Somewhere Blog: HADITHI ZA KUSISIMUA

Somewhere Blog: HADITHI ZA KUSISIMUA:


JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide        ...


Ilikuwa ni alhamisi tulivu yenye upepo mwanana huku watu wakiendelea na shughuli za ujenzi wa taifa.Madaktari nao walikuwa bise na taaluma yao ya kuokoa roho za watu.Ndani ya hospitali ya lugalo wagonjwa wengi walifurika huku madakaktari nao wakiendelea kutoa huduma, kama ilivyo ada ndugu wa wagonjwa walikaa nje kusubiri taarifa za maendeleo ya wagonjwa wao, basi hali ilikuwa hivyo kwa mzee John ambaye alikuwa akimngoja mkewe amletee nuru dunia yaani ameletee mwana atakae kuwa mrithi wake wa baadae. Akiwa amejiinamia mzee John aliwaza sana ni namna gani atampenda huyo mtoto wake mpendwa atakae zaliwai ukizingatia kuwa huyo ndie atakae kuwa kifungua mimba chake pasi wazo hilo kuisha jingine la jinsia yai mtoto liliingia la hasha! hilo halikumchanganya sana mzee John kwa alijikuta akisema”yote namwachia Mungu”. Ndani ya hospitali ya Lugalo madaktari waliendelea kumhudumia mkewe na mzee John, hali haikuwai nzuri sana kwa upande mkewe na mzee John kwani alitokwa na damu nyingi sana wakati wa kujifungua hali iliyomfanya Dr.Martin awaambie madaktari wenzake “doctors her condition is get worse she bleed a lot” baada ya kauli hiyo daktari akamwagiza nesi ampeleke mgonjwa chumba cha wagonjwa mahututi( I C U) bila kupoteza wakati mgonjwa alikimbizwa ICU kisha jopo la madaktari watatu kufuata.Juhudi za kunusuru maisha ya mtoto na mama ziliendelea, lakini mara dkt.Martin aligeukia kipimo kilochokuwa kikionyesha mwendo wa mapigo ya moyo ya mgonjwa.oooopssss daktari aliguna kwa mshangao……….
je nini kitaendelea? kesho usikose kuingia somewhere blog ili kujua mwendelezo wa story hii….utamuu ndo huooo umeanza songa nayo episode 2. hapo chini...



JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.2.

Dkt.Martin aliguna kwa mshangao mara baada ya kuona mapigo ya moyo yakienda kasi yaani presha ilikuwa juu sana,daktari akaamua kuchukua maamuzi ya haraka kwa kumwekea mgonjwa mashine ya kumsaidia kupumua.Madaktari wengine waliendelea kuzuia damu zisiendelee kutoka zaidi na hatimaye walifanikiwa,kazi iliyobaki ilikuwa ni kushusha presha(mapigo ya moyo).Dkt. Martin aliangalia tena kile kipimo kwa umakinizaidi kisha akasema"dah!! tumshukuru Mungu hali yake imewezakutengamaa" mapigo ya moyo yakienda kwa kasi ya kawaida. Jopo zima la madaktari lilimgeukia kichanga aliyezaliwa na kukikuta kikiwa kinalia,hii ilikuwa ni ishara tosha kwamba kichanga kilikuwa hai.Huku nje wasiwasi ulizidikumtawala mzee John kwani muda ulizidikwenda pasipo yeye kupokea majibu yeyote yanayohusu hali ya mkewe,hali iliyompelekea mzee John kuzungukazunguka kwenye benchi aliliokuwa amekalia.Punde kidogo dkt.Martin alitoka nje na kumpahongera mzee John ,alimshukuru sana daktari kwa kazi nzima ya kumuhudumia mkewe na akamwomba aingie kumwona mkewe pamoja na mtoto wake,daktari alimruhusu huku akimsitisizia asikawie kutoka kwani mgonjwa bado anahitaji mapumziko.Pasi kuchelewa mzee John aliingia wodini na kumpahongera mkewe na kukigeukia kichanga chake kwa furaha iliyopitiliza akakibusu "mwaaa".Mzee John alianza kufuatilia ruhusa kwa daktari ili waweze kuondoka siku ile ile.Ilikuwa yapata majira ya saa mbili usiku ndipo walipopata ruhusa ya kurudi nyumbani kwao kimara.Majira ya saa tatu kasorobo( na dakika arobaini na tano) usiku safari ya kuelekea kwao9 ilianza hasa baada ya kukodi taxi toka Lugalo hospitali.Safari ilianza vizuri huku mzee John na mkewe wakifurahia ujio wa mtoto wao mpendwa.Wakiwa njiani kuelekea nyumbani mzee John alimhimiza dereva aongeze mwendo ili wawahi kufika nyumbani,naye dereva bila ubishi alitii kwani alichokuwa anajali yeye ni pesa yake tu.Basi wakiwa ndani ya mwendokasi huo mara taa za mbele za gari zilizimika ghafla na mara dereva alipiga kelele" tunakufaaaaa,kisha mshindo mkubwa ukasikika"paaa" kisha ukimya mkubwa ukatanda****************unataka kujua nini kilifuata? shuka chini katika episode.3!!

