaisha kutokana wewe kumuhakikishia tatizo lake linaweza kwisha kama lako bila kwenda popote. Naye aliamini na kumpa nafasi Jini Balkis kufanya mapenzi na mpenzi wake usingizini hadi kufikia hatua ya kutokuwa na hamu naye.

Siri ya Jini Balkis imewekwa hadharani, je, ufumbuzi utapatikana au ndiyo kumwagia mafuta kwenye moto?
 
 
 
 
 
JINI WA DARAJA LA SALENDA......EP.10.


ILIPOISHIA;
“Nawe ulipakwa mafuta yale ambayo hutumia majini wa kike, kujipaka sehemu za siri ambayo huongeza raha ya mapenzi kiasi cha kumfanya mwanaume asikuchoke na yeye kusikia raha ya mapenzi. Hata wewe hukuchoka na kusikia raha muda wote wa kufanya mapenzi na ulipoamka hukusikia uchovu wa mwili. Kwa kutumia mafuta yale unaweza kufanya mapenzi kila siku bila kuchoka.”
“Mmh! Kumbe.”

“Wakati wewe unakula raha ndiyo siku hiyo shoga yako yalimtokea kama yaliyokutokea siku za nyuma za mumeo kupoteza nguvu za kiume. Shogayo alikuja kazini akiamini ungeungana naye kwenye tatizo lake, lakini ilikuwa kinyume kitu kilichomchanganya mwenzako na kuwa njia panda tatizo la nguvu za kiume za mpenzi wake lilitokana na nini.

“Baada ya jini Balkis kuwachanganya wazo la kutafuta ufumbuzi wa tatizo lenu lilifutika. Hali ile mwenzako aliamini huenda itaisha kutokana wewe kumhakikishia huenda tatizo lake likaisha kama lako bila kwenda popote. Naye aliamini na kumpa nafasi jini Balkis kufanya mapenzi na mpenziwe usingizini kufikia hatua ya kutokuwa na hamu naye. SASA ENDELEA...

“Baada ya kuweza kukuchanganyeni akili, penzi mlilofanya na mumeo lilirudisha mapenzi yaliyoanza kutoweka. Kitu kile kilimuudhi sana jini Balkis na kuamua kukukomoa. Najua alichokufanya nikikueleza utaogopa lakini kwa vile umetaka mwenyewe sina budi kukueleza,” kauli ya mganga ilinitisha lakini kwa vile maji nilikwisha yavulia nguo nilikuwa sina budi kuyaoga. Basi mganga akaendelea.

“Usiku mlipokuwa mkifanya mapenzi bila kuzima taa jini Balkis alishindwa kufanya kitu chochote, kosa kubwa mlilofanya japo msingeweza kujua madhara yake. Nina imani mapenzi uliyofanya wakati wa giza na mwanga kuna mabadiliko yalitokea ulipofanya mapenzi?”
“Ndiyo.”

“Mlipokuwa mkifanya mapenzi gizani ulihisi maumbile ya mumeo kuwa makubwa na kusababisha uumie sana badala ya raha ikawa maumivu.”
“Ni kweli kabisa.”

“Basi wakati mlipokuwa mkifanya mapenzi gizani, mumeo aliondolewa juu yako na jini Balkis aliingiza mguu wake uliokuwa na kwato kama mbuzi na kuanza kukusukumia ndani.”
Kauli ile ilinifanya nisijikie vibaya mpaka tumbo likaanza kunikata chini ya kitovu, nikiwa navuja jasho la hofu. Mganga aliendelea kunieleza maneno niliyohisi yananikata maini.

“Basi ulijikuta ukivumilia huku ukiumia, ilifikia hatua kutotamani tena kufanya mapenzi na mumeo kwa kuamini maumbile yake yameongezeka ukubwa. Lakini ulipowasha taa ulishangaa kuyaona ya kawaida uliyoyazoea, kweli si kweli?”

“Kweli,” nilijibu huku nikizidi kumuogopa mganga kuwa na uwezo wa ajabu kuyajua mambo ambayo hakuyaona lakini utafikiri alikuwepo.
“Ajabu hukumwambia mumeo, kwa nini?”
“Hata sijui,” nilimjibu.

“Baada ya kuamua kutofanya mapenzi na mumeo kuogopa kuumizwa badala ya kupewa raha, uliamua kutafuta visingizio ili usikutane naye kimwili, uongo kweli?”
“Kweli.”
“Jana kuna kitu cha ajabu kimekutokea ndiyo sababu ya kumpigia simu Bi mkubwa wako?”

“Ni kweli.”
“Basi, baada ya kuona hufanyi tena mapenzi na mumeo, jana ulipolala uliota ndoto kuna mtu anakuingiza mkono sehemu zako za siri na kuanza kukukoroga kama anavuta kitu toka sehemu zako cha siri na ulipoamka ulijikuta ukitoka damu ambazo uliamini ni za hedhi japo ulishangaa kutokwa na damu ya hedhi mara mbili kwa mwezi kitu ambacho hakikuwahi kukutokea maishani mwako.”
“Ni kweli.”

“Unajua madhara yake?”
“Hapana!.”
“Naomba uwe na moyo mgumu kwa vile alichokifanya kwa tiba ya kubabaisha hutapona milele.”
“Mungu wangu,” kauli ilitushtua mimi na mama na kujiuliza ni ugonjwa gani tena huo Yaillah.

“Baba ni ugonjwa gani tena huo?” Ilibidi mama aulize baada ya mimi kuwa katika wakati mgumu nilishika mikono kifuani, nilimuomba Mungu aniepushe na balaa linalotaka kunikumba.

“Jina Balkis alijiulaumu kwa kuamini alifanya kosa ambalo aliliona limempotezea mapenzi ya mumeo kwake,” mganga alimjibu mama.
“Mapenzi yapi hayo?” Mama aliendelea kuuliza.

“Kosa kubwa alilofanya ni kumpaka mafuta ya kuongeza ladha ya mapenzi mwanao, kumbuka maumbile ya jini na mwanadamu yanatofautiana, kwa vile yako ya kibinadamu baada ya kukupaka ilizidi raha mara dufu na thamani yake kwa mumeo ilishuka. Alichokifanya kilikuwa kukutoa kizazi kitu ambacho ndicho kitakacho vunja ndoa yenu. Katika ndoto ulichokiota ndicho kilichotendeka usiku wa jana. Jini Balkis alikutoa kizazi na sasa hivi huwezi kuzaa tena maishani mwako.”

“Mungu wangu,” kauli ya mganga ilinikata maini.
“Sasa baba utatusaidia vipi?” Mama bado alikuwa na ujasiri kutaka kujua nini hatima ya ukatiri wa jini Balkis kwangu.
“Mmh! Ndiyo maana nikasema ipo kazi tena kazi kubwa sana si ya kitoto na tukifanya mchezo tutapotea wote.”

“Jamani, tupotee kivipi?”
“Vita yake ni kubwa sana, kumdhibiti naweza lakini kama nitakufanyia kinga ya kukufunga huwezi kupona tena. Na kosa lolote linaweza kuhatarisha maisha yetu. Hawezi kukubali kuona anazuiwa kutimiza dhamira yake, kwa kutumia nguvu zake anaweza kututeketeza wote.”

“Unataka kutuambia kuna uwezekano wa kupona?”
“Upo, lakini ndiyo mzame sana.”
“Baba wewe huwezi?” Mama aliuliza tena kwa vile mimi nilikuwa nimechanganyikiwa kwa niliyoyasikia.

“Uongo mbaya, mimi siwezi kukirudisha kizazi chake, si yeye ni wanawake wengi wametolewa na yote kaenda kuiweka chini ya bahari kwenye mwamba wa maji yaliyotulia pia hayafikiwi na kitu chochote kitakachoweza kugusa kizazi kile. Kama utaenda hospitalini wanawake wengi wanasumbuliwa na maradhi ya tumbo na wengi maradhi yao kwa tiba ya kisasa hayaonekani lakini siri ni kwamba wengi wao wameondolewa kizazi na kingine sasa hivi matatizo ya nguvu za kiume yamekuwa mengi ambayo yameweka migogolo lakini mabwana hao wakifanya mapenzi ndotoni na mwanamke mzuri hujikuta hawana hamu na wake zao.”

“Ni kwa sababu gani?” Mama aliuliza.
“Hakuna sababu nyingine ni ya huyo huyo jini Balkis ambaye amekuja duniani kwa sababu ya kuharibu ndoa za watu pia kupata tiba ya tatizo lake la uzazi. Tatizo hili litakwisha akiisha maliza kazi yake ya kupata vizazi mia, ambao walipata bahati ya kutokutana naye. Lakini wengine wote ambao hawatapata tiba mapema ndiyo watakuwa tasa milele.”

Siri nzito za jini Balkis zinazidi kufunguka, nini hatma ya yote je kuna tiba sahihi ya tatizo hilo? Kuyajua yote hayo tukutane EPISODE 11. KESHOOO........
JINI LA DARAJA LA SALENDA.......EP.11


ILIPOISHIA:
Eneo hilo halifikiwi na kitu chochote kinachoweza kugusa kizazi kile. Kama utaenda mahospitalini wanawake wengi wanasumbuliwa na maradhi ya tumbo. Wengi maradhi yao hayaonekani kwa vipimo vya kisasa lakini siri ni kwamba wengi wao wameondolewa vizazi.

Kingine sasa hivi matatizo ya nguvu za kiume yamekuwa mengi ambayo yamesababisha migogoro mikubwa. Wanaume hao wakifanya mapenzi ndotoni na mwanamke mzuri hujikuta hawana hamu na wake zao.”
“Ni kwa sababu gani?” Mama aliuliza.

“Hakuna sababu nyingine zaidi ya huyo huyo jini Balkis ambaye amekuja duniani kwa sababu ya kuharibu ndoa za watu pia kutafuta tiba ya tatizo lake la uzazi. Tatizo hili litakwisha akishamaliza kazi yake ya kupata vizazi mia. Watakaokuwa na bahati ya kutokutana naye watasalimika. Lakini wengine wote ambao hawatapata tiba mapema ndiyo watakuwa matasa milele.” SASA ENDELEA...

“Unafikiri ni mganga gani anaweza kutusaidia?” Nilimuuliza nikiwa nimekata tamaa.

“Mmh! Nendeni Bagamoyo kwa mzee mmoja maarufu sana maeneo ya Mlingotini, anaitwa Ustaadh Sudi Makata.”
“Una uhakika?”

“Japo sina uhakika kwa asilimia mia, lakini yule bwana namwamini sana.”
“Tutamjuaje?”
“Mkifika pale Bagamoyo maeneo ya Mlingotini muulizeni mzee Njiwa Manga.”

“Ni tofauti na ustaadhi Makata?”
“Hapana ndiye huyo huyo Makata, jina la Njiwa Manga kapewa na watoto aliokuwa akiwatuma wamkamatie njiwa manga kwa ajili ya kazi zake za majini. Kila mtoto aliyetumwa akimuona alimwita babu wa njiwa manga. Basi ikawa njiwa manga, njiwa manga mpaka leo.”
“Mmh! Tutajitahidi twende haraka.”

“Wala msiwe na haraka, jipangeni kwani tatizo limekwishatokea,” mganga alitutuliza.
“Sawa tutafanya hivyo.”

“Ila leo nitakupa dawa ya kuoga na kufukiza ndani mwako, lakini hapa naona itakuwa vigumu kwa vile mumeo haamini ushirikina. Kwa hiyo dawa ya kufukiza iache ila utaoga hii ambayo itakusaidia kumfukuza jini Balkis asikusogelee. Pia kuna kitu nilisahau kuwaeleza, leo wakati mnarudi nyumbani kutoka ofisini, mlipofika daraja la Salenda mlimuona mwanamke mmoja mrembo sana akiwa amesimama pembeni ya barabara chini ya mti?”
“Ndiyo.”

“Baada ya hapo gari lilizima ghafla?”
“Ndiyo.”
“Yule mwanamke mlimuona akibadilika mavazi?”
“Ndiyo.”
“Basi yule ndiye jini Balkis, ni mwanamke mzuri sana ambaye hakuna mwanaume yoyote anayemtaka akamkataa. Lakini ana roho mbaya, kwa sababu ana matatizo ya uzazi, dawa aliyoelezwa ni kutafuta vizazi vya wanawake mia moja ili atengenezewe dawa ya kupata mtoto.”

“Mungu wangu, kama ni hivyo unafikiri nitaweza kupona kweli?” Niliuliza kwa sauti ya kukata tamaa.
“Ukiwahi utapona! Mpaka sasa inaonesha ana vizazi ishirini na mbili, bado vingi na havipati kwa urahisi namna hiyo.”
“Mbona mzuri sana, jini gani anavaa nguo kama binadamu, si huwa nasikia wana mabawa?”

“Wenye mbawa si majini bali malaika, wao ni kama binadamu kabisa, wanaishi maisha kama watu ila wamepewa uwezo wa kujibadili kuwa katika umbile lolote watakalo, pia wana nguvu za ajabu walizobarikiwa na Mungu za kuonekana wanapopenda wao.”
“Kumbe!”

“Alifanya vile ili mmuone, baada ya hapo aliondoka na ninyi gari lenu liliweza kuondoka, kitu ambacho kiliwahi kumtokea shoga yako siku aliyohudhuria sherehe ya kuagwa jini Balkis kuja duniani rasmi. Mlipofika nyumbani kwako kuna kitu kimoja kilitokea ambacho shoga yako ilifikia hatua ya kukufikiria vibaya na kuamini huenda na wewe ni jini.”

“Mungu wangu, kitu gani hicho?”
“Alipoingia ndani taswira ya sura ya jini Balkis ilitanda kwenye uso wa mama yako, kitu kilichomshtua sana. Baadaye alijiondoa na bi mkubwa kuwa katika hali yake ya kawaida. Shoga yako aliondoka akiwa hakuamini kabisa. Kama unabisha ukirudi nyumbani muulize kaona nini.”

Basi baada ya maelezo yale tulirudi, huwezi kuamini kidogo gari linishinde kuendesha kutokana na mshtuko nilioupata. Lakini mama alinipa moyo kwa kuniambia ili nipate ukweli wa kile nilichoambiwa na mganga lazima niende kwa waganga zaidi ya mmoja. Lakini nilimweleza mama mbona yote aliyoyasema yana ukweli kwa asilimia mia?

Lakini mama alinieleza inawezekana ni kweli kwa asilimia kumi, mengine tusiyoyajua huwa ni uongo wa waganga ili kujipatia pesa. Nilimueleza mbona hakutaka pesa zaidi ya kutueleza twende kwa mganga mwenye uwezo zaidi yake.

Mama alinikata maini kwa kunieleza kuwa waganga wana tabia ya kutafutiana wagonjwa na kugawana pesa kwa kuufanya ugonjwa uonekane mkubwa usioweza kutibiwa. Tukienda kwa mganga mwenzake tutaambiwa pesa nyingi ambazo hatutaweza kukataa.

“Kwa hiyo mama hata kutolewa kizazi ni uongo?” Nilimuuliza.
“Uongo, nilishindwa kumkatalia angeona namuingilia kwenye kazi yake.”

“Kwa hiyo mama nisiwe na wasiwasi?”
“Ondoa wasiwasi, kitu kama hicho hakipo.”
Basi shoga niliporudi kidogo moyo ulitulia japo maelezo yote kila nilipoyafikiria mwili ulisisimka. Niliporudi hata bila kupumzika nikakupigia simu. Basi shoga habari ndiyo hiyo tumekamatwa na jini sijui Balkis,” Sharifa alimueleza Suzy aliyekuwa ametulia kama sanamu asiamini alichokisikia toka kwa shoga yake.

“Sharifa acha kuligeuza jina lake si umesema anaitwa Balkis.”
“Kweli, Balkis.”
“Mmh! Mbona kama...”
“Kama nini?”

“Sijaelewa basi inaonekana hata mimi ana mengi juu yangu, kuna umuhimu kesho kunipeleka na mimi,” Suzy alimweleza shoga yake huku wasiwasi ukiongezeka moyoni mwake kwa kuamini mpenzi wake anaweza kumuacha kwa penzi la ndotoni na jini Balkis linalotumia dawa ya kuongeza ladha ya mapenzi na yeye kuonekana si mali kitu.

“Sawa tutakwenda.”
Waliagana kwa Suzana kurudi nyumbani kwake kutafakari aliyoelezwa na Sharifa, moyoni alikuwa na mambo mawili; kukubali na kukataa. Akili yake ilikuwa kwenye kukataa na kuamini hakuna vitu kama vile.
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA.......EP.12.Basi shoga niliporudi kidogo moyo ulitulia japo maelezo yote kila nilipoyafikiria mwili ulisisimka. Niliporudi hata bila kupumzika nikakupigia simu. Basi shoga habari ndiyo hiyo tumekamatwa na jini sijui Bakils,” Sharifa alimueleza Suzy aliyekuwa ametulia kama sanamu asiamini alichokisikia toka kwa shoga yake.

“Sharifa acha kuligeuza jina lake si umesema anaitwa Balkis.”
“Kweli, Balkis.”
“Mmh! Mbona kama...”
“Kama nini?”

“Sijaelewa basi inaonekana hata mimi ana yangu mengi juu yangu, kuna muhimu kesho kunipeleka na mimi.” Suzy alimueleza shoga yake huku wasiwasi ukiongezeka moyoni mwake kwa kuamini mpenzi wake anaweza kumuacha kwa penzi la ndotoni na jini Balkis alinalotumia dawa ya kuongeza ladha ya mapenzi na yeye kuonekana si mali kitu.

“Sawa tutakwenda.”
Waliagana kwa Suzana kurudi nyumbani kwake kutafakari aliyoelezwa na Sharifa, moyo alikuwa na mambo mawili kukubali na kukataa. Akili yake ilikuwa kwenye kukataa na kuamini hakuna vitu kama vile.
sasa endelea...

Tatizo la Brighton kukosa nguvu za kiume lilimnyima raha na kuamua kwenda hospitali kutafuta ufumbuzi wa tatizo ambalo hata yeye hakuelewa limetokana na nini. Alikwenda hadi katika hospitali ya TMJ kwa rafiki yake, baada ya kumuelezea tatizo lake daktari alitaka kumpima ili ajue tatizo ni nini.

Brighton aliingizwa kwenye chumba maalumu na kuvua nguo zote na kubakia na nguo ya ndani, kisha alielelezwa apande kwenye kitanda nilichokuwa mule ndani na kujilaza kusubiri kufanyiwa uchunguzi. Baada ya daktari kuingia chumbani na boksi la gloves kwa ajili ya kumfanyia uchunguzi wa awali. Alichukua gloves ili aanze kufanya uchunguzi hata kabla hajamgusa sauti ilisikika toka nje.
ilimwita:

“Dokta kuna mgonjwa yupo serious sana.”
“Sorry Mr Brington, nakuja mara moja,” daktari alisema huku akigeuka na akitoka chumbani kumuwahi mgonjwa.

“Hakuna tatizo,” Brighton alijibu akiwa bado amejilaza kitandani.
Baada ya muda mchache alishangaa kumuona muuguzi wa kike akiingia chumbani mule bila hodi. Brighton alishtuka kumuona muuguzi wa kike mwenye asili ya kiarabu akiingia bila hodi wakati yeye amelala kitandani na nguo ya ndani tu.

“Wee vipi?” Brighton alishtuka na kutaka kuziwahi nguo zake.
Lakini muuguzi alikuwa ameishawahi kuingia na kumshika kifuani kumrudisha kitandani.
“Brighton hebu tulia.”
Kauli ile ilimshtua Brighton na kujiuliza yule muuguzi amejuaje jina lake, lakini bado alitaka kuamka ili achukue nguo zake.

“Brighton mbona unakuwa si muelewa, nimetumwa nije nikusaidie tatizo lako.”
Kauli ilimshangaza sana Brighton na kuamua kutulia, lakini hakupenda mwanamke yule aliyeonekana ni muuguzi kumchunguza matatizo yake. Baada ya kutulia yule muuguzi ambaye alikuwa mrembo kupindukia huku akinukia manukato mazuri sana ambayo hakuwahi kuiyasikia alisema:

“Sikiliza Brighton, tatizo lako si la dawa za kizungu, si lilitokea wakati ukifanya mapenzi na mpenzio?”
“Ndiyo,” Brighton alikubali huku akijiuliza taarifa zile nani kamwambia.
“Basi nitakupa dawa ya kupaka, wala usikubali dawa za kizungu italala moja kwa moja.”

“Hiyo ni dawa gani?”
“Dawa ya asili ya mafuta mazuri,” Alisema huku akitoa kichupa kidogo kwenye matiti na kujipaka mkononi, bila kuvaa gloves alitelemsha nguo ya ndani kidogo na kuanza kumchua sehemu za siri. Ilikuwa ajabu sehemu zake zilisimama na kumfanya Brighton azidi kushangaa.

“Sasa hii dawa nitakuachia, kwa vile muda huu natoka, tutaonana siku nyingine. Ila hapa hospital sitakuwepo naacha kazi.”
“Kwa nini mrembo?”

“Nimeamua tu.”
“Nikitaka kukuona?”
“Si rahisi, la muhimu umepona kampe raha wifi?”
“Umeolewa?”
“Ukitaka mazungumzo mengi utanikuta nje, sasa hivi vaa nguo zako akija daktari mwambie umekwishapona na usikubali kumjibu zaidi ya kuondoka.”

Baada ya kusema vile yule muuguzi mrembo alitoka na kumuacha Brington akivaa nguo. Akiwa anamaliza kuvaa viatu daktari aliingia na kumkuta anataka kuondoka.

“Vipi best, mbona unataka kuondoka, samahani nimechelewa hata mgonjwa mwenyewe nimemuona?”
“Una maana gani?”
“Hata hao wauguzi nawaelewa wanasema alikuja dada mmoja wa Kiarabu, alipofika katikati ya korido alidondoka na kuanza kutoa povu, ndipo waliponifuta ili nikampe msaada wa haraka. Lakini ajabu mgonjwa mwenyewe sikumkuta.”

“Sasa kaenda wapi?”
“Hata wanajua.”
“Labda kapata nafuu kaondoka.”
“Si rahisi kwa hali aliyokuwa nayo si rahisi kuondoka.”

“Mmh! Sasa atakuwa amekwenda wapi?”
“Hata najua, hebu tuendelee na matibabu yetu.”
“Nimepona,” Brighton alijibu kwa mkato.

“Mr Brighton najua nimekuchelewesha, samahani sana hebu rudi nikufanyie uchunguzi.”
“Mr Paul nipo sawa.”
“Si kweli, najua umekasirika.”

“Sijakasirika Mr nipo sawa, nimeshangaa kujiona nipo sawa nikiwa nimelala kitandani, kama itarudia nitakueleza.”
“Heri tungejua tatizo ili lisije likarudia tena.”
“Halitatokea tena.”

“Si kweli najua umekasirika.”
“Niamini Mr Paul wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu, kwani umetumia muda gani wa kunifanya nikasirike. Na kwa nini nikasirike wakati ulikimbilia kuokoa maisha ya mtu.”
“Kama hujakasirika sawa.”

Brighton aliagana na Dokta Paulo na kutoka nje ya hospitali, alipofika nje aliingia kwenye gari lake na kuamua kurudi nyumbani. Ili kuiamini dawa yake kabla ya kuondoka alimpigia simu mpenzi wake Suzana.

“Mpenzi naomba leo uje nyumbani nina imani tiba ya tatizo langu imepatikana.”
“Tiba ya nini?”
“Kwani nasumbuliwa na nini?”
“Lile tatizo la kitandani?”

Ni kweli Brighton amepona? Yule aliyempa dawa ni muuguzi kweli?
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.13


Hilo hilo.”
“Brighton hebu acha utani.”
”Kweli mpenzi wangu, huwezi kuamini ugonjwa ulivyopona.”
“Au ulikwenda kwa Babu?”

“Walaa, tukikutana nitakueleza maajabu yaliyonitokea, ilikuwa kama bahati ya mtende.”
“Basi leo mtoto hatumwi dukani nina usongo na wewe ile mbaya.”

Baada ya Suzana kukata simu alijikuta akizidi kuchanganyikiwa na maelezo ya mganga kuhusu mpenzi wake na taarifa za kupona kwake. Alijikuta akianza kuamini maneno ya mama Sharifa kuwa waganga wengi ni waongo, kazi yao kuwatisha wagonjwa ili wapewe pesa nyingi.

Alijikuta akifuta wazo la kwenda kwa mganga ili na yeye akaangaliziwe mambo yake. Aliona kuna uongo mkubwa kati ya maneno ya mganga na mpenzi wake, alipoambiwa kuwa mpenzi wake hamhitaji tena kwa vile anafanya mapenzi na jini Balkis kwenye ndoto.

Ujumbe wa mpenzi wake kumhitaji kimapenzi ulidhihirisha jinsi mganga alivyowadanganya. Aliona kwenda kwa mganga ni kupoteza muda na kumpa pesa za bure. Muda ule ule alimpigia simu Sharifa kuahirisha safari ya kwenda kwa mganga.

“Shoga, kesho safari ya kwa mganga imekufa.”
“Vipi shoga, mbona hivyo?”
“Aah! Basi tu, tutakwenda siku nyingine.”
“Mmh! Sawa.”

Wakati Suzana akiahirisha kwenda kwa mganga kuangalia matatizo yake, Brighton baada ya kutoka ndani ya hospitali alipepesa macho labda atamuona muuguzi aliyemtibu. Lakini hakumuona, alitaka kwenda kumuuliza ndani ya hospitali, lakini alikumbuka kauli ya yule muuguzi ambaye hata jina lake hakulijua, alimkataza asimuulize mtu yeyote habari zake.

Aliingia ndani ya gari yake na kuondoka huku akiwa na shauku ya kumuona yule dada mrembo mwenye roho ya huruma. Mpaka anaondoka eneo la hospitali hakumuona. Alijikuta akiwa na shauku ya kumuona yule mrembo ambaye alisema mengi wangezungumza nje ya hospitali.

Alipokaribia maeneo ya Makumbusho alishtuka kumuona yule dada akiwa katika vazi refu zuri lenye mvuto, lililoongeza uzuri wake akilipungia mkono gari lake. Alilisimamisha mbele yake kidogo, yule mwanamke mrembo alisogea hadi kwenye gari na kufungua kisha aliingia ndani na kukaa kwenye siti.

Baada ya kukaa na kufunga mlango wa gari, Brighton aliondoa gari bila kujua mrembo anaelekea wapi. Baada ya mwendo mfupi aliitwa jina lake.
“Brighton.”
“Naam.”

“Za muda?”
“Nzuri.”
“Unaelekea wapi?”
“Nilikuwa narudi nyumbani, lakini nitakusikiliza wewe unakwenda wapi.”
“Umeoa?”

“Bado.”
“Na Suzana?”
“Suzana! Umemjuaje?”
“Jibu swali,” yule mwanamke alisema huku akimuangalia jicho lililolegea.
“Ni mchumba wangu, si mke wangu.”
“Ina maana ukipata mtu mwingine utakuwa tayari kumuoa na kumuacha Suzy?”
“Itategemea.”

“Itategemea nini, wakati tayari Suzana ni mchumba wako?”
“Itategemea uwezo wake katika ufahamu wa maisha, Suzana mchumba wangu pamoja na kunipenda, tatizo lake anapenda sana starehe. Kwangu namuona kama si mwanamke anayefaa kuwa mke wangu.”

“Kwa mfano mimi nikitaka unioe itakuwaje?”
“Mmh! Nitakuweza?”
“Kivipi?”

“Unaonekana unatoka katika familia ya watu wenye uwezo.”
“Familia yangu ingekuwa na uwezo ningefanya kazi pale hospitali?”
“Hata mimi nashangaa.”

“Niambie kweli kama utakuwa tayari kunioa niwe mkeo, kila kitu nitashughulikia mimi, nakuahidi kuyabadili maisha yako.”
“Mmh! Nipe muda.”
“Brighton sina muda mwingine zaidi ya huu.”

“Nimekubali.”
“Kama umekubali naomba leo nikalale kwako.”
“Mmh! Kwa nini tusifanye siku nyingine?”
“Au kwa vile umemwita Suzana?”
“Umejuaje?” Brighton alishtuka tena.

“Brighton, nimekueleza sitaki maswali ninapokuuliza swali nataka jibu.”
“Ni kweli, leo nilimualika aje tulale pamoja.”
“Tatizo nini?”
“Sasa itakuwaje wewe uwepo na yeye aje?”

“Wee mwache aje alale, mimi nitalala chumba kingine.”
“Si atakuona?”
“Hawezi kuniona, labda umwambie wewe.”
“Kwa hiyo utaingia nyumbani saa ngapi?”

“Muda wowote, usiwe na wasiwasi.”
Brighton alielekea nyumbani kwake akiwa na wasiwasi wa kugonganisha wanawake.

Brighton anakutana na mtihani mzito wa kuvunja uchumba wake na Suzy, Suzy atakubali kirahisi kumpoteza mpenzi wake?
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.14.


****
Walipofika nyumbani yule mwanamke aligundua wasiwasi wa Brighton, alimgeukia na kumuuliza:
“Mbona una wasiwasi?”
“Bado siamini kama Suzana akija hawezi kukuona, kwa nini nisimzuie asije?”
“Hapana Brighton, kwa vile umemuita, mwache aje tu.”
“Anaweza kuja chumba utachokuwemo itakuwaje?”
“Naomba uwe mwelewa, wee mwache aje na mimi hawezi kuniona.”

“Mmh! Sawa.”
Brighton alikubali kwa shingo upande, lakini moyoni alikuwa na kiburi cha ajabu, kama Suzana atamuona mgeni wake, atakuwa tayari kwa atakachokiamua.
“Brighton bafu lipo wapi?” Mgeni aliuliza.
“Lipo ndani ya chumba cha kulala.”
“Naomba nikaoge.”

“Ruksa.”
Mwanamke mrembo alielekea chumbani ili aende bafuni kuoga, kila hatua aliyopiga kuelekea chumbani ilimchanganya sana Brighton, alijiuliza imekuwaje mwanamke mzuri kama yule kumpenda yeye kwa haraka. Katika maisha yake aliwahi kuona wanawake wazuri lakini yule alikuwa ni zaidi.
Baada ya mgeni kuingia chumbani, wazo la haraka kwa Brighton lilikuwa kumpigia simu Suzana kumzuia asije. Ili mgeni asisikie alitoka nje lakini ilikuwa ajabu simu ya Suzana haikupatikana, kitu kilichozidi kumweka kwenye wakati mgumu wa kuweza kumzuia asifike nyumbani kwake.

Akiwa bado anatafakari jinsi ya kutatua tatizo lile, sauti ndani ilimwita.
“Mpenzi upo wapi?”
“Nipo nje.”
“Njoo basi.”

Brighton aliingia ndani huku akijitahidi kuficha hofu yake, picha aliyoiona mbele yake ilimfanya afikiche macho kujiuliza anachokiona ni kweli au yupo ndotoni. Mbele yake alikuwa amesimama mwanamke mrembo ajabu akiwa amejifunga mtandio mwepesi sehemu ya makalio na kifuani. Sehemu nyingine ya mwili wake ilikuwa wazi. Lilikuwa umbile lenye kumtia msisimko mwanaume yeyote rijali. Alijikuta akipigwa na butwaa kama ameona meli ikitembea barabarani.
“Mbona unanishangaa?” Mgeni alimuuliza.
“Lazima niseme ukweli, wewe ni mwanamke mzuri sana.”

“Asante, hata wewe ni mwanaume mzuri sana.”
“Nashukuru.”
“Brighton mbona unajiweka roho juu, hebu mwache Suzana aje.”
“Umejuaje?” Brighton alishtuka kusikia vile.
“Unaniuliza nimejuaje, ina maana ninachosema ulifanya siri?”
“Hapana, sipendi litokee tatizo lolote, unaweza kuniona sina maana.”
“Aliyekueleza umruhusu Suzana aje nani?”

“Wewe.”
“Sasa tatizo nini, nimekueleza mwache aje kwani chumba nitakachokuwa hawezi kuingia.”
“Wewe unajiamini nini?”
“Utajua baadaye sasa hivi ni haraka, mimi si mkeo mtarajiwa?”
“Ndiyo.”
“Kipi kimekufanya ukubali niwe mkeo?”

“Hata sielewi lakini kitendo chako cha kujitolea kunitibu bila gharama ugonjwa ambao ulinisumbua sana, imeonesha jinsi gani ulivyo muhimu sana kwangu.”
“Kingine?”
“Nimetokea kukupenda na kila dakika mapenzi yangu kwako yanazidi kuongezeka.”
“Nashukuru kusikia hivyo, nina imani kuna vitu umehisi kuvikuta kwenye mwili wangu, basi nakuhakikishia kukufurahisha katika maisha yangu yote.”
“Nitashukuru.”
“Brighton nipo chumbani, Suzana amekaribia kufika.”

“Umejuaje?”
“Brighton mbona kila ninachokizungumza kwako kinakushangaza?”
“Unanishangaza kuzungumza vitu ambavyo kwa mtu yeyote ni vigumu kuvijua.”
“Brighton najua una hamu kunifahamu kwa undani, hata jina langu hulijui?”
“Ni kweli, hebu niambie jina lako unaitwa nani?”
“Sasa mbona mpaka nimekueleza mimi au hukupenda kulijua jina langu?”
“Huwezi kuamini, jinsi nilivyopagawa kukupata, hata kuuliza jina niliona kazi, najiona kiumbe mwenye bahati ya mtende.”

“ Naitwa Balkis Bakilas, naomba nikuache Suzana anaingia sasa hivi, nakusihi usioneshe wasiwasi wowote.”
“Umejuaje?’
“Kuwa mwelewa,” baada ya kusema vile aligeuka na kuelekea chumba cha wageni.
Kila hatua aliyopiga kuelekea chumbani huku akimuachia Brighton sehemu za nyuma ambazo ziliumbwa kwa mpangilio. Alijikuta akimeza mate huku akimsindikiza kwa macho. Hata alivyoingia mpenzi wake Suzana hakumuona, alishtuka alipoulizwa swali.

“Brighton mbona umeshangalia huko hadi naingia wewe huna habari, kuna nini?”
Suzana aliuliza huku macho yake yakiangalia alipoelekea Balkis.
“Aa..aah,” Brighton alibabaika kujibu.
“Brighton kuna nini?”
“Ha..ha..kuna kitu.”

“Au ulifikiri siwezi kuja?” Suzana alisema huku akimbusu na kukaa pembeni yake.
“Wala.”
“Mbona kama haupo sawa?”
“Nipo sawa.”
“Nakuja.”

Suzana alisema huku akinyanyuka na kuelekea chumba alichoingia Balkis, Brighton alijikuta akipatwa na mshtuko, wasiwasi wake ulikuwa huenda Suzana alimuona akiingia hivyo alikwenda kumfumania. Alitaka kumkataza lakini mdomo ulikuwa mzito.

Ni kweli Suzana kamuona Balkis? Na kama kamuona nini kitatokea?
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.15.


Suzana alikwenda hadi mlango wa chumba cha wageni na kuingia ndani, Brighton mapigo ya moyo yalikuwa makubwa. Alijisogeza hadi kwenye kochi na kujilaza akiwa ameshikilia mkono mmoja kifuani kuizuia presha kutokana na vurugu itakayotokea chumbani.

Siku zote Suzana alimhakikishia Brighton kuwa siku atakayomkuta na mwanamke ndiyo siku atakielewa kichaa chake. Akili nyingine ilimtuma awahi chumbani kabla Suzana hajafanya lolote. Alinyanyuka alipokuwa amejilaza na kwenda chumba cha wageni.

Alipofika alifungua mlango na kuingia ndani, Suzana aliyekuwa akianua nguo yake ya ndani, alishtuka na kumuuliza:
“Vipi mbona umeingia kama unafukuzwa?”

“Aa..aa..,” alijibu kwa kubabaika huku akipepesa macho chumbani kumtafuta Balkis.
“Vipi mbona unatembeza macho chumba kizima kuna nini?” Suzana alimuuliza.
“Walaa, niliweka CD yangu kwenye meza.”
“Sasa ulivyokuja hivyo, umeniona mimi mwizi?”
“Walaaa, nilikuwa najiuliza niliiweka huku au wapi?”
“Brighton, umeanza lini kuweka vitu vyako humu chumbani?”

“Suzana hii ni nyumba yangu, nina uhuru wa kuweka kitu popote.”
“Mbona leo Brighton sikuelewi?”
“Kivipi?”
“Umekuwa mtu mwenye mawazo mengi pia mwenye hasira tofauti na siku zote.”
“Nipo sawa.”
Brighton bado hakuamini kama kweli chumbani hakuna mtu, wasiwasi wake huenda amekwenda choo cha wote kilichokuwa upande wa mwisho wa nyumba ile. Bila kuongeza neno alitoka na kwenda moja kwa moja msalani ili kumuwahi kama Balkis yuko huko asitoke.

Alipofika msalani hakukuta kitu, alijikuta akibaki akilishangaa bafu huku akijiuliza Balkis amekwenda wapi, ikiwa hakuna mlango mwingine wa kutokea. Akiwa bado ameshangaa Suzana alisimama tena nyuma yake na kumuuliza:
“Brighton upo sawa?”
“Nipo sawa.”

“Hapana, kuna kitu kinakusumbua hutaki kuniambia.”
“Suzy, nipo sawa.”
“Hapana Brighton una tatizo unanificha, mimi nani kwako?”
“Mpenzi wangu.”
“Nani wa kumueleza shida zako?”
“Lakini Suzy mimi sina tatizo lolote,” Brighton aliendelea kujitetea japo maji yalikuwa shingoni.

“Sikubali, kuna kitu unanificha, basi mimi nipo chumbani ukimaliza matatizo yako utanikuta.”
Suzana alisema huku akielekea chumba cha kulala, baada ya kuondoka Brighton aliendelea kuelea kwenye bahari ya mawazo juu ya kitu kilichotokea muda mfupi pale alipomshuhudia Balkis akiingia chumba cha wageni na wakati huo Suzana alikuwa anaingia. Bila kupumzika, alikwenda moja kwa moja chumba cha wageni alichoingia Balkis.

Lakini cha ajabu, Balkis hakuwepo chumbani wala msalani, alijiuliza atakuwa wapi? Alijikuta akirudi tena chumba cha wageni kupata uhakika kama kweli Balkis hayumo. Chumba cha wageni hakikuwa na vitu vingi vya kuweza mtu kujificha, kitanda na tivii ndogo. Alipofungua mlango na kuingia, alishtuka kidogo akimbie alipomkuta Balkis akiwa amejilaza kitandani akiwa amepitiwa na usingizi. Kwake aliona kama maruweruwe, alifikicha macho kutaka kupata uhakika wa kile alichokiona mbele yake.

Akiwa bado kapigwa na butwaa, Balkis aligeuka na kufumbua macho, alipomuona Brighton aliachia tabasamu na kusema:
“Mpenzi mbona umeingia bila hodi?”
“Aah! Ulikuwepo?”
“Kuwepo wapi?”
“Chumbani.”
“Chumba gani?”

“Si humu ndani.”
“Ndani wapi?”
“Sijakuelewa, hebu nieleweshe vizuri, nilikuwa wapi kivipi?”
“Muda mfupi ulikuwa wapi?”
“Brighton, swali gani hilo? Nimekuaga nakuja chumbani na umekuja umenikuta, sasa unaniuliza swali gani hilo?”
“Mbona nimekuja chumbani sikukukuta?”

“Hukunikuta! Hapa unazungumza na nani?”
“Suzana alikuja huku, kwa wasiwasi wa kukuona ilibidi nije ili isitokee vurugu lakini sikukuona.”
“Sijui unamaanisha nini, hebu nenda kwa Suzana ukamuondoe wasiwasi, nimekueleza mapema acha kujitia jakamoyo.”

“Umejuaje?”
“Ukirudi nitakuambia, muwahi mchumba wako.”
Brighton alitoka kwenda chumbani kwake na kumuacha Balkis akimsindikiza kwa macho.
Ni kweli Suzana alimuona Balkis? Mbona hakuonekana mwanzo chumbani?
 
 
 
 
 
 
 
 JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.16.Brighton alijitahidi kurudi katika hali yake ya kawaida kabla ya kuingia chumbani. Alipoingia alimkuta Suzana amekaa upenuni mwa kitanda akiwa ameshika tama.
“Suzana mpenzi wangu vipi?”
“Vipi nikuulize wewe?”
“Mbona mimi nipo sawa, hebu twende tukaoge mpenzi wangu tuje tulale.”

Alimshika mkono na kumnyanyua kisha waliongozana naye bafuni, baada ya kuoga walirudi kitandani. Kwa vile Suzana alikuwa na hamu na mpenzi wake, baada ya kuikosa huduma ya kitandani kwa muda mrefu. Brighton hakujiamini kwa asilimia miamoja kukifanya alichomuitia mpenzi wake.

Lakini ilikuwa kama alivyoelezwa na Balkis kuwa dawa aliyompa inafanya kazi, Suzana aliweza kufurahia mapenzi kwa muda wote, Brighton alijikuta akijisahau kuwa Balkis naye anamhitaji, baada ya kumstarehesha mpenzi wake alipitiwa na usingizi mzito.
Ulipofika usiku wa manane Brighton alishtuka usingizini na kujikuta akifanya mapenzi na Balkis tena chumbani kwake. Baada ya penzi tamu la Balkis ambao aliamini hakuwahi kupewa chini ya jua zaidi ya ndotoni. Alipepesa macho mule chumbani labda atamuona Suzana lakini hakumuona.

Ili kupata uhakika Suzana yupo wapi alimuaga Balkis kwenda msalani, pamoja na kuwa na choo cha chumbani lakini alitoka kwenda cha watu wote. Ajabu Balkis hakumuuliza chochote, alitoka mpaka chumba cha wageni na kukikuta kitupu. Alikwenda hadi msalani pia hakumuona.
Alijiuliza Suzana atakuwa wapi au ameondoka, lakini haikuwahi kutokea Suzana aondoke usiku tena bila kuaga. Alijikuta akijiuliza bila kupata majibu kuwa yupo ndotoni au kweli, alitoka hadi nje ya nyumba lakini hakukuwa na dalili zozote za kuwepo Suzana.

Alimfuata mlinzi wa Kimasai na kumuuliza kama Suzana ametoka.
“Rafiki shemeji yako ametoka?”
“Sijaona yeye ikitoka, niliiona inaingia tu.”
“Rafiki lazima ulilala, mbona ndani hayupo?”
“Sijasinzia rafiki, shemeji haijatoka imo ndani.”
“Kweli?”

“Kweli kabisa rafiki.”
Brighton aliamini kabisa mlinzi alipitiwa usingizi wakati Suzana anatoka, akiwa bado anajiuliza ni kweli Suzana alikuja au ilikuwa ndoto. Lakini akili yake ilimweleza kuwa Suzana alikuja kweli wala haikuwa ndoto na kufanya naye mapenzi na kila mmoja alipitiwa na usingizi mzito.

Lakini aliposhtuka na kujikuta akifanya mapenzi na Balkis tena penzi tamu adhimu, bado alikuwa njia panda kujiuliza kilichotokea ni nini yupo ndotoni au ni kweli. Kwa maelezo ya mlinzi kuwa kweli alimuona anaingia lakini hakumuona anatoka ilizidi kumchanganya.

Hata kama kweli alitoka bado asingeondoka bila kuaga, na kitu kile hakikuwahi kutokea toka waanze uhusiano wao. Akiwa bado yupo njia panda kwa kile alichokuwa akikiwaza juu ya kuyeyuka kwa mpenzi wake . Sauti ya Balkis alimtoa kwenye dimbwi la mawazo.
“Brighton huku ndiko msalani?”
“Aa..aah... nilikuwa napunga upepo.”

“Imeanza lini na leo iwe ya pili?”
“Ni kawaida yangu wala si leo.”
“Kweli?”
“Kweli kabisa.”
“Kwa hiyo nikuache uendelee kupunga upepo?”
“Hapana, wacha turudi ndani.”

Brighton alirudi ndani na Balkis, walipofika kitandani bado alikuwa na mawazo, lakini hakutaka kuumia kichwa alimuuliza Balkis.
“Eti Suzana wakati anaondoka ulimuona?”
“Swali gani hilo Brighton?”
“Ooh! Basi.”

“Kwanini unaniuliza habari za mpenzi wako mimi zinanihusu mimi?” Balkis alimuuliza kwa sauti kali kidogo.
“Hapana mpenzi, inawezekana ulikuwa ninaota.”
“Kuota nini?”

“Kuwa Suzana alikuja leo.”
“Kama alikuja yupo wapi?”
“Inawezekana nilikuwa naota.”
“Kama ulikuwa unaota basi tulale,” Balkis alimkumbatia Brighton, hakuchelewa usingizi mzito ulimpitia.

****
Suzana aliposhituka usingizini hakuamini macho yake alipojikuta yupo nyumbani kwake amelala kitandani. Alirudia kutazama tena ni kweli au alikuwa akiota, akili yake ilimjulisha kuwa jana alipigiwa simu na mpenzi wake Brighton kuwa amepata dawa ya matatizo ya nguvu za kiume na alipokwenda kweli alikuwa amepona.

Alikumbuka Brighton alimpa penzi tamu na kujikuta wote wakipitiwa usingizi, lakini ilikuwa ajabu kuamka asubuhi na kujikuta amelala kitandani kwake. Alijiuliza simu aliyopigiwa alikuwa anaota au kweli, kila alipolazimisha labda ni ndoto akili ilikataa na kuamini kabisa alikwenda kwa Brighton.

Alijiuliza labda baada ya kufanya mapenzi alirudishwa nyumbani, lakini kwa upande wake kitu kama kile hakikuwahi kutokea. Kingine kilichomshangaza hata kama alirudishwa akiwa amelala hakuwa na fahamu. Alikaa kitandani kwa muda na kukumbuka anatakiwa kujiandaa kwenda kazini.
Aliamka na kwenda kujiandaa, alipofika kazini bado akili yake haikumpa alimtafuta Sharifa amueleze kilichomtokea.

Suzana na Brighton kilichowatokea watakigundua? Wakikigundua watachukua hatua gani? Balkis atatimiza dhamira yake?
 
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.17.Alipofika alimkuta ndiyo kwanza anafuta vumbi kwenye kompyuta yake, Sharifa alipomuona Suzana aligundua ana matatizo.
“Karibu shoga.”

“Asante,” alijibu huku akisogeza kiti na kuketi.
“Mbona uko hivyo?”
“Mmh! Kuna kitu kimenitokea jana sikielewi hata kidogo!”
“Kitu gani hicho?”
“Unakumbuka jana nilikupigia simu?”
“Ndiyo.”

“Nikakueleza kuwa nimeahirisha kwenda kwa mganga?”
“Ndiyo.”
“Basi, Brighton si aliniita na kunieleza kuwa amepata dawa ya tatizo lake na kukosa nguvu za kiume.”
“Ehe?”

“Baada ya kunieleza vile nikaona hakuna sababu yoyote ya kwenda kwa mganga kwa vile dawa imepatikana.”
“Ehe!”
“Basi jana saa moja usiku nikaenda kwa mpenzi wangu.”
“Lete raha dada.”
“Tumekutana kama kawaida, baada ya kuoga tulipanda kitandani, si unajua usongo niliokuwa nao.”

“Najua sana.”
“Basi shoga, kama alivyonieleza ndivyo ilivyokuwa, mtoto wa kike nikajilia raha nilizozipoteza muda mrefu.”
“Alikuwa na nguvu kama kawaida?”
“Tena ziliongezeka mara mbili.”

“Mmh! Makubwa, kampata mganga gani huyo?”
“Anasema alikwenda hospitali.”
“Jamani ona sasa, kumbe tunakimbilia kwa waganga tiba ipo hospitali, nilikueleza toka awali waganga wengine wanatengeneza ugonjwa, ionekane kweli tuna matatizo makubwa ili tuwape fedha nyingi.”
“Shoga bado nakuja sijafika kwenye pointi yangu.”
“Ipi tena?”

“Sababu iliyonifanya nisiingie ofisini kwangu na kuja moja kwa moja kwako.”
“Una tatizo gani?”
“Tulipomaliza kufurahishana na mpenzi wangu huku nikifurahia mafanikio makubwa baada ya kupona tatizo lake, tulipitiwa na usingizi mzito. Lakini kwa maajabu makubwa nimeamka asubuhi na kujikuta nipo kwangu!”
“Kujikuta kwako kivipi?”

“Kitandani kwangu nimelala!”
“Sasa kipi cha ajabu?”
“Ina maana hujanielewa?”
“Nimekuelewa! Yaani jana baada ya kukutana na mpenzi wako asubuhi ulipoamka ulijikuta umelala, sasa kipi cha ajabu kama ulilala usiku na asubuhi ukajikuta kitandani?”

“Hebu nielewe vizuri nisemayo, jana nilikwenda kwa Brighton kama ilivyo kawaida, ninapokwenda hulala huko huko, hata safari yangu ya kuja kazini huianzia kwake.”
“Hilo nalijua, sasa hapo tatizo nini?”
“Jamani huoni tatizo! Nilale kwa Brighton niamke kwenye kitanda nyumbani kwangu tena nikiwa peke yangu.”

“Suzana! Unayosema ni kweli au ulikuwa unaota?”
“Sharifa, yaani niote mchana na usiku? Sikukupigia simu?”
“Ulinipigia?”
“Saa ngapi?”

“Mchana”
“Sasa huko kuota gani?”
“Mmh! Basi kama ni kweli usemayo kuna namna lazima tuliangalie kwa macho mawili.”
“Yaani toka nimeamka sijielewi kabisa.”
“Umempigia simu Brighton kumuuliza?”

“Huwezi amini kila nikipiga simu yake inaonekana anazungumza.”
“Basi kuna umuhimu wa wewe kwenda kwake ili ukapate ukweli, japo mimi bado naamini baada ya kunipigia simu inawezekana kabisa ulipitiwa na usingizi na kuota ulikuwa na Brighton na asubuhi ulipoamka ukajishangaa upo kitandani kwako. Lazima utaamini kabisa umetokewa na kitu kisicho cha kawaida.”

“Sharifa hiki ninachokueleza ni kweli kabisa si cha kuota, haya ni maajabu.”
“Au ndiyo Jini Balkis?”
“Jini Balkis! Kama ni Balkis, Brighton asingeweza kufanya kazi.”
“Nimekueleza yule jini ana mambo mengi ya kukuchanganya pale unapokaribia kuujua ukweli.”
Suzana anaanza kuingia kwenye mtihani mzito wa Jini Balkis, nini hatima ya yote?
 
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.18.


“Kwa hiyo kuna umuhimu wa kwenda kwa mganga?”
“Ikiwezekana, lakini kwanza nenda kwa mwenzako ili umuulize kama kweli jana mlilala pamoja.”
“Mmh! Itabidi nifanye hivyo.”
“Asubuhi hii?”

“Sharifa siwezi kufanya kazi vizuri, akili yangu bado ipo njia panda ukweli wa kitu hiki nitaupata kwa Brighton.”
“Kazi?”
“Lazima niombe ruhusa, nimechanganyikiwa, sijui itakuwaje kama huyo jini atakuwa kanivaa na mimi?”

“Kama kukuvaa kakuvaa muda mrefu, sasa inawezekana ndiyo anajionesha kwamba na wewe upo kwenye mtandao wake.”
“Mungu wangu! Kama ni hivyo nitakuwa nimekwisha,” Suzana aliingiwa na hofu.
“Suzana acha kujikatia tamaa, hebu tafuta ukweli ili tujue tufanye nini, ikiwezekana twende leo leo, nitaomba ruhusa nikusindikize.”

“Basi wacha nikaombe ruhusa niende kwa Brighton nikapate ukweli, bila hivyo nitachanganyikiwa.”
“Haya shoga utanijulisha,” Suzana aliagana na Sharifa na kwenda kuomba ruhusa kisha alielekea nyumbani kwa Brighton.
***
Balkis akiwa amejilaza kitandani na Brighton, alimuona Suzana akielekea pale, kama kawaida yake alimueleza mpenzi wake:
“Suzana anakuja.”
“Umejuaje?”

“Nijue vipi, la muhimu jiandae kumpokea mpenzi wako.”
“Sasa nimpeleke chumba gani?”
“Mlete humu humu.”
“Wewe unatoka?”
“Niende wapi?”

“Si chumba wa wageni.”
“Mi sitoki, Suzana anakuja kukuuliza kama jana alikuja kulala hapa.”
“Umejuaje?”
“Nisikilize kwanza ndipo uliniulize maswali.”
“Mh!”

“Naomba unisikilize, ukijichanganya shauri yako.”
“Mbona unaniambia hivyo?”
“Ndiyo maana nakueleza, nisikilize kwa makini.”
“Sawa.”
“Suzana anakuja kuulizia kama kweli jana alikuja hapa, mjibu kuwa hakuja. Tumeelewana?”
“Lakini mbona mimi nafahamu jana alikuja?”

“Kama alikuja mbona asubuhi hukumuona?”
“Hata mimi nashangaa.”
“Wewe na Suzana mliota ndoto ya aina moja kuwa jana mlikuwa pamoja lakini kila mmoja alipoamka hakumuona mwenzake.”

“Balkis! Mbona unanitisha, wewe ni nani?”
“Kwani wewe unanionaje?”
“Nakuona mtu wa kawaida, lakini unayozungumza yananishangaza sana.”
“Mbona ya kawaida, ni kipawa ambacho mwanadamu hupewa na Mungu kujua yajayo.”
“Mmh! Nilikufikiria vibaya.”

“Ulinifikiria vipi?”
“Labda jini!”
“Brighton tokea lini jini akazungumza na mwanadamu?”
“Huwa nasikia majini huweza kujigeuza na kuwa wanadamu na kuishi nao.”
“Kama ningekuwa jini ungefanyaje?”
“Ningekufa kwa mshtuko.”

Mara kilipita kimya cha ghafla, kitu kilichomshangaza Brighton. Haukupita muda mlango wa chumbani uligongwa.
“Mkaribishe Suzana,” Balkis alimwambia Brighton aliyepatwa na mshtuko.
“Wapi?” Ilikuwa ajabu Balkis alizungumza kwa sauti ya juu, lakini Brighton aliuliza kwa sauti ya kunong’ona.

“Kuwa muelewa, nimekueleza mkaribishe humu ndani.”
“Ili atufumanie?”
“Ndiyo.”
“Ili iweje?”
“Utajua akiishaingia ndani.”

Sauti ya kugonga mlango iliendelea nje huku ikionekana kabisa kitendo cha kuchelewa kufunguliwa mlango kilimuudhi sana Suzana.
“Brighton kama hutaki nije kwako si uniambie kuliko kunifanyia visa?”
“Mkaribishe,” Balkis alimueleza Brighton kwa kumkaripia.
“Ingia,” alimkaribisha akiwa na wasiwasi mkubwa.

Suzana aliingia na kwenda kukaa kitandani, pembeni kabisa ya Balkis. Brighton alikuwa kama mtu aliyeshikwa na ganzi na kushindwa kuelewa kama mpenzi wake ameingia ndani. Suzana baada ya kuingia alimshangaa kwa mara nyingine.
“Brighton upo sawa?”

“Eeh.... aah.. Unasema?” Brighton alijikuta akibabaika kujibu.
“Makubwa ina maana hujaniona naingia?”
“Nimekuona.”
“Hata kunikaribisha? Kweli mapenzi yamekwisha,” Suzana alizungumza kwa sauti ya kilio.
“Suzana...,” Brighton alipotaka kusema alimtupia jicho Balkis aliyekuwa amejilaza pembeni ya Suzana huku akitabasamu.

“Brighton, una nini mpenzi wangu?”
“Si..si..sina,” majibu ya Brighton yalizidi kumshangaza Suzana.
“Kuna nini humu ndani, mbona sikuelewi? Jana nilikuja ukawa katika hali hii hii na leo tena, kuna kitu gani mpenzi wangu! Kwa nini hutaki kuniambia?”
“Brighton mkatalie kwamba jana hakuja hapa,” Balkis alimwambia kwa sauti aliyosikia Brighton peke yake.

“Brighton mbona kama haupo na mimi! Una nini mpenzi wangu?” Suzana aliporomokwa na machozi na kumfuata Brighton alipokuwa amesimama kama kapigwa na shoti ya umeme. Alianza kumpapasa huku akiendelea kumuuliza jinsi alivyoonekana mtu aliyehama kimawazo.

Je, nini kitaendelea? Brighton atamsikiliza nani kati ya Suzana na jini Balkis?
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.19.


Brighton alikuwa kama yupo ndotoni akijiuliza yanayotokea mbele ya macho yake ni kweli au ni kiini macho. Chumbani kulikuwa na watu watatu, Balkis hakujificha zaidi ya kulala kitandani, tena peupe. Hata Suzana alipoingia, pamoja na kukaa pembeni yake hakuonesha kuona kitu cha tofauti mle ndani.

Alizidi kuingiwa na wasiwasi kuwa huenda Balkis si kiumbe cha kawaida, hata sauti yake aliyompa maelezo bado ilionesha kuisikia peke yake. Kuhama kimawazo kulizidi kumnyima raha mpenzi wake ambaye naye alikuwa na yake yaliyotakiwa kupata majibu kutoka kwa Brighton.

“Brighton jana nimekuja hapa na kulala na wewe, lakini ajabu nilipoamka asubuhi nimejikuta nipo kitandani kwangu. Ni kweli jana nilikuja au nilikuwa naota?”
“Brighton, kataa! Sema hakuja?” Balkis alipaza sauti ya juu.
Lakini Brighton alijikuta mdomo ukiwa mzito kumjibu mpenzi wake huku jasho la hofu likimtoka.

“Brighton una nini mpenzi wangu, nijibu basi, si ni wewe ndiyo ulinipigia simu jana na kuniambia nije?”
“Brighton kataaa,” Balkis alizidisha sauti iliyoumiza ngoma za sikio.
“Brighton kuna nini hapo kitandani mbona unapaangalia sana, au kuna mwanamke?”
“Ha..ha..kuna..ki..”

“Brighton unafanya nini?” Balkis alipiga kelele iliyokuwa na mlio mkubwa kama radi iliyofanya ngoma za sikio za Brighton zisikie maumivu makali.
“Brighton mpenzi wangu una nini au umeshavamiwa na jini Balkis?”
“Nani?” Jina la Balkis lilimshtua.

Kauli ile ilimuudhi jini Balkis, akapuliza upepo uliompata usoni Suzana ambaye aliishiwa nguvu na kupitiwa na usingizi mzito. Brighton alimuwahi kabla hajaanguka chini na kumlaza kitandani pembeni ya Balkis.
“Suzana... Suzana,” alimwita kwa kumtikisa.

Suzana hakujibu kitu, alionekana mwenye usingizi mzito. Brighton alimuona Balkis jinsi alivyompuliza hadi kupitiwa na usingizi mzito.
“Balkis umemfanya nini Suzana?”
“Acha upumbavu,” Balkis alimjibu kwa hasira.

“Balkis mbona sikuelewi?”
“Hunielewi kivipi?”
“Itakuwaje umpulize mtu apoteze fahamu?”
“Nilikwambia nini?”
“Nilikwambia utoke, kwa nini hukutoka?”

“Mimi ni nani yako?”
“Kwa tabia yako ya miujiza siwezi kukuoa, unaonekana si mtu wa kawaida.”
“Unasemaje?” Kauli ile ilimchefua Balkis.
“Siwezi kukuoa.”
“Kweli?”

“Kweli,” Brighton alijibu kwa kujiamini.
“Asante.”
Baada ya kusema vile Brighton alishangaa kuona sura ya Balkis ikijikunja na kuwa kama mzee, uzuri wote ulipotea. Wasiwasi ilizidi kumjaa kwa kuamini huenda kweli Balkis si mwanadamu wa kawaida bali ni jini.

Baada ya kugundua kuwa Balkis si kiumbe wa kawaida, aligeuka ili awahi kuchukua Biblia ili amkemee, hakupiga hata hatua moja, mkono wa Balkis alinyooka na kuwa mrefu, ukamrudisha alipokuwa, kisha alimshika sehemu za siri na kuzivuta kwa nguvu kama anatoa kitu.

Brighton alihisi kama amepigwa shoti ya umeme sehemu za siri kisha alizisikia zikiwa za baridi kama zimetoka kwenye jokofu. Kwa sauti kali ya hasira Balkis alisema:
“Hutasimamisha milele, na mkeo hatazaa milele.”

Baada ya kusema vile aliingiza mkono sehemu za siri za Suzana ili amtoe kizazi, kabla hajamtoa Brighton alipiga kelele:
“Hapana, Balkis usifanye hivyo.”
“Lazima niwatie adabu, binadamu gani asiye na shukrani.”
“Nisamehe Balkis nipo tayari kukuoa.”

“Mpaka kwa shinikizo?”
“Siyo hivyo, mambo yako yananichanganya nashindwa kukuelewa wewe ni mtu wa aina gani?”
“Mimi ni jini?”
“Eeh!” Brighton alishtuka.
“Unashtuka nini, mimi ni jini la chini ya bahari.”

“Mungu wangu nimekwisha miye.”
”Uishe kivipi, katika muda tuliokuwa wote uligundua tofauti gani kwangu?”
“Sijagundua.”
“Penzi langu na wanadamu wenzio lipi lilikuwa tamu?”
“La kwako.”

“Mimi na mchumba wako nani mzuri?”
“Wewe.”
“Nani aliyesema kwamba Suzana hafai kuolewa?”
“Mimi.”

“Nilijitoa kwako ili kurudisha furaha iliyopotea, pamoja na kukubali kunioa bado nilimheshimu mpenzi wako, kosa langu nini?”
“Nisamehe.”
“Nitakusamehe, lakini nakurudishia ugonjwa wako ambao hautapona milele.”
“Nisamehe Balkis nilikuwa sijajua.”

“Hujajua nini?”
“Hata sijui nilimaanisha nini nimechanganyikiwa Balkis, nisamehe sana.”
“Mimi nakusamehe, lakini nakuacha na matatizo yako na mpenzi wako.”
“Hapana usinifanye hivyo.”
Balkis atamsamehe Brighton?
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.20.“Nimekubali kuendelea kuwa na wewe Balkis usinifanye hivyo,” Brighton alijitetea kwa kupiga magoti mbele ya Balkis.
“Kwa nini hutaki kunisikiliza?”
“Nilichanganyikiwa baada ya kukuona ndani, nilijua lazima Suzana atakuona.”
“Nilikueleza mimi ni nani?”

“Jini.”
“Jini huonekana kwa kupenda, Suzana asingeniona hata mara moja.”
“Ningejuaje bila kuniambia?”
“Kweli kosa ni langu la kutokukueleza mapema, nitakurudishia nguvu zako na leo hii nitaondoka na wewe kwenda kwetu kuishi maisha mazuri.”
“Wapi?”

“Ujinini,” Balkis alizungumza kwa sauti ya upole huku akijirudisha katika hali yake ya uzuri wa shani.
“Na Suzana?”
“Mwache tu, sitamdhuru, nitamrudisha kwake akiamka atajikuta kitandani amelala.”
Baada ya kusema vile alimkumbatia Brighton na wote walitoweka mle ndani na kutokea pembeni ya bahari maeneo ya Daraja la Salenda.

“Unanipeleka wapi?”
“Brighton mpenzi acha woga, tunakwenda kwetu chini ya bahari.”
“Si nitakufa na maji?”
“Huwezi, ni sehemu nzuri sana ukifika hutakumbuka kurudi duniani.”
“Nitaishi vipi na majini na mimi ni mwanadamu?”

“Kama nilivyokueleza majini tupo kama wanadamu wa kawaida na kufanya mambo kama ninyi.”
“Mmh! Sawa.”
Walitembea taratibu kuelekea ndani ya maji, Brighton alikuwa na wasiwasi wa kuzama, wasiwasi wake labda Balkis anataka kumzamisha na kumuua baada ya kuonesha kiburi.
“Balkis usiniue,” alijitetea.

Balkis badala ya kumjibu alicheka sana, jambo lililozidi kumtisha Brighton, hakusimama aliendelea kusogea mbele katikati ya bahari akiwa bado amemshika mkono. Maji yalimfika magotini, tumboni yakaanza kuelekea kifuani mwishowe yakavuka mabega.
“Balkis naomba unisamehe usiniue kwenye maji.”
“Brighton hakuna mtu anaweza kuitupa shuka yake wakati wa baridi.”
“Una maana gani?”

“Wewe ndiye shuka langu, siwezi kukupoteza, bora nipotee mimi.”
Wakati huo maji yalikuwa yamewafika chini ya kidevu, Balkis alimshika Brighton kichwani na kumzamisha ndani ya maji kwa nguvu, alitaka kupiga mayowe lakini alikuwa amechelewa. Aliposhtuka alijikuta wametokea kwenye mji mzuri ajabu.

“Brighton, karibu sana huu ni mji wetu, nawe utaishi kama mfalme, mimi ni mtoto wa Mfalme wa Majini. Baba yangu anaitwa Bashami Hudirud.”
“Asante.”
Walikuja vibaraka weusi kama wanadamu wa kawaida lakini miili yao ilikuwa na nguvu sana. Juu walikuwa vifua wazi na chini walikuwa wamejifunga shuka kama nepi wakiwa wameongozana na vijakazi waliojifunga shuka nyeupe na kuiacha migongo yao nje wakiwa wamebeba maua na farasi weupe wawili waliokuwa wametandikwa matandiko ya dhahabu.

Vibaraka wenye nguvu walimbeba Brighton na kumketisha juu ya farasi, baada ya kukaa walimbeba Balkis na kumketisha kwenye farasi mwingine aliyekuwa mzuri kuliko aliyembeba Brighton. Baada ya wote kukaa kwenye farasi, safari ilianza kuelekea kwenye jumba la kifahari.
Brighton alipatwa na wasiwasi kukuta mji unaosemwa ni wa majini ni mzuri ajabu na viumbe wake ni watu wa kawaida kama wa duniani. Ila njia nzima hakuna gari wala chombo chochote kinachotumia moto.

Alikaribishwa ndani huku akipigiwa muziki wa vyombo vitupu lakini ulikuwa mtamu masikioni. Kabla ya kuingia ndani lilitandikwa zulia jekundu ambalo hakuwahi kuwaza kulikanyaga katika maisha yake. Baada ya kuingia ndani alikaribishwa na wasichana wazuri waliovalia magauni meupe yaliyowapendeza, walimwaga maua ya kunukia.
“Brighton karibu kwetu,” Balkis alimkaribisha Brighton kwenye sofa lililotengenezwa kwa manyoya ya kondoo.

“Asante,” alijibu huku akikaa kwenye sofa lililomfanya ahisi usingizi.
“Jisikie upo nyumbani.”
“Asante, mbona ni tofauti na nilivyofikiria?”
“Kuhusu nini?”
“Nilijua ninyi ni viumbe wa ajabu wenye mikia na meno ya kutisha, mbona ni binadamu kama sisi, kwa nini mnaitwa majini?”

“Majini ni viumbe wenye uwezo mkubwa wa kufanya jambo lolote tofauti na wanadamu. Lakini nasi tunamuabudu Mungu kama ninyi.”
“Mbona mnaua watu?”
“Unatushangaa kwani hakuna wanadamu wanaoua wenzao?”
“Wapo.”

“ Mbona mnatushangaa sisi?”
“Lakini nasikia majini hutumika kuwaua watu?”
“Bado hakuna kitu tofauti na wanadamu, kuna wanadamu wachawi mbona hao hamuwazungumzii.”
“Lakini mbona nasikia kuna majini kazi yao ni kuua tu sijui Jini Makata.”

“Brighton hakuna wanadamu wanaotumwa kuua, hakuna majambazi wanaoua na kuchukua mali zao? Duniani sasa hivi kuna vita, wanadamu wanauana mamia kwa mamia bila sababu, hapo napo kuna majini?”
Swali lile lilimfanya Brighton akose jibu, Balkis aliendelea kuzungumza.

Je, nini kitaendelea?........TUKUTANE KESHO KWA MUENDELEZO WA STORY HII.........TUPIA MAONI YAKO HAPA?UMEJIFUNZA NINI?STORY UNAIONAJE? JE HAYA HAYAWEZI KUTOKEA KTK MAISHA HALISI?.....
 
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.22
sorry ep.21 imefutika....

IIPOISHIA;
“Ewe mwanadamu, acha kumkosea heshima mtukufu mfalme, kila utakalojibu tanguliza neno mtukufu mfalme.” Mkuu wa watwana alimkumbusha tena Brighton.
“Ndiyo mtukufu mfalme.”
“Vizuri, Balkis.”
“Mtukufu Mfalme.”

“Unajua sababu ya kukutuma duniani?”
“Ndiyo mtukufu mfalme.”
“Mbona imekuwa kinyume?”
“Mtukufu mfalme nimekwisha kujibu kila kitu.”
“Bado hujanibu.”

“Unataka jibu gani mtukufu mfalme?”
“Sababu kuu ya kukutuma huko, hujanijibu.”
“Ni kweli mtukufu mfalme shida kubwa ni kuongeza familia yetu.”
“Sasa kwa nini umekaidi amri yangu, nakuomba urudi duniani akaifanye kazi niliyokutuma.” SASA ENDELEA...

“Mtukufu mfalme, kupitia huyu mwanadamu nitapata mtoto unayemtaka. Nina imani tatizo lilikuwa damu zetu kukosa virutubisho. Lakini damu ya mwanadamu huwa ina virutubisho vingi.”
“Hatutaki mtoto mchanganyiko.”
“Lakini mtukufu mfalme si atakuwa mwanangu?”
“Sipo tayari kuchanganya damu.”

“Mtukufu mfalme, nami sipo tayari kumpoteza mpenzi wangu.”
“Tunabishana?” mfalme Barami alikuja juu.
“Baba hatubishani, ila ukweli ni huo.”
“Mwana wa mfalme mwite mtukufu mfalme si baba,” mtwana mkuu, Kulani alimwambia Balkis aliyekuwa amemvunjia heshima baba yake na kusimama wima.

“Wewe nani unayeingilia mazungumzo na baba yangu? Nani kakupa ruhusa ya kunikemea. Huna heshima, kibaraka mkubwa wee,” Balkis alimfokea mkuu wa watwana.
“Balkis umekosa heshima?” mfalme Barami alimfokea mwanaye.
“Sijakosa baba, natetea haki yangu.”

“Kulaniiii, wachukueni mkawaweke kwenye chumba cha giza haraka.”
Mfalme Barami alisema kwa sauti ya juu baada ya kumuona mwanaye amemvunjia heshima. Kulani na wenzake waliwabeba juu juu na kwenda kuwafungia katika chumba cha giza.

****
Suzana alishtuka siku ya pili na kujikuta akiwa amelala kwa mara nyingine kitandani kwake. Alijiuliza kuwa pale kitandani ni kweli au anaota, kumbukumbu zake zilimkumbusha kuwa jana yake alitoka nyumbani na kwenda ofisini na kisha alitoka.

Breki yake ya kwanza ilikuwa ofisini kwa shoga yake Sharifa na kumuelezea yaliyomsibu baada ya kulala kwa mpenzi wake Brighton, lakini ajabu siku ya pili alijikuta kitandani kwake. Alikumbuka baada ya kumuelezea shoga yake alimpa ushauri kabla ya kufanya lolote aende kwa Brighton kupata ukweli kama ni ndoto au kweli.

Suzana akiwa bado amekaa kitandani aliendelea kuvuta kumbukumbu ya mambo aliyoyafanya jana yake. Alikumbuka baada ya kushauriana na Sharifa aliaga kazini na kwenda moja kwa moja kwa mpenzi wake. Alipofika Brighton alionesha kubabaika hata majibu yake yalikuwa kama mtu aliyemfumaniwa.

Baada ya hapo hakumbuki kilichoendelea mpaka alipoamka na kujikuta tena kitandani kwake. Tukio la kujikuta kwake tena wakati anaamini jana asubuhi alikwenda kwa Brighton lilizidi kumchanganya akili.
Kabla hajafanya lolote simu yake iliita alipoangalia ilikuwa ya Sharifa, aliipokea na kuzungumza.

“Haloo Sharifa.”
“Eeh, Suzy vipi, ndiyo ukaondoka kimoja na simu ukazima. Lakini hiyo ni tabia gani ukiwa na tatizo tuko pamoja likikuishia ananisahau?” Sharifa alilalamika upande wa pili.
“Najua utanilaumu bila kujua.”
“Suzy hata kama ulichokifuata kimekwenda vizuri, kwa vile uliniacha na mimi na maswali ulitakiwa kunijulisha.”

“Sharifa nashindwa sijui nikuambie nini?”
“Uniambie nini Suzy? Kitendo cha kukosa uungwana kwa kweli siyo kizuri hasa tukiwa watu wa karibu.”
“Kabla sijakuambia kitu naomba nikuulize swali?”
“Uliza tu. ”

“Ni kweli jana nilikuja ofisini kwako asubuhi?”
“Mbona unaniuliza hivyo?”
“Shoga yangu nina maana kubwa sana ya kukuliza hivyo naomba unijibu usinidanganye.”
“Ni kweli ulikuja.”

“Si nilikuja kukueleza maajabu yaliyonitokea nilipolala kwa mpenzi wangu na kujikuta kitandani kwangu?”
“Ndiyo.”
“Ni kweli asubuhi sikufanya kazi nilikuaga nakwenda kwa Brighton.”
“Ndiyo.””Basi dada yangu yaliyonitokea juzi kuamkia jana ndiyo aliyonitokea jana kuamkia leo.”

“Una maana gani kusema hivyo?”
Suzana alimweleza yote aliyokutana nayo na siku ya pili alipoamka na kujikuta kitandani kwake.
“Suzana usiwe unachanganya mambo, pengine ulipotoka hapa badala ya kwenda kwa Brighton ulikwenda kwako ukalala na kupitiwa na usingizi mzito?”

“Sijafikia huko kiasi cha kupoteza kumbukumbuku hivyo, nilipotoka ofisini nilikwenda moja kwa moja kwa Brighton. Jamani hata kama nilirudi nyumbani asubuhi ile ndiyo nilale nishtuke asubuhi ya siku ya pili?”
“Mmh! Suzana kuna tatizo.”

“Yaani huwezi kuamini sasa ndiyo inajidhilisha kuwa kuna kitu kinanichezea akili.”
“Kwani Brighton yeye anasemaje?”
“Lazima na yeye atakuwa na tatizo, siku mbili hizi simwelewi kabisa, amekuwa kama mtu aliyechanganyikiwa.”

“Suzana umezidi ubishi kila kitu nilikueleza, lakini hutaki kuamini wacha yakukute.”

Suzana yupo njia panda anataka kujua yaliyomzunguka ni kweli au ni ndoto.
 
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.23


“Tuache masihara, hebu nipelekwe kwa huyo mtaalamu, kilea kidonda mwisho kukatwa mguu.”
“Leo ndiyo unagundua, nilikueleza toka mwanzo kuwa majini wana hadaa inayokuchanganya na mwisho wa siku wanakuingiza sehemu mbaya.”
“Sharifa huu si wakati wa kunilaumu, nahitaji msaada wako la sivyo nitachanganyikiwa.”
“Kama upo tayari, twende pamoja Bagamoyo.”

”Lini?”
“Leo hii.”
“Saa ngapi?”
“Safari yetu itakuwa saa tatu?”
“Basi shoga tutakuwa wote hali inatisha.”

Walikubaliana kwenda wote Bagamoyo, baada ya kukata simu Suzana alinyanyuka kitandani ili kujiandaa na safari ya Bagamoyo.
Baada ya maandalizi waliingia kwenye gari kwenda nyumbani kwa Sharifa kumpitia kwenda kwa mganga Bagamoyo. Njiani alijitahidi kumpigia simu Brighton simu yake haikuwa hewani, aliachana naye na kuendelea na safari yake mpaka kwa Sharifa.

Aliwakuta wameisha jiandaa wakimsubiri, walipomuona tu hawakutaka kupoteza muda.
“Jamani tutatumia magari yote?” Suzana aliuliza.
“Hakuna haja ya kutumia magari yote, moja tu linatosha”
“Hakuna tatizo.”

Walikubaliana kwenda kwenye usafiri mmoja walipanda kwenye gari la Sharifa na kuelekea Bagamoyo. Walitumia dakika arobaini na tano kufika Bagamoyo, walipofika waliuliza wenyeji sehemu aliyopo mganga Njiwa Manga.
“Samahani kaka,” Sharifa alimuuliza kijana mmoja aliyepita karibu na mlango wa gari lake.
“Bila samahani dada yangu,” kijana yule alijibu huku akisogea karibu.
“Habari za saizi?”

“Nzuri tu dada.”
“Eti, Njiwa Manga anaishi wapi?”
“Njiwa Manga! Yupi, yule mganga?”
“Eeh, huyo huyo.”
“Unaona hii barabara kubwa?”
“Ndiyo.”

“Ifuateni, acha barabara ndogo mbili zinazokatisha kulia, ya tatu ufuate nenda moja kwa moja mpaka mbele utaona kuna nyumba ina bendera nyekundu hapo hapo kwa mzee Njiwa Manga.”
“Asante,” Sharifa alishukuru huku akimpa elfu mbili.
“Nashukuru dada yangu.”

Waliachana na yule kijana na kufuata maelekezo yake, walipofika barabara ya tatu inayoingia kulia waliifuata na kwenda mwendo kidogo mpaka kufika kwa mganga Njiwa Manga. Walipaki gari sehemu iliyo salama na kutelemka, ilikuwa sehemu yenye eneo kubwa lililokuwa na nyuma kubwa moja na pembeni kulikuwa na mabanda madogo.
“Karibuni,” binti mmoja aliyekuwa amevalia gauni refu na kitambaa kichwani aliwakaribisha.
“Asante,” waliitikia kwa pamoja.

“Karibuni kwenye benchi hapo chini ya mti.”
“Asante,” walikwenda wote kukaa chini ya mti kusubiri maelekezo.
Ilipita zaidi ya saa nzima bila kupata maelezo yoyote zaidi ya kukaribishwa kana wageni wengine na kuonesha sehemu ya kukaa.

“Samahani dada,” Sharifa alimwita yule msichana aliyewakaribisha na kuendelea kuwakaribisha wageni wengine kama watatu, mmoja alikuja na gari na wengine wawili walikuja kwa miguu kuonesha walikuja na usafiri wa daladala.
“Bila samahani,” alisema huku akisogea kuwasikiliza.
“Eti mganga tumemkuta?”

“Yupo, kama asingekuwepo nisingewaacha mkae mpaka muda wote huu.”
“Kwa hiyo tutaonana naye saa ngapi?”
“Mmh! Sijajua ila si muda mrefu, leo hakuna wagonjwa wengi.”
“Wengine wapo wapi?”
“Wapo ndani, wakipungua nanyi mtaingia.”

“Haya,” waliachana na yule msichana aliyerudi sehemu yake kusubiri wateja wengine.
Baada ya nusu saa waliitwa ndani, wakati huo ilikuwa imefika saa tatu na nusu asubuhi. Waliongozana wote watatu mpaka kwenye sebule kubwa iliyokuwa imetandikwa zuria bila kiti. Baada ya kuketi msichana aliyewafuata aliingia chumbani na kuwaacha wasubiri.

Ilipita kama robo saa tena waliitwa ndani, waliingia wote watatu. Chumbani kulikuwa na mzee wa makamo aliyeonekana kula chumvi nyingi kutokana na kuenea mvi sehemu kubwa ya nywele zake. Alionekana ni mtu wadini kutokana na mavazi yake ya kanzu iliyokuwa nyeupe sana na juu alivalia kilemba cheupe. Pembeni yake kulikuwa na msahafu.
“Asalamu aleykum,” mama Sharifa alimsalimia mganga.

“Waleyku msalamu, karibuni.”
“Asante,” waliitikia kwa pamoja.
“Shikamoo,” Sharifa na Suzana walimwamkia mganga.
“Marahaba mabinti zangu, karibuni.”
“Asante.”
“Haya, mna shida gani?”

“Kuna vitu vimewatokea mabinti zangu, mpaka sasa vinawachanganya, japo kuna sehemu tulikwenda na kuelezwa tatizo lao, mmoja hakuwepo na mwisho wa yote ilionesha tatizo lile kwa upande wake ni zito hivyo alituelekezwa kuja kwako,” mama Sharifa alitoa maelezo mafupi.
“Mmh, nimekupateni, nipe majina yao.”

Nini kitaendelea, watapata msaada kwa mganga Njiwa Manga?
 
 
 
 
 
 
 
 
 JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.25.

LIPOISHIA:
“Nina imani mmebahatika kumuona Balkis jinsi alivyo mwanamke mzuri sana, ambaye hakuna mwanaume atakayemtaka akamkataa. Mchumba’ako akaingia kichwa kichwa kumtaka kimapenzi, kana kwamba hana shida na mumeo, alipoonesha dalili za kumtaka alimuuliza maswali ya mitego, kama angekuwa na akili angetambua kuwa yule si mtu wa kawaida. SASA ENDELEA...

Lakini kutokana na kuchanganyikiwa na mapenzi, hakupata muda wa kujiuliza, Balkis alimuuliza maswali kuhusiana na uhusiano wenu, hakushangaa mtu kuonana naye mara ya kwanza kumuulizia vitu ambavyo hata watu wenu wa karibu hawajui.

Alipomuulizia kuhusu kumtaka yeye wakati wewe ni mchumba wake, mwenzio alikukana na kusema kuwa wewe ni mpenzi wake si mke wake. Alipoulizwa kama yupo tayari kuoa mwanamke mwingine na kuachana na wewe, kutokana na kiwewe cha mapenzi alikubali kuwa yupo tayari na kuusema udhaifu wako.

“Alipoulizwa tena yupo tayari kumuoa yeye Balkis alikubali. Aliutumia udhaifu wa mchumba wako kujenga uhusiano wa haraka na kutaka kuwa naye siku ile, pia alikubali. Walikubaliana kwenda nyumbani kwa mchumba wako, ili kutowagonganisha, mchumba wako alitaka kukupigia simu ili usiende, lakini Balkis alimzuia asikupigie simu na kukueleza uende na ulipokwenda ulimuona jinsi alivyobabaika baada ya kuingia na kwenda moja kwa moja chumba cha wageni alichokuwa ameingia Balkis muda ule ule. Ulishtuka baada ya kumuona ameingia ghafla chumbani, ni kweli?”

“Ni kweli,” Suzana alijibu kwa sauti ya chini huku akiwa anaona muujiza mkubwa kutokana na maneno ya mganga ambayo mwanzo aliyaona kama simulizi ya kusisimua isiyo na ukweli. Lakini swali lile lilikuwa kama kitu kilichomtoa kwenye bumbuwazi.

“Basi kitendo cha kuingia na kwenda moja kwa moja kilimtia wasiwasi mkubwa mchumba wako kwa kujua lazima utamkuta Balkis na kumfumania. Hata lugha zenu ziligongana kitu kilichokushangaza. Kingine kilichokushangaza kilikuwa kwa mpenzi wako kuwa tofauti na siku zote kukujibu kwa ukali jambo la kawaida.

Baada ya kumuona humuelewi, ulikwenda chumba cha kulala, yeye alirudi hadi chumba cha wageni na kushangaa kumkuta Balkis akiwa amejaa tele kitandani. Alipotaka kujua alikuwa wapi alimwambia akuwahi chumbani ili akurudishe kwenye hali ya kawaida.

Baada ya kuingia chumbani, penzi alilokupa ndilo lilikuchanganya na kusahau yaliyotokea muda mfupi. Usiku jini Balkis alikuja kukuchukua ukiwa usingizini na kukurudisha kwako na yeye kulala na mchumba wako mpaka asubuhi. Wote mlipoamka mlishtuka lakini hakuna aliyejua ukweli wa tukio la usiku ni kama ndoto au kweli.

Ulipokwenda kwake asubuhi ya jana kupata uhakika kwa kilichotokea, ndani walikuwa mchumba wako na Balkis, ndiye aliyemweleza ujio wako. Ulipofika alikuwa mule mule chumbani amelala kitandani. Wewe hukumwona ila mwenzako alimwona kama kawaida, kitu kile ndicho kilichompa kigugumizi.

Hali ile ilikuchanganya na kumuona kama mtu mwenye matatizo, wakati huo Balkis alimwambia mchumba wako kwa sauti ya juu ya kumkemea kuwa akikuuliza useme hukuja jana ili ujue kilichotokea si kweli bali ni ndoto.