 

 JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.3.

 Tayari gari lilikuwa limetumbukia mtaroni na watu wa mitaa ya karibu nao hawakuchelewa kuona vile walisogea chapuchapu ili kujaribu kuokoa.Baada ya dakika mbili hivi kupita tayari watu wengi walikuwa wameshajaa kulizunguka gari ili kutaka kujua nini kinaendelea.Basi raia mmoja akashuka chini na kuukaribia mlango wa dereva kisha kuchungulia ndani na kumwona dereva akiwa anavuja damu kwenye paji lake la uso huku akiwa hajitambui.Kuona hivyo akaamua kuita watu wengine ili waweze kumsaidia kumtoa yule dereva kupitia dirisha la lile gari.kisha kumtoa yule dereva yule raia alirudi kwenye gari na kuchungulia kwenye mlango wa katikati na kuona watu kwa mbali alipoangalia vizuri alimwona mwanamke mmoja pamoja na mwanaume wakiwa wameshika katoto kadogo.Basi aliwaita wenzake na kuanza kuwatoa.Mara tu baada ya kutolewa kwenye lile gari mzee John na mkewe waliwashukuru wote kwa kuja kuwaokoa kwani wao walitoka salama , wote wakaongozana mpaka pale alipokuwa amelazwa yule dereva taxi.Wakajaribu kumpima kasi ya mapigo ya moyo wakaona yana piga taratibu sana hivyo ikawalazimu kukodi taxi nyingine ili kumuwahisha yule dereva hospitalini.Mzee John na mkewe walipasika kukodi taxi nyingine mpaka nyumbani kwao kimara.Baada ya yule dereva kufikishwa hospitali manesi wa zamu walipokea haraka haraka na kumpeleka ICU madaktari walianza kumuhudumia.Baada ya masaa mawili dereva aliweza kuzinduka na kujielewa lakini baada ya dakika kumu dereva alilaanza kulalamika kuwa kifua kinambana sana,nesi kuona vile akakimbia kumwita daktari, daktari alipofika alimwona mgonjwa akizidikuishiwa nguvu,daktari akaita « dereva»sauti kwa mbali iljibu«na...a...a..m» daktari akaita tena «dereva»kwa mara hii hakuna sauti iliyosikika ikijibu chochote**********je nini kitaendelea? check out episoe 4!!


JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.4.