Lakini kwa yeye kuwepo pembeni ya kitanda karibu na Balkis aliyekuwa amelala pembeni yako bila wewe kumuona, ilizidi kumchanganya.

Mchumba wako alipatwa na kigugumizi kwa kujua utanamuona Balkis, kubabaika kwake kulikufanya umtilie wasiwasi na kumuuliza swali ambalo lilimchanganya pale ulipotaja jina la Balkis kama jini, jina ambalo lilikuwa la mpenzi wake, kumtaja kama jini ilimuudhi sana Balkis na kukupuliza upepo uliokufanya upoteze fahamu.

Kitendo kile mchumba wako alikiona na kumpandishia na kutaka kujua amekufanyia nini, Kauli ile ilimfanya Balkis kukasirika na kuondoa nguvu za kiume za mchumba wako na kutaka nawe kukutoa kizazi.”

“Mama yangu!” Suzana alishtuka na kushika mdomo kusikia vile.
“Usiogope, hakukutoa kizazi baada ya mchumba wako kumuomba msamaha na kuwa tayari kumuoa baada ya kumkataa kutokana na vitendo vyake visivyo vya kawaida. Baada ya Balkis kumsamehe aliamua kuondoka naye kwenda kuishi chini ya bahari.”

“Mamaaa!” Suzana alipiga mayowe ya mshtuko.
“Mungu wangu unataka kutuambia Brighton yupo ujinini?” Mama Sharifa aliuliza.
“Ndiyo, lakini kwa sasa yupo katika matatizo.”
“Matatizo! Matatizo gani tena jamani?” Suzana aliuliza kwa huzuni.

“Baada ya kufika katika mji wa majini, baba mzazi wa Balkis alishtuka kuona mwanaye amekwenda na mwanadamu akimsema ndiye mume wake badala kupeleka alichotumwa.
Hapo palitokea kutoelewana kati ya Balkis na baba yake, baba akitaka mwanaye arudi duniani kuendelea kutafuta vizazi zaidi vya wanawake ili apate dawa ya kuweza kupata ujauzito ili aolewe na jini mwenzake.

Lakini Balkis hakuwa tayari kuolewa na jini mwenzake baada ya kuonja penzi la mwanadamu. Yeye aliamini kuolewa na mwanadamu kusingekuwa na haja ya kuendelea kuwatoa uzazi wanawake. Kwani angekutana kimwili na mwanadamu angeweza kupata bila kutumia dawa hiyo.

Hapo ndipo palipozuka mvutano wa mtoto na baba, Balkis aliamini kwa vile anapendwa sana na baba yake atakubaliwa, lakini baba yake hakuwa tayari kuchanganya damu ya jini na mwanadamu. Baada ya kuona mtoto wake amemkosea adabu, alimuamuru mkuu wa Watwana anaitwa Kulani, Jini mweusi lakini mwenye nguvu. Kumchukua Balkis na mchumba wako kuwapeleka katika chumba cha giza.”

“Kwa hiyo ndiyo harudi tena?” Suzana aliuliza.
“Anaweza kurudi lakini mpaka atoke sehemu aliyofungwa.”
“Bila ya hivyo hawezi kutoka?” Sharifa aliuliza.

“Inategemea na uamuzi wa mfalme wa bahari kumtoa.”
Mambo yanazidi kuwa mazito. Je, Brighton atapona au atauawa katika mji wa majini? Mganga njiwa Manga atawasaidia?
 
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.28.


Ilipoishia:
“Bila ya hivyo hawezi kutoka?” Sharifa aliuliza.
“Inategemea na uamuzi wa mfalme wa bahari kumtoa.”Sasa endelea:


“Hawezi kumuua?” Suzana aliuliza kwa sauti ya kukata tamaa.
“Hawezi, nina imani atatoka tu, kinachotakiwa ni kuvuta subira.”
“Mmh! Na mimi tatizo langu?” Sharifa aliuliza.

“Wewe tatizo lako limepata bahati moja kubwa ambayo sawa na bahati ya mtende.”
“Bahati gani?” Sharifa aliuliza huku akijiweka sawa.
“Kitendo cha kufungiwa Balkis katika chumba cha giza, kimewawezesha kuja huku bila ya matatizo.
“Una maana gani?” Sharifa aliuliza.

“ Majini ni viumbe wasiokubali kuona wanavurugiwa mipango yao, Balkis kama angekuwa hajafungiwa lazima angeizuia safari yenu.”
“Angeizuia kivipi?”
“Mngekutana na vitu vya ajabu njiani hata kupinduka na gari lenu.”
“Si tungekufa?”

“Msingekufa, mngeumia tu ili msiweze kumfuatilia.”
“Na bahati nyingine?”
“Bahati nyingine wakati wa kufanya dawa ya kurudisha kizazi chako hakutakuwa na upinzani wowote. Wala kazi yako haitahitaji vitu vingi vya kufanya na itaanza leo saa sita za usiku baharini.”
“Kama angekuwepo?”

“Mmh! Pangechimbika, waganga wengi wamepoteza maisha kwa ajili ya kutaka kuvuruga mipango ya majini. Pia tungehitaji vitu vya gharama ili kumdhibiti hapo kazi ingetakiwa kufanyika saa nane za usiku baharini katika maji ya shingo.”
“Mmh! Sasa akitoka si ataweza kutuua?”

“Balkis ni jini lenye huruma sana, katika maisha yake hapendi kufanya vitu vibaya, hata kuolewa ilikuwa ni shinikizo la wazazi wake tu ambao walimlazimisha kutafuta vizazi vya wanawake ili aweze kupata tiba ya matatizo yake ya kushindwa kupata ujauzito.

“Mwanzoni alikataa katakata lakini aliahidiwa kupewa zawadi kubwa kama atapata mtoto hasa wa kiume. Alikubali kuifanya kazi ile kwa shingo upande, lakini moyoni mwake hakupenda hata siku moja kutenda kitendo chochote kibaya kwa wanadamu, siku zote aliwaza kuishi duniani na kuolewa na binadamu.

“Hata kazi ya kutoa vizazi ilimchukua muda mrefu sana, kitu kilichowafanya wazazi wake kumleta duniani moja kwa moja ili aweze kupata vizazi hivyo kwa muda mfupi, bila kujua Balkis hakupenda kuifanya kazi ile.

“Siku Suzana alipoona sherehe ya ajabu juu ya bahari, hiyo ndiyo ilikuwa siku rasmi ya kuja duniani kwa Balkis kusaka vizazi vya wanawake na kuvipeleka baharini. Aliandaliwa jini mwingine ambaye kazi yake ilikuwa ni kuvipokea vizazi hivyo juu ya bahari katika eneo lile la Daraja la Salenda na kuvipeleka kwenye stoo chini ya bahari.

“Lakini ilikuwa tofauti na walivyotegemea wazazi wake, tangu Balkis alipofika rasmi duniani kwa kazi hiyo, kwa siku moja alipeleka vizazi vinne tu na chako kikiwa kimojawapo.
Kazi aliyotumwa alisahau baada ya kuvutiwa na uzuri wa mchumba wa Suzana na kujikuta akianzisha uhusiano wa siri bila mwenzako kujua.

“Katika harakati za kuhakikisha anamdhibiti mchumba wako, muda mwingi aliutumia kuhakikisha anamchukua jumla badala ya kuifanya kazi aliyotumwa.
“Aliweza kuwagonganisha kwa kuziua nguvu za kiume za mchumba wako na usiku ulipoingia alizirudisha ili afaidi yeye.

“Hali ile ndiyo iliyowasukuma kutafuta suruhu ya tatizo lenu, alipoona mmeanza kupata mwanga aliwachanganyeni kwa kuzirudisha kitu kilichokufanya uone kama hakuna tatizo.Balkis alipofanikiwa kumnasa mchumba wako kwenye mtego wake, hakupanga kuondoka naye mapema.
“Mngeendelea kushea mapenzi bila wewe kujua mpaka angeshika ujauzito.
“Kosa alilolifanya mchumba wako ni kwenda kinyume na yale aliyokuwa akielekezwa na Balkis.

“Kubabaika kwake kulipelekea wewe kuingia wasiwasi na kutamka neno lililomchukiza Balkis na kukupulizia hewa iliyokupoteza fahamu.
Hali ile ilimfanya Balkis aone mpango wake umeharibika mapema, ili asiweze kumpoteza mpenzi wako aliamua kuondoka naye kwenda chini ya bahari.

“Kutokana na huruma yake aliamini kama ataolewa na binadamu atakuwa ameokoa tatizo la wanawake kutolewa vizazi. Lakini ilikuwa tofauti na walivyotegemea wazazi wake ambao wao walimtuma kuishi duniani ili kufanikisha kupatikana kwa vizazi vingi vya mwanamke vitakavyomuwezesha kupata dawa ya kushika ujauzito ili aolewe na jini mwenzake.

“Walishangaa kumuona akiwa na mwanaume wa kibinadamu na kumtambulisha kwao kama ni mume wake. Kitendo kile kiliwaudhi sana, naye hakutaka kukubali.Baada ya mvutano Balkis na mchumba wako waliwekwa kwenye chumba cha giza.”
“Sasa kama unasema wazazi wake hawakukubali wataweza kumtoa salama Brighton?” Suzana aliuliza.

“Hapa inaonesha maisha yake yapo zaidi ya hapo, Kwa hiyo hawezi kuuawa.”
“Kama umeona anaweza kuendelea kuishi, itakuwa wapi duniani au kuendelea kufungwa kwenye chumba cha kiza?” Suzana alikuwa na shauku kutaka kujua hatma ya mchumba wake.
“Kwa kweli haioneshi ataishi wapi ila kuna maisha marefu ya mchumba wako.”
“Vipi kuhusu kazi yangu ya kurudisha kizazi kuna vitu vinatakiwa kwenda kununua?” Sharifa aliuliza.

“Anatakiwa njiwa mwekundu tu, kwenye mabanda yangu anapatikana.”
“Na mimi kumpata mchumba wangu utanisaidiaje?”
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.27

LIPOISHIA;
“Sasa kama unasema wazazi wake hawakukubali wataweza kumtoa salama Brighton?” Suzana aliuliza.

“Hapa inaonesha maisha yake yapo zaidi ya hapo, kwa hiyo inamaanisha hawezi kuuawa.”
“Kama umeona anaweza kuendelea kuishi, itakuwa wapi duniani au kuendelea kufungwa kwenye chumba cha giza?” Suzana alikuwa na shauku kujua hatima ya mchumba wake.

“Kwa kweli haioneshi ataishi wapi ila kuna maisha marefu ya mchumba wako.”
“Na kuhusu kazi yangu ya kurudisha kizazi kuna vitu vinatakiwa kwenda kununua?” Sharifa aliuliza.
SASA ENDELEA...

“Anatakiwa njiwa mwekundu tu, kwenye mabanda yangu atapatikana.”
“Na mimi kumpata mchumba wangu utanisaidiaje?”
“Kama akitoka kwenye chumba cha giza tutampata, lakini kumtoa kule ni kazi ngumu, haonekani kila nikimtafuta.”

“Kwa hiyo utanisaidia vipi?”
“Kwa vile kazi ya mwenzako ni nyepesi ngoja tuifanye usiku wa leo, ya kwako itabidi nichimbe sana kuona kama kuna uwezekano wa kumtoa hata akiwa chumba cha giza.”
Walikubaliana kuifanya kazi ile usiku wa siku ile, mganga aliwaruhusu wakapate chakula na kupumzika ili kuvuta muda.
***
Majira ya saa sita usiku Sharifa alisimamisha gari lake pembeni kabisa na bahari maeneo ya pwani ya Bagamoyo, sehemu aliyoelekezwa na Mganga Njiwa Manga. Hali ya hewa ilikuwa giza la wastani, kwa mbali ilionekana miale ya moto ya wavuvi wa usiku.
Baada ya kusimamisha gari hakuteremka walisubiri maelekezo ya mganga. Mganga Njiwa Manga alianza kuteremka kisha aliwaita, wote walitoka nje ya gari.

Baridi la ufukweni lilikuwa kali, kila aliyekuwepo pale lilimchonyota hadi kwenye mifupa. Mganga alitoa vifaa vya kufanyia kazi, njiwa wa kazi alikuwa ameshikiliwa na Sharifa.

Wote walikuwa kimya wakimsikiliza mganga ambaye alikuwa akitembea kuelekea baharini, mawimbi muda ule hayakuwa makali sana yalipiga taratibu. Mganga aliingia majini usawa wa maji ya mafuti na kumwaga vitu huku akizungumza maneno kwa sauti ya juu.
“Ewe jini la bahari nakuletea zawadi hii ili bahari iwe tulivu, pia nimekuletea zawadi ya njiwa ili kuniruhusu niifanye kazi yangu bila kikwazo.”

Baada ya kusema vile aligeuka bila kutoka ndani ya maji na kumwita Sharifa.
“Kavue nguo zote kisha ujifunge upande wa kanga halafu uingie ndani ya maji na njiwa wako.”

Sharifa alifanya kama alivyoelekezwa na mganga, aliingia ndani ya maji na kuwaacha mama yake na Suzana wakiwa wamesimama huku wakiendelea kupigwa na baridi kali ya upepo utokao baharini. Aliingia ndani ya maji ya baridi huku akiwa na hofu ya kutojua mganga anataka kumfanya nini hasa akiwa amejifunga upande wa kanga bila kitu chochote mwilini.

Alipomfikia mganga alisogea naye mbele hadi maji ya shingo njiwa wake akiwa amemnyanyua juu. Baada ya kufika kimo kile cha maji, mganga alimwambia Sharifa amuweke kichwani, naye alifanya vile. Mganga alimshika sikio la kushoto na kuanza kuomba kwa lugha ya kiganga.

Aliomba kwa kuzungumza maneno haraka haraka bila kumeza mate kwa zaidi ya nusu saa. Baada ya robo saa Sharifa alianza kusikia vitu vikikoroga tumboni, Sharifa alishindwa kufanya kitu kutokana na mikono kuwa kichwani amemshikilia njiwa.

Mganga aliendelea kuzungumza maneno ya kiganga akiwa bado amemshikilia sikio, tumbo nalo liliendelea kumkoroga huku mwili ukizidi kupungua nguvu. Mara alianza kuona kiza mbele na kuangukia ndani ya maji na njiwa wake mkononi.

Mganga aliwahi kumdaka na kujitahidi kumsimamisha lakini miguu haikuwa na nguvu, alipiga kelele kuomba msaada kwa mama Sharifa na Suzana waliokuwa nje ya maji. Nao walijikuta wakiingia kwenye maji na nguo zao bila kujijua kuwahi kutoa msaada kwa mganga.

Walipofika ndani ya maji ya shingo walimsaidia mganga kumsogeza ufukweni, walipofika ilionesha kama Sharifa amepoteza fahamu.
“Mganga mbona hivi?” Mama Sharifa aliuliza.
“Ni kawaida kuna kitu kilikuwa mwilini mwake kimetoka lakini baada ya muda atakuwa katika hali ya kawaida.”

Pamoja na Sharifa kupoteza fahamu mganga aliwaomba wambebe hadi ndani ya maji ili aendelee na tiba yake.
“Sasa baba si unamuona alivyo kwa nini tusisubiri arudiwe na fahamu kisha uendelee na tiba?” Mama Sharifa aliuliza akiwa amejawa na wasiwasi juu ya hali ya mwanaye.
“Mama unanifundisha kazi?” Mganga alimuuliza kwa sauti ya ukali.
“Samahani baba.”

“Sipendi kufundishwa kazi kama ulikuwa unajua kwa nini mlimleta kwangu?”
“Nisamehe baba yangu.”
“Basi naomba kila utakachokiona hapa ukae kimya.”
“Nimekuelewa baba yangu nisamehe sana.”
“Haya mbebeni muda unakwenda.”

Mama Sharifa na Suzana walimbeba Sharifa mpaka maji ya chini ya mafuti mganga alimuomba Suzana akae chini ili ampakate mgonjwa. Suzana alifanya kama alivyoelezwa na mganga kisha Sharifa alilazwa chali juu ya Suzana. Mama yake alimshika sehemu ya kichwani ili kisiingie kwenye maji. Baada ya kulazwa mganga aliendelea na tiba yake kwa kuendelea kusema maneno ya kiganga kwa zaidi ya nusu saa. Huku njiwa aliyekuwa amelowana akimshikilia kwenye tumbo la Sharifa.

Baada ya muda mganga alinyamaza ghafla na kupita kimya kizito kikifuatiwa na upepo mkali. Baada ya muda upepo ulikoma. Suzana na mama Sharifa kila mmoja aliingiwa na wasiwasi kutokana na hali iliyojitokeza mle baharini. Kila moja alimuomba Mungu kimoyomoyo.

Baada ya upepo kutulia ilisikika sauti ya Sharifa ikiita.
“Mama...mama...mama.”
Mama Sharifa hakuitikia alimuangalia mganga aliyekuwa bado akitazama upepo ulipotokea na kunyanyua mkono.
 
 
 
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.29.


ILIPOISHIA:
“Nipo mimi” Suzana alijibu.
“Haya fanyeni haraka mkimaliza mniite.”
Walimbeba Sharifa ambaye hakuwa na nguvu hadi ndani ya gari na kumbadili nguo zake kisha walimwita mganga ili waondoke kurudi nyumbani.
SASA ENDELEA...

Mganga aliingia kwenye gari, Suzana aliliendesha mpaka nyumbani kwa mganga, walipofika walimteremsha Sharifa ambaye alitembea kwa tabu. Walipomfikisha sebuleni walimlaza kwenye mkeka na kumsuburi mganga aliyekuwa amemshika njiwa aliyekuwa tayari ameshamchinja tangu baharini.

Mganga alimwomba mkewe awape nguo za kujifunga wateja wale kutokana na nguo zao kulowana na maji ya bahari walipokuwa wakimtoa Sharifa kwenye maji. Baada ya kubadili nguo alimpa mkewe yule njiwa na kumweleza amnyonyoe na kumchemsha. Mkewe alimchukua na kuondoka naye na kuwaacha kina Suzana sebuleni.

Majira ya saa kumi za usiku mganga alimwamsha Sharifa na kumpa dawa ya njiwa aliyechemshwa kwa ajili ya kumla akiwa katika sufuria ile ile aliyochemshiwa.
“Mle njiwa wote na unywe na supu yake,” mganga alimwambia Sharifa ambaye bado mwili wake ulikuwa hauna nguvu.

Sharifa alianza kumla njiwa na kunywa supu yake kwa shida kwa vile alichemshwa bila kuwekwa chumvi, alipomuona kama anamshindwa kutokana na kutokuwa na kiungo hicho aliuliza.

“Mbona hana chumvi?”
“Huyo hawekwi chumvi, jitahidi umle vivyo hivyo, tena una bahati njiwa ni mdogo, watu wanakula kuku mzima bila chumvi.”

Sharifa hakuongeza neno alimuinamia njiwa wake na kuendelea kumla taratibu mpaka alipommaliza, wakati huo Suzana na mama yake walikuwa wakikoroma. Baada ya kumaliza kumla njiwa aliruhusiwa kuendelea kulala na wenzake ambao walikuwa hawajitambui kwa usingizi.

Wote waliamshwa alfajiri kwa ajili ya tiba ya mwisho ya kuoga maji ya bomba yaliyochanganywa na yale ya baharini. Baada ya kuoga waliingia kwenye chumba cha mganga kwa ajili ya mazungumzo ya mwisho kabla ya kuruhusiwa kwenda nyumbani.

Wote walikaa kwenye mkeka baada ya mganga kutulia kwa muda huku akipitia maelezo kwenye karatasi nyeupe iliyoandikwa kwa wino mwekundu kisha alisema kwa sauti ya chini:
“Nina imani kazi yetu imekwenda vizuri sana tofauti na nilivyofikiria, shughuli kama hii niliifanya siku za nyuma kwa muda wa wiki nzima, tena nikiwa na majeraha mengi kutokana na kushindana na jini.”

“Unataka kuniambia nimepona?” Sharifa aliuliza.
“Umepona.”
“Kwa hiyo nina uwezo wa kushika mimba?”
“Bila shaka.”

“Nashukuru sana mzee wangu,” Sharifa alinyanyuka kwa lengo la kumpigia magoti.
“Hapana mama kaa tu, wakushukuriwa ni Mungu yeye ndiye mwenye kukubali au kukataa maombi yetu.”

“Ina maana kama Balkis angekuwa hakufungwa kazi isingeisha leo?” Suzana aliuliza.
“Kazi ya kushindana na majini ni ngumu msione imekwenda kirahisi kiasi kile, kama Balkis angekuwa hajafungwa vita ingekuwa kubwa asingekubali tuchukue kizazi katika stoo yake. Lazima ingetakiwa niwe na vijana wangu wa kazi na katika kumdhibiti wangetakiwa mbuzi wekundu wawili, shuka nyekundu mbili na vitu vingine vingi.”

“Kutokana na kauli za mganga wa awali kuwa matatizo mengi ya tumbo yanatokana na jini Balkis kuchukua vizazi vya wanawake, lakini mbona ni wanawake wengi wana matatizo tofauti na idadi ya vizazi vilivyoko kwenye stoo ya Balkis?” Sharifa aliuliza.

“Kama nilivyowaeleza majini wanaishi kama wanadam, jinsi matatizo yetu yanavyofanana basi na ya majini huwa ni vivyo hivyo. Majini wengi wenye matatizo ya kukosa uzazi hutumwa duniani kuifanya kazi kama ya Balkis, hivyo vita si vyake peke yake ni kwa majini wengi.”

“Mungu wangu sasa tutapona vipi?” Suzana aliuliza.
“Kupona inategemea na wewe kuonana na watu wenye uwezo kama sisi au kusimama katika imani yako.”
“Kusimama kwenye imani una maana gani?” Sharifa aliuliza.

“Kila anayesimama katika imani humtanguliza Mwenyezi Mungu mbele kwa kila jambo, kabla ya kulala huomba ulinzi wake na baada ya kuamka humshukuru kwa kumvusha usiku salama, kisha humuomba tena amlinde na mchana wote.”
“Mbona tunafanya hivyo?” Alisema Suzana.

“Unaweza kuwa unafanya kutimiza wajibu wa maombi lakini imani yako si kamili, siku zote imani husimama kwa matendo siyo kwa maneno.”
“Unataka kuniambia aliyesimama kwa imani ya matendo mema hawezi kupatwa na tatizo hili?’

“Litaingilia vipi wakati Mungu ndiye mlinzi wake, hata hao majini wanamuogopa na kumuabudu yeye.”
“Kutokana na maelezo yako sasa hivi nimepona kabisa?” Sharifa aliuliza.
“Umepona na wala haitakutokea tena.”
“Kwa mfano Balkis akitoka gerezani, akijua nimerudishiwa kizazi changu si litakuwa tatizo?”

“Tatizo litabakia kwake, wewe utakuwa salama kuanzia asubuhi hii.”
“Ile hali ya tumbo kuvurugika nilipokuwa pale baharini ilitokana na nini?”
“Kizazi chako kilikuwa kikirudi sehemu yake.”

“Baba tunashukuru kwa msaada wako,” mama Sharifa alisema kwa niaba ya mwanaye.
Nini kiliendelea?
 
 
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.30.


ILIPOISHIA;
Uso wake ulionesha huzuni kitu kilichomtisha mumewe ambaye alitaka kujua kulikoni.
“Vipi mahabuba wangu?”
“Mambo yameharibika.”
“Kivipi?”

“Mpango wetu umeingia kwenye mtihani wa kwanza.”
“Mtihani upi?”
“Kizazi kimoja kimechukuliwa.”
“Tufanye haraka kabla hakijarudishwa kwa mwenyewe tumtume Kulani akaifanye kazi hii kabla hakujapambazuka.”

“Tumechelewa tayari kimeisharudishwa kwa mwenyewe.”
“Umejuaje?”
“Damu ya sehemu kilipotoka nilipoigusa imeganda kidoleni.”

“Ooh! Nani anataka kuchezea himaya yangu lazima nimkomeshe,” Mfalme Barami Hudirud alisema kwa hasira.
“Hebu kaniletee damu ya sehemu iliyotoka kizazi ili nimjue ni nani?”
SASA ENDELEA...

Malkia Huleiya alikwenda hadi kwenye chumba cha siri na kurudi na damu ya sehemu iliyochukuliwa kizazi cha Sharifa na kumpelekea mumewe.
“Naomba niilambe.”
Malkia Huleiya alimlambisha mumewe, mfalme alitulia kwa muda kisha alisema:
“Nimeishamjua, nitamtuma Kulani akishindwa nitakwenda mwenyewe.

Lazima nitamuonesha mimi ni nani.”
“Umemgundua ni nani?”
“Kuna mshenzi mmoja anataka kushindana na nguvu zangu, nataka mpaka kutakapopambazuka awe amebakia jina.”

“Kulaniiiiii,” aliitaka kwa sauti ya juu ambayo kama mwanadamu angeisikia basi angepasuka ngoma za masikio.
Kulani aliyekuwa mbali alikuja mbio na kupiga magoti mbele ya mfalme.
“Rabeka mtukufu mfalme.”
“Nataka uende duniani, damu hii itakuongoza mpaka kwa mtu huyu, nataka umfutilie mbali, sawa?”

“Sawa mtukufu mfalme.”
“Haya ondoka mbele yangu, usirudi mpaka umemfutilia mbali kiumbe huyo dhaifu anayetaka kucheza na nguvu zangu.”
Kulani alizama chini ya ardhi na kutoweka, baada ya muda alikuwa pembeni ya bahari eneo la Bagamoyo, aliilamba damu aliyopakwa kidoleni ambayo ilimuelekeza aende upande upi. Alitoka eneo baharini na kuelekea kwa Mganga Njiwa Manga.

Alitembea taratibu toka eneo la bahari akiwa katika umbile la kibinadamu, hakuchelewa kufika kwenye makazi ya watu. Aliilamba tena ile damu iliyokuwepo kidoleni mwake, kwa vile kulikuwa na giza, sehemu ya Mganga Njiwa Manga ikawaka mwanga wa taa.

Mwanga ule ulimuongoza hadi karibu kabisa na nyumba ya Mganga Njiwa Manga. Nia yake kubwa ilikuwa kwenda mpaka mlangoni na kugonga ili akifungua tu wakutane uso kwa uso na ammalize pale pale kisha aondoke kabla hakujapambazuka.

Alitembea kuelekea eneo la nyumba ya mganga, ajabu alipokaribia nyumba yake alishangaa kuona moto ukiwaka kuizunguka nyumba ile. Hali ile ilimshtua sana, aligeuka na kutimua mbio hadi baharini ambako alikunywa maji mengi na kurudi hadi kwenye eneo la nyumba ya mganga.

Alipoikaribia moto uliwaka tena, alilisogelea eneo la nyumba huku akimwaga maji aliyoyachukua baharini kwa lengo la kuuzima moto ule. Alifanikiwa lakini alipotaka kuingia kwenye himaya ile moto uliwaka tena. Alijikuta akifanya kazi ya kwenda baharini na kurudi, kila alipouzima moto na alipotaka kuingia uliwaka tena.

Kulani alijikuta akitumia muda mwingi kwenda baharini kuchukua maji na kurudi huku moto ukizimika na kuwaka. Mpaka kulipokuwa kunakaribia kupambazuka hakuweza kuingia katika himaya ya Mganga Njiwa Manga. Kwa upande wake aliiona kazi imekuwa ngumu au maji yalikuwa marefu na kuamua kurudi chini ya bahari, aliogopa kutokana na kauli aliyopewa na Mfalme Barami Hudirud kuwa asirudi chini ya maji mpaka ahakikishe amemmaliza Mganga Njiwa Manga.

Kulani alijikuta kwenye wakati mgumu katika kazi ile, tofauti na zilizotangulia ambazo alizifanya kwa muda mchache. Lakini ile ilikuwa ngumu kwake, baada ya kukutana na kikwazo cha moto.
Aliamua kurudi hadi baharini akiwa katika umbile lile la kibinaadamu, alisubiri jua litochomoze ili aweze kwenda jirani kwa mganga na kumsuburi akitoka ammalize.

Jua lilipotoka na watu kuwa wengi kujaa ufukweni kwa ajili ya kununua samaki na wengine wakipanda ngarawa kwenda kuvua.
Kulani alijichanganya na watu bila ya kujulikana kama ni jini. Baada ya pwani kuchanganya na watu kuongezeka, alijitoa eneo la bahari na kwenda kwa mganga kwa kutembea kama mtu wa kawaida.

Kila aliyemuona hakumdhania vibaya, aliacha eneo la bahari na kuingia makazi ya watu, alipokaribia maeneo ya nyumba ya mganga aliuona moto ukiwaka tena. Alikwenda kwenye nyumba ya jirani na kuomba kupumzika, kutokana na kuonekana kama mstaarabu, alikaribishwa na kupewa kiti. Mwenyeji wake hakujishughulisha naye aliendelea na shughuli zake na kumuacha Kulani akitupia jicho njia ya kutokea kwa Mganga Njiwa Manga.
Jini Kulani ataweza kutimiza azma yake ya kumuua Mganga Njiwa Manga?
 
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.31

ILIPOISHIA:
Kila aliyemuona hakumdhania vibaya, aliacha eneo la bahari na kuingia makazi ya watu, alipokaribia maeneo ya nyumba ya mganga aliuona moto ukiwaka tena. Alikwenda kwenye nyumba ya jirani na kuomba kupumzika, kutokana na kuonekana mstaarabu alikaribishwa na kupewa kiti. Mwenyeji wake hakujishughulisha naye aliendelea na shughuli zake na kumuacha Kulani akitupia jicho njia ya kutokea kwa Mganga Njiwa Manga.
SASA ENDELEA...

Muda ulikwenda bila mganga kuonekana, kila alipopata wazo la kwenda kwenye nyumba ile alishangaa kuuona moto ukiwaka, lakini ulipotulia nyumba ilikuwa katika hali ya kawaida. Alijikuta yupo kwenye wakati mgumu akiamini kabisa ngoma ile ni nzito kwake kuchezeka.

Kilichomchanganya zaidi ilikuwa ni kauli ya mfalme Barami Hudirud ya kuhakikisha anammaliza mganga ndipo arudi, japo muda aliopewa ulipita.
Kulani alipata pigo baada ya mwenyeji wake kutaka kuondoka, akiwa bado kichwa kinamuuma alimwambia:

“Samahani kaka.”
“Bila samahani.”
“Nataka kuondoka kwenda pwani.”
“Hakuna tatizo funga mlango wako mimi niache hapa nimekaa baada ya muda nitaondoka.”
“Hapana kaka sikujui nimekukaribisha kibinadamu, lakini siwezi kukuamini kukuachia nyumba yangu, dunia haiaminiki siku hizi.”

“Sawa.”
Kulani alikubali kuondoka pale, lakini sehemu iliyokuwa nzuri kupaona kwa mganga ilikuwa kwenye nyumba ile iliyokuwa ikitazamana na ya mganga. Aliondoka kwa kuzunguka nyumba ile na kujigeuza haraka kuwa mjusi. Aliupanda ukuta haraka na kwenda kujificha chini ya bati bila kuonekana.

Mwenye nyumba ile alishtuka na kuzunguka nyuma ili kupata uhakika kama kweli yule mgeni atakuwa ameondoka. Lakini ajabu alipozunguka nyuma ya nyumba iliyokuwa na uwazi mkubwa wa kumuona mtu kama anatembea kutoka pale, hakumuona mgeni wake. Alijiuliza kwa sauti:

“Sasa atakuwa amekwenda wapi, mtu azunguke sasa hivi asionekane, mmh! Lisiwe jini lile, Mungu aniepushie mbali.”
Kulani alimtazama na kutulia akiwa amejilaza kwenye ukuta chini ya bati. Baada ya kusema yale mwenye nyumba ile aliondoka na kumwacha Kulani palepale nyumbani bila kujua.

Baada ya kuondoka, Kulani aliendelea kumsubiri mganga palepale ukutani chini ya bati katika umbile lile lile la mjusi kama atatokea Mganga Njiwa Manga amvae na kumuulia mbali. Alisubiri kwa saa kumi mpaka jioni ilipoingia ndipo alipomuona akiwa anamsindikiza mmoja wa wateja wake.

Jini Kulani aliteremka na kurudi katika umbile la mwanadamu na kumfuatilia kwa nyuma bila ya mganga kujua. Nia yake ilikuwa kukutana naye wakati anarudi ili amvae. Taratibu alitembea kumfuata kwa nyuma mganga aliyekuwa mbele akitembea huku akizungumza na wateja wake.

Njiani Mganga Njiwa Manga alianza kuhisi kama ardhi inatetemeka na mwili kuwa mzito, kitu kile kilichomfanya ageuke na kutazama nyuma. Alishtuka kukiona kiumbe cha ajabu kwa mbali kikija taratibu. Kwa haraka alichutama chini na kushika michanga huku akilikemea jitu lile ambalo liligundua limejulikana.

Wakati Kulani akijitayarisha kumvaa Mganga Njiwa Manga baada ya kugundua amejulikana, kabla hajamfikia alirusha vumbi la mchanga lililomuingia machoni na kumpofua macho. Alipiga kelele za maumivu na kujipiga chini kwa hasira na kusababisha kishindo kizito kilichotikisa eneo kubwa la Bagamoyo.

Kishindo kile kilisababisha watu waliokuwa karibu na sehemu kilipotokea waanguke na kupoteza fahamu. Nyumba nyingine zilipata nyufa kutokana na kushindo cha Kulani kupasua ardhi na kupotea. Baada ya robo saa hali ya eneo la Bagamoyo ilirudi kuwa ya kawaida.
Baada ya kurudi hali ya utulivu Mganga Njiwa Manga alinyanyua alipokuwa ameangukia baada ya kurushwa na udongo uliotoka kwenye shimo alilozama jini Kulani baada ya kupofuka macho. Alimtuma mtu kwenda nyumbani kumletea dawa ambayo alikunywa na kujimwagia kichwani.

Baada ya kuyafanya yale alikwenda hadi kwenye shimo lililokuwa limechimbika kama kumelipuka bomu. Sehemu ile aliweka dawa kisha aliondoka na kurudi nyumbani kwake. Alipofika nyumbani mwili ulikuwa umechoka sana, hakuweza kuendelea na kazi ya matibabu, aliwaomba wagonjwa wake apumzike baada ya kunusurika kifo toka kwa jini ambaye hakujua ametoka wapi.

Siku ile hakufanya kazi yoyote, alilala mpaka siku ya pili huku akiviona viungo vyake vikipoteza nguvu. Hata alipolala hakuweza kujigeuza mpaka siku ya pili, kwake ulikuwa upinzani mkubwa katika kazi yake. Mara nyingi upinzani uliishia nje ya ngome yake, lakini hakikuwahi kiumbe chochote cha ardhini majini au angani kilichoweza kumdhuru.

Pia katika kazi yake haikuwahi kutokea kiumbe kilichowahi kumvizia njiani kwa ajili ya kumdhuru. Wengi walivamia sehemu aliyokuwa akifanya kazi na kukutana na vikwazo. Lakini uwezo wa kinga yake ya mwili ndiyo uliomsaidia, bila hivyo angemalizwa na jini yule.
***

Jini Kulani baada ya kuzama chini ya ardhi kwa kujipigiza kwa hasira, aliibukia pembeni ya bahari. Alitembea taratibu huku akipapasa ili kuingia majini. Baada ya kutembea kwa muda alibahatika kuyakanyaga maji. Pale pale alizama chini.
Mfalme wa bahari alishangaa kumuona Mkuu wa Watwana Kulani amesimama mbele yake akiwa haoni.

“Kuna nini tena kimekusibu mtwana wangu mtiifu?”
“Mtukufu mfalme, safari yangu imekuwa mbaya.”
“Kulani umefanya makosa, kwa nini jana hukurudi?”
“Niliogopa mtukufu mfalme kurudi bila kutimiza ulichonituma.”
“Umekitimiza?”

“Hali yangu kama unavyoniona.”
“Tatizo nini?”
“Nimepofuka mtukufu mfalme.”
“Lakini hujanijibu, umemmaliza?”
“Sikuweza, yule mtu hata wewe sikushauri uende.”
“Kwa nini?”

“Amejidhatiti, ana nguvu za ajabu sijawahi kuona, ameizindika ngome yake haiingiliki, na yeye mwenyewe alichonifanya sitasahau mpaka nakufa.”

Jini Barami Hudirud, mfalme wa bahari atakubali ushauri wa Kulani kuachana na Mganga Njiwa Manga?
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.32


“Hapana lazima niende, hawezi kushindana na nguvu zangu.”
“Mtukufu mfalme, bado himaya ya chini ya bahari inakuhitaji lazima atataka kutumia nguvu za ziada kukumaliza. Nashukuru sikugusana naye ningeweza kupoteza maisha.”
“Kwa hiyo tuwaache wanadamu watuchezee?”

“Hapana, ila nguvu zinazidiana, yule mwanadamu ana nguvu za ajabu sana, nilijitahidi kuuzima moto alioutega kwenye himaya yake, nilishindwa kila nilipouzima na nilipotaka kuingia uliwaka tena nikajikuta kukipambazuka bila ya kuweza kuingia kwenye himaya yake. Ndiyo sababu ya kuchelewa kurudi na kuamua kubaki ili nihakikishe nammaliza akitoka kwake. Lakini haikuwa hivyo matokeo yake nimekuwa kipofu.”

“Mmh! Nimekuelewa, basi mpelekeni akapate tiba.”
Watwana wengine walimchukua Kulani na kwenda kumpatia tiba ya macho, baada ya kuondoka, mfalme alimgeukia mkewe aliyekuwa kimya akimuangalia Kulani kwa huruma.
“Mke wangu umeona hali ilivyo, unanishauri nini kutokana na hali aliyorudi nayo Kulani?”

“Mmh! Mume wangu hali inatisha, inaonesha wazi vita ni nzito, tukifanya mchezo tutakwisha, mpaka Kulani kusema hivyo ujue kuna kazi. Kwa nini tusiachane na mpango wa kumfuatilia huyo mwanadamu?”
“Lakini mke wangu si unajua uwezo wangu? sijawahi kushindwa na kitu,” Mfalme alijitapa.

“Naujua vizuri, hata Kulani anaujua lakini mpaka kakukueleza vile naomba umsikilize huenda kuna kitu amekiona kinaweza kukupotezea maisha kama utashindana na yule mwanadamu.”
“Lakini kumbuka jini ana nguvu kuliko mwanadamu?’
“Lakini mwanadamu ndiye kiumbe mwerevu kuliko viumbe wote wa Mungu?”
“Hilo nalijua lakini bado hawawezi kushindana na sisi.”
“Mume wangu majini sisi hatuna ushirikiano, kuna majini wengine huwakinga mwanadamu na kuwafanya kuchanganya nguvu za kijini na akili ya kibinadamu lazima tu atakushinda.”
“Kwa hiyo tufanye nini?”
“La muhimu tuachane na mpango huo.”

“Na suala la Balkis kuolewa na jini mwenzake?”
“Hilo nalo ni gumu, tuendelee kumshawishi aweze kubadili mawazo na kuendelea na kazi ya kukusanya vizazi vya wanadamu na kutengenezewa dawa.”
“Mimi nina hasira, jaribu kuongea naye wewe.”

“Nitafanya hivyo jioni nitazungumza naye.”
Walikubaliana mke wa mfalme azungumze na Balkis ili aweze kubadili uamuzi wake wa kung’ang’ania kuolewa na mwanadamu.
****
Baada ya kuamka siku ya pili, Mganga Njiwa Manga bado mwili wake haukuwa na nguvu, wagonjwa wengi waliofika siku ile hawakupata huduma kutokana na hali yake. Ilibidi siku ile na yeye kutumia dawa za kujifusha na kunywa ili kujirudisha katika hali ya kawaida, baada ya kukumbwa na upepo wa jini Kulani.

Kilichomshangaza kilikuwa rangi ya jini yule, alikuwa mweusi kama rami tofauti na majini wote aliowahi kukutana nao. Siku ya pili tangu akutane na dhahama nzito ya jini Kulani, aliendelea na kazi ya kutoa huduma kwa wagonjwa wanaotoka mbali.

Baada ya kuingia katika chumba chake kutoa huduma, alitulia kwenye mkeka kisha aliweka ubani kwenye kitezo na kutulia kwa muda ili ajiandae kwa matibabu ya wagonjwa waliokuwa wameongezeka kutokana na kusimama kwa huduma yake.

Ilikuwa ajabu baada ya moshi wa ubani kupanda juu, ulimfuata mbele ya uso wake na akaanza kuona picha asiyoielewa. Alikiona kiumbe cha ajabu kikitoka kwenye maji na ghafla kiligeuka na kuwa mwanadamu, kisha kilitembea taratibu toka kwenye ufukwe na kuingia maeneo ya watu.

Baada ya kiumbe kile kilichojigeuza kuwa binaadamu kukaribia ngome yake, kilijigeuza umbile na kurudia lile alilotoka nalo chini ya maji. Ajabu kilipotaka kuingia kwenye himaya yake aliona moto ukiwaka kuzunguka eneo lake, ghafla kiumbe kile kilitoka mbio kurudi baharini na kuchota maji kisha kuja kuzima moto.

Kiliendelea kuzima moto mpaka kulipopambazuka, kila kilichoendelea alikiona mpaka kupambana na jini lile. Hapo ndipo alipogundua jini lile lilitoka wapi, alicheka na kuona kinga aliyokuwa nayo ndiyo iliyomsaidia bila hivyo angekufa vibaya.
Taratibu moshi ulipungua na hali ya ndani ikarudi kuwa ya kawaida, Mganga Njiwa Manga aliendelea kuweka tena ubani uliotoa moshi wa kawaida bila kuwepo na kitu kisichokuwa cha kawaida. Alimtuma msaidizi wake kuwaita wagonjwa.

Nini kiendelea baada ya mganga kuonekana kudhibiti nguvu za kijini? Je, nini hatma ya Brighton katika chumba cha giza?
 
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.33
CHINI YA BAHARI
Malkia Huleiya, mama mzazi wa Balkis alikwenda hadi chumba cha giza na kuomba Balkis atolewe, baada ya kutolewa alimpeleka kuoga na kukaa naye kwenye pwani ambayo huitumia kupumzika familia ya kifalme. Muda wote Balkis alikuwa akibubujikwa na machozi.
Baada ya kukaa kimya kwa muda malkia Huleiya alimwita mwanaye.
“Balkis”

“Abee mama.”
“Najua utatuona sisi wazazi wako makatili lakini unajua kabisa ubaya wa wanadamu na pia ni aibu jini kutoka katika ukoo wa kifalme kuzaa na mwanadamu.”
“Mama kabla ya kuzungumza lolote naomba mumtoe mpenzi wangu na kama hamtaki awe huku naomba mumrudishe duniani.”

“Hakuna tatizo.’ Alitumwa mtu kwenda kumtoa Brighton kwenye chumba cha giza na kumpa maji ya kuoga kisha kuwekwa kwenye chumba kizuri. Baada ya hatua zile mazungumzo yaliendelea.
“Nina imani imefurahi?” Mama yake alimuuliza.
“Siwezi kufurahi kwa vile sijatimiza dhamira yangu.”
“Ipi?”

“Ya kuolewa na mwanadamu.”
“Hilo ndilo baba yako hataki kusikia.”
“Lakini kumbuka tunachokifanya hakimpendezi Mwenyezi Mungu.”
“Kipi hicho.”

“Cha kuwafanya wanawake matasa.”
“Ni kweli, lakini tunafanya hivyo kwa ajili yako.”
“Kama unaona kufanya vile ni dhambi kwa nini msiniache na mpenzi wangu aliyekuwa tayari kukaa huku hata watoto wangezaliwa wangekuwa wetu.”
“Mwanangu hujui vita ya wanadamu ni kubwa, huwezi kuamini kizazi kimoja kimechukuliwa. Kama kizazi kimechukuliwa je, mwanadamu watakubali aishi huku?”
“Mwanadamu kanipenda mwenyewe wala sikumlazimisha.”

“Lakini si ana mchumba wake?”
“ Alimkana mbele yangu na kuwa tayari kunioa.”
“Kwa sababu hakujua kuwa wewe ni jini.”
“Hata alipojua alikubali ndiyo maana nimekuja kuishi nae huku.”
“Lakini kumbuka baba yako alikuwa akikutegemea sana, ulichokifanya kimemchanganya sana.”

“Lakini mama tatizo nini, kutafuta vizazi vya wanawake na kuzaa bila vita na wanadamu kipi bora, ona kama ulivyoniambia mkuu wa watwana Kulani kawa kipofu, kwa nini tusiachane na vita na wanadamu ili hamu ya mtoto apatikane bila kupata madhara zaidi.”
“Uamuzi wako umemuweka baba yako katika wakati mgumu, kumbuka anakupenda kuliko kitu chochote, hakuota hata siku moja utamkosea heshima.”

“Ni kweli najua baba ananipenda lakini alitakiwa kunisikiliza kuliko kuchukua maamuzi mazito, ona katumia nguvu nyingi matokeo yake Kulani kawa kipofu.”
“Balkis mwanangu hakuna jini anayekubali kushindwa na mwanadamu.”
“Ni kweli lakini kuna wanadamu nao huamini kabisa majini hawawawezi, kama wameweza kuchukua kizazi kimoja wanashindwa nini kuvichukua vyote?”

“Balkis mwanangu kama ungekwenda kwa kitu tulichokutuma, nina imani kazi yako ingekuwa nyepesi sana kuliko ulichokifanya cha kuanzisha uhusiano na mwanadamu.
“Kitendo kile kilituchanganya sana hasa baba yako, hata kuzungumza na wewe alishindwa na kunituma mimi. Anaamini hata matatizo ya Kulani chanzo ni wewe.”
“Chanzo ni mimi kwa vipi? Wakati niliwakataza tuachane na vita na wanadamu lakini mkawa wabishi.”

“Balkis mwanangu naomba uifanye kazi tuliyokutuma, tunaamini wewe ni mtoto mwenye heshima na usikivu. Nakuomba chonde chonde mwanangu msikilize baba yako.”
“Mamaa kwa nini msinikubalie, kwani kuna ubaya gani?”
“Kumbuka baba yako ni mfalme wa majini, ni aibu kwa mwanaye kuolewa na mwanadamu, ndiyo maana alikutuma kutafuta kizazi cha mwanamke ili kuhakikisha unapata tiba na kuolewa na jini mwenzako.”

“Kwa hiyo nimrudishe Brighton duniani?”
“Ikiwezekana.”
“Mbona unasema ikiwezekana.”
“Lazima tumuulize baba yako ataamua nini juu ya mwanadamu aliyejua siri yetu.”
“Sasa naona unataka kuharibu mazungumzo, mmenikataza kuolewa na mwanadamu basi nimrudishe kwao.”

“Lakini si atakuwa amejua siri yetu?”
“Sasa mnataka kumfanya nini?”
“Sijajua mpaka tupate maelekezo ya baba yako.”
“Sikiliza kama nimekubaliana na uamuzi wenu wa kuachana na mwanadamu ili niendelee na kazi yangu ya kutafuta vizazi vya wanawake, naomba kwenye suala la kurudi kwao mpenzi wangu msiniingilie.”

“Lakini kumbuka mwanangu chini ya bahari hii mwenye sauti ya mwisho ni baba yako.”
“Hata awe na sauti gani uamuzi wowote tofauti na kumrudisha duniani hatutaelewana.”

Nini hatima ya Brighton? Je, ataruhusiwa na mfalme kurudi duniani baada ya kuijua siri ya majini?
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.34“Mbona umefika mbali, ngoja nimpelekee taarifa hizi, atafurahi sana kusikia kuwa umekubali kurudi dunia kutafuta vizazi vya wanawake. Pia nitamueleza suala la mpenzi wako la kurudishwa duniani. Siamini kama atakuwa na maamuzi mazito ya kukuumiza.”
“Mmh! Haya basi naomba nafasi ya kuzungumza na Brighton.”
“Mmh! Basi ataletwa huku ili baba yako asijue chochote.”

Baada ya kusema vile, Huleiya aliondoka na kumuacha Balkis akiwa amejilaza kwenye kiti cha uvivu. Japo moyo ulimuuma kumuacha Brighton mwanaume aliyeamini ndiye mume wa maisha yake. Bado hakuamini kama anaweza kutoa siri za majini. Lakini aliamini hakuwa akijua lolote katika siri za chini ya bahari kutokana na kufikia kwenye chumba cha giza.

Baada ya muda Brighton alifikishwa bustanini na kukutana na Balkis, baada ya kukutana Balkis alimueleza hali halisi na yeye kuwa tayari kumrudisha duniani. Kwa upande wake Brighton alijikuta akizama kwenye dimbwi la mahaba ya Balkis na kumuomba atafute njia yoyote ili asirudishwe duniani.

“Mpenzi kwa nini usimbembeleze baba yako ili tuishi pamoja?”
“Hilo ndilo lilikuwa lengo langu lakini limeleta mtafaruku mkubwa ndani ya familia. Kwa hiyo nakuomba ukubali kurudi duniani ila sitakuwa mbali nawe.”

“Mmh! Sawa lakini nitalikosa penzi lako.”
“Ni kweli, lakini lazima nikubaliane na matakwa ya wazazi wangu.”
“Sawa, sina jinsi,” Brighton alikubali kwa shingo upande.

Malkia Huleiya baada ya kuzungumza na mwanaye alipeleka taarifa ya kikao kwa mumewe mfalme Barami. Alipofika alimkuta akimsubiri kwa hamu.
“Karibu malkia wangu.”

“Asante mfalme wangu.”
“Mh, nijuze yaliyojiri huko?”
“Mmh! Namshukuru Mungu yamekwenda vizuri.”
“Kakubali?”

“Ndiyo.”
“Ooh! Afadhali.”
“Lakini..”
“Lakini nini tena malkia wangu?” Mfalme alishtuka.

“Kuhusu yule mpenzi wake.”
“Ana nini?”
“Anataka arudishwe duniani.”

“Ina maana hajui sheria yetu mwanadamu anayejua siri zetu huwa harudi tena duniani?”
“Hapo ndipo penye tatizo.”
“Tatizo gani?”
“Mwanao anataka amrudishe duniani.”
“Haiwezekani.”
“Amesema iwe isiwe lazima tumrudishe duniani.”

“Yeye ni nani anayetaka kutulazimisha tufanye anavyotaka, siwezi kuwa na sauti mbili katika himaya yangu ya chini ya bahari.”
“Lakini mume wangu..”
“Hakuna cha lakini, aendelee na kazi ya kutafuta vizazi tena tutampangia kwa siku moja alete vingapi ili awahishe kutimiza lengo la kuolewa tuondokane na adha hizi.”
“Mume wangu si vyema kila wakati kutumia nguvu, ifike wakati mwingine uwe unawasikiliza walio chini yako.”

“Siwezi, nasema kauli yangu ni ya mwisho na maamuzi yangu yaheshimiwe,” mfalme alikuwa mkali.
“Mume wangu hii itakuwa vita nyingine, kwa jinsi nilivyomsikiliza mwanao hawezi kukubali hili.”
“Nitakachomsikiliza ni kumuacha hai, lakini si kumrudisha duniani.”
“Mwanao amesema kwa hili hamtaelewana.”
“Hebu kamlete hapa,” mfalme alisema kwa hasira.

Alitumwa kijakazi kumfuata bustanini, Balkis alifika mbele ya baba yake kusikiliza kile alichoitiwa.
“Abee mtukufu mfalme,” Balkis aliitikia akiwa amesimama mbele ya baba yake.
“Kwanza nimefurahi kusikia umeweza kubadili uamuzi wako ila umeniudhi kwa kunilazimisha nifanye utakavyo.”
“Baba kukulazimisha kitu gani?”
“Kuhusu kumrudisha mwanadamu duniani.”

“Sasa tatizo liko wapi? Mmemkataa asinioe sasa si nimrudishe nilipomtoa.”
“Ina maana hujui sheria za majini, kama mwanadamu atajua siri zetu?”
“Nazijua lakini huyu nimemleta miye hakujileta mwenyewe, wala hakuletwa kwa lipizo.”
“Sheria za huku mwanadamu yeyote atakayeingia huwa hatoki salama, lakini kwa heshima yako hatutamuua bali ataishi huku milele.”

“Kwa hilo baba sitakubali hata kwa kukatwa kichwa, ni mimi ndiye niliyemlazimisha kuja huku iweje mumshikilie?”
“Hiyo ndiyo sheria ya huku kamwe haibadiliki.”
“Nasema kwa hili itabadilika.”
“Tunabisha?”

“Hatubishani ukweli ndiyo huo, ikifanywa kinyume nikiondoka hapa sitarudi tena.”
“Sooba,” alimwita mtwana msaidizi wa Kulani kwa sauti ya juu.
“Rabeka mtukufu mfalme,” Sooba aliitika na kusimama imara mbele ya mfalme.

“Mpeleke huyu kwenye chumba cha giza.”
Balkis alichukuliwa tena na kurudishwa kwenye chumba cha giza.
Nini kiliendelea?
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.35Baada ya mwezi mmoja na nusu kupita, Suzana akiwa ofisini kwake, muda mfupi baada ya kuingia alijikuta akiwa na mawazo mengi. Hiyo ilikuwa ni kutokana na maneno ya Mganga Njiwa Manga alipokwenda kwake jana yake kufuatilia suala la kurudi mchumba wake Brighton, aliyekuwa chini ya bahari katika chumba cha giza.

Majibu ya mganga yalimkatisha tamaa tofauti na alivyofikiria kupatiwa matibabu kama ya Sharifa ya kuingizwa ndani ya maji ya bahari usiku wa manane. Alishangaa kuambiwa baada ya kukutana naye na kuchukua vitabu vyake vya uganga na kuvisoma kwa muda. Alipomgeukia alimueleza:

“Kazi yako inanichanganya sana, mpenzi wako bado yupo chumba cha giza, inaonesha alitolewa na kurudishwa tena, kuna utata mkubwa juu ya hatima ya mumeo kutolewa chini ya bahari kurudishwa duniani.”
“Mungu wangu! Si atauawa?” Suzana aliuliza.
“Hawezi kuuawa, inaonesha uhai wake bado mrefu.”
“Sasa itakuwaje ikiwa kila siku mambo yanazidi kuwa mabaya kwake, huoni kama maisha yake yapo hatarini?”

“Ni kweli yapo hatarini lakini..”
“Lakini nini mganga? Naomba msaada wako wa kumtoa huko.”
“Nilikueleza toka siku ya kwanza kuwa ni vigumu kumtoa kwenye chumba cha giza kwani kila nikimtafuta haonekani. Kuna siku mchana nikiwa katika shughuli zangu nilikiona kivuli cha mchumba’ako, ilionesha ametolewa chumba cha giza lakini usiku nilipotaka kuifanya kazi ile sikumuona.

“Kitendo kile kilinichanganya sana, hasa baada ya kuwa nimefika baharini na mbuzi wangu wawili, mweupe na mwekundu. Nilijikuta nikimtafuta tena lakini sikuweza kumuona. Niliamua kurudi nyumbani ili kuangalia upya, wasiwasi wangu nilidhani labda amekwisharudi duniani.

“Nilimtafuta kila kona ya dunia mpaka chini ya udongo sikumuona, kila nilipomtafuta ilionesha bado yu hai, lakini alikuwa haonekani zaidi ya kiza kinene. Baada ya kuhangaika sana niliweza kukiona kivuli chake kwa taabu sana kikionesha yupo kwenye chumba cha giza.

“Lakini kila nilivyojaribu kumvuta hakuonekana, huwezi kuamini kazi yako nimeifanya kwa muda mrefu bila mafanikio kuliko kazi nyingi nilizowahi kufanya. Wakati nikiendelea kuhangaika kutafuta nilishangaa kuona taarifa ikinionesha kuwa mumeo atatoka chini ya bahari bila kutumia dawa yoyote.”

“Sasa atatokaje ikiwa bado ameshikiliwa na majini?”
“Mara zote huongozwa na maandiko ya vitabu vya uganga ili niweze kumtibu mgonjwa, siwezi kukurupuka ndiyo maana dawa zangu huwa sibahatishi.”
“Hakuna njia nyingine ya kunisaidia?”

“Siwezi kukudanganya ila nakuhakikishia mpenzi wako atarudi bila dawa yoyote.”
Suzana alikubali kwa shingo upande kwa kuamini sifa za mganga yule kuwa hashindwi na kitu ni za uongo. Aliona ni ajabu Brighton kurudi bila dawa yoyote. Baada ya kuondoka na kurudi nyumbani aliondoa tumaini la kurudi kwa mpenzi wake.

Akiwa bado ofisini, katikati ya mawazo ya kukumbuka maelezo ya mganga yaliyomkatisha tamaa, baada ya kuonekana ameshindwa kumrudisha mpenzi wake na kuweka visingizio lukuki. Alishtushwa na sauti ya Sharifa aliyeingia ofisini kwake bila kumuona kutokana na kuzama kwenye dimbwi la mawazo.

“Suzana vipi shoga mbona unaonekana upo mbali, una tatizo gani?”
“Ooh! Shoga karibu.”
“Mbona hivyo, una tatizo gani maana nimeingia bila wewe kuniona?”
“Sharifa ina maana huyajui matatizo yangu?”
“Nayajua lakini leo umekuwa tofauti na siku zote.”

“Ni kweli.”
“Tatizo nini?”
Suzana alimtonya Sharifa aliyoelezwa jana yake na Mganga Njiwa Manga alipofuatilia kumrudisha duniani mpenzi wake. Kutokana na majibu yake juu ya mganga, ilionesha kabisa hakukuwa na uwezekano wa kurudishwa kwa mchumba wake.

“Nina imani mzee yule si mganga, wala hana lolote! Anafanya kazi kwa kubahatisha, iweje aweze kumuona ashindwe kumrudisha? Kisa, oooh, nilimuona mchana usiku akapotea, mwongo mkubwa hana lolote yule,” Suzana alilalamika.
“Lakini si alikueleza atarudi, tena kizuri hakukudanganya, au ulitaka akudanganye ili achukue fedha zako?”

“Kuna mtu gani anaweza kutoka kwa majini bila dawa au maombi?”
“Muamini yule babu, analokueleza ndilo linalokuwa.”
“Kipi cha kunifanya nimuamini zaidi ya sifa za kusikia?”
“Basi shoga mguu huu ni wako.”
“Una maana gani?”

“Mambo yamejibu.”
“Mambo gani?”
“Kazi ya mzee Njiwa Manga.”
“Kazi gani?”
“Kweli Suzana umechanganyikiwa.”

“Unafikiri kidogo, mtu siku zinakatika hakuna dalili zozote za kurudi kwa mpenzi wangu.”
“Suzana kwa mganga Njiwa Manga si nilikwenda kwa ajili ya kurudishiwa kizazi?”

“Ndiyo.”
“Basi majibu yametoka.”
“Ina maana wewe ni mjamzito?”
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.36“Ndiyo maana yake.”
“Utani huo.”
“Kweli shoga nimeamini yule babu ni mganga kweli.”
“Kama ni hivyo basi hataki kunisaidia.”
“Amekataa vipi wakati kakueleza ukweli juu ya ramli yake ilivyomuongoza. Ingekuwa hawezi kitu angekwambia japokuwa hajawahi kushindwa matatizo ya majini.”

“Mmh! Kwa hiyo una uhakika kuwa Brighton atarudi bila kufanya dawa yoyote?”
“Kama amekueleza atarudi ujue atarudi, si alikwenda baharini na mbuzi wawili. Kama angekuwa hataki kukusaidia asingeona umuhimu wa kwenda kujisumbua baharini saa nane za usiku.”
“Mmh! Mimi nilijua labda ni njia ya kujitetea tu.”

“Suzana, kwa taarifa nilizozipata kutoka kwa mama, Njiwa Manga kazi ya uganga huu ni mwaka wa thelathini na siyo watu wa hapa tu nchini, kuna watu wanatoka mbali kwa ajili ya kufuata tiba zake. Si hivyo tu, ameshachukuliwa sana na watu wa mbali kwa ajili ya kwenda kufanya matibabu, kuna kipindi alikuwa akiondoka zaidi ya mwaka, kitu ambacho baadaye alikiona kuwa si kizuri kwa watu wengi hukosa huduma zake na kuamua kutosafiri.

“Si wewe hata mimi siku tulipokwenda baharini na hali iliyonitokea kisha kusema eti tayari kizazi changu kimerudi niliona ni uongo. Lakini hali iliyonitokea hivi karibuni na kufanya vipimo vyote na kujiona nina ujauzito nimekubaliana na mama kuwa, kweli mzee Njiwa Manga ni mganga wa kweli.

“Kwa hiyo shoga yangu nakuomba uvumilie kama amekuhakikishia uhai wa mpenzi wako ni mrefu ni kiasi cha kuvuta subira, nina uhakika alichosema kitakuwa kweli.”
“Mmh! Itabidi nikubali lakini moyo haunipi kabisa.”
“Sikuzuii kufikiria hivyo, lakini amini usiamini mzee Njiwa Manga ni mganga wa kweli.”
“Mmh! Haya,” Suzana alikubali kwa shingo upande.

“Basi shoga mguu ulikuwa wako kukujulisha mzee Njiwa Manga amefanya mambo, punguza mawazo kila alilosema mganga litatimia mimi naamini Brighton atarudi bila ya dawa kama alivyosema.”
“Kama alichokisema ni kweli nitampa zawadi kubwa.”
“Hata mimi najiandaa kumpelekea zawadi kubwa, sijui hata nimpelekee nini?”
“Utakachojaaliwa.”

“Shoga baadaye.”
“Sawa, wacha na mimi nianze kazi kidogo umeichangamsha akili yangu bila hivyo siku ya leo ingekuwa ngumu kwangu.”
“Najua hata mimi baada ya kuona mabadiliko ya mwili moyo wangu ndipo ulipofunguka.”
“Wacha na mimi nisubiri.”
Sharifa alirudi ofisini kwake na kumuacha Suzana akijiandaa kuanza kazi za siku ile.
****

Baada ya Balkis kupelekwa katika chumba cha giza, mfalme alionekana kuzidi kukasirika kwa kuona mtoto wake amemkosea adabu. Mkewe muda wote alikuwa ameinama bila kusema kitu, baada ya mwanaye kurudishwa chumba cha giza alimgeukia mumewe na kumuuliza kwa sauti ya ukali ambayo hakutakiwa kuitoa mbele ya mfalme.
“Sasa ulinituma kufanya nini na umefanya nini?”

“Kwanza punguza sauti yako ujue unaongea na nani?”
“Nazungumza na mume wangu na aliyepelekwa katika chumba cha giza ni mwanangu,” bado malkia Huleiya hakushusha sauti yake.
“Unabishana na mimi?” Mfalme aliuliza kwa sauti ya juu.
“Sibishani na wewe kwa vile anayeteseka ni mwanangu.”
“Lakini huoni kama amevunja sheria ya majini pia na wewe unanivunjia adabu kama mumeo na mfalme wako?”

“Nimekuvunjia adabu kivipi wakati nakueleza kitu cha kweli?”
“Kwa hiyo nivunje sheria kwa ajili ya mwanao?”
“Kwani unataka aolewe na jini mwenzake au atoroke?”
“Siwezi kuvunja sheria, majini wengine watanielewa vipi?”

“Kwani si ni wewe ndiye uliyeiweka sheria hii kwa roho mbaya yako baada ya majini wengi kuwa na uhusiano na wanadamu. Umemkataza mwanao asiolewe na mwanadamu, anakuomba umrudishe duniani mpenzi wake hutaki. Kuna faida gani kuwa mfalme wakati huna mapenzi hata na familia yako.”

“Kwa hiyo nawe unaungana na mwanao?”
“Ndiyo na pia nasema hivi, Soobaaa,” malkia Huleiya alimwita mkuu wa watwana msaidizi kwa sauti kubwa.

“Wa nini?” Mfalme Balami aliuliza.
“Naam Malkia mtukufu,” Soba aliitikia akiwa amesimama mbele ya malkia.
“Soba kamtoe haraka Balkis.”
Soba alibakia amesimama na kusita kutekeleza amri hiyo kwa kuhofia kupingana na mfalme.

Ni kweli kauli ya mganga Njiwa Manga itatimia? Mfalme wa majini atasalimu amri kwa mkewe?
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.37

Soba alibakia amesimama kama sanamu, malkia Huleiya alipaza sauti yake tena:
”Soooba hujanielewa, kamtoe haraka Balkis chumba cha giza.”

Bado Soba alibaki amesimama huku akisubiri mfalme ataamua nini baada ya mkewe kutoa amri ya kupingana na mumewe kwa mara ya kwanza. Siku zote alijua mwenye sauti ya mwisho ni mfalme, malkia sauti yake siku zote aliitoa kwa taratibu tena ya chini. Toka awe ndani ya jumba lile la kifalme hakuwahi kusikia amri kali ya malkia.

“Sooooba, unanidharau?” Alimuuliza huku akiteremka sehemu ya juu alipokuwa amesimama pembeni ya mumewe.

Soba bado alisimama kikakamavu kusubiri kauli ya mfalme aende au la, aliamini siku zote mke wa mfalme hakuwa na maamuzi tofauti na mumewe. Kitendo cha Soba kukataa kwenda kumtoa Balkis kilimuudhi sana malkia na kuona umevunjiwa heshima.

Pembeni yake kabla hajafika kwa Soba alichomoa upanga uliokuwa kiunoni kwa mmoja wa walinzi wa nyumba ya mfalme na kulipunga hewani usawa wa shingo ya Soba. Wengi walijua anamtisha ili akubali kumfuata Balkis chumba cha giza alipofungiwa na mumewe.

Soba naye aliendelea kusimama kikakamavu akisubiri kauli ya mfalme aliyekuwa amepata kigugumizi kwa kitendo cha mkewe kumvunjia heshima mbele ya wasaidizi wake na watwana.
Panga alilopunga hewani bila hiyana lilitua kwenye shingo ya Soba na kutenganisha kichwa ni mwili. Kitendo kile kilimtisha kila mmoja aliyekuwepo pale, hata mfalme hakuwahi kuona hasira nzito ya mkewe kama siku ile. Kila mtwana aliyekuwa pembeni yake aliingiwa na mchecheto wa kuhofia maisha yake.

Malkia Huleiya baada ya kuona mwili wa Soba ukianguka chini kama gunia na kichwa kikigaagaa chini, alishtuka kwa kuona ameua, alilitupa upanga chini kisha aliangua kilio na kukimbilia chumbani. Kila tukio lililotokea muda ule lilimshangaza kila mmoja.

Mfalme alijikuta amebaki amesimama kama sanamu asielewe kilichotokea ni kweli au alikuwa akiota. Ulikuwa mwaka wa sabini na tano toka amuoe mkewe aliyekuwa msikivu na mtulivu pia mnyenyekevu kwa mumewe muda wote. Malkia Huleiya siku zote alikuwa kiumbe mwenye huruma na kumkanya mumewe pale anapotumia nguvu bila kutumia muda wa kufikiri katika maamuzi yake ya kutoa adhabu kwa majini yanapofanya kosa.

Lakini siku ile kwa mara ya kwanza alifanya kitendo kilichomshtua kila mmoja aliyemfahamu. Hata adhabu anapotoa mfalme, yeye ndiye aliyesimama kutetea.
Lakini kitendo cha kutenganisha kichwa na kiwiliwili cha jini hakuwahi kukifanya zaidi ya mumewe ambaye kila alipokosewa adhabu yake kubwa ilikuwa kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Kitendo cha mkewe kumuua mtwana mkuu msaidizi aliyekuwa akitegemewa na mfalme baada ya Kulani kuwa kipofu kilimfadhaisha sana.

Alitoka sebuleni na kumfuata mkewe aliyekuwa amejitupa kitandani akilia kwa uchungu huku akijutia kitendo cha kumuua Soba.
Japo Soba alionesha jeuri lakini moyoni alijuta kwa uamuzi mzito alioutoa kwa kumtenganisha kichwa na mwili.

“Malkia wangu,” mfalme Balami alimwita mkewe kwa sauti ya upole.
“Nisamehe mume wangu, nimeshindwa kuzuia hasira zangu, yote ni kwa ajili ya mapenzi mazito kwa mwanetu wa pekee Balkis.”

“Najua mke wangu, lakini kitendo chako kimenifanya nijione nina mke mwenye maamuzi mazito.”

“Hapana sikutarajia kutoa uamuzi mzito kama ule, lakini yote umeyasababisha wewe.”
“Hapana mke wangu, ningejuaje uwezo wa maamuzi yako bila kufanya vile?”
“Si kwa kutoa roho ya kiumbe kisicho na hatia.”

“Ile imeonesha kumbe hata nikiondoka au nikifa hakuna mtu wa kukuchezea, kwa kitendo kile Balkis namtoa kwenye chumba cha giza pia kumrudisha duniani mchumba wake bila masharti.”
“Unasema kweli?” Malkia Huleiya alishtuka kusikia kauli ya mumewe.

“Kweli kabisa, hii itakuwa kama zawadi kwa ujasiri uliouonesha mbele yangu.”
“Asante mume wangu kwa uamuzi wako uliorudisha furaha yangu.”
“Si kurudisha furaha yangu tu bali kuendelea na msimamo huo huo ili kuongeza heshima ndani ya himaya yangu.”

Baada ya makubaliano alitumwa kibaraka kwenda kumtoa Balkis kwenye chumba cha giza lakini aligoma kutoka kama hawatamuachia Brighton. Waliamuliwa kwenda kuwatoa wote, walifanya hivyo na Balkis alikubali kutoka ndani ya chumba cha giza.

Pia alitoa masharti kuwa, kabla ya kuzungumza lolote wahakikishe Brighton anatolewa chini ya maji na kurudishwa duniani. Kwa vile uamuzi ulikuwa amepitishwa ombi lake halikupingwa na baba yake. Lakini kabla ya kurudishwa duniani Brighton alipewa masharti na mfalme kuwa siku atakayoitoa siri ya majini ndiyo siku ya mwisho ya uhai wake.

Baada ya kukubaliana na masharti, Brighton alisindikizwa na watwana kumi baada ya kumfikisha pembeni mwa bahari walimlaza pembeni. Ubaridi wa alfajiri na maji vilimfanya Brighton ashtuke na kujikuta amelala ufukweni, miguu ikiwa majini na mwili nchi kavu. Baada ya kunyanyuka alipokuwa amesimama kwa mshtuko. Aliifahamu sehemu ile ilikuwa ni eneo la daraja ya Salenda.

Baada ya kujinyanyua alipokuwa amekaa, alitembea kuelekea barabarani ili apate lifti ya kumrudisha kwake.

Je, kurudi kwa Brighton ndiyo mwisho wa Balkis kuchukua wanaume wa kibinadamu?
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.38Brighton alitembea kusogea barabarani kwa mwendo wa taratibu kutokana na mwili wake kukosa nguvu. Alikuwa akitembea kwa mwendo wa kuyumba yumba hadi alipofika chini ya mti uliokuwa pembezoni mwa barabara na kuuegemea kutokana na kuishiwa nguvu.

Suzana akiwa kwenye gari lake akielekea kazini, alishtuka kuona kitu ambacho hakukitegemea kwa muda ule. Roho ilimwambia aamini kitu anachokiona lakini akili ya kawaida ilikataa kwa kuamini kitu kile. Baada ya kuvuka eneo lile bado roho ilimwambia kuwa kitu alichokiona ndicho chenyewe.

Alisimamisha gari na kuliegesha pembeni, kisha aliteremka kwenye gari na kurudi sehemu alipomuona mtu aliyemfananisha. Alitembea taratibu hadi sehemu ile alipokiona kitu alichokifananisha. Brighton alikuwa kama mtu aliyelewa pombe kutokana na kuzidi kuishiwa nguvu.

Suzana alipomkaribia, alipunguza kasi ya mwendo wake zaidi huku akimkazia macho mtu yule, alipomsogelea karibu aligundua aliyekuwa mbele yake ni kipenzi chake Brighton.
“Brighton,” alimwita kwa sauti ya juu japo hakuwa mbali naye.
Brighton alinyanyua kichwa na kumtazama aliyekuwa akimwita, macho yake yaliona maluweluwe japo alimfahamu aliyekuwa mbele yake.

“Brighton,” Suzana alimwita tena huku akiogopa kumgusa.
“Suzana,” Brighton alimwita baada ya kuitambua sura ya mpenzi wake.
“Ni wewe Brigton?”
“Ni mimi Suzana umejuaje kama nipo hapa?”
“Ha! Siamini,” Suzana alimvamia Brigton na kumkumbatia kwa furaha.

“Ni mimi mpenzi wangu,” Brighton alisema huku akitokwa na machozi.
“Hapana Brighton, twende nyumbani,” alimshika mkono na kwenda naye kwenye gari.
Suzana aliligeuza gari na kurudi nyumbani kwake kwa kuwa alijua nyumbani kwa Brighton kusingekuwa katika hali ya usafi baada ya nyumba kukaa kipindi kirefu bila ya matunzo. Alipofika nyumbani alimtengea maji ya kuoga, kisha akamtayarishia chakula.

Baada ya kula Brighton alionekana kuwa na uchovu, aliamua kujilaza na usingizi mzito ukamchukua. Suzana alijikuta akiahirisha kwenda kazini ili aweze kuwa karibu na mpenzi wake aliyemtafuta kama maji kwenye ardhi kame.

Alijikuta akiyakumbuka maelezo ya mganga Njiwa kuwa, Brighton angerudi bila tiba yoyote, hamu yake kubwa alitaka kujua mpenzi wake alikuwa wapi na aliishi maisha gani. Alijikuta akisahau hata kutuma ujumbe kazini kuwaarifu mabosi wake kama amepata dharura, muda mwingi alimuangalia mpenzi wake aliyekuwa amelala.

Alimpapasa akiwa haamini kama kweli mtu aliyekuwa amechukuliwa na majini angeweza kurudi salama. Akiwa katika dimbwi la mawazo simu yake iliita. Alipoangalia juu ya kioo aliliona jina la Sharifa.
“Haloo Sharifa.”
“Suzana, upo sawa?”
“Nipo sawa.”

“Mbona hujaonekana kazini?”
“Huwezi kuamini yaliyosemwa yametimia?’
“Yepi hayo?”
“Brighton amerudi.”
“Acha utani!”

“Kweli kabisa na sasa hivi nipo pembeni yake.”
“Suzana hebu acha kunirusha roho.”
“Sharifa, naamini kabisa mzee Njiwa Manga ni mganga wa kweli.”
“Si ulikuwa unamuona tapeli.”
“Wee dada wee, kuchanganyikiwa kubaya.”

“Kwa hiyo kazini itakuwaje?”
“Naomba uniombee ruhusa kuwa naumwa nitakuja kuchukua ‘sick sheet’ baadaye.”
“Mmh! Huwezi kuamini furaha niliyoipata leo haina kifani ili kujiridhisha na maneno yako nitaomba ruhusa kuja kumuona shemeji.”

“Njoo dada umuone, huwezi kuamini amerudi amenenepa na kupendeza.”
“Basi nakuja na sick sheet yako kabisa.”
“Utakuwa umefanya jambo la mbolea.”
“Basi nakuja,” Sharifa alionekana kuwa na mshawasha wa kumuona Brighton.

****
Baada ya kutolewa kwa mpenzi wake chini ya bahari, Balkis alifurahi sana na kukubaliana na wazazi wake kurudi duniani kutafuta tena vizazi. Kitendo cha kukubali kulimfanya mfalme afanye sherehe kubwa ya kumuaga kwa mara ya pili. Sherehe ilifanyika juu ya bahari.

Majira ya saa saba za usiku Balkis aliagwa eneo la bahari na kuingia duniani kwa mara nyingine tena. Aliondoka eneo lile kwa kutembea taratibu pembeni mwa barabara eneo la Daraja la Salenda kuelekea maeneo wanayoishi binadamu. Alipokaribia njia panda ya Masaki aliona gari dogo likisimama ghafla na kuteremka mwanamke na baadaye akafuatia mwanaume.

Balkis amerudi tena duniani, nini kitatokea?
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.39

Hakutaka kujionesha kwao, alisimama pembeni yao aone kuna nini. Cha kwanza kilichomvutia kilikuwa tumbo lililoonesha ujauzito la mwanamke aliyetoka kwenye gari. Kingine kilikuwa sura na mvuto wa mwanaume aliyefuatia. Mwanamke alionekana mwenye hasira sana kutokana na maneno yake.

“Umenifuata ili iweje? Nimekwambia niache na maisha yangu na ujauzito huu nautoa.”
“Lakini mbona umefikia huko mke wangu?”
“Wewe si unaniona mimi si mwaminifu, basi kwa taarifa yako kuanzia leo achana na mimi.”

“Mke wangu mimi mumeo nina haki ya kukuuliza jambo lolote linalokwenda kinyume na maadili ya ndoa.”
“Kama umeniona nimetoka nje ya maadili ya ndoa si uniache.”
“Siwezi kukuacha kwa vile bado ni mke wangu.”

“Kwani ndoa lazima, ukiona hivyo ujue sina shida na wewe.”
Mwanamke alionesha jeuri kwa mumewe, Balkis alitulia ajue mwisho wake.
“Mke wangu bado tuna nafasi ya kulizungumza hili,” mwanaume alimbembeleza mkewe.
“Ngoja nikueleze kitu, ujauzito huu sio wako na mwenye ujauzito huo utamuona muda si mrefu.”

“Mke wangu umefikia hivyo?”
“Ulikuwa hujui?”
“Usifanye hivyo mke wangu bado nakupenda sana.”
“Mimi sikupendi,” mwanamke alisema huku akifunua simu na kupiga namba, alimsikia akizungumza.

“Eeh... nipo njia panda ya Masaki... njoo utanikuta.”
“Mke wangu unampigia simu nani?”
“Mume mwenzio anayejua kulea asiye na gubu kama wewe.”
“Mke wangu ni maneno gani hayo?”
“Najua litakuuma na mwaka huu wako, kama ulimwacha mkeo kwa ajili yangu sasa imekula kwako.”

Maneno yale yalimchoma sana Balkis aliyekuwa amesimama pembeni yao akifuatilia mazungumzo yale. Alimuonea huruma mwanaume aliyekuwa akimbembeza mwanamke mpaka kumpigia magoti na machozi yakimtoka. Alitamani kuingilia ugomvi ule lakini hakuna ambaye angemuelewa kwa muda ule kutokea mbele yao.

Alitulia kufuatilia mazungumzo yale bila kuzungumza chochote, mwanaume akiwa bado anaendelea kumbembeleza mkewe, gari aina Toyota VX lilisimama pembeni ya gari la wanandoa wale.
Baada ya kusimama aliteremka mwanaume mwenye mwili uliojengeka kimazoezi aliyekuwa amevaa bukta na fulana ya mikanda. Yule mwanamke alimsukuma mwanaume aliyekuwa amepiga magoti na kumfuata aliyekuja na VX.

“Vipi Sweet?” aliuliza yule mwanaume.
“Si huyu bwege ndiyo anayeniwekea usiku.”
Walizungumza wakiwa wamekumbatiana pembeni ya mwenye mke aliyekuwa bado amekaa chini baada ya kusukumwa na mkewe. Kitendo kile kilimtoa machozi Balkis na kuapa kuwashikisha adabu.
“Pole sweet, twende zetu.”

Walishikana mikono na kwenda ndani ya gari na kumuacha mwanaume akilia kwa uchungu huku akizungumza maneno yaliyokwenda na upepo lakini Balkis aliyasikia.
“Kweli mwanamke shetani yaani yote niliyokufanyia umeniona sifai, nimekosana na familia yangu kwa ajili yako. Mwisho unanivua nguo mbele za watu, sioni faida ya kuishi bora nife.”

Kauli ile ilimtoa machozi Balkis na kuona jinsi gani wanawake wanavyoweza kuwaingiza wanaume kwenye matatizo. Alimuona yule mwanaume kama mtu aliyechanganyikiwa akienda ndani ya gari na kutoka na kipande cha kamba ili ajinyonge.

Alisogea kwenye mti wa pembeni na kuifunga ile kamba, akatafuta tawi zuri ambalo alifunga kamba ili ajinyonge. Kabla hajajitundika Balkis alijitokeza mbele yake, jamaa alishtuka kumuona mwanamke mzuri kasimama mbele yake usiku ule wa manane. Alipomuona alisogea pembeni ya kamba ili Balkis asijue kama alikuwa anataka kujinyonga.
“Mudy kwa nini unataka kujiua?” Balkis alimuuliza.

Balkis atamuacha Mudy ajiue nini adhabu ya mke wa Mudy? Kuyajua yote tukutane Risasi Jumatano.
Mudy kama alivyoitwa na Balkis alishangaa kuona mwanamke mzuri mbele yake usiku ule tena akimfahamu kiufasaha.
“Umenijuaje?” alimuuliza.

“Kukujua si muhimu kuliko kujibu swali langu kwa nini unataka kujinyonga?”
“Nani kakwambia?”
“Mudy niambiwe na nani wakati naiona kamba ikining’inia?”
“Basi tu nimeamua.”

”Uamue nini wakati umekataliwa na mkeo.”
“Wewe umejuaje?”
“Kwani uongo?”
“Hata kama si uongo wewe umejuaje na usiku kama huu unatoka wapi huogopi?”
“Mudy si muda wa kutaka kujua nimejuaje au natoka wapi? Unataka kuniambia wanawake wamekwisha mpaka umng’ang’anie mwanamke asiyekupenda?”

“Sio kumng’ang’ania, bali kanitia umaskini wa kutumia fedha nyingi kwa ajili yake.”
“Sikiliza Mudy, ulitakiwa kumshukuru Mungu kwa kukuonesha hili mapema, au ulitaka ufilisike kabisa ndiyo akuache.”
“Kama hivi nimekosana na ndugu na jamaa zangu kwa ajili yake wakisikia ameniacha nitakuwa mgeni wa nani?”

“Sikiliza Mudy, hakuna mtu anayechukiwa milele, kama utaomba msamaha watakusamehe.”
“Mmh! Kwangu ni ngumu, kuwa na mwanamke yule niligeuka adui wa familia, wote waliniombea mabaya. Leo wasikie si utakuwa sherehe, kwa vile hunijui sikujui kwa nini usiniache nitimize dhamira yangu?” Mudy alimuomba Balkis amuache ajiue.

Balkis atamuacha Mudy ajiue nini adhabu ya mke wa Mudy?
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.40“Sina budi kufanya hivyo.”
“Sikiliza Muddy, ulitakiwa kumshukuru Mungu kwa kukuonesha jambo hili mapema, au ulitaka hadi ufilisike ndipo mkeo akuache?”

“Nimekosana na ndugu na jamaa zangu kwa ajili yake, wakisikia ameniacha nitakuwa mgeni wa nani?”
“Sikiliza Muddy, hakuna mtu anayechukiwa milele, kama utawaomba msamaha ndugu na jamaa zako watakusamehe.”

“Mmh! Kwangu ni vigumu, kwa kuwa mwanamke yule alinifanya niwe adui wa familia, wote waliniombea mabaya. Leo wakisikia si itakuwa sherehe, kwa vile hunijui sikujui kwa nini usiniache nitimize dhamira yangu?” Muddy alimuomba Balkis.

“Inawezekana wewe ndiye hunijui lakini mimi nakujua vizuri, toka ulipoanza maisha ya shida, hadi pale mpenzi wako wa kwanza alipoiba fedha kwao zilizokufanya upate utajiri na kukuvimbisha kichwa kwa dharau na kukufanya uwatelekeze mkeo na mtoto wako.

“Mkeo kwa aibu kutokana na kuidharau ya familia yake, baada ya kumtelekeza aliamua kunywa sumu pamoja na mtoto wake. Kwa vile ulikosa shukrani wala fadhila, kifo cha mkeo na mtoto wala hakikuugusa moyoni mwako, ukaamua kuendelea na maisha yako na mpenzio mpya ambaye mlifunga ndoa ndani ya wiki tatu baada ya vifo hivyo.

“Fedha zilikupa jeuri na kudharau wazazi na nduguzo waliokueleza tabia chafu za mkeo, kwako uliona kama wanaleta fitina ili muachane. Lakini ukweli uliuona baada mambo kuanza kukuendelea kombo, mke uliyemuoa tabia yake ni kuharibu ndoa za watu baada ya kukufilisi mwisho wake ndiyo kama ulivyokuwa ukitaka kufanya.