Daktari alimsogelea dereva kisha kumgusa sehemu ya moyo na kuinamisha kichwa chake .daktari hakuamini alichokuwa anakishuhudia akaamua kuweka kifaa chake cha kupimia mapigo ya moyo katika sehemu ya usawa wai moyo na kukivaa vizuri masikioni mwake.Loo!!!maskini dereva alikuwa amekwisha aga dunia(kwisha fariki) basi daktari akamwagiza nesi kumfunika marehemu kisha kufanya taratibu za kumpeleka mochwari ,hati ya kifo iliandaliwa na kila la kitu kilikuwa sawa kusubiri taratibu za mazishi. Mzee John pamoja na mkewe walifika nyumbani kwao salama salimi,basi wote kwa pamoja walimshukuru Mungu kwa kuwaepusha na ajali mbaya sana ya gari. Maisha mapya kwa Mzee John yalianza hasa baada ya mwanafamilia mmoja kuongeza.Mzee John alizidisha upendo wake kwa mkewe hata kufikia kumpikia chakula hakika kila mmoja wao alifurahia maisha ya ndoa huku akiomba mwenzake aishi maisha marefu.Baada ya miezi mitatu kupita mkewe na mzee John alirejea katika hali yake ya kawaida yaani alikuwa amepona kabisa,tayari walikwisha mpa jina mtoto wao ambaye sasa anaitwa Lulu.Mzee John alirejea katika shughuli yake ya uvuvi katika bahari ya hindi na siku hiyo ilikuwa ni jumatatu ndipo mzee John alikwenda baharinni na kukutana na wavuvi wenzake walio mtania wakisema"annhaa mzee John naona nyavu zako zimecheuaa...na sasa ka mwaka haka umepata kabinti"hahaha!!! wote walicheka.Baada ya makaribisho hayo yote mzee John aliuliza,jamani kazi zinaenda????!wakamjibu kwa tabu sana.kisha mazungumzo walikubaliana kwamba usiku wataenda kuvua,waliagana na kilammoja akaenda nyumbani kwake kujiandaa na safari ya usiku.Mkewe na mzee John alimsubiri mumewe kwa hamu na mara mzee John alitokea basi mkewe alimuwao kisha akamkaribisha chakula nao wote wakajumuika katika chakula hicho.Ilipofika jioni mzee John alimuaga mkewe tayari kwa safari ya baharini.Majira ya saa mbili usiku wavuvi wote waliingia ndani ya boti yao kuanza safari.Mara walipokaribia kilindi boti ilianza kuyumba kwa kasi huku maji yakiingia ndani hasa sababu ya upepo mkali uliokuwa ukivuma baharini**********

 

JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.5.

Mzee John na wenzake walichukua ndo zilizokuwamo mle kwenye boti kisha kuanza kutoa maji yaliyokuwamo kwenye boti, walijitahidi kutoa maji haraka haraka ili mradi boti yao isizame.Hiyo botiwanayoitumia ilikuwa ni boti ya kijiji ambayo hukodishwa kwa vikundi mbalimbali vya wavuvi basi na sasa ilikuwa mikononi mwa kundi la akina mzee John.Waliendelea kutoa maji ambayo sasa yalionekana wazi kuanza kupungua.Upepo mkali uliendelea kuvuma kwa kasi zaidi hali8 iliyowapelekea akina mzee John kuendelea kuogopa lakini walijipa moyo kwamba hali hiyo ya upepo ni ya muda mfupi tu.Tayari ilikwisha8 timu saa saba usiku wakiwandani ya bahari mzee John na wenzake walijaribu kutega nyavu zao ili waweze kuambulia chochote,basi walifanya hivyo haraka haraka hukuwakiogopa isije kufika asubuhi wangali bado hawaja pata kitu.shughuli nzima ilimalizika na wao akina mzee John wakatulia botini huku wakiwa wamewasha taa zao ilikuwavuta samaki.Dakika ishirini mbele hali ya hewa ilianza kubadilika taratibu wingu zito lilianza kujikusanya angani.Mzee John alihamaki kuona hali ile lakini wenzake wakamshauri kwamba wasubiri kidogo ili waweze kubahatisha samaki wanakurudi nao nyumbani .Wote wakakatashauri kusubiri kwa muda kidogo.Wakati wakiendelea kusubiri radi nazo zilianza kuunguruma mvululizo hivyo kuzidi kuogopesha,mzee John alipepesa macho kulia kushota,kaskazini kusini na mashariki magharibi bila kuona taa yoyote iliyokuwa ikiwa hivyo kuashiria kwa kulikuwa nakuna wavuvi wengine karibu katika bahari kubwa ya Hindi.Kuona hivyo alishauri waondoke mida hiyo lakini wenzake walionekana kulipinga hilo wazo.Huku wakiendelea kubishana mara mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali ulioshahabiana na radi za kutosha ilanza.Mzee John na wenzake wakaamua kuvuta nyavu zao haraka haraka ilikuangalia kama watakuwa wamepata walau kidogo basi walifanya hivyo na wakahesabu .....moja.....mbili....tatu kisha wakavuta nyavu zao kwa haraka.Lo!!!! walikuwa wameambulia samaki kumi tu.Mvua kubwa iliendelea kunyesha huku upepo nao ukizalisha mawimbi makubwa sana.Mzee John na wenzake wakaanza safari ya kurudi nchi kavu lakini kiisha kwenda umbali wa mita kumi boti ilianza kujaa maji huku mawimbi yakiisukuma sukuma na kutaka kuipindua.Wakaanza tena shughuli ya kutoa maji nje, wakiwa katikati ya shughuli lilikuja wimbi moja kubwa likaibetua ile boti ambayo sasa ikawa ipo wimawima*********