“Lakini kwa tabia hiyo nitawakomesha, siwezi kuona familia zinahangaika kwa ajili ya upumbavu wa watu wachahe,” Balkis alisema kwa sauti ya hasira.
“Kwani dada wewe ni nani na utawakomesha vipi?”
“Utajua muda si mrefu.”

“Samahani dada yangu wewe ni nani maana unanijua vizuri kuliko hata watu wangu wa karibu.”
“Naitwa Balkis.”
“Hii siri yangu nani kakwambia?”
“Narudia tena usitake kumjua aliyeniambia,zaidi ya kujua ubaya wa mtu uliyekuwa naye. Kwa mchezo wake ndoa yako ni ya tano kuvunjwa na yeye na kila alipopita aliacha msiba, ningechelewa kidogo jina lako lingebaki historia midomoni mwa watu.”

“Mmh! Wewe huku unatoka wapi usiku huu?”
“Kwetu siyo mbali naomba ikiwezekana ukalale kwa vile najua huwezi kuendesha gari kutokana na kuchanganyikiwa. Ningekuwa nimeaga nyumbani ningekupeleka kwako.”
“Unataka nikalale kwako na mumeo?” Muddy aliuliza.

“Sijaolewa.”
“Unakaa na nani?”
“Nipo na wazazi wangu.”
“Ulijuaje kuna tukio hili?”

“Nilipokuwa nimelala nilisikia mkibishana, nikatoka ndani na kusogea hadi pembeni yenu kwa vile kila mmoja alikuwa na hasira hamkuweza kuniona. Nilipowaona niliwatambua kutokana na maelezo ya watu juu ya matatizo yenu ya ndoa kutokana na kuijua tabia ya mkeo toka zamani.

“Mambo mengi nilikuwa nayajua, nilipotoka nje na kuwakuta sikushangaa kusikia tambo za mkeo. Baada ya kuondoka nilijua nini kinafuata, nilijua utataka kujinyonga tu kama walivyofanya wanaume wengi walioachwa kama wewe. Kwa vile ulikuwa hujui upande wa pili wa mkeo.

“Hata mkeo alipoondoka anaamini kabisa uamuzi utakaochukua ni huo, hushangai alikueleza uchukue kamba bila kukupa maelekezo. Kesho anasubiri kusikia kifo chako na kuchukua vitu vyako vyote bila familia yako kuambulia chochote.

“Na hata akisikia hujafa lazima atafungua kesi ya kudai mgawane mali kuhakikisha anakufilisi kabisa. Utavumilia lakini mwisho wake ni kujiua kwa sumu au kamba.

“Niliona kuna umuhimu wa kukueleza kilichokuzunguka katika ndoa yako, yule si mwanamke ila ni mwizi tena muuaji. Hebu niangalie mimi nilivyo mrembo, yule mkeo tapeli ananifikia?” Balkis alimuuliza Muddy huku akijigeuza na kupigwa na mwanga wa taa za barabarani.

“Hawezi kukufikia.”
“Sasa mwanamke kama mimi nikikupa penzi la kweli bila kuhitaji fedha zako unasemaje?”
“Unataka kuniambia mwanamke mzuri kama wewe hujaolewa?”
“Sijaolewa bado nipo kwa wazazi wangu kama nilivyokueleza awali.”

”Maeneo haya unakaa nyumba gani?”
“Ingia kwenye gari nikakuoneshe.”
Muddy aliingia kwenye gari na Balkis naye aliingia upande wa dereva na kuanza kuendesha gari. Baada ya mwendo mdogo gari lilikata kushoto na kuingia kwenye jumba la kifahari.

Muddy pamoja na kuwa mwenyeji wa eneo lile lililopo karibu na Daraja la Salenda hakuwahi kuliona jumba zuri la kifahari. Baada ya gari kuingia katika jumba lile ambalo toka azaliwe hakuwahi kuingia, Balkis alimkaribisha hadi chumbani.

“Karibu mpenzi nikupoze machungu yote.”
“Asante.”
Balkis alimshika mkono Muddy na kumuongoza, hakuamini mahaba aliyooneshwa na Balkis mwanamke mwenye uzuri wa ajabu.

Nini hatima ya Muddy mikononi mwa Balkis? Kuyajua yote tukutane kesho hapa hapa UNLIMITED SWAGGAZZ!!!!!
*story unaionaje?
*mpk sasa umejifunza nini?
*je tufanyeje ili kuepukana na balaa km hili???
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.41.


ILIPOISHIA:
“Karibu mpenzi nikupoze machungu yote.”
“Asante.”
Balkis alimshika mkono Mudy na kuingia naye ndani, Mudy hakuamini mahaba aliyooneshwa na Balkis, mwanamke mwenye uzuri wa ajabu.
SASA ENDELEA...

Muddy aliingizwa kwenye jumba la kifahari lililokuwa na mapambo ghali ambayo aliwahi kuyaona katika picha za majumba ya Falme za Kiarabu.
“Karibu sana.”
“Asante.”

“Muddy naomba ukaoge kwanza ndipo tupumzike.”
Muddy alinyanyuka na kupelekwa kwenye bwawa la kuogelea lililokuwa mbele ya nyumba. Baada ya kuoga alipewa taulo laini la sufu na kupewa makubazi ya kuvaa kisha alirudi ndani. Kwa vile usiku ulikuwa umeingia sana alipelekwa moja kwa moja kitandani.

Kila mmoja alilala chumba chake, Muddy alilala usingizi mzuri ajabu ambao hakuwahi kulala katika maisha yake. Alijikuta akitamani siku moja aishi maisha kama yale. Balkis aliingia katika mawazo ya Muddy na kuamini kama atatumia udhaifu ule basi atampata kirahisi.

Majira ya saa kumi na nusu za usiku Balkis alimuamsha Muddy kisha alimpa chai yenye viungo na kumueleza:
“Muddy muda wa kurudi baba yangu umekaribia, naomba nikurudishe kwako.”

“Mmh! Sawa lakini bila ya baba yako nisingeamka mapema sijawahi kulala usingizi mtamu kama leo.”
“Muddy, jitahidi kumuondoa akilini mkeo tapeli ambaye hatarudi kwako tena baada ya kukamilisha kilichomleta. Ukimuona anarudi ujue anaifuata roho yako. Kama utaachana naye nakuhakikishia kuishi maisha mazuri. Kama utakuwa mkweli na mwaminifu, nitayabadilisha maisha yako,” Balkis alimueleza Muddy ambaye hakuamini nguo zake kufuliwa usiku ule na kupigwa pasi kisha kupuliziwa manukato.

“Kama unayosema ni kweli mke wangu hatarudi basi, nitakuwa na wewe.”
“Muddy usitake kuniudhi, wewe ni mwanaume gani mkeo anachukuliwa mbele yako unaishia kulia, kwa kinywa chake kakueleza hakutaki, unataka upate ukweli gani?”

“Ni kweli usemayo, lakini kumbuka yule bado ni mke wangu, hivyo tunaweza kuzungumza na kuyamaliza.”
“Muddy nikueleze mara ngapi? Siku utakayorudiana na mkeo ujue ndiyo siku ya mauti yako. Wewe si mtu wa kwanza kufanyiwa hivyo, kama huamini kesho utaletewa karatasi itakayokutaka ufike mahakamani kwa ajili ya madai ya kugawana kidogo ulichobakia nacho.

“ Kibaya ni kwamba una deni la mkeo ambalo litasababisha usipate hata fedha nusu ya kuuza vitu vyenu. Kwa vile hukujua deni alilokukopesha riba yake inazidi thamani ya vitu ulivyobakia navyo.
“Kwa vile ni mzoefu wa mchezo ule, lazima atashinda kesi na wewe utachanganyikiwa, kitakachofuatia itakuwa ni kuokota makopo. Inawezekana una masikio ya kenge mpaka utoke damu ndipo usikie, usinitafute wala ukiniona usinifuate.”
“Sasa dada utanisaidiaje?”

“Niite Balkis.”
“Sasa Balkis utanisaidiaje?”
“Nakuomba chochote atakachokifanya asikushtue, wewe kubaliana nacho, mimi nitakuwepo mahakamani siku ya mwisho.”

“Nitashukuru.”
“Basi acha nikuwahishe kabla baba hajarudi.”
Walitoka na kuingia kwenye gari, kisha Muddy aliendesha kurudi nyumbani kwake baada ya akili yake kuwa imetulia kidogo. Alipofika waliingia wote ndani, Balkis hakukaa sana aliondoka na kumuacha Muddy amalizie usingizi.

***
Muddy alishtuka saa nne asubuhi na kujikuta akiwa na mawazo juu ya matukio yaliyomtokea jana ya kuachwa na mkewe pia kukutana na mwanamke mrembo mwenye mapenzi na huruma, Balkis. Pamoja na kuoneshwa ukarimu wa hali ya juu bado kitendo cha mkewe kumkataa kilimuumiza na kukumbuka vitu vingi alivyopoteza kwa ajili yake.

Alikumbuka jinsi alivyotelekeza familia yake kwa ajili yule mwanamke na kusababisha kupoteza mke na watoto. Bado hiyo haikutosha, aliweza kutumia fedha nyingi alizowekeza mke wake wa kwanza vibaya kiasi cha kumtia katika umaskini.

Pia alisababisha kutengwa na familia yake na kuwa adui yao mkubwa baada ya kugoma kutoa fedha za matibabu zilizosababisha dada yake mkubwa kupoteza maisha baada kukatazwa na mkewe asitoe kitu.
Kila alipokuwa akifikiria yote yale moyo ulikosa amani, aliamini njia nyepesi ya kukimbia aibu ile ni kunywa sumu au kujinyonga. Akiwa katikati ya uamuzi mzito, hodi mlangoni iliyahamisha mawazo yake yaliyokuwa yamefanya atokwe na machozi na macho kuwa mekundu kutokana na maumivu ya moyo.
Alifuta machozi na kwenda hadi mlangoni na kufungua, alikutana na kijana mtanashati.

“Karibu,”
“Asante, siingii ndani natoka mahakama ya mwanzo kuna barua ya madai toka kwa aliyekuwa mkeo.”
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.42.LAKINI likatokea jambo la ajabu, Muddy kila alipokuwa akikitafuta kisu hakukiona. Alihangaika nyumba nzima, hakukiona. Wazo lingine lilikuwa ni kutafuta kamba ili ajinyonge, vile vile alishangaa kuikosa kamba hata ile aliyotaka kujinyongea usiku na kuiacha kwenye gari, alipoifuata pia hakuikuta.

Hakurudi ndani, alikwenda dukani na kuchukua sumu ya panya, aliichanganya katika chupa ya maji ya kunywa kisha akanywa yote na kwenda kulala akisubiri malaika wa kifo amchukue.
***
Ashura mke wa Muddy alikuwa mwenye furaha, yeye pamoja na mwanaume wake walikuwa wakipongezana kwa kazi kubwa waliyoifanya ya kumfilisi Muddy.
“Nina imani kazi imekwenda vizuri,” mwanaume huyo alisema.

“Ni kweli, lakini pamoja na kuyafanya yote bado namuonea huruma Muddy. Kwa nini tusimuachie gari na nyumba?” Ashura alisema katika hali ya kumuonea huruma Muddy.
“Tukiwa na huruma hatuwezi kuifanya kazi hii, ona leo tulivyo na utajiri wa kutisha.”
“Mmh! Kweli.”

Wakati Ashura na mwanaume wake wakiwa katikati ya mazungumzo, mlango uligongwa. Wote walikaa kimya kusikiliza, mlango ulipogongwa tena mwanaume alinyanyuka na kwenda mlangoni. Alipoufungua alikutana uso kwa uso na Balkis, akamkaribisha.
“Karibu mrembo.”

“Ahsante sijui Ashura anakaa hapa?”
“Wewe nani?”
“Sasa kaka yangu badala ya kunijibu, unaniuliza mimi nani?”

“Eeh, si vibaya kukujua wewe ni nani kwa vile unayemuuliza ni mke wangu na wewe ni mgeni kwangu.”
“Mimi naitwa Balkis, ina maana Ashura ameshaachana na Muddy?” Balkis aliuliza swali la uongo.
“Hiyo haikuhusu, sema kilichokuleta.”
“Kilichonileta ni kuonana na Ashura.”
“Karibu ndani.”

Alimkaribisha sebuleni ambapo alimkuta Ashura amejilaza kwenye kochi. Ashura alimshangaa yule mgeni kutokana na uzuri wake wa ajabu, pia vito vya thamani alivyovaa mwilini mwake. Hata manukato yake yalikuwa mageni puani ambayo yaliifanya nyumba nzima kunukia.
“Habari Ashura?”

“Nzuri, umenijuaje?”
“Ina maana jina lako ni siri? Wanapaswa kulijua watu wachache?”
“Siyo kwamba ni siri ila sikujui.”
“Huwezi kuwajua wote mdogo wangu.”
“Mh! Nikusaidie nini?”
“Nimetumwa na Muddy.”
“Muddy! Muddy ndiye nani?”
“Mumeo.”

“Mimi nina mwanaume anayeitwa Muddy?”
“Sasa unashangaa au unakataa? Ndoa yako na Muddy imevunjika lini wakati mpaka jana usiku majira ya saa sita mmenipita Daraja la Salenda mkiwa pamoja, leo hii unamkana?”
“Basi muda mfupi baada ya kutuona wewe ndipo tulipoachana.”
“Sasa nani kamuacha mwenzake?”
“Maswali gani hayo?”

“Ndiyo maana nipo hapa,” Balkis alisema kwa kujiamini.
“Wewe ni nani kwa Muddy?” Ashura alihamaki.
“Kabla sijakujibu nataka useme ukweli mbele ya mwanaume wako, upo tayari kurudiana na Muddy?”
“Sipo tayari.”

“Na ukirudiana naye tena?”
“Nitembee uchi.”
“Rudia.”
“Nitembee uchi.”
“Kaka umesikia?” Balkis alimgeukia mwanaume wa Ashura na kumuuliza.
“Umesikia?”

“Kuwa?”hi akirudiana na Muddy.”
“Basi ni hayo niliyofuata hapa.”
“Mbona umeniuliza hivyo?” Swali la Balkis lilimtisha Ashura.
“Si umeachana na Muddy?”

“Ndiyo, nirudiane naye kwa kitu gani alichonacho, tena muda si mrefu ataokota makopo.”
“Usiokote makopo wewe, tena kabla sijaondoka nawapeni onyo mchezo wenu wa kudhulumu mali za watu utawatokea puani,”
Balkis alimweleza Ashura ambaye bado alikuwa akimshangaa kwa maswali yake.

Nini kiliendelea? Fuatilia katika Gazeti la Risasi Jumamosi.
Vituko
ndani ya daladala
Abiria wawili ambao majina yao hayakujulikana, juzikati walitwangana makonde mazito baada ya mmoja wao kutoa nauli ya shilingi 200 badala ya 300.

Abiria wa kwanza alipanda daladala hiyo Buguruni akielekea Gongo la Mboto na wa pili Vigunguti.
Kondakta alipoanza kutoza nauli, abiria wa kwanza alitoa shilingi 200. Kitendo hicho kilionekana kumkera abiria wa pili kwa kumwambia kwa nini katoa nauli nusu.

Abiria hao walianza kuzozana na kondakta akaungana na kauli ya abiria wa pili ya kumtaka wa kwanza kutoa shilingi 300 na si 200.
Hali hiyo ilionekana kumkera abiria wa kwanza na kuamua kumrushia ngumi abiria wa pili. Kitendo cha abiria huyo kurusha konde kilisababisha timbwili kali kwa washkaji hao kuanza kutwangana kavukavu.

Mbaya zaidi abiria wa kwanza alikuwa amekaa kiti cha mbele na walipoanza kurushiana makonde mazito gari lilianza kuyumba na kusababisha abiri wengine kuanza kupiga kelele ya kumuomba dereva asimamishe gari.

“Dereva simamisha gari utatuua, tunakuomba sana tumeshinda salama tunataka tufike nyumbani tukiwa wazima, tafadhali,” alisikika abiria mmoja huku wengine wakimuomba Mungu awaepushe na balaa hilo.

Wakati abiria wakipiga kelele, daladala hilo ilikuwa mwendo mkali. “Jamani mnataka kutuua kwa sababu ya shilingi 100? Acheni kugombana nitampa konda,” jamaa mmoja alisikika akisema.
Gari liliposimama jamaa hao walishuka na kuanza kukunjana vema na abiria wengine wakaingia ndani ya gari na kumwambia dereva aendeshe.
Mabondi hao wasiotambuliwa na shirikisho la ngumi Bongo waliachwa kituoni hapo wakitifuana.
 
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.43.


Muddy alishtuliwa katika usingizi mzito na sauti ya Balkis, aliposhtuka alijishangaa kujiona bado yupo hai hakufa kama alivyodhamilia.
“Muddy vipi?”
Muddy hakumjibu alimshangaa Balkis aliyekuwa ameshikilia barua mkononi.

“Muddy mbona unanuka sumu ya panya?”
Bado Muddy hakuwa najibu aliendelea kupepesa macho na kuitazama glasi aliyokunywa sumu ilikuwa juu ya sturi.
“Muddy kwa nini unataka kujiua?” Balkis alimuuliza akiwa ameshika glasi iliyokuwa na sumu.
“Umejuaje?”

“Muddy nikufundishe mara ngapi swali mwenzake jibu na si swali kwa swali.”
“Umeisoma hiyo barua?”
“Niisome ili iwe nini, haya nilikueleza tokea awali kwa nini hutaki kunielewa?”
“Samahani Balkis nimechanganyikiwa.”

“Nilikueleza toka awali hutakufa bali unaelekea kwenye wendawazimu na usiponisikiliza sasa hivi utaokota makopo.”
Muddy alishangaa jinsi Balkis mwanamke mrembo mara kumi Ashura ameonesha mapenzi ya kweli kwake. Kingine kilikuwa uelewa wa ajabu wa Balkis kuonekana kumfahamu vizuri yeye na Ashura bila kuhadithiwa na mtu.

Hatua ya kupelekwa mahakamani ili wakagawane vitu pia deni la mkewe lililokuwa likizaa liba kila kukicha lilizidi kumchanganya. Alijikuta akinyanyuka na kuketi kwenye kitanda na kumuuliza Balkis.
“Balkis unaonekana unajua mambo mengi juu yangu ya Ashura?”
“Ndiyo maana nipo hapa kuokoa maisha yako, kwa vile lengo la mkeo wa uongo limetimia.”
“Yote haya umeyajulia wapi?”

“Utajua ukinipa moyo wako uliojeruhiwa niuponye.”
“Kwa ukweli niliouona nipo tayari kukukabidhi moyo wangu.”
“Je, Ashura akirudi kukubembeleza?”
“Kwa uliyonieleza siwezi kurudiana na mwanamke yule ambaye kwangu ni muuaji.”

“Nakuhakikishia kama utakuwa mkweli nitayabadili maisha yako, lakini chonde unigeuke baada ya kuwa na maisha mazuri utanisamehe.”
“Nikuhakikishia nitakupenda kwa moyo wangu wote, najiona kiumbe mwenye bahati kupendwa na mwanamke mrembo tena mwenye maisha mazuri. Nakuapia kukupenda mapenzi ya dhati.”
“Asante Muddy.”
***
Balkis baada ya kujua Muddy ataletewa barua ya kuitwa mahakamani aliingia ndani kwa Muddy bila kuonekana na kwenda kukaa sebuleni kusubiri kitakacho tokea. Baada ya barua kuletwa na kukabidhiwa Muddy, alijua nini kitafuata. Baada ya kuisoma na kuonekana amechananyikiwa alitumia muda ule kuficha kila kitu ambacho angetumia kwa ajili ya kujitoa uhai. Hata alipokwenda dukani aliyemuuzia sumu ya panya, Balkis alijigeuza na kumuuzia kitu kingine kisicho na madhara yoyote.

Kwa vile alikuwa amechanganyikiwa hakuichumza aliiweka kwenye glasi na kuichanganya na kuinywa kisha aliinywa. Lakini Balkis alikuwa amemuwekea dawa za usingizi ambazo zilimlevya baada ya kunywa na kulala usingizi mzito. Baada ya kumuona amelala, ndipo alimpomwacha na kwenda kwa Ashura mke wa Muddy.
******
Siku ya pili Muddy alifika mahakama kama ilivyopangwa, baada ya kesi kusikilizwa iliahilishwa wiki moja. Muddy alishangaa kutomuona Balkis mahakamani, baada ya kutoka mahakamani aliamua kwenda nyumbani kwao Balkis ili akajue nini kimemsibu baada ya kukosekana asubuhi ile kama alivyomuahidi kufika. Aliendesha gari lake ambalo kutokana na maelezo ya Balkis kuwa litapigwa mnada pamoja na nyumba na kugawana fedha zake, ambazo nazo zitachukuliwa na mtalaka wake na kumuacha bila kitu.

Njia nzima alikuwa na mawazo juu ya hatima ya maisha yake kama atanyang’nywa kila kitu. Alipofika maeneo ya Daraja la Salenda alitembea taratibu kuitafuta nyumba ya kina Balkis ambayo aliamini ilikuwa maeneo yale.
Lakini alijikuta akichanganyikiwa kutoliona jumba la kifahari alilopelekwa na Balkis. Mawazo yake yaliamini huenda amekosea eneo.

Kutaka kupata uhakika wa sehemu aliyopelekwa usiku na Balkis, aliendesha gari mpaka sehemu waliyotelemka na mkewe usiku. Alipofika pale alirudi taratibu huku akipepesa macho kuangalia labda ataliona jumba la kifahari. Lakini hakuona chochote zaidi ya miti na bahari kwa nyuma.

Alijikuta akijiuliza lile jumba alilolala mbona halionekani, alipanda ndani ya gari na kuanza kulitafuta kwa kuendesha gari taratibu kuelekea Masaki labda ataliona jumba lile. Aliendesha gari taratibu huku akipepesa macho labda ataliona jumba la kifahari kama lile ambao katika maisha yake hakuwahi kuona.

Lakini gari lilizidi kwenda bila kuliona, majumba mengi alioyaona yalikuwa mazuri lakini hayakuweza kufikia hata robo ya uzuri wa jumba la kina Balkis Ambalo lilikuwa na eneo kubwa tofauti na majumba yaliyokuwa yamepangana pia maeneo yake yalikuwa madogo.

Mpaka anafika Sea cliff Hotel hakuona jumba lile alilopelekwa na Balkis, aliamini kabisa atakuwa amekosea tu. Aligeuza gari na kurudi tena hadi sehemu aliyoachwa na mkewe usiku na kuonana na Balkis. Aliamua kutelemka kwenye gari na kutembea kwa miguu kufuata njia aliyopelekwa na Balkis, alikumbuka hakwenda njia ya Masaki bali alirudi kama anakwenda Daraja la Salenda.

Muddy alitembea taratibu huku akipepesa macho huenda akaliona jumba lile la kifahari, lakini mpaka anavuka Daraja la Salenda bado hakuona jumba lile.
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.44.


Hakukata tamaa alitembea hadi Agha Khan, pia nyumba zilikuwa zile zile za siku zote alizozizoea. Baada ya kutembea kwa muda mrefu alijikuta akichoka sana na kuamua kurudi taratibu kulifuata gari lake ili arudi nyumbani. Alitembea kwa mwendo wa kivivu huku kiu na njaa ikiwa kali.

Alimwita muuza maji ambaye alimletea maji, alikunywa kidogo na mengine alijimwagia kichwani kupunguza uchovu. Lakini ilikuwa tofauti na alivyofikiria, alihisi usingizi wa ajabu na mwili kuchoka maradufu. Alitafuta mti wa kivuli uliokuwa pembeni ya bahari na kujilaza chini yake.

Usingizi mzito ulimpitia uliomfanya alale kwa muda mrefu, alishtuka saa moja usiku, giza lilianza kuimeza nuru ya mchana. Alijikuta amelala pembeni ya maji yaliyokuwa yakirudi baada kupwa kuanzia asubuhi. Alishangazwa na sehemu aliyojikuta kuwa eneo la ndani ya bahari wakati yeye alilala nje ya bahari kwenye miti ya pembezoni. Alinyanyuka na kujikung’uta kisha taratibu alielekea sehemu lilipokuwa gari lake. Wasiwasi wake mkubwa gari linaweza kuibwa au kuchukuliwa baadhi ya vitu.

Alijiuliza kama gari litaibwa ataieleza nini mahakama, lakini ilikuwa ajabu gari lilikuwa lipo katika usalama pia hakuna kitu chochote kilichopotea. Alimshukuru Mungu na kuingia kwenye gari ili arudi nyumbani, lakini kabla hajawasha gari ili aondoke alishtuka kumuona Balkis.
Balkis alitokea mbele yake na kulisogelea gari huku akichanua tabasamu pana, alipomfikia alimsemesha:
“Muddy vipi?”

“Safi.”
“Za toka jana?”
“Nzuri.”
“Mbona upo huku?”
“Mbona hukuonekana mahakamani kama ulivyoniahidi?”

“Kwa hilo naomba samahani mpenzi wangu, nilitumwa na baba asubuhi nilijua nitawahi lakini amini usiamini ndiyo narudi. Na hivi nilikuwa nimetumwa tena nashangaa kukuona hapa.”
“Balkis huwezi kuamini toka nizaliwe leo nimesulubika vibaya.”
“Kwa nini tena mpenzi wangu?”

“Baada ya kutoka mahakamani...”
“Kabla ya kuendelea hebu nielezee imekuwaje huko?”
“Kesi imehahirishwa mpaka wiki ijayo.”
“Hakuna kitakachobadilika, kila kitu wamekwishakamilisha hata hakimu wa kesi yako ameshachukua chake mapema, kinachosubiriwa ni kukumaliza tu. Lakini nakuhakikishia fedha watakazochukua zitawatokea puani.”
“Utawapeleka polisi?”

“Wakafanye nini, ila utasikia tu nini kitawatokea.”
“Alafu...”
“Nimekuelewa Muddy, kwanza samahani kwa kutotokea mahakamani, umesema umesulubika kivipi?”
“Hivi kwenu wapi?”
“Muddy, si hapo mbele.”
“Wapi?”

“Unataka kupajua au kufika, twende maana sasa hivi nipo peke yangu.”
“Sehemu gani?”
“Si hapo mbele? Unaona nyumba ile kwa nyuma.”
“Mbona jana tulikwenda huku?”
“Si ndipo tunapopitia, kwani tatizo nini?”

“Hakuna tatizo twende nikapumzike nimechoka hapa nilipo pia nina kiu na njaa kali.”
Kama kawaida Balkis aliingia kwenye gari na kuliendesha, pamoja na Muddy kukaza macho ili ajue nyumba ile ipo wapi. Gari lilienda kidogo na kukata kidogo, Muddy hakuamini kuona jumba la kifahari lile lile alilolala jana yake. Baada ya kupaki gari sehemu yake aliteremka na kumfungulia mlango Muddy kisha alimshika mkono na kumuongoza mpaka ndani.

“Karibu mpenzi wangu,” alimwambia kwa sauti ya mahaba huku akimlegezea macho na kumfanya Muddy asahau tabu zote alizokutana nazo.
Kama kawaida alipelekwa kuoga kisha alifungwa vazi refu na kupelekwa kwenye meza iliyokuwa na vyakula tayari. Wakati akiendelea kula chakula kitamu ambacho kwake ilikuwa siku ya kwanza kukila, Balkis alimuaga kwenda kuoga. Aliondoka kwa mwendo wa madaha na kumfanya Muddy aache kula na kumsindikiza kwa macho huku akiusifia utundu wa Rabuka kumuumba binti mrembo kama yule.

Kwake aliona kama ndoto kumpata msichana mzuri kama Balkis pamoja na uzuri wake lakini umemuonesha mapenzi ya kweli kiasi cha kumsahau mkewe Ashura. Akiwa katikati ya chakula, alimuona Balkis akisogea mezani akiwa amejifunga upande wa khanga.

Kila dakika Balkis alizidi kujijaza moyoni kwa Muddy ambaye kwake aliona ngekewa kuokota dhahabu katikati ya soko la Kariakoo. Baada ya chakula kama kawaida alipelekwa kwenye chumba alicholala jana yake. Kwa raha za muda mfupi hakutamani kufa na kujilaumu kwa uamuzi wa kijinga aliotaka kuchukua.

Kama kawaida alfajiri alirudishwa kwake huku akijiuliza kwa nini baba yake arudi alfajiri tu anatoka wapi. Kitu kingine kilichomchanganya kilikuwa jumba zuri analoishi Balkis lipo sehemu gani mbona hajawahi kuliona. Wazo lake lilikuwa mchana arudi tena kulitafuta.

Lakini aliporudi alipitiwa na usingizi na kuamka jioni ya siku ile na wakati huo Balkis alikuwa amekwishafika na kumfanya siku ile aimalize nyumbani, lakini bado alitaka kutoka usiku ule kama Balkis akiondoka ambaye alikuwa halali pale na kwenda kufanya uchunguzi wake.
 
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.45.


Baada ya Balkis kuondoka majira ya saa nne usiku, Muddy aliamua kurudi tena maeneo ya Daraja la Salenda kufanya uchunguzi wa jumba lile la ajabu. Aliingia kwenye gari lake na kwenda hadi sehemu aliyokutwa na Balkis. Alisimamisha gari lake na kufunga kila sehemu kwa usalama wa gari lake kisha aliteremka na kutembea taratibu kuifuata njia aliyopita na Balkis.

Kila alivyolitafuta lile jumba la kina Balkis hakuliona, alijikuta akitoka sehemu moja kwenda nyingine bila mafanikio. Saa zilimkatikia kwa kuzurula kulitafuta lile jumba ambalo aliamini kwa muono wake akiwa ndani yake kama akiwa kwa mbali angeliona kutokana na kuwa na taa kila kona ya jumba lile zilizokuwa na mwanga mkali.

Lakini kila alipotupa macho labda ataziona taa angani, kulikuwa na kiza tu kilichotawala angani. Bado hakuamini alirudi sehemu aliyoanzia zaidi ya mara kumi ili aanze upya kulitafuta jumba la kifahari la kina Balkis. Muda ulizidi kukatika, kutokana na kutembea sana kulitafuta jumba hilo alijikuta akichoka sana na kukaa chini ya mti mmoja apumzike kidogo ili arudi kwenye gari lake na kurudi nyumbani kulala kwani usiku ulikuwa mkubwa.

Alipokaa chini ya mti usingizi haukuchelewa ulimchukua, ulikuwa usingizi mtamu ajabu uliomfanya alale kama yupo kitandani. Kibaridi cha alfajiri kilimshtua kwenye usingizi mzito na kujikuta amelala pembeni ya ufukwe chini ya mnazi, sehemu ambayo ilimchanganya kidogo.

Alitembeza macho yake na kuwaona watu waliokuwa wakiteremsha samaki kwenye boti. Sehemu ile ilimchanganya sana na kujiuliza pale ni wapi? Pamoja na kuwa amejilaza chini ya mnazi bado hakuna mtu aliyekuwa na habari naye kwani kila mmoja alikuwa na hamsini zake.

Wengi walipita pembeni yake wakiwahi kununua samaki walioletwa na majahazi asubuhi ile. Akiwa bado amekaa chini akitafakari yupo wapi, kijua nacho kilianza kuchomoza kwa mbali lakini bado baridi iliendelea kumchonyota mwilini.

Alijinyanyua taratibu alipokuwa amekaa na kuanza kutembea taratibu pembeni ya bahari huku akijitahidi kuyakumbuka maeneo yale ambayo yalikuwa mageni kichwani mwake. Aliona akikaa kimya atazidi kupotea, ilibidi amuulize kijana mmoja aliyekuwa na kapu lililoonekana limejaa samaki wabichi, alionekana ni mchuuzi aliyelangua na kwenda kuwauza mitaani.

“Samahani ndugu,” Muddy alimuuliza baada ya kumkaribia.
“Bila samahani kaka yangu.”
“Kwanza ni vizuri kutanguliza salamu kuonesha uungwana, habari za asubuhi?”
“Nzuri tu.”
“Eti hapa ni wapi?”
“Kigamboni.”

“Mungu wangu, kuja huku si lazima utumie pantoni?”
“Kutoka wapi?”
“Mjini.”
“Ndiyo.”
“Sasa mimi nimefikaje bila kutumia Pantoni?”
“Kutoka wapi?”
“Mjini.”
“Kwani wewe umefikaje huku?”
“Hata najua, hii kali ya mwaka.”

“Samahani kaka, mbona kama unajishangaa kwani wewe mara ya mwisho ulikuwa wapi?”
“Njia panda ya barabara ya Ali Hasani Mwinyi na Masaki.”
“Ulikuwa ukifanya nini?”
“Mmh! Tuachane na hayo, hebu nioneshe njia ya kuelekea kivuko cha Pantoni?”
“Twende pamoja na mimi naelekea huko huko.”

Muddy aliongozana na yule kijana kuelekea kwenye kivuko cha Pantoni, njiani alijawa na mawazo jinsi alivyojikuta Kigamboni wakati yeye alikuwa maeneo ya Daraja la Salenda. Alijiuliza kuhusu gari lake atalikuta kwenye hali gani, alipofika kivukoni bahati nzuri alikuta kivuko ndiyo kinapakia abiria na magari.

Alipanda na kutulia kwenye siti huku kichwa chake kikiwa hakikubaliana na kilichotokea.
Bado alijawa na mawazo juu ya kujikuta Kigamboni bila kujielewa, kivuko kilivyofika mwisho aliteremka na kuelekea kwenye daladala za kuelekea Mwenge iliyomrudisha mpaka njia panda ya kuelekea Masaki. Alipofika alilikuta gari lake lipo katika hali ya usalama.

Aliingia ndani ya gari lake na kurudi hadi kwake, alishangaa alipofika kwake kumkuta Balkis amekaa mlangoni akilia. Alijikuta akishtuka, akateremka kwenye gari bila kufunga mlango na kumfuata alipokuwa amekaa.
“Mpenzi unalia nini?”
“Muddy hunipendi.”
“Mimi?” Muddy alishtuka kusikia vile.

“Muddy nazungumza na nani?”
“Na mimi.”
“Ulikuwa wapi?”
“Nilitoka kidogo alfajiri kuna sehemu nilikwenda mara moja.”
“Muddy unanipenda?”
“Tena sana.”
“Niambie ukweli ulikuwa wapi?”
“Kama nilivyo kueleza mpenzi,” Muddy alijua Balkis alikuja asubuhi ile.
“Nikuambie nini mpenzi zaidi ya hayo.”

“Mbona kichwani una majani na mwili na nguo zimechafuka?”
Kauli ile ilimshtua Muddy na kujikuta akijikagua upya na kujikuta kweli alikuwa amechafuka kwa mchanga wa bahari pia kichwani alikuwa na majani. Alijikuta akipatwa na kigugumizi, alijifikiria amjibu nini Balkis aliyekuwa akimtazama usoni huku machozi yakimtoka.
 
 
 
 
 
 

JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.46.“Muddy nipo hapa toka saa tano usiku baridi lote limeniishia nikijua haupo mbali, kumbe umekwenda kwa wanawake zako,” Balkis alijiliza kiuongo.
“Nisamehe Ba..Ba..lkis,” Muddy alijitetea baada ya kujua kuwa ameumbuka.
“Niambie ukweli ulikuwa wapi?”

“Nilikufuata kwenu.”
“Kufanya nini, wakati niliondoa kwako hukuniambia kitu?”
“Nililipenda jumba lenu nilitaka kuliona kwa macho yangu nikiwa kwa nje.”
“Si ungenieleza unataka kupajua kwetu ili nikupeleke kuliko kunichunguza au huniamini?”

“Nakuamini lakini basi tu, yaani nimechanganyikiwa, jumba kama lile sikuwahi kuliona hata mchana huwa silioni maeneo yale.”
“Narudia tena, kwa nini usiniulize jumba letu lilipo? unaweza kulitafuta mwaka mzima na usilione.”

“Naomba unisamehe kwa yote yaliyojitokeza.”
“Muddy nilishakusamehe tangu siku ya kwanza nilipokuona ukipasuliwa moyo wako kwa kisu butu bila ya ganzi na mkeo wa bandia, niliamini mtupo uliotupwa haukujua ungeangukia wapi na muanguko wako ungekuwa mkubwa sana na usingesimama tena.”

“Nashukuru Balkis kwa kuyaokoa maisha yangu, nisamehe kwa yote, siyo kwamba sikuamini la hasha, bali nilipenda kuuona utukufu wa utajiri wa familia yako. Bado nipo njia panda kujiuliza jumba zuri kama lile limejengwa lini maeneo yale.”
“Maeneo gani?”

“Si pale pembeni ya njia panda ya kuelekea Masaki.”
“Nataka nikutaadharishe kitu kimoja, yaani usije tena maeneo yale kwani baba yangu akikuona anaweza hata kukutoa uhai.”
“Atanijuaje?”

“Mbona anakujua, aliponiuliza nilimdanganya, sasa kama atakuona tena maeneo yale lazima atajua namdanganya na atakufanyia kitu kibaya.”
“Je, akinikuta kwenu?”
“Kwa sasa baba yupo, hivyo hutuwezi kwenda tena mpaka tutakapooana.”
“Kwa hiyo utakuwa unakuja kulala hapa?”

“Ndiyo maana yake.”
“Si umesema nyumba hii itapigwa bei itakuwaje?”
“Usiwe na wasiwasi kila kitu niachie mimi, ukitoka mahakamani nitakupeleka kwenye nyumba yako mpya.”

“Nitashukuru mpenzi wangu.”
Balkis baada ya kuingia ndani aliisikia nyumba ukinuka sana, aliogopa kusema kwa kuhofia kumuudhi mpenzi wake. Alitafuta mbinu ya kumuondoa Muddy ili afanye usafi ndani mle.

Alimtuma kitu ambacho alijua hawezi kukipata karibu, alijua nafasi ile ingempa fursa ya kuwaita wajakazi wake kufanya usafi kwa muda mfupi. Alimuomba samahani kabla ya kumtuma:
“Samahani mpenzi wangu.”
“Bila samahani.”

“Najua umechoka lakini naomba nikutume kitu.”
“Nitume tu mpenzi wangu.”
“Kwa vile nataka kufanya usafi, naomba kaninunulie udi sehal”
“Upo sehemu gani?” ”Kwenye maduka wanayouza manukato utaupata.”
“Hakuna tatizo wacha niwahi.”

“Nioneshe ufagio.”
Baada ya kumpa ufagio Muddy alitaka kuondoka na gari lakini Balkis alimkataza alijua akitembea kwa miguu atachukua muda mrefu kurudi kuliko akitumia gari.
“Unaweza kuupata karibu wala usitumie gari.”
“Hakuna tatizo.”

Muddy aliondoka na kumwacha Balkis akijifanya anafagia, baada ya kuondoka tu, aliacha kufagia na kujishika kwenye paji lake la uso. Haikuchukua sekunde wajakazi kumi walikuwa mbele yake wakiwa wamepiga magoti.
“Rabeka mwana wa mfalme una shida gani?” Waliuliza kwa pamoja.

“Nataka mfanye usafi wa nyumba yote, sitaki kusikia harufu mbaya kama hii.”
Mara moja wajakazi walianza kusafisha nyumba nzima, ilikuwa ajabu waliondoka vitu vyote vya ndani na kuviweka vipya na vyenye thamani kwa muda mfupi, ndani pakabadilika, pakapendeza na kuvutia kila kona ya nyumba ilinukia kwa harufu nzuri.

Muddy alijikuta akitembea umbali mrefu kutafuta udi sehal, kila alipouliza watu hawakuujua. Alijikuta akikata tamaa na kuamua kurudi kumweleza Balkis kuwa udi wenye jina hilo kila alipouliza watu hawakuujua. Kutokana na kwenda umbali mrefu ilibidi wakati wa kurudi apande gari, jasho likimvuja kwa kutembea.

Alipofika nyumbani aliingia ndani lakini alishtuka kukuta nyumba yake ikiwa imebadilika na kupendeza sana, aliviona vitu tofauti kiasi cha kuamini kuwa alikuwa amekosea, hakukuwa kwake. Alitoka nje ili akaitafute nyumba yake lakini mlangoni alikutana na Balkis akiwa amebeba siagi na jam.

“Vipi mpenzi mbona nimekuona umeingia na unatoka?”
“Ha! Hapa ni kwangu?” Alishtuka.
“Eeh! Kwako, kwani vipi?”
“Umefanya usafi mkubwa hivi kwa muda gani?””Usinione nipo hivi mimi ni mwanamke wa shoka.”

“Na mbona kuna vitu vipya?”
“Sasa kipi cha ajabu, yote haya nimeyapanga kwa muda mrefu, nilipokuwa nakuja kulala hapa. Nilimtuma mtu avilete vitu hivi, wakati unaondoka vilikuwa vinaingia.”
“Sasa nyumba ikiuzwa?”

“Achana na wazo hilo hebu nenda kaoge ufungue kinywa.”
Muddy hakujibu kitu alichukua taulo na kwenda kuoga, nyumba ilikuwa ikinukia kama ujinini kwa akina Balkis. Muddy alipotoka kuoga alikuta chai imeshatayarishwa juu ya meza, ilikuwa tamu ambayo Muddy aliwahi kuinywa nyumbani kwa akina Balkis tu.

Pamoja na kuisifia chai lakini Muddy kila alipomuangalia Balkis moyo wake haukuamini kama alikuwa na mwanamke mzuri kama yule tena tajiri mwenye mapenzi ya dhati kwake.
 
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.47.


“Muddy nihakikishie kuwa huwezi kurudiana na Ashura?”
“Nakuhakikishia kukupenda siku zote na kamwe sitarudiana na yule mwanamke muuaji.” “Muddy unayosema yanatoka moyoni au mdomoni?”
“Yanatoka moyoni mwangu?”
“Ukinigeuka?”
“Nifanye lolote.”

“Muddy kama unayosema ni kweli basi kitu nilichotaka kukifanya naachana nacho.”
“Kipi hicho?”
“Nilitaka kusimamia kesi yako kuhakikisha hawachukui kitu chochote.”
“Kwa nini usifanye hivyo?”
“Naacha ili maisha yako yakiwa mazuri mtu yeyote asikuguse.”
“Kwa hiyo nitakuwa na maisha mazuri zaidi ya haya?” Muddy aliuliza.
“Mara kumi ya haya.”

“Usiniambie!”
“Kwangu fedha si tatizo, ninachokitaka kutoka kwako ni mapenzi ya kweli, sihitaji kitu kingine.”
“Nakuahidi utayapata hapa.”
“Basi tegemea kuishi maisha ya raha mpaka kufa kwako.”
“Asante mpenzi wangu,” Muddy alisema huku akimkumbatia Balkis.
***
Muda ulipofika Muddy aliitwa mahakamani na hukumu ilikuwa ile ile ya kugawana mali. Kwa vile alishaelezwa na Balkis maisha yake baada ya hukumu, hakuchanganyikiwa baada ya kuelezwa yale. Baada ya hukumu ile, Muddy pia alitakiwa kumlipa fidia ya fedha ambayo ilimfanya asipate kitu katika mali zitakazouzwa, vikiwemo gari na nyumba.

Ashura alishangaa kumuona Muddy pamoja na pigo zito yupo katika hali ya kawaida. Baada ya hukumu Muddy alitoka nje ya mahakama na kwenda moja kwa moja kwa Balkis aliyekuwa akimsubiri. Muddy alishtuka kumuona Balkis akiwa pembeni ya gari la kifahari.
“Karibu mpenzi.”
“Asante.”
“Pole na masaibu yote.”
“Asante,” walikumbatiana, kitendo kile hakuna aliyekiona zaidi ya Muddy peke yake.
“Nina imani mambo yamekwenda kama nilivyokueleza?”
“Yaani umekuwa kama wewe ndiye uliyeyapanga yote, hakuna hata kimoja kilichokwenda kinyume.”

“Basi huyo ndiye Ashura ambaye pia hilo si jina lake halisi.”
“Una maana gani kusema hivyo?”
“Nitakueleza, kila mwanaume aliyemchezea mchezo huu anamjua kwa jina hili lakini jina halisi anaitwa Shuuna.”
“Ina maana hata hayo majina aliyotumia kwa hao mabwana wa awali unayajua?”
“Nayajua.”
“Alikuwa anaitwa nani?”
“Twende kwanza nyumbani ukapumzike, mengine tutazungumza tukifika.”
Muddy aliingia kwenye gari na kuondoka, kabla ya kuingia kwenye gari Ashura alishtuka kumuona Muddy na mwanamke mrembo aliyejitambulisha kuwa ndiye mkewe siku aliyokwenda kwake kumuonya.

Alijikuta akikosa raha na kujiona wamefanya kazi bure sawa na kutwanga maji kwenye kinu. Waliona kama hawakufanya kitu na kujikuta akimuuliza mwanaume wake.
“Yule mwanamke mwenye fedha Muddy kamtoa wapi?” Ashura aliuliza.

“Hata mimi nashangaa, ni wazi wameanza uhusiano kipindi mkiwa wote.”
“Ndiyo maana hata ilipotolewa hukumu hakushtuka.”
“Hata mimi nilishangaa kuona anakubali kila kitu.”
“Kwa hiyo tutakuwa tumefeli?”
“Hapana, hatujafeli kwani tulivyovitaka tumevipata, ila kuna biashara nyingine nzuri,” mwanaume wa Ashura alisema.

“Biashara gani?”
“Tukafungue mashitaka ya kudai kuhujumiwa penzi lako lililosababisha muachane na mumeo wakati bado unampenda.”
“Aisee, wazo zuri sana! Kweli wewe bwana mipango, sasa mpango huo tuufanye lini?”

“Kwanza tupajue wanapoishi ili tufanye mpango wa kufungua mashitaka.”
“Hilo wazo, mbona mwaka huu tutatengeneza fedha mpaka zitukimbie.”
“Hiyo ndiyo kazi yetu.”
“Lakini Mussa kuna jambo nimekumbuka.”
“Jambo gani hilo?”

“Unakumbuka yule mwanamke alivyotuonya kuhusu tabia yetu kuwa itatutokea puani?”
“Sasa wewe unamuogopa, atatufanya nini mwanamke yule?”
“Mmh! Nashangaa moyo unanienda mbio nilipomkumbuka.”
“Si kwa vile amekuchukulia mumeo.”

“Yule si mume wangu nilikuwa naye kibiashara zaidi.”
“Basi mpango wa haraka ni kudili na Muddy kuhakikisha anaokota makopo.”
 
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.48.Wakati wakipanga kuchukua fedha za Balkis, muda huo Muddy alikuwa akikaribishwa kwenye jumba la kifahari.
“Karibu mpenzi wangu hapa ndipo kwako ishi kwa furaha na mapenzi ya kweli,” Balkis alimkaribisha kwa sauti tamu.
“Ha! Siamini.”

“Hata lile gari ni lako.”
“Usiniambie!” Muddy alizidi kupigwa na butwaa.
“Ukweli ni huo, leo usiku kutakuwa na sherehe fupi ya kufunga ndoa yetu ili uweze kunitumia kihalali kama mkeo.”

“Hakuna tatizo, asante sana mpenzi.”
Muddy alishukuru kwa kupiga magoti huku machozi yakimtoka na kujiuliza bila ya Balkis maisha yake yangekuwaje baada ya kufanyiwa utapeli na Ashura.

****
Ashura na mwanaume wake baada ya kutoka mahakamani waliongozana na madalali kwenda kuuza mali za Muddy zikiwemo gari na nyumba siku ile ile, kutokana na mipango iliyopangwa mapema. Baada ya kufanikiwa kuuza gari na nyumba waliendelea kufurahia mafanikio yao kufuatia kazi yao ya utapeli na kujipanga kwa ajili ya kupambana na Balkis kuhakikisha wanapata fedha kupitia kwa Muddy.

Pamoja na kupata vitu walivyovitaka kutoka kwa Muddy, bado Ashura moyo wake ulikosa raha, alijiuliza atamtazamaje Muddy siku wakikutana kutokana kuonekana ameingia kwenye maisha mazuri tofauti na awali walipokuwa pamoja.

Baada ya kumuacha Muddy na kuonesha kuchanganyikiwa, alitegemea kusikia amejinyonga. Kufuatia kupona kifo hicho, Ashura alitegemea siku ya hukumu angemuona Muddy akitoka mahakamani na kuanza kuokota makopo, lakini ilikuwa ni kinyume na mategemeo yake.

Wasiwasi wake Muddy lazima angelipa kisasi, wazo lake lilikuwa kumuwahi kabla hajawahiwa yeye. Akiwa amekaa na mwanaume wake, Ashura alimueleza jambo:
“Mussa nina jambo linaniumiza akilini mwangu.”
“Lipi tena mpenzi?”

“Nina wasiwasi na Muddy kutulipizia kisasi.”
“Ni kweli hata mimi nilikuwa na wazo hilo.”
“Sasa tufanye nini kabla hajafanya lolote, maana akitulia atajipanga na yule dada anaonekana ana fedha hivyo anaweza kutufanyia kitu kibaya.”
“Ondoa hofu hawawezi kutufanya lolote zaidi ya sisi kuwamaliza wao.”
“Hayo ndiyo maneno.” Ashura alipata faraja.
***
Wakati Ashura na Musa wakipanga mipango yao, usiku wa siku ile ufukweni mwa Bahari ya Hindi maeneo ya Daraja la Salenda kulikuwa na sherehe kubwa ya harusi kati ya Balkis na Muddy. Katika kundi la watu wote waliokuwepo kwenye sherehe ile Muddy peke yake ndiye aliyekuwa mwanadamu, lakini waliobakia walikuwa majini.

Lakini hakuwajua kwa vile walikuwa katika maumbile ya kibinadamu, Muddy alimuoa rasmi Balkis na kuwa mkewe wa halali. Ilikuwa sherehe kubwa kuwahi kutokea katika maisha ya Muddy. Baada ya harusi walilala kwenye kitanda cha bembea kilichowabembeleza mpaka kunakucha.

*****
Taarifa ya ndoa ya Balkis ilifika chini ya bahari kwa Mfalme Barami Hudirud, kitendo kile kwake alikiona kama ni dharau kutoka kwa mwanaye kufunga ndoa na mwanadamu. Alimfuata mkewe aliyekuwa amekaa kwenye bustani akibembea kwenye kiti.

“Mama Balkis,” alimwita kwa sauti ya juu iliyomshtua.
“Mtukufu Mfalme wa chini ya bahari, mbona sauti kali, kuna usalama?”
“Mwanao ananitafuta nini?”

“Kwani kafanya nini tena mtukufu mfalme?”?”Tunamkataza nini na anafanya nini?”
“Amefanya nini?”
“Anaweza kuvunja amri yangu?” Mfalme Barami alisema huku akipiga ngumi kifuani kwa hasira.

“Mume wangu, lakini si bado anaendelea kuleta vizazi vya wanawake?”
“Kwa nini ameolewa na mwanadamu?”
“Ha! Ndiyo kafanya hivyo!” Malkia Huleiya alishtuka.
“Eeh! Tena nasikia watwana na vijakazi walikuwepo kwenye harusi hiyo.”
“Usiniambie!”

“Kwa jinsi alivyovunja amri yangu, wote waliohudhuria harusi ile watakutana na adhabu kali,” alisema kwa hasira mpaka povu likamtoka mdomoni.
“Mume wangu usimguse mtu yeyote ni wewe uliyempa amri mwanao kwa watwana na vijakazi juu ya kuheshimu amri zake.”

“Basi kama sivyo hivyo nitamtuma mtwana mkuu Muhuru akammalize huyo mwanaume.”
“Bado hujatumia busara, kumbuka kosa lako lolote litatugharimu, kitendo cha kukataa kumuondoa mwanaume wa kwanza huku kilizua patashika na ulipotaka kumuua ulisikia alichosema mwanao. Hivi umuue huyu aliyefunga naye ndoa itakuwaje?”

“Sasa kuna haja gani kuendelea kuleta vizazi vya wanawake wakati ameishajiamulia kuolewa na mwanadamu?”
 
 
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.48...B

ILIPOISHIA:
“Bado hujatumia busara, kumbuka kosa lako lolote litatugharimu. Kitendo cha kutaka kumuondoa mwanaume wa kwanza huku kukiwa na patashika ulipotaka kumuua ulisikia alichosema mwanao. Hivi umuue huyu aliyefunga naye ndoa itakuwaje?”
“Sasa kuna haja gani kuendelea kuleta vizazi vya wanawake wakati ameshajiamulia kuolewa na binadamu?”
SASA ENDELEA...

“Labda ana sababu zake, ngoja akija tumuulize.”
“Hakuna cha kumsubiri, tumtume Muhuru aende akamwite mara moja.”
“Siamini, kama jana kafunga ndoa leo aje huku, hebu kuwa na subira mume wangu.”
Walikubaliana kumsubiri ili aje awaeleze kwa nini amevunja amri ya mfalme wa bahari, tena akiwa binti wa mfalme.

BAADA YA MIEZI MIWILI
Maisha ya Muddy yalibadilika ghafla, kila aliyemuona alimshangaa. Mmoja kati ya watu waliomshangaa alikuwa ni Ashura aliyemuona akitoka super market akiwa ameongozana na Balkis katika mwonekano wa mahaba mazito. Roho ilimuuma na kujikuta akipata wivu wa kutaka kuwa na Muddy.
Aliamini kuwa kilio cha Muddy alichokitoa siku alipomuacha, kama angemuomba warudiane angeweza kukubali. Alipanga kumtafuta na kumuomba msamaha.

Ashura aliamua kumtafuta Muddy kwa udi na uvumba kila kona ya mji. Lakini alishangaa kila alipomuona Muddy na kumfuata alipomkaribia Balkis alitokea bila kujua ametokea wapi, kitu ambacho kilimkosesha amani ya moyo wake. Hata alipojaribu kumfuatilia kwa nyuma alimpotea kimiujiza. Aliamini njia rahisi ya kumrudisha mikononi mwake ni kwenda kwa mtaalam wake aliyekuwa anakaa Mbagala Kimbangulile, Mzee Chujio.

Aliwasha gari na kuelekea Mbagala kwa mtaalam ili akamvute tena Muddy kama alivyofanya mwanzo na kupelekea kuisahau familia yake. Alipofika Mtoni kwa Azizi Ali dada mmoja aliomba msaada kwenye gari lake. Hakutaka kumnyima lifti, alimsaidia.

“Unafika wapi dada yangu?” alimuuliza baada ya kuingia kwenye gari na kufunga mlango.
“Mbagala Zakheem,” alijibu yule dada kwa sauti ya chini.
“Ooh! Mimi nafika mbele, nitakushusha kituoni.”
“Nitashukuru.”

Wakati safari ikiendelea mwanamke aliyeomba msaada alianzisha mazungumzo.
“Dada yangu huku ni mwenyeji?”
“Hapana nakwenda kumuona mtu mmoja Mbagala mwisho.”
“Nani mganga Chujio?”
“Mmh!” Ashura alishtuka.

“Mbona umeshtuka?”
“Walaa, siendi huko.”

“Lakini dada shida ya nini kumuendea Muddy kwa mganga wakati mmekwisha achana?” Kauli ile ilimshtua sana Ashura.
“Nani amekwambia mimi nakwenda kwa mganga, pia habari za Muddy nani kakueleza?”
Ashura alishtuka kujiona yupo uchi japo amevaa nguo, alijuta kumpa lifti yule mwanamke ambaye aliharibu safari yake yote.

“Ashura,” mwanamke aliyepewa lifti kwenye gari alimwita jina lake.
“Ha! Umejuaje jina langu?” Ashura alizidi kumshangaa mtu aliyempa lifti kwa kumjua kwa mapana.

“Nijue unataka kufanya nini nitashindwa kujua jina lako? kwanza jina lako si Ashura.”
“Kama siitwi Ashura naitwa nani?”
“Shuuna.”

“Mungu wangu! Umenijuaje?”
Ashura nusura aliingize gari kwenye mtaro kwa mshtuko, ilibidi alisimamishe pembeni maeneo ya Mbagala Misheni.

“Kwani kuna siri, la muhimu achana na Muddy endelea na maisha yako, pia mpango wenu wa kumfuatilia Muddy na mkewe mtaokota makopo ninyi kabla ya huyo Muddy.”
“Wewe ni nani?” Ashura alimuuliza huku jasho likimtoka.
“Mke wa Muddy,” sauti ilijibu pembeni.

“Muongo...Ha!” Ashura alijibu huku akigeuka kumtazama aliyejiita mke wa Muddy, wakati huo manukato makali yalinukia ndani ya gari. Hakuamini kumuona mtu aliyempa lifti amebadilika na kuwa mke wa Muddy, Balkis.

“Punguza hofu, sipo hapa kwa shari bali kukuonya kwa kitu unachotaka kukifanya, kumbuka nilikuuliza mapema kuhusu kurudiana naye nawe ulinihakikishia hutarudiana naye tena.

“Sasa sikiliza Ashura, huenda utashangaa kuniona hapa. Sitaki kujieleza sana, ila ukitaka vita na mimi ambavyo najua hutaweza kushinda endelea na mambo yako. Nitakufanya kitu kibaya ambacho kitabakia katika kumbukumbu zako mpaka unafukiwa chini.

“Mwambie na mpumbavu mwenzako mpango unaopanga wa kutaka kuichukua mali yangu mtakufa kifo kibaya. Leo sikuja kwa shari nimekuja kistaarabu. Mara ya pili utashangaa na hutaamini kuwa ni mimi,” Balkis alisema kwa sauti kali kidogo iliyomtisha Ashura.
 
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.49


ILIPOISHIA:
“Sasa sikiliza Ashura huenda utashangaa kuniona hapa, sitaki kujieleza sana ila ukitaka vita na mimi najua huwezi, nitakufanyia kitu kibaya ambacho kitabakia katika kumbukumbu yako mpaka unafukiwa chini.

“Mwambie na mpumbavu mwenzako kwamba mpango mnaoupanga wa kutaka kuzichukua mali zangu mtakufa kifo kibaya. Leo sikuja kwa shari bali kwa ustaarabu, mara ya pili utanishangaa, hutaamini kuwa ni mimi,” Balkis alisema kwa sauti kali kidogo iliyomtisha Ashura. SASA ENDELEA...

Baada ya kusema maneno yale, Balkis aliufungua mlango wa gari na kutoka nje huku akifyonya kwa sauti kali, alipolizunguka gari akatoweka.
Baada ya kuondoka eneo lile, Ashura alishtuka kama mtu aliyetoka usingizini na kujiuliza alichokiona na kukisikia kama kilikuwa ni cha kweli au alikuwa akiota.

Wazo lililomjia haraka aliamini kabisa kuwa ile ilikuwa ni ndoto, aliamua kwenda kwa mganga kupata tiba ya kumrudisha Muddy mikononi mwake.
Alijishangaa mwanaume aliyemgeuza mradi amekuwa kero moyoni mwake kila dakika alijikuta akimpenda na kumtamani kuwa naye tena.

Aliendesha gari huku akiapa kutompa msaada kiumbe yeyote kwa kuhofia kukutana na matatizo ambayo bado aliamini kuwa ni ndoto.
Hakuamini kama mtu angeweza kugeuka mara mbili katika hali ya kawaida, kwake alijua ile ilikuwa ni ndoto mbaya tu.

Alipofika Mbagala Rangi Tatu alikata kushoto na kuelekea Kimbangulile, alipofika kwa mganga alishangaa kukuta watu wakiwa wamejaa kuonesha kulikuwa na jambo.

Alisimamisha gari mbali kidogo na nyumba ya mganga na kuteremka kisha akajisogeza kwenye kundi la watu ambapo kila mmoja alikuwa akisema lake. Alimsikia mmoja akisema;
“Lazima yule atakuwa ni jambazi aliyefanyiwa kitu kibaya na mganga.”
“Hapana mbona hakutoka mle ndani yule lazima atakuwa ni jini tu.”

Yalikuwa naneno yaliyomchanganya Ashura na kujiuliza mganga amefanya nini, ilibidi amwite pembeni dada mmoja ili apate kumhoji vizuri.
“Samahani dada yangu kuna nini?”
“Mmh! Kuna jambo limetokea linawachanganya watu wengi.”
“Jambo gani?”

“Mzee Chujio ameuawa.”
“Mzee Chujio gani?”
“Yule mganga.”
“Mganga?” Ashura aliuliza kwa mshtuko.
“Eeh, unamfahamu?”

“Sasa dada yangu nani asiyemjua mzee Chujio sehemu hii?”
“Basi ndiyo hivyo, ameuawa katika mazingira ya kutatanisha.”
“Una maana gani?”

“Nasikia kuna dada mmoja mrembo alikuja na kuingia ndani kwa mganga na kuwaacha wateja wachache wakiwa kwenye foleni. Lakini inasemekana hakutoka, baada ya wateja kusubiri kwa muda bila kusikia wakiitwa ndani waliamua kuingia lakini cha ajabu wakamkuta mganga amelala chini akiwa amekufa na kutoka funza mdomoni kama aliyefariki wiki moja iliyopita.”

“Funza mdomoni?”
“Ndiyo.”
“Sasa jamani mtu wa kutoka funza si mtu aliyekufa zaidi ya wiki?” Ashura alisema kwa mshtuko.
“Hapo ndipo watu walipochanganyikiwa na kuamini kuwa yule mwanamke mzuri alikuwa ni jini.”

“Jini! mna maana gani?”
“Wanasema alikuwa mzuri sana, tena alikuwa akinukia na alipoingia ndani hakutoka.”
“Alivaa nguo gani?”
“Mmh! Hebu muulize yule dada aliyesimama katikati ya watu,” alimuonesha dada mmoja aliyekuwa akizungumza na watu huku akilia na kuweka mikono kichwani.
“Naomba uniitie.”

Yule binti alimfuata yule dada aliyekuwa akizungumza huku akitokwa na machozi, baada ya kusogea karibu ya Ashura, ilibidi ajitambulishe kuwa ni mmoja wa wateja wa mzee Chujio mtu aliyemtegemea kwenye mambo yake.
“Samahani mdogo wangu hata mimi nilikuwa nimekuja kwa mzee Chujio lakini kuna habari zimenichanganya sana. Nini kimemsibu mganga wetu?”

“Dada yangu hata kuzungumza nashindwa, siku tano zilizopita mzee Chujio alinisaidia matatizo yaliyonitesa kwa miaka kumi. Dawa alizonipa zilinionesha yote aliyonieleza, dada yangu walimwengu ni wabaya, niliteswa na mke mwenza na kufikia hatua ya kunuka mwili mzima hata kukaa mbele za watu nilikuwa siwezi.

“Nilitengwa na watu, wanaume walinipenda kwa kuniona, lakini waliponisogelea walikuwa wakikimbia kutokana na harufu kali kama ya mzoga uliooza. Leo dada yangu nilikuwa nafuata dawa na kupatiwa kinga baada ya awali kuondolewa tatizo langu.

“Ajabu wakati nasubiri kuingia kwa mganga alipita dada mmoja mrembo na kuingia ndani bila kufuata foleni. Kwa vile ilikuwa ni zamu yangu nilitaka kumfuata ndani kumtoa kwani hakuonesha ustaarabu, lakini wenzangu walinisihi nikamuacha amalize shida yake ndipo nami niingie.
“Baada ya muda kidogo tulisikia watu wakibishana, kauli ya mganga ilikuwa ya juu akionesha kuna kitu hakukubaliana na yule mwanamke mrembo mwenye kunukia manukato.

“Mganga alisema hawezi kufundishwa kazi na mtu, mara tulisikia sauti ya yule mwanamke mrembo akisema kuwa hana jinsi ile ndiyo zawadi yake.
“Baada ya hapo kilipita kimya kirefu huku muda ukizidi kuyoyoma.

“Baada ya nusu saa bila kusikia mazungumzo wala yule mwanamke mrembo kutoka, niliamua kuingia ndani kujua kilichokuwa kikiendelea.
“Nilipoingia nikamkuta mganga akiwa amelala chini, kilichonishtua zaidi ni funza waliokuwa wakimtoka mdomoni kama mtu aliyekufa muda mrefu.”
 
 
 
 
 
JIINI LA DARAJA LA SALENDA........EP.50“Funza?” Ashura aliuliza tena japo taarifa ya kutoka funza alielezwa mapema.
“Funza dada, kama mtu aliyekufa muda mrefu.”

“Unataka kuniambia kabla ya kutokea tukio lile ulionana naye?”
“Tena alitoka nje na mgonjwa aliyekwenda kumfanyia tiba nyuma ya nyumba yake, aliponiona alitaka kujua hali yangu, nilimweleza ninavyoendelea na kuniambia vitu vyote alivyovitafuta kwa ajili ya kazi yangu vimepatikana...Yaani..,” Kufikia pale yule dada aliangua kilio mikono kichwani, Ashura aliingia kwenye kazi ya kumbembeleza.

“Mdogo wangu hebu nyamaza kwanza.”
“Dada inauma, haiwezekani niwe miye, nimeteseka muda mrefu, napata tiba mganga anauawa katika mazingira ya utata,” aliendelea kulia kilio cha kukata tamaa. Ashura, japo alijitahidi kujikaza na kumbembeleza kwa kumlalia kifuani, lakini moyoni alikuwa na maumivu makali kama angepata sehemu iliyojificha, basi naye angeangua kilio ambacho hakuna mtu ambaye angeweza kumbembeleza.

Kifo cha mzee Chujio kilikuwa pigo kubwa maishani mwake, ndiye aliyekuwa tegemeo lake katika mambo yote aliyoyafanya ya kuwatapeli wanaume kwa kuwapumbaza kwa dawa. Alijiuliza nani atakayemsaidia katika maisha yake baada ya kifo cha mzee Chujio ambaye alimgeuza kama Mungu wa pili.

“Unasema ulimuona?” Ashura kwa kuchanganyikiwa alijikuta akiuliza swali alilojibiwa awali.
“Ndiyo.”
“Unasema alipoingia ndani hakutoka?”
“Ndiyo.”
“Au wakati anatoka huyo mwanamke ulikuwa umesinzia?”
“Dada yangu kusinzia tusinzie wote tulio
kuwa tunasuburi huduma?”
“Alivaa nguo gani?”
“Gauni refu jekundu lenye maua shingoni na kifuani, sielewi maua yale ya rangi gani kutokana na kumeremeta.”
“Mmh! Shingoni alikuwa na mkufu wenye herufi M?”
“Eeeh.”
“Mtandio wake wa bluu yenye maua ya kumetameta?”
“Huo huo!”
“Ana kipini cha mkufu?”

“Eeeh dada, umemjuaje?”
“Mmh! Kazi ipo,” Ashura aliguna na kusema kwa sauti ya chini.
“Kwani unamfahamu?”
“Kuna mtu nilikutana naye njiani uliponielezea alivyovaa nilikisia basi lazima atakuwa yeye.”
“Kwa hiyo si jini kama watu wanavyomdhania?”

“Mmh! Sijajua, kwani hakuna mlango wa kutokea nyuma?”
“Dada kama wewe ni mteja wa mzee Chujio, chumba chake unakijua, mlango utoke wapi?”
“Mna uhakika hakutoka?”
“Angetoka tungemuona kama si mimi basi wenzangu wangemuona.”
“Mmh! Nina wasiwasi alitoka hamkumuona.”


“Sawa alitoka, kile kifo nacho cha muda mfupi mtu aoze na kutoka funza kwa sekunde chache kinatokana na nini?”
“Inawezekana alimnywesha sumu kali iliyomuozesha tumboni na kuzalisha funza.”
“Mmh! Labda.”

“Basi dada, acha nirudi zangu hata mimi nimechanganyikiwa sana.”
“Sawa dada, lakini mimi ndiye nimechanganyikiwa hata kuliko familia yake.”
Wakati huo polisi walifika kuchukua mwili wa marehemu, alishuhudia mwili wa mzee Chujio ukitolewa huku familia yake na wateja wakiangua vilio.

Ashura alishindwa kujizuia, alikimbilia kwenye gari lake na kujifungia, alilia hadi macho yakamvimba. Alijiuliza yule mwanamke atakuwa nani, japo ilikuwa vigumu kukubali kuwa Balkis ni jini, lakini mambo yaliyomtokea kwenye gari alipombadilikia kama kinyonga yalimfanya aanze kuamini kabisa mke wa Muddy ni jini.

“Mungu wangu Muddy atakuwa ameoa jini?” Alijikuta akipayuka kwa sauti.
“Haiwezikani lazima nifanye chini juu nimtoe kwenye balaa lile.”
Ashura alijiingiza kwenye vita nyingine ya kujua hatima ya Muddy kwa Balkis kwa kuamini kuna njia ya kuyafukuza majini. Aliwasha gari lake na kurudi nyumbani.
*duh!!tamuje??

ITAENDELEA KESHOOOOO...........
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.51.


ILIPOISHIA;
Katika kutembeza macho aliwaona wajukuu wa mzee Njiwa wakicheza nje ya uzio, aliona kama atamuua mmoja basi mzee Njiwa Manga ataacha kazi ya kuwatibu ili ashughulikie msiba na kuwafanya Ashura na mwanaume wake kuondoka ili warudi siku nyingine. SASA ENDELEA...

Aliamini kama watatoka bila kupatiwa kinga yoyote angetumia nafasi ile kuwamaliza wote ili aweze kuishi na Muddy bila tatizo japo alijuwa kwa upande wa baba yake kulikuwa na vita nyingine.

Kila alivyotaka kuteremka roho ilimkataza kwa kuwaonea huruma viumbe wasio na hatia.

Kutokana na uwezo wake aliweza kuyasikia yote yaliyokuwa yakizungumzwa ndani na kupanga kama atakubaliana nao kabla ya kuwapa kinga naye, hatakuwa na budi kuua mtoto mmoja.

Ashura na mwanaume wake waliingia katika chumba cha mzee Njiwa Manga na kukaa kwenye mkeka.
“Karibuni,” mzee Njiwa Manga aliwakaribisha.
“Asante,” walijibu kwa pamoja.

“Mh! Niwasaidie nini?”
“Mzee tunahitaji msaada wako, tuna vita nzito na mwanamke mmoja jini.”

”Mmejuaje ni jini wakati majini hayaonekani?”

“Anatutokea katika umbile la kibinadamu na wakati mwingine katika maumbile tofauti, pia tunatokewa na mambo ya kutisha.”

“Tena jana kamuua mganga mmoja Mbagala kifo cha kutisha,” Ashura aliongezea.

“Mmh! Majina yenu?” Aliwauliza huku akichukua kibao cheusi na chaki.

“Naitwa Shuuna.”

“Shuuna...” mganga alilirudia jina lile kwa sauti ya chini huku akiliandika kwenye kibao.

“Mbona unaonekana una majina mengi?” Mganga Njiwa Manga alimuuliza Ashura.

“Lakini hili ndilo langu la kuzaliwa.”

“Sasa nikusaidie kwa jina gani kwani yote uliyatumia na watu tofauti wanakujua kwa majina hayo?”

“Kwa sasa natumia jina hili.”

“Kama ukifanikiwa kurudi kwa Muddy utatumia jina gani?”

Swali lile lilimfanya Ashura akae kimya na kukosa la kujibu kwa kuona kama siri yake inatoka nje.

“Lakini mzee suala la Muddy tulishaachana nalo, kama kutusaidia msaidie kwa jina la Shuuna,” Tonny aliingilia kati mazungumzo.

“Najua mmekuja pamoja lakini kila mmoja ana mawazo yake ambayo sitaki kuyaingilia kwa vile siyo kazi yangu,” mzee Njiwa Manga alijibu kwa fumbo lililomuacha gizani Tonny bila kujua dhamira ya Ashura kwa Muddy ilikuwa nini.

“Naomba niachane na mwenzako kwanza, hebu nawe nieleze jina lako?”
“Naitwa Antony.”
“Antoniii,” alilirudia jina lile kwa sauti ya chini huku akiliandika kwenye ubao.
Baada ya kuandika alitulia kwa muda akiandika vitu kwenye ubao na kukohoa kidogo kisha akauliza:

“Nimeona yote, sasa shida yenu nini hasa?”

“Mzee kama tulivyokueleza kuwa tuna tishio la mwanamke mmoja ambaye ni jini, anatishia maisha yetu.”

“Kwa hiyo mnataka nini?”

“Tunataka utukinge ili tuweze kupambana naye.”
“Mnamjua jina lake?”

“Balkis,” Ashura alijibu.
Mganga aliliandika jina lile, kama kawaida alilirudia kwa sauti ya chini.
“Balkis...Balkis.”
Baada ya kutulia kwa muda alisema:
“Lakini mbona mimi sioni madhara ya huyu mnayemuogopa?”

“Mzee huyu ni mtu mbaya sana, amenitokea mara nyingi kwenye gari katika sura tofauti na kutishia maisha yetu,” Ashura alisema huku macho yamemtoka pima kwa kusistiza.

“Mbona hapa panaonesha jini huyo ni mpole sana kuliko majini wengine?”

“Si kweli, ana roho mbaya sana, amemuua mzee Chujio kifo kibaya sana,” Ashura alisema.
“Unajua sababu ya kuuawa mzee Chujio?” mganga aliuliza.

“Kutokana na maelezo ya huyo mwanamke jini anasema aliingilia kazi yake na kuwa mbishi ndio akaamua kumfanya vile.”

“Sasa hamuoni na mimi nikiingilia kazi si yangu anaweza kunifanya kama mzee Chujio?”

“Hawezi.”

“Kwa nini asiweze?”

“Tunasikia wewe ndio kiboko ya majini.”

“Ni kweli kazi yangu ni kutibu na si kushindana na majini.”

“Lakini mzee kazi yako si kutusikiliza wateja shida yetu na kukupa kiasi ukitakacho,” Tonny alimueleza mganga..

“Sikiliza kijana, mimi si mchawi ni mganga wa kuwasaidia wenye matatizo, ndiyo maana nipo mpaka leo.Waganga wengi wamepoteza sifa zao kutokana na kuingilia kazi ya wachawi.

“Tumekuwa tukifanya makosa ya kuingia kwenye kazi ya kutesa, kuua au kuingia kwenye vita na viumbe kama majini ambayo wakati mwingine huwa hayana matatizo na watu.”

“Sasa mzee utatusaidiaje?”

“Mpaka sasa sijajua shida yenu nini?”

“Tunataka kinga ili tusiweze kudhuriwa na jini.”

“Jini gani wa kuwadhuru ninyi?”

“Balkis,” Ashura alijibu.

“Balkis atawadhuru vipi bila ninyi kumchokoza?”

“Yule hana cha kumchokoza bali huamua kuua bila sababu,” Ashura alitengeneza uongo.

“Sitawapa dawa yoyote zaidi ya kauli ya Balkis mwenyewe.”

“Mbona hatukuelewi, kauli gani?”

“Mtaisikia muda si mrefu kutoka kwake Balkis.”

Mzee Njiwa alitoka nje na kurudi na kitezo chenye moto, akakiweka mbele yake, akatoa mavumba kwenye chupa kisha akasema:

“Hii dawa kazi yake kuyavuta majini mazuri, kama Balkis ni jini mbaya hatakuja nikimwita.”

Baada ya kusema vile alianza kuweka mavumba kwenye moto huku akisema:

“Balkis binti mfalme wa bahari, naamini wewe ni jini mwema nakuomba uje mbele yangu, lakini kama si jini mwema ukiingia himaya yangu ndiyo mauti yako...Balkis njoo mbele ya wanadamu hawa wana mashtaka juu yako.”

Je, Balkis ni jini mzuri au mbaya?
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.52.


“Nimewaonesha ishara nyingi za vitisho ili wajue mimi si kiumbe wa kawaida ili wachane na mimi, lakini wamekuwa wabishi, kabla ya kuja huku niliwapa onyo zito lakini wamekuwa kama kenge, hawasikii mpaka watoke damu masikioni.

“Tena wana bahati kubwa leo ningepata dhambi nyingine, wakati natoka nyumbani niliwaona wamekaribia kwako lakini kasi yangu ilichelewa kidogo na kuwakuta wameshaingia kwenye ngome yako.


“La sivyo kama ningefanikiwa kuwatia mikononi ningewaulia mlangoni kwako na kama ungewasikiliza na kuwapatia tiba kabla tiba yao haijatimia ningemuua mjukuu wako mmoja ili uhalalishe kazi hii na wangetoka ningewamalizia mbali,

” Balkis alisema kwa sauti isiyotaka mzaha, huku kauli yake ikizidi kuwatisha moyoni walioomba msaada wa mzee Njiwa Manga.


“Nimekuelewa sana Balkis binti wa mfalme Barami, sasa ulikuwa unataka nini?”
“Kama nilivyowaeleza waachane na mimi, waendelee na maisha yao.”
“Wakifanya hivyo utakuwa na vita nao?”


“Niwe nao ili iwe nini ikiwa kila mmoja na maisha yake, ila tofauti ya hapo nitakachokifanya Mungu anajua.”
“Nina imani mmesikia yote aliyosema Balkis, niliwaeleza ni mpole mwenye huruma na upendo kwa viumbe wenzake.

Napenda kuwaeleza kuwa maelezo yake ndiyo tiba yenu na mkitoka hapa mkienda kinyume na haya aliyosema, nisione mtu hapa, mtamalizana wenyewe, mmenisikia?”


Alijibu kwa kunyanyua vichwa kwani hata midomo ilikuwa mizito, baada ya majibu yao ya kibubu mzee Njiwa Manga alimgeukia Balkis.


“Nina imani wamekuelewa ila wakienda kinyume mimi simo.”
“Wewe unasema hivyo lakini mioyo yao imejaa tamaa ya mali na uhai wa watu, narudia tena sitawaua ila nitawaadhiri mbele za watu, hilo litakuwa pigo kubwa na mkizidi nitawageuza mbwa.”


“Nimekuelewa sana Balkis unaweza kwenda,” mzee Njiwa Manga alisema.


Baada ya kuruhusiwa kutoka alinyanyuka na kutoka chumbani katika umbile la kibinadamu, wote walimsindikiza kwa macho hadi nje.Waliokuwa wamekaa nje kusubiri huduma macho yao yalishuhudia mwanamke mzuri akipita mbele yao huku wakijiuliza amepita saa ngapi kutokana na watu wengine kuwepo kwa muda mrefu. Balkis baada ya kutoka katika uzio wenye nguvu wa mzee Njiwa Manga alitoweka.


Baada ya kuondoka Balkis, mzee Njiwa Manga aliwageukia wateja wake na kusema:
“Nina imani tatizo lenu limekwisha?”
“Mzee litakwisha vipi wakati umemsikia mwenyewe amesema nini,” Tonny alihoji.
“Kasema nini?”
“Si amesema tukifuatilia mambo yake atatugeuza mbwa,” Ashura alijibu.
“Sasa mnataka kufuatilia mambo yake?”
“Hapana.”
“Sasa tatizo nini?”
“Tulikuwa tunaomba kinga.” Tonny alisema.
“Ya nini?”
“Ili tujikinge na matatizo ya wanadamu na majini.”
“Ili?”
“Mzee kama hujui kazi yako, kwani wanadamu wanakuja kwako kutafuta nini?”
“Tiba ya matatizo yao.”
“Sasa mbona hutaki kutusaidia?”
“Kwani shida yenu iliyowaleta hapa ni nini?”
“Kuzuia nguvu za jini Balkis.”
“Sasa niwape kinga ya nini?”
“Anaweza kutugeuka na kutufanyia kitu kibaya.”
“Hawezi na sina tiba yoyote labda muwe na tatizo lingine.”
“Hatuna, ni hili hili la huyu mwanamke ndilo linalotutisha, unamuona kwa macho tu lakini ni kiumbe kibaya sana.”


“Yule hana ubaya kama nilivyowaeleza, lakini mioyoni mwenu mna dhamira mbaya naye, kwa hilo mimi halinihusu kama mnataka ushindani dawa hiyo sina.”
“Kwa hiyo huna msaada wowote kwetu?” Tonny aliuliza.


“Msaada niliowapa ni mkubwa kuliko kukuchanjeni au niwape dawa ya kufukiza.”
“Mzee msaada gani uliotupa zaidi ya kutuacha njia panda?” Tonny alizidi kuhoji.


“Msaada niliowapa hamuujui lakini ni mkubwa sana, najua mmezunguka kwa waganga wengi kwa kazi zenu za dhuluma. Hamkuwahi kukutana na tatizo kisha mkatibiwa bila kunywa, kujifusha au kuchanjwa dawa? Mliyekuwa mnamuona adui ameeleza hataki kitu gani, sasa mnataka nifanye nini?”
”Basi inatosha inawezekana na wewe umemuogopa,” Tonny alisema kuonesha alitaka zaidi ya yale aliyoelezwa.


“Kweli nimemuogopa nipo kwa ajili ya kutibu si kujiingiza kwenye matatizo ya kujitakia, kutokana na maelezo yake nilikuwa nampoteza mjukuu wangu kwa ajili yetu. Nawaeleza mkikosea kwenda kwa mganga mwingine kitakachowakuta hamtakisahau mpaka mnakufa.”
“Tumeelewa.” Tonny alijibu kwa shingo upande.
“Basi mnaweza kwenda ili niendelee na wenzenu.”
“Sasa mzee tukupe kiasi gani?”
“Nina imani hamkuona nilichokifanya, nendeni msitoe kitu chochote.”
“Hapana mzee hata ya kuangalizia, sijui elfu moja?”
“Hapana nimewasamehe kila kitu.”
Walitoka huku wakiamini mzee Njiwa Manga uwezo wa kutibu umepungua ndiyo sababu ya kushindwa kuwasaidia kupambana na Balkis.
 
 
 
 
 
 
 JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.53.


“Sauda,” walisema mashoga zake waliokuwa wakilia huku mikono ikiwa kichwani, wengine hata nguo ziliwaanguka bila kujua.


“Sauda kafanya nini?”
“Ame...”
“Amefanya nini mbona mnanichanganya, mke wangu kafanya nini jamani?” mganga alijikuta kwenye mtihani mzito wa kujua mkewe amefanya nini kwani muda mfupi uliopita alimtuma dukani.

Mara aliingia mwanamke mwingine aliyekuwa akilia huku akisema:
“Haiwezekani Sauda atutoke kirahisi namna hii.”
“Huu lazima uchawi haiwezekani njiwa amgonge afe,” mwingine alisema huku akijitupa chini kwa uchungu.
“Jamani mke wangu kafanya nini?” pamoja na kuwasikia wakisema lakini hakuwaelewa.


Mara watu waliingia na mwili wa mkewe ambaye alikuwa amekwishapoteza uhai.


\“Ha! Amefanya nini?” Kakakuona alitaharuki.


Alimvamia mkewe ambaye alikuwa amefunikwa kanga, akamfunua na kumwinamia! Hakuamini alichokiona mbele yake.


“Sauda mke wangu umepatwa na nini? Kwa nini nilikutuma kwenda kuchukua dawa? Kwa nini nilikuwa na wazo baya? Maskini mke wangu nimekuponza, ulikuwa ukizungumza na wanawake wenzako, ona sasa umebadilika jina na kuitwa marehemu! Nini faida ya kazi yangu?” Mganga alilia kama mtoto mdogo huku akimgeuza mkewe ambaye alikuwa ameanza kupoa.


Ashura na mwanaume wake nao walikuwa wametoka na kushuhudia tukio lile. Balkis naye hakuwa mbali, moyo ulimuuma kwa kitendo chake cha kuyachukua maisha ya kiumbe kisicho na hatia.

Machozi ya damu yalimtoka.

Kila mganga alipokuwa anamlilia mkewe kwa maneno ya uchungu na yeye ndivyo alivyokuwa akiumia na kulia zaidi.


Ashura alipoangalia pembeni alishtuka baada ya kumuona Balkis akiwa katika kundi la watu huku naye machozi yakimtoka. Baada ya kumuona alipatwa na mshtuko mkubwa, akaanguka na kupoteza fahamu. Hali ile iliwatisha watu wote waliokuwa pale.


Mganga alimwacha mkewe na kukimbilia ndani kuchukua dawa ya unga kwa ajili ya kuzuia nguvu zozote mbaya.

Aliimwaga hewani lakini Balkis aliwahi kuondoka eneo lile na kwenda kukaa njiani kuwasubiri Ashura na mwanaume wake. Mganga baada ya kufanya vile bado hakuamini, aliuchukua mwili wa mkewe na kuuingiza ndani kujaribu tiba zote anazozijua akiamini atafanikiwa kumrudisha mkewe.