    • JINSI JINI ALIVYOLITESA PENZI LANGU; Eposide.6.

  •  ile wimbi liliibetua ile boti kisha kuipindua kabisa basi mzee John na wenzake wakakupwAhuko na kuiacha boti ikielea peke yake.Basi mzee John na wenzake walijitahidi kilammoja kupiga mbizi ili kuikaribia ile boti,kutokana na upepo mkali ile boti ilizidi kwenda karibu na kilindini.Mzee John aliizama na kuibuka huku akijaribu kwenda kwa kasi sana ili awezekulifikia botti,alifanya kuhudi sana na kufanikiwa kulikuta boti ambalo sasa lilikuwa umbali wa mita kama sabini hivi toka pale lilipopindukia basi pasi kukawia mzee John alilikwea lile boti kisha kuliwasha.kila alipojaribu kuliwasha lilikataa kuwaka alijaribu kwa mara ya mwisho huku akirushwa rushwa na mawimbi ya baharini,wale wenzake nao wakaifikia boti mara baada ya kupiga mbizi vya kutosha.walipofika tu wakakutana na taarifa kutoka 8 mara ikawaka wote wakashangila y....e...ssssssss.Safari ya kurudi inchi kavu ilianza tena sasa wakikatika mwendo wa tahadhari,wakiwa bado safarini na huku mvua kubwa ikinyesha mara wakaona samaki mkubwa akijichomoza mbele ya boti yao kisha kuzama.Hilo halikuwatisha sana akina mzee John kwani ni kitu cha kawaida katika bahari ya hindi .Basi waliendelea na safari yao,wakiwa theluthi moja ya safari alitoke samaki mkubwa akaipindua ile boti na kuwatupa mbali akina mzee John na ilikuwa saa kumi na moja kasorobo.kila mmoja alijitahidi kupiga mbizi ili kunusuru maisha yake.Lile boti nalo likazama na huo ndo ukawa mwisho wa boti.Mzee John aliendelea kupiga mbizi huku akijaribu kuangaza huku na huko akijaribu kuomba msaada,Mzee John alianza kuishiwa nguvu huku njaa kali ikiwa imembana,aliendelea kupiga mbizi.Huku nyuma mkewe na mzee John alianza kuingiwa na hofu mara baada ya kuona kwamba mumewe harudi kwani haikuwa mazoea yake kuchelewa kurudi kiasi kile akaamua kuendelea kusubiri zaidi.Ilipofika majira ya saa mbili asubuhi mzee John akiwa hoi bin taabani alikatatamaa na kuamua kusubiri kifo huku hisia kali za kumbukumbu ya mwanae Lulu pamoja na mkewe kumjia kwa machungu yote akawa anaona sasa kwamba mwanzo wa maisha magumu kwa mwanae na mkewe umewadia.Akiwa katika dimbwi zito la mawazo Mzee John akasikia sauti kwa mbali alipo nyanyua kichwa aliona boti ikiwa inaelekea upande wake***********

No comments:

Post a Comment