Alikuwa amesahau kuwa hakuna mtu wala kiumbe chochote dunia chenye uwezo wa kurudisha roho ya mtu au kiumbe zaidi ya Muumba peke yake.
Licha ya kuhangaika zaidi ya saa nzima kurudisha roho ya mkewe iliyopotea, bado hakufanikiwa.

Hatimaye alikubaliana na ukweli kwamba mkewe amefariki.

Ilibidi atoe taarifa za kifo cha mkewe kwa ndugu na jamaa, mipango ya mazishi ikaanza. Kutokana na kuchanganyikiwa na kifo cha mkewe alisahau hata kama kuna wateja aliokuwa akiwashughulikia.


Ashura baada ya kupata nafuu alijikuta akichanganyikiwa kwa kuamini kabisa kifo cha mke wa mganga kimefanywa na Balkis. Wasiwasi ulizidi kumpanda na kujiuliza kama ni yeye basi hata maisha yao yalikuwa hatarini.


“Tonny nimemuona Balkis?”
“Wapi?”
“Alikuwa kwenye kundi la watu.”
“Mwongo!”
“Kweli! Tena alikuwa analia machozi ya damu.”
“Mungu wangu! Unataka kuniambia aliyefanya haya ni yeye?”
“Inawezekana kabisa, si unakumbuka kauli aliyotoa kwa mzee Njiwa Manga kuwa kama angetusaidia angemuua mjukuu wake.”
“Sasa unafikiria anaweza kutufanyia kitu kibaya?”
“Hata mimi nimechanganyikiwa.”
“Sasa mganga atatusaidia nini?” Tonny aliuliza huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi.
“Wee! Tena nyamaza, inavyonekana sisi ndiyo chanzo cha kifo cha mkewe.”
“Kwa hiyo unaniambia nini?”
“Tuondoke, ikiwezekana tusirudi tena na Balkis tuachane naye,” Ashura alisema huku akitetemeka.

Wakati huo watu walizidi kusogea eneo la tukio, kila mtu alikuwa akisema lake juu ya kifo cha ghafla cha mke wa Kakakuona.


Wapo walioelezea jinsi walivyomuona njiwa yule akimpiga kichwani mke wa mganga na kutoweka kisha kuanguka chini na kupoteza uhai.


“Kweli kabisa Balkis ndiye aliyemuua mke wa Kakakuona,” Tonny alipata uhakika.


“Sasa unaona tumechokoza nyuki wakati hatuna mbio.”
“Sijui tufanye nini ili Balkis atuelewe?”
“Nimekueleza tuachane naye.”
“Atatuelewa?”
“Mmh! Kazi ipo, kama amejua tunataka kumuua unafikiri atatufanya nini?” Ashura alisema kwa sauti ya kukata tamaa.


“Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, kwa nini tusiendelee kuwa hapa ili mganga atupe hata kinga ili asitudhuru?”
“Tonny hebu kuwa na akili, umesikia aliyefanya vile ni Balkis mganga atatufanya nini, hiyo milioni mbili yako itarudisha roho ya mkewe?”
“Mmh! Na kweli, kwa hiyo unasemaje?”
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.55.

LIPOISHIA Jumamosi
“Nilikuwa na mambo yangu binafsi wala hayahusiani kabisa na majini,” Ashura alipindisha kwa kuamini mwanaume wake akijua kuwa alifuata dawa ya kurudiana na Muddy angekasirika.
SASA ENDELEA...

Ashura alikuwa na siri nzito moyoni mwake kama angefanikiwa kurudiana na Muddy, mwanaume aliyeamini kuwa bila ya mipango yao ya utapeli alikuwa ndiye sahihi kwake. Mpango wake ulikuwa kumuua mwanaume wake kwa kumuwekea sumu kwenye chakula ili aishi na Muddy katika maisha ya ndoa.

“Kama nilivyokueleza kabla ya kujua kuwa yule mwanamke ni jini, nilikwenda kwa ajili ya kuangalia jinsi ya kumuingia na kuweza kuchukua mali yake.
Lakini ilionesha si kiumbe wa kawaida na kama ulivyosikia, mzee Chujio alizidiwa nguvu na yule mwanamke. Lakini kwa mzee Njiwa Manga kutokana na historia ya watu hajawahi kushindwa suala la majini.”

“Tonny mbona hatuelewani nani ana majini mpaka twende kwa mzee Njiwa Manga?”
“Kumbuka tunataka mali ya Muddy na mkewe ambaye ni jini, huoni tunahitaji msaada wa mtu mwenye uwezo wa kupambana na majini.”

“Mmh! Kama ana uwezo huo kuna umuhimu wa kwenda kwake.”

“Hakuna njia nyingine kwa mambo niliyoyaona yamenitisha bila hivyo tunaweza kupotea.”

Walikubaliana kwenda siku iliyofuta kwa mganga Njiwa Manga ili kutafuta uwezo wa kupambana na Balkis.

****
Siku ya pili Ashura na mwanaume wake walikwenda Bagamoyo kwa mganga Njiwa Manga, kwa vile Tonny alikuwa hajakwenda kipindi kirefu, ilibidi aulizie sehemu anayoishi. Alielekezwa na kwenda moja kwa moja hadi nyumbani kwa mganga huyo, walipofika walikuta magari aina tofauti zaidi ya kumi kuonesha kuwa siku ile kulikuwa na wateja wengi.

Ilibidi wakae kwenye benchi kusubiri kwa muda mbele yao kulikuwa na wagonjwa zaidi ya ishirini, walijumuika pamoja na kusubiri tiba. Wingi wa watu ulitaka kuwakatisha tamaa na kutaka kuondoka.

“Tonny kwa nini tusiondoke turudi kesho mapema, huoni tutachelewa kutoka?” Ashura alimwambia mwanaume wake.

“Kwani tunawahi nini? Kwa vile tumeishafika hata usiku tutarudi, nataka nikueleze ukweli pamoja na kujionesha siogopi kitu, lakini siri niliyokuwa nayo moyoni ni Mungu tu anajua.

Kama yale maajabu yangerudia basi ningekufa kwa hofu.

“Nilikuona ulikuwa mwenye hofu kubwa na niliyasikia mapigo yako ya moyo yakikimbia kama gari lililokatika breki na kunifanya nisimame kidete,” alisema Tonny.

“Mmh! Wee acha tu, kama angezidisha ningekufa, yaani maneno yako yalinitia nguvu ya ajabu. Kwa kweli nimeanza kuwa muoga wa kila kitu hata upepo sasa hivi ukivuma naogopa najua amekuja,” alijibu Ashura.

“Wee acha, baada ya kugundua yule mwanamke ni jini niliishiwa nguvu na kuamini simuwezi kwa lolote zaidi ya kutumia nguvu za ziada kuja hapa kwa mzee Njiwa Manga ndipo penye ufumbuzi bila hivyo tutaumia,” alisisitiza Tonny.
“Kwa hilo hata tukikaa siku mbili sioni tatizo, sasa hivi namuogopa yule mwanamke kama kifo,” alimalizia Ashura.

Wakati wakibadilishana maneno hayo, Balkis hakuwa mbali na nyumba ya mzee Njiwa Manga, wakati alipokuwa akitoka kwa wazazi wake chini ya bahari aliwaona Ashura na mwanaume wake wakikaribia kuingia kwa mganga Njiwa Manga. Alijitahidi kuwawahi wasiingie, kasi yake iliishia nje ya uzio wa nyumba ya mganga huyo.

Alijipiga chini kwa hasira na kusababisha patokee mtikisiko mdogo uliowashtua watu, hakutaka kukubali kushindwa, alijigeuza njiwa na kwenda kwenye mti mrefu uliokuwa pembeni ya nyumba ya mganga Njiwa Manga.

Aliweza kuwaona wateja wa mganga huyo akiwemo Ashura na mwanaume wake, lakini nguvu za dawa za mzee Njiwa Manga zilimzuia asiweze kufanya lolote.

Akiwa na hasira alipanga kuwasubiri na kuwatia adabu baada ya kuonesha kiburi. Wasiwasi wake ulikuwa kwenye nguvu za yule mzee zingeweza kummaliza na kudhurumiwa mpenzi wake.
Kwa upande wa mali yake aliamini hakuwepo wa kuichukua kwa vile ilikuwa ndani ya uwezo wake.

Katika vitu alivyovipanga maishani mwake vilikuwa ni kubeba mimba ya Muddy kuwafanya wazazi wake hasa baba yake asiwe na nguvu ya kumlazimisha kuolewa na jini mwenzake.
Alijua kama Ashura akifanikiwa kupata kinga ya kumdhibiti, lazima atamnyang’anya mume wake na kumlazimisha kuendelea kufanya kazi asiyoipenda ya kuchukua vizazi vya wanawake.

Akiwa juu ya tawi la mti akichanganyika na ndege wengine, moyo ulimuuma na kujiuliza amfanye nini mganga ili asiwape uwezo wa kudhulumu haki yake. Alijikuta akiwachukia baadhi ya binadamu ambao aliamini kabisa hawakutakiwa kuhurumiwa zaidi ya kuuawa japo siku zote roho yake haikupenda kufanya vile.

Akiwa anawatazama wateja waliokuwa wakienda kupata tiba kwa mzee Njiwa Manga, aliwaona Ashura na mwanaume wake wakinyanyuka na kwenda kuonana na mganga huyo. Alijikuta akipandwa na hasira lakini eneo lile lilikuwa lina nguvu za ajabu zisizowezesha nguvu za kichawi na kijini kuingia katika himaya yake.

Alipotazama huku na kule, aliwaona wajukuu wa mganga wa Njiwa Manga wakicheza, akaamua kumuua mmoja.

Kwanini Balkis alitaka kumuua mjukuu mmoja wa mganga Njiwa Manga?
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.57.


ILIPOISHIA:
Mzee Njiwa alitoka nje na kurudi na kitezo chenye moto na kukiweka mbele yake, alitoa mavumba kwenye chupa na kusema:
“Hii dawa kazi yake kuyavuta majini mazuri, kama Balkis ni jini mbaya hatakuja nikimwita.”
Baada ya kusema vile alianza kuweka mavumba kwenye moto huku akisema:
“Balkis binti mfalme wa bahari, naamini wewe ni jini mwema nakuomba uje mbele yangu, lakini kama si jini mwema ukiingia himaya yangu ndiyo mauti yako...Balkis njoo mbele ya wanadamu hawa wana mashtaka juu yako.”
SASA ENDELEA ...

Moshi ulikuwa mwingi kiasi cha kujaa chumbani, baada ya muda upepo mkali ulianza kuvuma na kusababisha baadhi ya vitu kutaka kupeperuka lakini mzee Njiwa Manga aliutuliza kwa kusema:
“Najua una hasira lakini naomba uwe mpole kama ulivyo, wewe ni mpole tena mwenye upendo kwa wanadamu.”
Upepo ulitulia taratibu wakati huo Balkis akiwa katika umbile la njiwa alijikuta akizidiwa na nguvu na kudondoka toka juu ya mnazi na kujikuta akijitahidi asianguke na kuingia kwenye dirisha la chumba cha uganga cha mzee Njiwa Manga.
Alitua pembeni ya mzee Njiwa Manga, Ashura na mwanaume wake walishtuka kumuona njiwa mzuri sana mwenye rangi nyeupe aliyepakwa wanja mwekundu uliozunguka katika macho yake.
Manyoya yake yalikuwa kama ya plasitiki iliyokuwa ikimelemeta.
“Karibu Balkis kwa mzee Njiwa Manga.”
Balkis katika umbile la njiwa hakujibu kitu alitulia akiwatizama Ashura na mwanaume wake. Mzee Njiwa Manga alisema:”Najua hukupenda muda huu kuwa hapa, lakini nimekuita kwa nia njema kwa vile wewe ni jini mwema mwenye upendo kwa wanadamu. Nakuomba uwe kwenye umbile tunaloweza kuzungumza kibinaadamu.”
Baada ya kusema vile kilipita kiza cha ajabu na baada ya muda ilirudi hali ya kawaida. Sehemu aliyokuwa njiwa alikuwepo Balkis katika umbile la kibinaadamu.
Ashura na mwanaume wake kidogo wakimbie kwa hofu.”Msihofu, kama nilivyowaeleza kwa dawa niliyoichoma ni jini mwema tu anayeweza kuingia katika himaya yangu. Balkis asalam aleykumu.”
“Waaleiykum msalaam,” alijibu kwa sauti tamu.
“Karibu.”
“Asante.”
Balkis aligeuza uso wake na macho yake yaligeuka rangi na kutoa machozi ya damu, kitu kilichozidi kuwatisha Ashura na mwanaume wake.
“Hapana Balkis huna sifa hiyo wewe ni mpole nimekuita hapa kwa makusudi ya kuwaeleza hawa wanadamu ubaya wao mbele yako.” Mganga Njiwa Manga alisema huku akimshika kichwani na kumpigapiga taratibu kumpunguza hasira. Balkis alitikisa kichwa kuonesha amekubali.
“Balkis.””Abee.”
“Nataka uniambie unataka nini wafanye hawa wanadamu wajue wewe si adui yao?””Wanajua wenyewe, nilizungumza nao nini,” Balkis alijibu kwa sauti tamu kama kinanda.
“Naomba unieleze mbele yao.”
“Nikisema mimi nitaonekana muongo, napenda waseme kwa vinywa vyao.”
“Eti mlizungumza nini na Balkis?” mzee Njiwa Manga aliwageukia na kuwauliza.
“A...ali...nikataza nisimfuate mume wake ambaye ni mtalaka wangu,” Ashura alijibu katika hofu kubwa.
“Na kingine?”
“Tusimfuatilie maisha yake.”
“Mmefanya yote aliyowaeleza?”
Wote walibakia kimya wakitazama chini, mganga alimgeukia Balkis na kumuuliza.
“Wewe umeona nini?”
“Hawa walio mbele yako ni viumbe wabaya kuliko hata nyoka, wamepoteza maisha ya wanaume zaidi ya wanne na Muddy kama nisingemuwahi alikuwa wa tano. Wamekuwa na tabia za kuwatafuta wanaume na huyu mwanamke kujifanya anawapenda sana, kisha anajitambulisha kwa majina tofauti.
“Kila mwanaume anamfahamu kwa jina tofauti kama waliokufa kwa ajili yao wakisimamishwa mbele yake watamtaja kwa majina tofauti, Muddy anamtambua kwa jina la Ashura lakini wengine walimtambua kwa majini ya Fatuma, Hilki, Masha.
“Lakini jina lake halisi ni Shuuna, kwa utaalamu wako nina imani majina hayo yote umeyaona alipojitambulisha kwako na kujua sababu ya majina hayo?”
“Ndiyo,” Mzee Njiwa Manga alijibu kwa sauti ya chini.
“Hawa si viumbe wa kuonewa huruma hata mara moja, hebu angalia kila kukicha wamekuwa wakipanga mipango ya kudhulumu mali za watu na kuwatoa roho zao bila hatia kwa kigezo cha uzuri wa Shuuna. Hivi mimi na yeye nani mzuri?”
Balkis alinyanyuka na kujigeuza pande zote kuonesha ufundi wa Maulana kumuumba katika umbile la uzani.
“Ni wewe Balkis mwana wa mfalme wa chini ya bahari.”
“Mbona siui watu kama ninyi? Mtauliza kwa nini nilimuua mganga Chujio, kiburi chake kilimponza. Nilijua mtakwenda kule na kutaka kinga ya kupambana na mimi kama alivyowasaidia kudhulumu na kutoa roho za watu wasio na hatia. Lakini kwa busara zangu nilimuonya na kuonesha kiburi kwake ndicho kilichomponza.
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis).........EP.59.

ILIPOISHIA;
Walitoka huku wakiamini mzee Njiwa Manga uwezo wake wa kutibu umepungua ndiyo sababu ya kushindwa kuwasaidia kupambana na Balkis.
SASA ENDELEA...

BAADA ya kutoka kwa mganga wakiwa ndani ya gari lao walianza kujadiliana kuhusiana na maneno ya mzee Njiwa Manga.
“Sasa tutafanya nini?”
“Kwa nini tusiachane naye?”

“Mmh! Lazima atatufanyia kitu kibaya, si umemuona ametokwa na machozi ya damu kwa hasira, anaweza kutufanya kitu kibaya.”
“Sasa tufanyeje?”

“Lazima tutafute njia nyingine, unajua mzee yule nimemtoa akili, shida yake ni fedha na si kutaka kujua tutafanya nini.”
“Tena namshangaa anajifanya hataki fedha wakati anafanya kazi ile ili kusukuma maisha yake,” Ashura aliongezea.
“Ooh! Nimekumbuka kuna sehemu moja kuna mtaalam mmoja nina imani anaweza kutusaidia. ” Tonny alisema.

“Kama ni hivyo tusirudi nyumbani tupitie huko huko maana bado simuamini yule mwanamke amenitisha sana, lakini Tonny asiwe kama mzee Chujio tukaumbuka?”
“Namuamini ameshawahi kunifanyia mambo mengi ambayo sikuwahi kukushirikisha, y ule mzee huwa haulizi ukimueleza chochote hata kuua anafanya,tena anapenda kuua kama nini.”

“Tena huyo ndiye mzuri sana, lakini tutafika salama?” Ashura alikuwa na wasiwasi.
“Sifa ya yule mganga ukiwa na wazo la kwenda kwake kuanzia hapo unakuwa salama hakuna kitu cha kukuzuia.”
“Tena huyo anafaa, kwa nini hukusema mapema?”
“Nilimuamini babu yule baada ya kujua ana sifa ya kutatua matatizo ya majini.”

“Basi tuelekee, leo hatuna kazi nyingine zaidi ya kuujua mwisho wa Balkis.”
Safari ilielekea kwa mganga mwingine, njia nzima ilikuwa ni mitihani mingi kutokana na gari kuteleza bila utelezi na kuona mambo ya kutisha lakini safari iliendelea. Matukio hayo yalimtisha sana Ashura kufikia hatua ya kumuomba mwanaume wake wasitishe safari yao.
“Tonny kwa nini tusirudi huoni safari yetu imejaa matukio ya kutisha tunaweza kupata ajali mbaya na kufa?”

“Shuuna hivi ni vitisho vya Balkis baada ya kugundua tunakwenda kwa mganga mwenye uwezo wa kumuangamiza. Hawezi kutufanya lolote ni kuhangaika kwake kwa mfa maji tu.”
“Mmh! Yaani naogopa kuna kipindi niliona mti wa ajabu umetokea ghafla barabarani, nilijua tunakufa na kufumba macho, nilipofumbua nilishangaa kuona tumevuka salama.”

“Shuuna hizo ni hila za majini, ule si mti ni kiini macho tu ukiukwepa tu umeumia lazima gari litapinduka.”
“Jamani! Ningekuwa mimi ningeukwepa.”
“Lazima ungepinduka, barabara hii umepita mara ngapi?”
“Mara nyingi tu.”

“Huo mti uliwahi kuuona?”
“Sijawahi kuuona.”
“Basi mimi nimepasua katikati ya mti ule hakuna kitu kilichoizuia gari kupita.”
“Mmh! Kweli yule mwanamke ni jini.”

“Awe jini mara ngapi?”
“Tukipata dawa itatusaidia sana.”
“Hesabu tumemkomesha, yule bwana alisema katika dunia hii hawezi kurudisha roho ya mwanadamu tu, kwa vile ni kazi ya Mungu peke yake. Lakini chochote kinachowezekana kwa mwanadamu kwa uwezo wa Mungu anakifanya kwa ukamilifu.”

Baada ya kufanikiwa kuvuka vizingiti vya Balkis walifika Vingunguti walikata kushoto njia ya kuingia Jeti Rumo, waliifuata njia ile mpaka maeneo ya Kijiwe Samli. Tonny alisimamisha gari mbele ya duka moja ambapo pembeni yake kulikuwepo na vijana wakicheza drafti.
“Tumefika,” Tonny alisema huku akizima injini ya gari.
“Mbona yupo kwenye makazi ya watu?” Ashura aliuliza.

“Siku hizi huduma zimewafuata watu, hakuna waganga wa kizamani kuwa kijijini nyumba za majani. Waganga wa siku hizi wanakwenda na wakati hata mavazi yao si kaniki na ngozi na shanga kibao.”
Baada ya kufunga gari na kuliacha katika hali ya usalama aliifuata njia ya uchochoro kati ya nyumba ya duka na ya kawaida na kutokea mtaa wa pili walikata kulia kuelekea kwa mganga.

“Tonny huku umepajuaje?”
“Kuhangaika, unafikiri kama tungekuwa tunamtegemea mzee Chujio peke yake ingekuwaje?”
“Mmh! Na kweli, ona kama alivyotutoa nishai yule mzee sijui kunguru, baada ya kifo cha mzee Chujio tungekwenda wapi?”
“Atajijua mwenyewe kama anaitwa Njiwa au bundi, mzee yule kanichefua hana lolote kumbe sifa za uongo.” Tonny alimkandia mzee Njiwa Manga.

Nini kitaendelea? Kweli mganga huyu ana uwezo wa kumdhibiti Balkis?
 
 
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.61.


Ilipoishia:
ILE ilimfanya akose raha na kutokwa na machozi, alipata wazo la kuwahi chini ya bahari kabla uchawi wa kumuua haujafanywa. Lakini alikumbuka ana deni na baba yake la kuachana na Muddy mwanaume aliyepanga kuachana naye baada ya kumpa ujauzito ambao wazazi wake hawatakuwa na nguvu na kumruhusu aishi naye.
Sasa endelea...

ALIJIKUTA akiuapia moyo wake kuwa atapigana mpaka tone la mwisho la damu yake lakini hatarudi chini ya bahari. Akiwa amesimama pembeni ya nyumba kwenye mti wa jirani katika umbile la njiwa, alijiuliza atafanya nini ili aweze kujiokoa na hatari ile.

Alishuhudia Ashura akitoa laki tano kwenye mkoba na kumpatia mganga ambaye alinyanyuka ili akachukue vifaa vya kutengengeneza dawa ya kummaliza. Balkis juu ya mtu alijikuta akipoteza uwezo wake wa kawaida baada ya kuamini wakati wowote anaweza kufanyiwa kitu kibaya.

Alijua waganga wengi huwavuta majini kwa dawa na kuwamaliza, akiwa ametota kwa jasho kwenye manyoya yake kwa hofu ya kifo. Alimuona mganga akitoka uani kwake na kumwita mkewe aliyekuwa akizungumza na wanawake wenzake.
“Mke wangu,” alimsikia akimwita mkewe kwa sauti ya juu kidogo.

“Abee mume wangu,” alimuona mkewe aliyekuwa amevalia nguo na vito vya dhahabu kila kona kuonesha kwamba wanaishi maisha ya kifahari.
“Hebu nenda dukani kaniletee ile kiboko ya majini.”

“Kuna mtu ana jini nini?” Alimuuliza huku akipokea fedha.
“Kuna jini mmoja anawakosesha raha wateja wangu.”
“Sasa unataka kumfanya nini, unataka kumtia kwenye chupa nini?”

“Namuulia mbali, unajua jini ukilifungia kwenye chupa likitoka linaweza kukumaliza. Dawa yake sasa hivi ni kulimalizia mbali, itakuwa wakijua wanakuja Kakakuona watakuwa wanakimbia wenyewe.”
“Ngapi nichukue?”

“Kwa vile nammaliza kazi kabisa nichukulie tano na ndimu kumi na nne na sindano kumi na nne.”
“Mmh! Mbona nyingi sana leo umepania.”
“Nimemuona ana kiburi, pia ana mchezo wa kutaka ushindani, nikimfunga anaweza kutoka, si unajua siku hizi watu wakikuta kitu lazima wakifungue.”

Kauli ile ilimshtua Balkis ambaye aliamini siku ile ndiyo ilikuwa ni mwisho wa maisha yake, wazo la haraka lilikuwa ni kurudi kwao na kuwa tayari kukubaliana na matakwa ya baba yake ya kuachana na Muddy ili awe salama.
“Mmh! Haya kazi kwenu,” mkewe mganga alisema huku akitokea mlango wa nyuma kwenda duka la dawa za asili.

Balkis alimuangalia mke wa mganga na kumuona ni mweupe asiye na kinga imara ya kuzuia nguvu za majini, kutokana na kukataa kuchanjwa na mumewe. Kwa vile mumewe alimpata baada ya kuja kutibiwa kutafuta dawa ya kuolewa na kigogo mmoja na mganga akamgeuzia kibao cha kutengeneza dawa ambayo ilimfanya yule mwanamke ampende mganga badala ya mtu aliyemkusudia.

Baada ya kufanikiwa kumpata, ilibidi akubaliane na mkewe ambaye hakutaka kuishi kiganga zaidi ya maisha ya kifahari ya kujirusha kwa kutembelea gari. Kutokana na uwezo wa mganga wateja wake wengi walikuwa watu wenye uwezo hivyo kumfanya asiwe na shida ya fedha ndogo ndogo.

Pamoja na mkewe kutoishi kama mke wa mganga na muda wote kuvaa nguo na vito vya thamani, bado alikuwa akijua baadhi ya dawa ambazo zilikuwa zikitumiwa na mumewe.
Hata pale mumewe alipokuwa safarini alielekezwa jinsi ya kuzitengeneza na kuwapa wateja lakini mumewe alipokuwa nyumbani yeye aliendelea na maisha yake ya kujiachia.

Balkis aliona ile ndiyo nafasi yake ya kufanya kitu kitakachomfanya mganga asifanye lolote juu yake. Alikurupuka kutoka juu ya mti kama njiwa na kumgonga kichwani mke wa mganga ambaye alikwenda juu na aliporudi chini hakuomba hata maji.

Waliokuwepo pembeni walimuona njiwa mweupe akimgonga kichwani na kupotea katika mazingira ya kutatanisha. Kelele na kilio cha mtu aliyeingia kwa mganga zilimshtua mganga aliyekuwa ameanza kuandaa vifaa vya kummaliza Balkis. Aliacha na kutoka na kukutana na mfanyakazi wake wa mapokezi.

“Vipi?” alimuuliza baada ya kumuona amechanganyikiwa.
“Mama.”
“Amefanya nini?”
“Ame....”

“Yupo wapi?” aliuliza huku presha imempanda.
“Yupo nje ya nyumba.”
“Kafanya nini?”
“Si...sijui.”

Mara alisikia sauti za vilio vya mashoga wa mkewe ambao walikuwa wakizungumza naye muda mfupi uliopita, vilio vile vilizidi kumtisha na kumchanganya.
“Jamani kuna nini?” Aliuliza tena macho yakiwa yamemtoka pima.
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.63.

ILIPOISHIA
“Hatuna jinsi
“Huu si wakati wa kulaumiana tutafute njia ya kujiokoa kwa Balkis.”

“Mmh! Huoni tukitafuta mganga mwingine ni sawa na kuongeza mafuta kwenye moto?”
“Sasa tutafanya nini?” Tonny alionesha kuchanganyikiwa na kusahau kama wanatakiwa kuondoka eneo lile na badala ya kujilaza kwenye usukani.
SASA ENDELEA...

“Tonny hebu ondoa gari kama huwezi nipishe miye niendeshe.”
“Ashura njoo uendeshe nina imani Balkis anajua mimi ndiye mbaya wake namba moja, hata sijui itakuwaje?”
“Tonny we twende nyumbani lolote litakalotokea tuwe tayari kukabiliana nalo.”

“Mmh! Haya sina jinsi yaani najuta kumfahamu Balkis.”
“Lakini si tumeambiwa ni kiumbe mwenye huruma?”
“Si umesema umeona akitokwa na machozi ya damu kuonesha hasira unafikiri mtu tuliyetaka kumuua atakuwa na huruma na sisi?”

“Bwana wee hebu tuondoke mengine tutayajua huko huko.”
Tonny alijikaza na kuwasha gari kisha waliondoka eneo la Kiwalani, Balkis aliwaona kwa mbali wakija, akiwa amejawa na hasira kutokana na kiburi walichokionesha alikosa adhabu inayowafaa kutokana na roho zao mbaya ili wasirudie tena kumfuatafuata. Adhabu aliyoipanga ilikuwa kuhakikisha kwanza anamtia aibu Ashura na mumewe kwa kumgeuza kiumbe wa ajabu asiyependwa na wanadamu au wanyama.

Hakutaka kuwasumbua aliwaacha warudi mpaka nyumbani kwao ili aweze kufanya alichokikusudia. Ashura na mwanaume wake walishangaa kwenda mpaka nyumbani kwao bila kukutana na tatizo lolote, walipofika walishukuru Mungu.
Baada ya kuingia ndani hata kabla hawajakaa vizuri mlango uligongwa, Tonny alikwenda kuufungua na Ashura alikwenda chumbani. Alipofungua alipatwa na mshtuko uliomfanya aanguke chini na kupoteza fahamu.

Ashura aliyekuwa chumbani alishitushwa na kishindo cha mtu kuanguka chini, alimwita mwanaume wake huku akitetemeka ili ajue kimetokea nini.
“Toooni,” aliita kwa sauti ya juu bila kupata jibu, woga ulimwingia.

Alirudia tena kumwita Tonny bila jibu lolote, alitoka chumbani huku akiwa na wasiwasi, kabla ya kufika sebuleni alisikia harufu ya manukato aliyoyazoea kuyasikia wakati Balkis akiwa karibu yake. Harufu ile ilimjulisha tayari walikuwa wamevamiwa ndani ya nyumba yao.

Mlangoni alikuwepo Tonny aliyekuwa amelala chini, alianza kutetemeka. Akiwa bado katika hali hiyo, mlango uligongwa tena, alitamani kurudi chumbani kwake lakini alijikaza na kusogea hadi mlangoni na kuufungua. Alipofungua alikutana uso kwa uso na Balkis, kwa woga alioupata haja ndogo ilimtoka bila kutarajia.
“Samahani Balkis,” aliomba msamaha huku akipiga magoti kwa kujua kiama kimefika.

“Ya nini?”
“Najua nimekukosea.”
“Kosa gani?”
“Unajua, naomba usituue.”

“Kuua ni kazi ya Mungu peke yake si ya kiumbe chochote.”
“Mbona ume..,” Ashura alisita kusema Balkis kamuua mke wa mganga Kakakuona kwa kuhofia kumzulia jambo ambalo huenda hakulitenda na kumuongezea hasira.
“Nimefanya nini?”

“Hujafanya kitu.”
“Najua ulitaka kusema nini.”
“Ha...ha...pana,” Ashura alitetemeka kwa hofu.
“Kwanza mmwagie maji mwenzako azinduke, nashangaa anakuwa mwoga wakati yeye ni bingwa wa kutoa roho za watu.”
“Naomba unisamehe Balkis najua kiasi gani tumekuudhi.”

“Hebu fanya kwanza niliyokuagiza,” Balkis alisema kwa sauti kali kidogo.
Ashura alikwenda jikoni na kurudi na maji kwenye bakuli.
“Mmwagie kidogo kichwani.”

Ashura alifanya kama alivyoelekezwa, baada ya kumwagia maji mwanaume wake alirudiwa na fahamu. Tonny alipozinduka alishtuka kujikuta yupo mbele ya Balkis. Alinyanyuka na kupiga magoti mbele ya Balkis kuomba msamaha.
“Samahani Balkis najua umekuja kutudhuru, lakini tunakuhakikishia hatutarudia tena kukufuata,” Tonny alisema huku akitokwa na machozi.

“Kabla ya kuzungumza lolote naomba Ashura aende akajisafishe, siwezi kuzungumza na mtu aliyejipaka najisi.”
Ashura alikwenda bafuni kujisafisha kisha kubadili nguo na kurudi mbele ya Balkis bila kujua nini hatima yao baada ya kumchokonoa kwa muda mrefu. Baada ya kurudi alisogea kwa mwanaume wake na kuungana naye kupiga magoti.

“Naomba mkae chini, magoti yenu yataniongeza hasira niwageuze kuwa manyani”
Baada ya kukaa alimuuliza Ashura swali lake la awali.”
“Ashura, uliuliza mbona nimemuua mke wa mganga?”

“Ha...ha...pana sikumaanisha hivyo.”
“Naona unataka kunichefua nikugeuze kuwa nyoka sasa hivi muuaji mkubwa, hivi mimi nikifa ninyi mtafaidika nini?”
Hakuna aliyejibu kitu, wote walibakia kimya nyuso zao wamezielekezea chini kwa aibu.
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.64.


ILIPOISHIA:
“Naomba ukae chini, magoti yenu yataniongeza hasira niwageuze nyani.”
Baada ya kukaa alimuuliza Ashura swali lake la awali.”
“Ashura ulisema mbona nimemuua mke wa mganga?”
“Ha..ha..pana sikumaanisha hivyo.”

“Naona anataka kunichefua nikugeuze nyoka sasa hivi muuaji mkubwa wewe, hivi mimi nikifa ninyi mtafaidika nini?”
Hakuna aliyejibu kitu, wote walibakia kimya wakiwa wameangalia chini kwa aibu. SASA ENDELEA...

“Kwa kweli wanadamu ni viumbe wenye kiburi kuliko kiumbe chochote kilichoumbwa na Mungu. Matendo yenu mabaya kuliko hata ya shetani. Shetani siku zote humvuta mtu kwenye dhambi lakini si kuua. Ninyi kila kukicha mnatoa roho za watu kwa ajili ya mali.

Mmesababisha nimuue mke wa mganga bila sababu kutokana na nia yenu ya kuhakikisha nakufa. Jamani kosa langu nini, kama Hemed mliachana baada ya kumfilisi, sasa hivi umemuona mzuri?”
Ashura hakujibu kitu, aliendelea kuinama na kumfanya Balkis aendelee kuzungumza kwa hasira huku machozi ya damu yakizidi kuichafua nguo aliyokuwa amevaa.

“Kwa vile mmekuwa kenge msiosikia mpaka mtoke damu masikioni, sasa chagueni adhabu yoyote ila iwe mbaya kuliko zote zilizowahi kutolewa chini ya jua.”
“Tunaomba utusamehe,” walisema kwa pamoja huku wakitamani kunyanyuka kwenda kumlamba miguu.
“Sitawasamehe, lazima niwape adhabu kubwa sana ambayo hata mimi mtekelezaji itaniuma moyoni mwangu kwa jinsi mtakavyoteseka,” Balkis alisema kwa hasira.

Wote walibakia kimya wakishindwa kujua wachague adhabu ipi, kila adhabu waliyoifikiria ilikuwa nzito kwao. Baada ya kukaa kimya, Balkis alisema huku akitembea taratibu ndani ya nyumba na kuifanya nyumba inukie vizuri:
“Ashura, adhabu yako ya kwanza ni kutembea uchi mbele za watu kama tulivyokubaliana, baada hiyo itafuata nyingine ambayo nitaijua mwenyewe.”
“Na wewe,” alimgeukia Tonny aliyekuwa amejikunyata kwa hofu ya maisha yake.

“Tena wewe ndiye nitakayekufanya kitu kibaya, kwanza nitakugeuza nzi wa kijani maisha yako yawe chooni na jalalani, adhabu nyingine nitajua hapo baadaye.”
“Ni semehe Ba..ba..lki....”
“Shatap mashetani nyie,” alimkata kauli kwa sauti kali.
“Nina imani mzee Njiwa Manga aliwaeleza vizuri japo mwanzo hata mimi niliwaeleza lakini mlijitia viburi, sasa kiburi chenu kitawatokea puani.”
“Tusamehe hatutarudia tena.”
“Hebu niambieni kosa langu nini?” aliwauliza huku akiwa amewakazia macho.
“Hu..hu..na kosa.”
“Sasa kwa nini mnataka kuniua?”
“Tu..tu..sa..sa..mehe.”
“Nina imani uwezo wangu mlikuwa hamuufahamu lakini leo ndiyo mtaujua.”
“Balkis haki ya nani tunakuahidi hatutarudia tena,” walirudia kupiga magoti mbele yake.

“Hivi mngefanikiwa kuniua haya magoti mngempigia nani? Kumbukeni nimepata dhambi kwa ajili ya mtu mwingine hivyo lazima nitimize nilichopanga kuwafanyia.”
Wakati wakizungumza yale, Balkis alihisi mabadiliko mwilini mwake yaliyomfanya ahisi kizunguzungu kikali.

Kwa haraka alishika kwenye paji la uso na kutoweka mle ndani. Ile hali ilimtisha na kuamua kwenda moja kwa moja chini ya bahari kuwahi kujisalimisha kwa wazazi wake. Wasiwasi wake ulikuwa huenda mganga ameamua kulipa kisasi baada ya mkewe kuuliwa.

Akiwa amechoka alijivuta huku kizunguzungu kikizidi, akatembea kwa kujivuta huku akipepesuka lakini alipofika lango kuu la kuingilia kwenye jumba la mfalme alianguka chini na kupoteza fahamu. Vijakazi na watwana walifika na kumuokota hadi ndani ya jumba kuu akiwa hajitambui kabisa.

Malkia Huleiya alishtuka kupata taarifa za kuletwa Balkis akiwa hajitambui, akiwa na kanga mkononi alikimbilia sebuleni na kumkuta Balkis akiwa amelazwa chini akiwa hajitambui.

“Amefanya nini?” aliuliza kwa mshtuko.
“Hatujui Malkia Mtukufu,” walijibu kwa pamoja.
“Mmemkuta wapi?”
“Lango kuu Malkia Mtukufu.”
“Mpelekeni chumbani mara moja.”
Walimbeba na kumpeleka chumbani na kumlaza kitandani, baada ya kumlaza walitoka.

Malkia Huleiya alichanganyikiwa na kujiuliza mwanaye kafanywa nini na wanadamu. Alijua ile itakuwa vita na wanadamu ambao ni viumbe hatari aliokuwa akiwaogopa usiku na mchana.
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.65.


“Mpelekeni chumbani mara moja.”
Walimbeba na kumpeleka chumbani na kumlaza kitandani, baadaye walitoka. Malkia Huleiya alichanganyikiwa na kujiuliza mwanaye kafanywa nini na wanadamu. Alijua ile itakuwa vita na wanadamu ambao ni viumbe hatari aliokuwa akiwaogopa usiku kucha. SASA ENDELEA...

ALITAKA kwenda kumwita mumewe Mfalme Barami aliyekuwa kwenye kikao na baraza lake la mawaziri lakini alipata wazo la kumfuata mganga mkuu Bunusa ili akaangalie hali ya Balkis. Alimtuma mtwana kumfuata mganga mkuu Bunusa.
Bunusa alifika mara moja na kupelekwa chumba alichokuwa amelazwa Balkis ambaye muda wote alikuwa amepoteza fahamu.
“Bunusa naomba msaada wako hali ya mwanangu ni mbaya sana.”

“Hakuna tatizo,” Bunusa alisema huku akifungua mkoba wenye vitendea kazi.
Alimshika Balkis kichwani, kifuani, tumboni na miguuni kisha alimshika kwenye paji la uso na kutulia kwa muda akipata ripoti za uchunguzi wa mwili wake. Baada ya muda alipumua pumzi nyingi kuonesha kuna jambo. Malkia Huleiya akimfuatilia kutaka kujua vipimo vile vina majibu gani.

Baada ya kuvuta pumzi ndefu alimgeukia Malkia Huleiya na kumwambia:
“Balkis haumwi ugonjwa wa kutisha ni hali ya kawaida.”
“Bunusa, Balkis hajatokewa na hali hii toka nilipomzaa, leo atokewe na tukio la kutisha useme hana ugonjwa wa kutisha?”

“Nimesema hali aliyonayo si ugonjwa, ila tatizo kubwa ni uchovu, inaoneka kafanya kazi kwa mwezi mzima bila kupumzika. Kutokana na hali aliyokuwa nayo lazima hali hii imtokee.”
“Hali! Hali gani hiyo?”
“Ya ujauzito.”

“Unasema ana nini?”
“Ana ujauzito ambao hakujua kama anao na ndiyo uliomfanya kuchoka baada ya kufanya kazi nzito.”
“Mungu wangu ujauzito wa nani, wa jini au mwanadamu?” Malkia Huleiya aliuliza huku akiweka mkono wake kifuani kuzuia mshtuko.
“Wa mwanadamu.”

“Ooh! Mbona mwana huyu amenitafutia matatizo, baba yake nitamweleza nini anielewe.”
“Ni kweli hili ni tatizo inaonesha taarifa hizi za kupata ujauzito wa mwanadamu zitakuwa na mpasuko mkubwa ndani ya familia.”
“Sasa nitafanya nini? Tuutoe kabla baba yake hajajua?”

“Mmh! Katika kosa lingine kubwa mtakalofanya ni kuutoa ujauzito huu, nia kubwa ya mwanao ni kubeba ujauzito na kuzaa na mwanadamu kisha arudi kwa baba yake kwa kuamini hatakuwa na jinsi tena ya kuzuia matakwa yake.”
“Ooh! Sasa Bunusa utanisaidia kitu gani ili kutoleta mtafaruku mkubwa.”
“Dawa ni kumrudisha duniani ili aendelee na maisha yake na mumeo asijue chochote.”
“Tutafanyaje?”

“Nitampa dawa ya kumrudisha katika hali yake kisha arudi duniani kuendelea na maisha yake.”
“Lakini watwana na vijakazi wanajua alikuja, si watamwambia?”
“Hao ni wa kuwaita na kuwaeleza wasizungumze chochote kuhusiana na Balkis na kutoa vitisho vikali.”
“Sawa nitafanya hivyo.”
Mganga mkuu Bunusa alianza kumshughulikia Balkis kwa kumnusisha dawa iliyomfanya apige chafya na kuzinduka. Balkis alijishangaa kuwa mbele ya mama yake na mganga mkuu Bunusa.

“Mama,” alimwita kwa sauti ya chini.
“Abee mwanangu, unaendeleaje?”
“Sijambo kidogo, baba yupo wapi?”
“Yupo kwenye baraza na mawaziri wake.”

“Mmh! Siamini kama nipo salama, asante Bunusa nilijua ndiyo basi.”
“Ndiyo basi kwa vipi?” Malkia Huleiya alimuuliza mwanaye.
“Nilijua mganga niliyemuulia mke wake kaamua kunimaliza.”
“Ni kweli alikuwa na wazo la kukumaliza lakini kiburi chako ndicho kilichokusaidia,” mganga Bunusa alisema.
“Ni kweli alinitumia kombora?”

“Walaa.”
“Sasa nini kile?”
“Ni kizunguzungu kikali, inaonesha umefanya kazi ngumu bila kupumzika na kusababisha uchoke sana.”
“Mmh! Mbona kazi hiyo ni ndogo, nimekwishafanya nyingi zaidi ya hizo bila matatizo.”
“Ni kweli, lakini sasa hali yako haikuruhusu kuusumbua mwili kwa muda mrefu.”
“Hali! Hali gani?”

“Ya ujauzito.”
“Ujauzito?” Balkis alishtuka huku akishika mikono kifuani kwake.
“Eeh, vipi hukuutegemea?” Bunusa alimuuliza.
Swali lile ambalo lilikuwa zito kulijibu mbele ya mama yake, Malkia Huleiya alimgeukia mwanaye aliyekuwa bado amekaa kitandani.
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.67.

ILIPOISHIA;
Balkis baada kurudi kutoka chini ya maji alikuwa na furaha isiyo na kifani alipogundua dhamira yake ya kubeba ujauzito wa mwanadamu imetimia. Alimkuta Muddy akiwa amejilaza kitandani, alipofika alimkumbatia na kumbusu, japo jambo lile lilikuwa ni la kawaida kila alipoondoka na kurudi baada ya kukaa siku moja bila kuonana na mpenzi wake. SASA ENDELEA...

LAKINI siku ile furaha iliongezeka mara mbili kitu kilichomshtua Muddy.
“Vipi mpenzi kulikoni mbona una furaha sana?”
“Muddy niambie zawadi yoyote unayoitaka kwangu nikupe.”
“Ya upendo.”

“Muddy ya kitu kingine kwani hakuna kiumbe nitakayempenda chini ya jua kama wewe.”
“Sihitaji zawadi zaidi ya hiyo.”
“Basi mimi nakuchagulia zawadi ya kuyafanya maisha yako yawe kama ya peponi hata kama sipo.”
“Ina maana unataka kuniacha?’

“Hapana mpenzi ni tahadhari tu, mimi ni kiumbe siwezi kuishi milele.”
“Nashukuru kwa hilo.”
“Nikwambie kitu?”
“Niambie.”

“Nina ujauzito wako.”
“Utani huo!” Muddy alishtuka kusikia vile.
“Ndiyo maana nimejawa na furaha isiyo na kifani na nikifanikiwa kujifungua salama nitakupa zawadi kubwa sana isiyo na mfano.”

Balkis alimkumbatia Muddy kwa furaha huku akiomba ajifungue haraka kabla baba yake mfalme Barami hajatimiza dhamira yake ya kuvunja mpango wa uhusiano wake na Muddy ili aolewe na jini mwenzake.
****
Balkis baada ya kupata habari njema za kupata ujauzito wa Muddy, alikuwa mwenye furaha kupita kiasi. Lakini aliamini furaha yake ingekamilika baada kuwakomesha wabaya wake. Adhabu aliyoipanga ingemfanya aishi kwa furaha mpaka muda wa kujifungua lakini hakutaka kuwaua.

Wakati akipanga adhabu ya kuwapa Ashura na mwanaume wake, upande wa pili ulishangaa kuona siku zikikatika bila kusikia chochote kutoka kwa Balkis. Waliamua kufanya kazi zao kama kawaida huku wakiachana kabisa na Balkis.
Ashura akiwa katikati ya mji akiendelea na mambo yake ya ununuzi wa vitu muhimu kwa ajili ya matumizi ya nyumbani. Balkis naye alikuwa karibu yake bila mtu yeyote kumuona. Alipomkaribia aliokota udongo kidogo kisha alimpulizia mwilini.

Ashura akiwa amebeba mfuko mkubwa akielekea kwenye gari alihisi kama kuna vitu vinamuwasha mwilini. Ilibidi aweke mzigo chini ili ajikune kwanza, kila muda ulivyozidi kwenda ndivyo alivyohisi nguo zake zikimuwasha kama vile zimemwagiwa upupu.

Alianza kuvua nguo huku akipiga kelele za kuwashwa, kila mtu alishtuka na kumshangaa kumuona mwanamke akivua nguo zote na kubakia mtupu. Wasamaria wema walimsogelea na kumvisha lakini alizikataa nguo zake na kusema zinamuwasha.

Ilikuwa ni kihoja Ashura aliadhirika mbele ya watu, kila alipopewa nguo na kinamama waliokuwa wameshikwa na mshangao kumuona mrembo kama yule akionekana amepandwa na mapepo. Ashura aliondoka pale na kuanza kutembea bila ya kuwa na kitu mwilini, alielekea baharini.

Ilikuwa ni adhabu aliyokubaliana na Balkis kama atamfuata Muddy aliyekuwa mumewe wa zamani. Baada ya kuridhika na adhabu yake alimtokea kwa mbele akiwa na upande wa kanga. Ashura alipomuona alipiga magoti kumuomba msamaha.
“Balkis najua jinsi gani tulivyokukosea lakini sasa hivi tumeachana na wewe, naomba utusamehe.”
“Adhabu ya kutembea uchi nani aliichagua?”

“Mimi.”
“Sasa mbona hukutaka kutembea uchi baada ya kujua kabisa dhamira yako ilikuwa nini juu ya Muddy?”
“Nisamehe Balkis.”
“Balkis unayemuomba akusamehe angefariki ungemuomba nani msamaha?”

“Najua tulikuwa na dhamira mbaya kwako lakini tumegundua makosa yetu tunakuahidi hatutakufuata tena.”
“Nilikuonyeni mara ngapi, kama ningekuwa na roho mbaya hata mali ya Muddy usingechukua. Lakini nilifanya vile ili muachane na mpenzi wangu, bado hamkusikia mliendelea kunichokonoa, kuonesha sitaki kuwafanya lolote nilimuua mganga wenu lakini bado mliendelea kunitafuta.

“Mzee Njiwa Manga alitukutanisha mbele yake na kukuonyeni lakini bado mliona labda utani na kufikia hatua ya kumdharau kuwa hana uwezo wa kukabiliana na mimi. Mkaamua kwenda kwa mganga mwingine kwa lengo la kuchukua mali yangu na kunimalizia. Hebu nieleze ni kiumbe gani mwenye moyo wa uvumilivu wa kiasi hicho?”
“Hakuna.”

“Basi adhabu yangu ya awali ya kukutembeza uchi baada ya wewe mwenyewe kutamka kwa mdomo wako imetimia kama utamfuata Muddy. Ya pili nitakugeuza mbwa atakayeishi kwa mateso mpaka hapo nitakapojifungua salama. Kama mwanangu akifariki na wewe na mumeo mtakufa.”

“Ni...ni...ni..sa...sa...,” hakumaliza kusema alitemewa mate usoni na Balkis huku akisema:
“Kuwa mbwa mweusi.”
Ashura aligeuka mbwa mweusi, Balkis aliendelea kusema:
Kazi imeanza Ashura ameshageuzwa mbwa.
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.68.

ILIPOISHIA;
Ya pili nitakugeuza mbwa atakayeishi kwa mateso mpaka hapo nitakapojifungua salama.

Kama mwanangu akifariki na wewe na mumeo mtakufa.”


“Ni..ni..ni..sa..sa..,” hakumaliza kusema alitemewa mate usoni na Balkis huku akisema:
“Kuwa mbwa mweusi.”


Ashura aligeuka mbwa mweusi, Balkis aliendelea kusema:
SASA ENDELEA...

“Hii ni adhabu itakayokufanya uhangaike, hutapendwa na wanadamu mpaka hapo utakapotoka kifungoni na sasa namfuata mwanaume wako, naye ana adhabu kubwa kuliko hii.”

Balkis baada ya kusema vile aliondoka na kumuacha Ashura kwenye umbile la mbwa asijue aende wapi. Wazo lilikuwa kuendelea kuwa pale ufukweni mpaka jioni ndiyo aende kwake.

Nyumbani, Tonny alikuwa akijiandaa kwenda kwenye mihangaiko yake akiamini kabisa Balkis aliamua kuwasamehe.

Alikuwa anakwenda kwenye kabati kuchukua glasi ili anywe juisi kabla ya kuondoka.

Hakujua kama Balkis tayari yumo mle ndani na alikuwa na hasira za ajabu baada ya kujua Tonny ndiye aliyekuwa na kimbelembele wa kumuua.


Wakati anakwenda kwenye kabati alimpulizia vitu kama matone ya maji, Tonny alishtuka lakini hakujali sana. Alipokaribia kwenye kabati alishtuka kujiona amegeuka kiumbe wa ajabu.

Kilichomshangaza ilikuwa ni kujiona kwenye kioo mwili wake ukiwa umeota mizizi na kutoka damu.

Tonny alishtuka na kujiangalia, akawa anashangaa kuuona mwili wake ukiota mizizi iliyoingia ardhini huku ukitoa damu.

Alianza kusikia maumivu makali zaidi ya mtu aliyeng’olewa jino bila ganzi.

Alijiuliza yale mateso makali yanatokana na nini na kwa nini aote mizizi mwilini kama mti lakini hakupata jibu.


Balkis alimwacha apate mateso makali kwa kuongeza kumpulizia maji maji mwilini na kuufanya mwili wa Tonny utoe ufa, kila sehemu ya mwili ilipasuka, damu zilimtoka na maumivu yake yalikuwa makali sana.

Kila alipopiga kelele kuomba msaada sauti yake haikutoka.


Alitamani ardhi ipasuke ili immeze lakini haikuwezekana.

Alishangaa kuona damu yake iliyokuwa ikitoka mwilini, kila ilipondondoka chini ilipotea, akajiuliza inakwenda wapi lakini hakupata majibu.

Maumivu aliyoyasikia hakukuwa na mfano wake. Alilia mpaka machozi yalimkauka kutokana na maumivu kuongezeka ukali kila dakika kutokana na mwili wake kupasuka kila kona.


Balkis alitoa adhabu ile kwa zaidi ya saa mbili kisha alijitokeza mbele yake, Tonny alipomuona alishtuka na kutamani kumlamba miguu lakini hakuweza kutembea baada ya sehemu ya mwili wake kuzama chini ya ardhi.

Kila alipofumbua mdomo kuomba msamaha sauti haikutoka akawa anarusha mikono kama anaimbisha kwaya bila ujumbe wake kumfikia mlengwa.


Balkis alisimama na kumtazama kwa hasira, mara machozi ya damu yalimtoka akifikiria ampe adhabu gani kubwa kuliko zote alizowahi kumpatia kiumbe aliyemchukiza.

Alitamani kumchuna ngozi na kumwacha atembee na maumivu bila kufa lakini alikumbuka adhabu ya kupasua pasua mwili ilikuwa inatosha kwani maumivu yake yalitofautiana kidogo na mtu aliyechunwa ngozi bila ganzi.

Tonny aliendelea kurusha mikono kuomba msaada kama mtu aliyekuwa anataka kukata roho.


Aliusikia mwili wake ukiwa umekauka kama kipande cha kuni kilichopigwa na jua kwa muda mrefu.

Ulimi nao ulikauka kama mti na kushindwa hata kuunyanyua.

Yalikuwa mateso makali kuliko hata shetani motoni, moyoni Tonny alijiapia kama atatoka salama kwenye mateso yale mazito asingerudia tena kufanya makosa.

Aliona kuokoka kwake ni sawa na ngamia kupita katika tundu la sindano.


Balkis alijikuta akiingiwa na huruma, alisogea karibu na kumshika kichwani.

Dakika ileile Tonny alirudi katika hali ya kawaida lakini bado mwili wake ulimuuma kama kidonda.

Tonny alipiga magoti mbele ya Balkis kuomba msamaha.


“Najua tumekukosea, lakini nakuahidi hatutafanya upumbavu mwingine, tupo chini ya miguu yako, tunaomba utusamehe.”


“Sawa mmekosa, hebu nielezeni kosa langu kwenu ni nini?”
“Huna kosa lolote.”


“Kwa nini mlidhamiria kuniua?”


“Tusamehe Balkis ni shetani mbaya tu alitupitia.”


“Leo unaniomba msamaha, ningekufa ungemuomba nani?”


“Najua tumekukosea kwa kiasi kikubwa.”


“Labda mlikuwa mnaona natania, mwenzako nimempa adhabu ya kutembea uchi mbele za watu muda si mrefu.”
“Ha!” Tonny alishtuka kusikia vile.
“Unashtuka nini, si alisema mbele yako akimrudia Muddy atafanya nini?”
“Atatembea uchi.”
“Mbona kamfuata mume wangu kupitia waganga.”
“Nilikuwa sijui.”
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.69.


“Najua tumekukosea kwa kiasi kikubwa.”
“Labda mlikuwa mnaona natania, mwenzako nimempa adhabu ya kutembea uchi mbele za watu muda si mrefu.”
“Ha!” Tonny alishtuka kusikia vile.
“Unashtuka nini, si alisema mbele yako akimrudia Muddy atafanya nini?”
“Atatembea uchi.”
“Mbona kamfuata mume wangu kupitia waganga hakutembea uchi?”
“Nilikuwa sijui.”
SASA ENDELEA...

“Utajuaje na roho yako imejaa tamaa na harufu ya damu za viumbe wasio na hatia?”
“Ni kweli nilikuwa na roho mbaya lakini nimeujua ubaya wangu, nitajirekebisha.”
“Kama nilivyokueleza Ashura amevua nguo mbele za watu na kupata aibu ya mwaka.”
“Mungu wangu yupo wapi?”
“Atakuja usiku kwa njia ya kujifichaficha.”
“Kwa hiyo nguo kavua kwa hiyari yake?”
“Kwani wewe adhabu uliyoipata umeipenda?”
“Hata.”
“Au nikuongeze?”
“U...u...usifanye hivyo ni...ni...”
“Baada ya tapeli mwenzako kuvua nguo mbele za watu, na kumpa adhabu ndogo aliyoichagua mwenyewe pia nimempa adhabu yangu atakayotesekanayo kwa muda mrefu.”

“Ungemsamehe nina imani hawezi kurudia tena,” Tonny alimuonea huruma Ashura na kujisahau yeye.
“Kwa sasa sitawasamehe lazima nitimize kile nilichokipanga kuwafanyia.”
“Usituue Balkis.”
“Niliapa kamwe sitawaua ili kizazi chenu kijue madhara ya ubaya ni nini?”
“Sasa utatufanya nini?”
“Mpenzio tayari nimeshamgeuza kuwa mbwa.”
“Mungu wangu!”
“Na wewe kama nilivyokueleza nitakugeuza kuwa nzi wa kijana, maisha yako yatakuwa jalalani na chooni hakuna mwanadamu atakayekupenda.”
“Jamani si nitakufa?”
“Hutakufa, hayo ndiyo maisha niliyowachagulia baada ya kuwabembeleza kwa muda mrefu, Lakini mmekuwa na viburi pamoja na kuwatisheni bado mkawa na masikio magumu kama kenge, nina imani adhabu ya leo itakuonesha mimi ni kiumbe wa aina gani.


Kwa vile sitaki dhambi ya kuua na kisasi ni haki ya kila kiumbe, nilichokuchagulia ndicho saizi yako.”
“Balkis naomba uni...sa...sa... “
Bwana wa Ashura hakumalizia kuomba msamaha alipuliziwa kitu kama unga huku Balkis akisema:
“Kuanzia leo utakuwa nzi wa chooni.”


Muda uleule Tonny aligeuka kuwa nzi wa kijani, ghafla mazingira ya pale nayo yakabadilika na kumfanya Tonny kuruka na kwenda moja kwa moja jalalani.

Alijikuta akiishi maisha mapya ambayo yalimlazimisha kuishi chooni na kwenye majalala.


Tonny pamoja na kuishi kwenye harufu kali ya mizoga na kinyesi hakuwa na jinsi kwa kuamini kuwa maeneo yale ndiyo yaliyokuwa salama kwake kwa kuogopa kuuawa na mwanadamu pale atakapokwenda ndani mwake kwa kuamini kuwa yeye ni binaadamu.


Balkis baada ya kutoa adhabu ile alirudi kuilea mimba yake kwa kuamini kuwa hakukuwa tena na mwanadamu atakayemfuatilia maisha yake.

Balkis alikuwa akiyafurahia maisha yake na Muddy kwa kuamini muda si mrefu wataitwa baba na mama.


Baada ya kiza kuingia, Ashura aliondoka ufukweni na kurudi nyumbani akiwa katika umbile lake la mbwa.


Alitembea huku akiomba Mungu afike salama nyumbani kwake, moyoni akijiuliza Tonny atamuelewa kutokana na umbile lake jipya alilokuwa nalo, alifikiria hivyo bila ya kujua kwamba mpenzi wake naye maisha yake yalikwishabadilika na kuwa kiumbe cha jalalani na chooni baada ya kugeuzwa kuwa nzi.


Hakutembea umbali mrefu mvua kubwa ilianza kunyesha, alikimbilia kwenye nyumba moja iliyokuwa njiani na kujibanza upenuni.


Mwenye nyumba alitoka na kumfukuza akiamini ni mbwa.

Kutokana na mvua kuwa kubwa na barabara kujaa maji, Ashura alijitahidi kumwambia yule mwanadamu kuwa yeye si mbwa bali ni mwanadamu.


Sauti yake ilikuwa ni ya mbwa kwa kuwa aliitoa kwa kubweka, tu hicho kilizidi kumuuzi mwenye nyumba ambaye aliingia ndani na kutoka na bakora na kumtoa mbio.

Ashura hakuwa na jinsi ilibidi aingie kwenye mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha huku akiogelea kwenye maji machafu yaliyokuwa yakitoka kwenye mitaro.


Aliendelea kunyeshewa na mvua kubwa iliyoambatana na radi, kuna kipindi alizama ndani ya maji na kujitahidi kuogelea ili kuendelea na safari yake.


Hata alipopata sehemu ya kujibanza bado hakuona umuhimu wa kufanya hivyo kutokana na kusikia baridi kali mwilini mwake iliyotokana na kulowana kwa mvua.


Aliendelea na safari yake yenye mateso huku akitaka amkute Tonny nyumbani na kuomba amtambue na kukubali kuishi naye kwenye umbile lile la mbwa.
 
 
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) EP.70.

ILIPOISHIA:
Alitembea ndani ya maji katika mvua kubwa ya radi, kuna kipindi alizama ndani ya maji na kujitahidi kuogelea na kuendelea na safari yake.Hata alipopata sehemu ya kujibanza bado hakuona umuhimu wa kujibanza kutokana na kusikia baridi kali kutokana na kulowa mwili wote na maji.


Aliendelea na safari yake yenye mateso ya shetani motoni huku akiomba Mungu amkute Tonny nyumbani pia amtambue na kukubali kuishi naye kwenye umbile la mbwa. SASA ENDELEA...

Alishangaa kutembea umbali mrefu bila kufika, alijikuta akichoka huku njaa kali na kiu ikiwa imemshika na kushindwa kujua atakula wapi.


Alipofika eneo ambalo alijua ndipo kwao alishangaa kuona hakuna nyumba yao, alizunguka mpaka kuna kucha huku akiteseka na baridi kali bila mafanikio.Ashura alitamani kifo lakini kilikuwa mbali naye, alijiuliza mateso yale mpaka lini au ndiyo ya kudumu lakini hakupata jibu.


Alitamani amuone Balkis mbele yake ili amueleze ya moyoni kuwa amekoma na hatarudia tena katika maisha yake.

Katika hali ya kawaida aliamini kabisa Balkis hakuwa na kosa lolote, japo walitaka kumuua mateso yale yalikuwa makubwa heri angemuua akajua moja lakini si mateso ya kutengwa na jamii kwa kumchukia kila atakapokwenda kwa kujulikana mbwa kumbe mwanadamu yalikuwa makubwa sana.


Wakati akiteseka vile, Tonny naye alikuwa kwenye mateso mazito pembeni ya jalala kwenye tawi la mti uliokuwa na afadhali kutokana na mvua kuwa kubwa sana.Baada ya mvua kukatika aliendelea kukaa kwenye tawi lile ambalo mvua haikufika sehemu ile kama ingefika aliamini angekufa.


Lakini chini yake kulikuwa na mzoga wa mbwa aliyekufa siku mbili zilizopita na kutoa harufu kali ambayo iliongezeka baada ya kunyeshewa na mvua.Harufu ilikuwa mbaya sana lakini hakuwa na jinsi, aliendelea kuvumilia kwa kuhofia kupoteza maisha yake kutokana na eneo lote kuwa na maji ya mvua iliyokuwa inanyesha kwa nguvu.


Yalikuwa mateso makubwa kutokana na adhabu ya kuvuta harufu kali ya uchafu na mizoga.Njaa na kiu ilikuwa kali pamoja, licha ya umbile la kugeuzwa nzi bado alikuwa na akili za binadamu asingeweza kula mizoga wala kinyesi.Aliamini asingefikisha siku nyingi lazima angekufa kwa njaa.


Aliwaza kama Balkis angetokea mbele yake angemuomba amuue kuliko kumtesa vile,

kama siku moja hali ilikuwa vile kwa mwezi mzima ingekuwaje.

Majira ya saa tisa za usiku akiwa amejikunyata kwa baridi kali la usiku kucha aliamshwa usingizini.


Alipofumbua macho hakuamini kumuona Balkis mbele yake, alitaka kufunua mdomo wake kumuomba msamaha, lakini angewezaje kuzungumza katika umbile kama lile la nzi.Balkis alimchukua na kwenda naye sehemu na kumtemea mate, palepale Tonny alirudi katika umbile lake la kawaida.


Alikuwa amemletea chakula kitamu, alimkaribisha.
“Karibu chakula, najua huwezi kula chakula cha nzi ambacho ni kinyesi na uchafu kwa vile wewe bado mwanadamu.”


“Ba..ba..ba..lkis naomba u..uni..samehe,” Tonny alipiga magoti huku akitetemeka.


“Tonny sikuja kusikiliza msamaha wako, ulishaomba sana siku za nyuma, nimekuletea chakula kula niondoke.”
“Basi niue kabisa chakula hiki sili,” Tonny alionesha jeuri kwa Balkis.


“Tonny hunijui hata kuwaletea chakula kizuri ni huruma yangu, lakini mlitakiwa mle kinyesi na uchafu.”
“Nimesema sili niue kabisa,” Tonny alionesha jeuri kwa Balkis kuonesha yupo tayari kwa lolote.


“Tonny usinione nakuchekea ukaniona ni bwege mwenzio, sasa hivi nitakugeuza funza maisha yako yawe ndani ya kinyesi usiniletee upumbavu unijue eeh! Alaa,” Balkis alibadilika na kusema kwa hasira huku macho yake yakiwaka kama taa na usiku ule yalikuwa kama tochi yenye mwanga mkali.
“Ba..ba..si ni..ni..


“Nyamaza mpumbavu mkubwa wewe, ni kiumbe gani anayeweza kuwaletea chakula na maji baada ya kutaka kumuua zaidi ya mara mbili?” Balkis alimuuliza huku amemshikia kiuno na kitumbo chake kilionekana kwa mbali.
“Na..na..te..seka Balkis harufu ni mbaya sana naomba unitafutie adhabu nyingine.”


“Huwezi kunichagulia adhabu kwa vile muda wa kubembelezana ulikwisha, hebu maliza kula nataka nimpelekee na mwenzako, muda unakwenda kukipambazuka ujue hali mpaka kesho kama saa hizi.”


Tonny hakuwa na jinsi, alikula chakula kile kilichokuwa kitamu ajabu, hakuwahi kula chakula kitamu kama kile, alikuwa akijiuliza Balkis ni kiumbe gani pamoja na ubaya waliomfanyia bado kawaletea chakula kitamu na maji. Moyoni aliamini huenda atamsamehe.


Lakini ilikuwa tofauti na alivyodhania baada ya chakula ambacho alishiba vizuri na kunywa maji matamu, alimpulizia vitu kama unga, vilipomgusa usoni palepale aligeuka hali yake ya mwanzo ya nzi........JE NINI KITAENDELEA?
 
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) .....EP.71.


ILIPOISHIA;
Lakini ilikuwa ni tofauti na alivyodhania baada ya kula chakula ambacho alishiba vizuri na kunywa maji matamu, Balkis alimpulizia vitu kama unga vilipomgusa usoni, palepale aligeuka hali yake ya mwanzo ya nzi.
SASA ENDELEA ...

Alitamani kuomba msamaha lakini alichelewa, alichukuliwa na kurudishwa kwenye tawi la mti na kukumbana tena na harufu kali ya uchafu wa mzoga wa mbwa aliyekuwa akinuka.

Kwa harufu ile kama angekuwa katika umbile la kibinaadamu basi angetapika mpaka utumbo. Lakini bahati nzuri alikuwa kwenye umbile la nzi, aliendelea kuteseka na harufu na baridi kali.

Balkis baada ya kutoka kwa Tonny alikwenda moja kwa moja kwa Ashura aliyekuwa amelala pembeni ya nyumba mbovu.
Karibu yake kulikuwa na mtaro wa maji machafu lakini yeye aliichagua sehemu iliyokuwa kavu. Lakini ukali wa ubaridi ulikuwa ukimpata kisawasawa.

Alijuta kwa mambo yote aliyoyafanya kwa kuwatepeli wanaume kwa ajili ya Tonny ambaye ndiye aliyemuingiza kwenye kazi ile ya kuolewa na wanaume na mwishowe kuwadhulumu kwa kuvunja uhusiano.

Kitu kilichowafanya wanaume zaidi ya wawili kujiua baada ya kufilisika na wengine kupatwa na ukichaa.
Aliamini hali ile ingemtokea na Muddy lakini kwa bahati ya ajabu Balkis aliyaokoa maisha yake. Alitamani Balkis atokee mbele yake amuombe msamaha lakini hakuonekana.
Usingizi ulimpitia pale alipokuwa amejilaza huku akichonyotwa na njaa pamoja na kiu.

Alishtuliwa kutoka usingizini na kujiona akiwa mbele ya Balkis, kama Tonny alivyotaka kuomba msamaha, naye alikuwa kama anataka kumuuma Balkis aliyemchukua na kumpeleka sehemu iliyokuwa nzuri, alimtemea mate na muda uleule alibadilika kurudia katika umbile lake la kibinadamu.

Ashura baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida alipiga magoti mbele ya Balkis na kuanza kuomba msamaha.
“Balkis nisamehe sana nimekosa, adhabu ya leo inatosha hali yangu ni mbaya,” alisema huku akibubujikwa na machozi.

“Hii si adhabu ya siku moja ni ya muda mrefu kama nilivyokueleza muombeni Mungu nijifungue salama, kama mwanangu akifa au mimba ikitoka mjue na nyinyi maisha haya yatakuwa ya milele kwenu.”
“Naomba unisamehe, sitarudia tena, niliyokutananayo leo yanatosha, ukiongeza zaidi nitakufa.”

“Ashura sikufuata kuombwa msamaha, nimekuletea chakula, kula haraka kabla hapajakucha, ukichelewa utalala na njaa, kuonana na mimi tena ni mpaka kesho muda kama huu, tapeli mwenzako kanichelewesha na wewe unataka kufanya hivyo.”

“Nani, Tonny?”
“Eeh.”
“Yupo wapi?”
“Yupo jalalani.”

“Anafanya nini?”
“Kwani nzi makazi yake wapi?”
“Mungu wangu umemgeuza kuwa nzi?”

“Tena ana bahati angeendelea kuniletea ujeuri ningemgeuza kuwa funza na makazi yake yangekuwa kwenye kinyesi milele.”
“Sa...sa...”
“Ee...eeh! Hebu kula niondoke.”

Ashura hakuwa na jinsi alikula chakula kitamu na kuamini kama Balkis ameamua kumletea chakula ambacho hakuwahi kula katika maisha yake ya kibinaadamu, lazima atakuwa amerudiwa na roho ya huruma na kumsamehe.

Lakini dhana yake ilikuwa ni tofauti, baada ya kumaliza kula alirudishwa katika umbile lake la mbwa na kurudishwa alipotolewa na Balkis akatoweka.
****
Siku zilikatika huku adhabu ya Ashura na mwanaume wake zikiendelea, walikuwa wakiteseka kwenye maumbile yao ya mbwa na nzi. Maisha ya Tonny yalikuwa ya jalalani na chooni japo hakuweza kula uchafu.
Ashura maisha yake yote yalikuwa ni kuzurura jiji zima kutafuta sehemu iliyokuwa salama kutokana na kukimbizwa kila kukicha na watoto watukutu.

Mimba ya Balkis iliendelea vizuri na baadaye alijifungua salama salmini watoto mapacha wa kike na kiume, kila mmoja alifanana na mzazi wake mmoja.
Wa kike alifanana sana na mama yake na wa kiume alifanana na baba yake. Balkis alifurahi sana na kuamini dhamira yake ilitimia.

Aliamua kwenda chini ya bahari na wanawe kuwatambulisha kwa wazazi wake, wakati akiwa njiani kuelekea chini ya bahari.
Baba yake Mfalme Barami alikuwa na mazungumzo mazito na mkewe juu ya kukosa taarifa za Balkis.

“Mke wangu hivi huyu mtoto anataka kupimana nguvu na mimi?”
“Kwani tatizo ni nini?”

“Hulioni? Tangu nilipomueleza aachane na yule mwanaume amepotea, haleti tena vizazi vya wanawake mwaka unakatika.”
“Mume wangu jambo hili linatakiwa busara siyo kutumia nguvu.”

“Kama anaona ni utani, nitamtuma Pweku mtwana mkuu akamuulie mbali huyo mwanaume wake.”
“Mume wangu unatafuta vita mpya.”
“Na nani?”

“Siamini kama Balkis atakubali kirahisi mwanaume wake auliwe, atawamaliza watwana wako wote kwa kuwaua.”

“Inamaana sasa hivi mwanao anataka kunipanda kichwani?”

Walinyamaza kuzungumza baada ya kusikia kelele za chereko chereko nje, zilikuwa ni shamrashamra zilizowashangaza wote.

Msafara ulikuwa ukiingia ndani, ukiongozwa na vijakazi na watwana akiwemo mtwana mkuu Pweku, sherehe kama ile hutumika kukaribisha mgeni aliyezaliwa.

Balkis alionekana akiwa juu kwenye farasi mwenye matandiko ya dhahabu.
Mama yake Balkis Malkia Huleiya alipowaona watoto wa Balkis, alikimbia kwenda kumpokea mwanaye na wajukuu zake kwa furaha ya ajabu.

Mfalme Barami alikuwa amebaki njia panda, asielewe kilichokuwa kikiendelea mpaka wageni wale walipokuwa wakiingia ndani, hakujua watoto wale aliokuwanao Balkis walikuwa ni wa nani.
 
 
 
 
 
 
JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) .....EP.72.


ILIPOISHIA:
Mama Balkis, Malkia Huleiya alipowaona watoto wa Balkis alikimbia mbio kwenda kumpokea mwanaye na wajukuu zake kwa furaha kubwa. Mfalme Barami alikuwa bado yupo njia panda, mpaka wanaingia ndani hakujua watoto aliokuwa nao Balkis ni wa nani.
SASA ENDELEA...

BAADA ya kuingia ndani, Balkis alijua amefanya makosa. Alipiga magoti mbele ya baba yake na kusema:
“Mtukufu mfalme wa bahari, najua nitakuwa nimefanya kosa kubwa la kuzaa na binadamu, lakini sikuwa na jinsi. Nimefanya hivi kutokana na moyo wangu kuwa na hofu kuu kwa Muumba wetu.

Niliamua kukaidi amri yako na kufunga ndoa na binadamu ambaye niliamini atanisaidia kupata watoto ambao ndiyo ilikuwa kiu yangu kubwa.

Pia nilijua nitaepukana na dhambi ya kuvunja ndoa za watu pia kuwanyima watu haki zao za kupata watoto. Najua nimekukosea lakini uamuzi huu niliona unafaa kwa kuamini siku ya mwisho mbele ya Muumba nitahukumiwa mwenyewe kwa vile tayari najua zuri na baya.

Hawa mbele yako ni wanangu wapendwa Zaaanuna na Labeiiki, kwa vile nimefanya kosa una haki ya kunifanya lolote, nipo radhi kwa adhabu yoyote ila nakuomba usiwaue wanangu.”
Kauli ile ilikuwa kama mshale mkali moyoni kwa Mfalme Barami.

Aligeuka bubu ghafla na kushindwa amfanye nini Balkis, mwanaye kipenzi aliyefanya kosa kubwa la kuzaa na binadamu. Lakini mke wake naye aliwahi mbele ya mume wake na kupiga magoti kumuombea msamaha mwanaye.

“Mume wangu, Balkis ndiye mtoto wetu wa pekee, kama kosa amekwishafanya. Najua amekuudhi sana lakini nakuomba umsamehe mwanao. Kama adhabu naomba unipe mimi mama yake, nipo radhi kwa adhabu yoyote lakini wajukuu zangu usiwaguse.”
“Kwa kweli hata sijui nifanye nini, basi tu kwa vile ni mwanangu lakini bila hivyo ningekuchemsha supu na kukunywa kwa jinsi nilivyochukia.”

“Najua nimekuudhi sana baba yangu lakini niliamini kuna aliye zaidi yako ambaye si mwingine bali Muumba wetu ambaye ana uwezo wa kufanya lolote bila kuingiliwa na mtu. Ni yeye ndiye mwenye adhabu kali yenye kuumiza.”
“Nimekuelewa mwanangu sina jinsi, karibu nyumbani wewe na wajukuu zangu ambao siwezi kuwafanya lolote kwa vile hawana hatia.”

“Baada ya kunisamehe naomba nimlete na mkweo mbele yenu mumtambue.”
“Kwa vile tayari una watoto wake hatuna la kufanya zaidi ya kukubali kumtambua.”
“Na hawa watoto watakuwa wa nani?” Malkia Huleiya alimuuliza Balkis.

“Ni wa kwetu wote.”
“Wataishi wapi?”
“Huku, duniani watakuja siku moja moja.”
“Kwa hiyo hata mimi nitafurahi kucheza na wajukuu zangu,” Malkia Huleiya alionesha furaha kubwa.
Ilikuwa ni furaha kubwa kusamehewa na kutambuliwa rasmi watoto wa Balkis kwa mfalme Barami.
***
Balkis baada ya kupata ruhusa ya kumpeleka mume wake kwao, alijikuta akijawa na mawazo juu ya kumweleza Muddy kuwa yeye ni jini, tena anayeishi chini ya bahari. Siku zote Muddy alijua Balkis ni binadamu wa kawaida.

Alirudi hadi duniani na kumkuta Muddy amejipumzisha sebuleni akisikiliza nyimbo laini kutokana na kuambukizwa na Balkis kupenda kusikiliza nyimbo za Bara Asia.
“Vipi mbona umerudi peke yako, watoto wapo wapi?” Muddy alimuuliza Balkis baada ya kumuona yupo peke yake.
“Nimewaacha nyumbani.”

“Mke wangu, watoto wadogo kama wale umewaacha nyumbani?”
“Nimekufuata wewe twende kwa wazazi wangu.”
“Mmh! Itakuwaje si ulisema baba yako mkali sana?”
“Ni kweli lakini kwa sasa hakuna tatizo, watoto wamemaliza kila kitu.”
“Sawa tunaweza kwenda.”

Siku zote Muddy alijua Balkis hakai nje ya Dar es Salaam, kabla ya kuondoka Balkis alijikuta akipata wakati mgumu kumueleza Muddy kuwa yeye ni jini, lakini mwenzake aliitambua hali ile mapema. Alimsogelea na kuzungumza naye kwa sauti iliyomtoa machozi Balkis.
“Nini tena malkia na kipenzi changu?”

“Muddy nina wakati mgumu wa kujieleza kwako.”
“Kujieleza nini tena mpenzi wangu?”
“Najua hunifahamu vizuri, nina imani ukinielewa unaweza kuniacha.”
“Siwezi kukuacha, hata ungekuwa jini siwezi kukuacha nakupenda sana Balkis.”

Kauli ya kusema hata kama angekuwa jini ilimshtua sana Balkis na kujiuliza anayosema ni kweli au ni kusherehesha maneno. Lakini kwa njia nyingine yalimpa nguvu ya kusema bila wasi.
“Muddy unanipenda?” alimuuliza huku akimtazama kwa jicho la mahaba.
“Zaidi ya kukupenda.”

“Nikikueleza kitu huwezi kuniacha?”
“Hata ukisema unahitaji uhai wangu, kwa mapenzi yangu mazito kwako nipo tayari na nitakufa nakupenda.”
“Kweli Muddy?”
“Kweli kabisa kwani bila wewe sasa hivi mimi ningekuwa nani?”
“Muddy mimi si binadamu.”

“Kama si mwanadamu wewe ni nani?”
“Mimi ni jini.”
“Nani?” Muddy alishtuka na kusogea nyuma toka alipokuwa amekaa, kitendo kile kilimfanya Balkis apige magoti mbele ya Muddy kuomba asimuache.
 
 
 
 
 
 
 

JINI LA DARAJA LA SALENDA (Balkis) .....EP.73.


ILIPOISHIA
“Muddy unanipenda?” Alimuuliza huku akimtazama kwa jicho la mahaba.
“Zaidi ya kukupenda.”
“Nikikueleza kitu huwezi kuniacha?”

“Hata ukisema unahitaji uhai wangu, kwa mapenzi yangu mazito kwako nipo tayari na nitakufa nikikupenda.”
“Kweli Muddy?”
“Kweli kabisa, kwani bila ya wewe sasa hivi mimi ningekuwa nani?”
“Muddy mimi si mwanadamu.”

“Kama si mwanadamu ni nani?”
“Mimi ni jini.”
“Nani?” Muddy alishtuka na kusogea nyuma kutoka alipokuwa amekaa, kitendo kile kilimfanya Balkis apige magoti mbele ya Muddy na kumuomba asimuache. SASA ENDELEA...

“Muddy usiniache
nakupenda sana.”
“Balkis unayosema ni kweli?”

“Kweli mpenzi wangu mimi ni jini la chini ya bahari na baba yangu ni mfalme wa majini katika bahari hiyo. Kukubali kuwa na mimi umeokoa vizazi vya wanawake mia ambavyo nilitakiwa nivitoe ili nipate dawa ya uzazi na kuniwezesha kuolewa na jini mwenzangu.”
“Balkis unayosema ni kweli?”

“Ni kweli kabisa.”
“Kwa nini hukunieleza mapema?”
“Ujini wangu ndiyo uliokoa maisha yako na hata kuendelea kukulinda na akina Ashura waliokuwa wakiendelea kuyafuatilia maisha yetu.”

“Balkis japo moyo wangu umeshtuka kusikia wewe ni jini lakini bado nitaendelea kukupenda maisha yangu yote. Sikuwahi kuamini kama jini ana roho nzuri kuliko mwanadamu, niliamini majini ni wabaya na kama ungenieleza mwanzo ningeachana na wewe.
Nakuahidi kwenda mbele ya wazazi wako kujitambulisha na kuwa tayari kuishi na wewe.”
Kauli hiyo ilimfanya Balkis alie machozi ya furaha na kumkumbatia Muddy.

“Asante Muddy kwa kuonesha mapenzi ya kweli, nitakupenda milele.”
“Nikushukuru wewe kuonesha mapenzi ya kweli kwangu pia, kulinda maisha yangu kwa nguvu zote.”
“Muddy niwafanye nini akina Ashura waliopanga kukuua na kuniua mimi?”
“Kwani bado wanatufuatilia?”

“Walikuwa wanataka kuniua nikawawahi na kuwageuza mbwa na nzi ili niweze kujifungua salama.”
“Kwa hiyo mpaka sasa bado wapo katika hali hiyo?” Muddy alishtuka.
“Ndiyo.”
“Wewe ulitaka kuwafanya nini?”

“Lolote utakaloliamua wewe nipo tayari kulifanya kwa vile umeusikia ubaya wao.”
“Naomba uwasamehe.”
“Kwa kuwa umesema wewe nitawasamehe.”
Naomba kabla ya kwenda kuwaona wazazi wako wawe wamerudi katika hali yao ya zamani.”

Baada ya makubaliano, Balkis alitoka na kurudi na mbwa na nzi aliyekuwa juu ya mgongo wa mbwa na kusema:
“Hawa ndiyo maadui zetu.”
Muddy hakuamini kuwaona mbwa na nzi na kuelezwa kuwa ni Ashura na mwanaume wake. Balkis aliwatemea mate wote wakarudi katika hali yao ya kawaida ya kibinaadamu.

“Mna bahati kubwa kwa kuwa mpenzi wangu amewasamehe, japo hata mimi nilikuwa na wazo la kuwasamehe, nashukuru Mungu nimejifungua salama. Kuanzia leo nina imani kwa adhabu ndogo ambayo hailingani na dhamira yenu ya kuniua kwa kipindi cha mateso imetosha kuwafanyeni viumbe wapya. Naomba mkaendelee na maisha yenu.”

“Asante Balkis, asante Muddy, tunaapa kwa mbigu na ardhi kuwa hatutathubutu hata kuua nzi, mateso tuliyoyapata yametosha. hatukufa lakini cha moto tumekiona.”
“Nakutakieni maisha mapya nina imani mtakuwa viongozi wema na kuwaeleza watu kuwa ubaya haulipi na jini si mbaya ila roho mbaya ya kiumbe chochote ndiyo mbaya.”

Ashura na mwanaume wake walirudi kwao na kukuta kila kitu chao kikiwa katika hali ya usalama. Balkis naye alikwenda mpaka chini ya bahari kumtambulisha mumewe Muddy. Ilikuwa sherehe kubwa ambayo haikuwahi kutokea chini ya bahari iliyobadilisha amri ya jini kuolewa na mwanadamu.

Pia, Balkis alichukua nafasi ile kuwarudishia vizazi vyao wanawake wote ambao baada ya kusumbuka sana kutafuta watoto, wote walifanikiwa kupata watoto bila kujua kuwa kitendo cha Muddy kumkubali Balkis ndiyo ilikuwa tiba yao.
Baada ya hapo maisha ya Muddy na Balkis yaliendelea bila watu kujua kama Balkis ni jini zaidi ya Ashura na mwanaume wake. Muddy na Balkis kila mmoja alimpenda mwenzake mapenzi ya dhati.
*******MWISHOOOOOO******************8

5 comments: