mimi ni msichana wa makamu sijaolewa ila nimepata mkaka ninaye mpenda ambaye ni mzungu, japo mimi nampenda sana lakini wazazi wangu hawataki kabisa kusikia nikiolewa naye(wakidai ni bora nitafute mume muafrica na mtanzania mwenzangu kama nataka kuolewa)....

kwasasa mimi ni mjamzito na bado sijawaambia wazazi wangu kwani najuwa hawatafurahia, lakini mimi na mpenzi wangu huyu tumefurahi sana kujuwa tunaleta mtoto duniani, na yeye anataka kunioa ili tuwe pamoja katika kumtunza mtoto kasheshe inabaki nyumbani wazazi nitawaelezaje wanielewe???????

saa ingine nafikiria kutoroka tu na yeye tukaishi bila ndoa lakini sisi ni binadamu kuna leo na kesho itakuwaje tukigombana na nyumbani nimetoroka? jamani nitafanyaje?



Maisha ya ndoa siyo maigizo, tafakari kwanza!



BADO tunaendelea kujifunza mbinu za kuwa wanandoa bora. Mada hii imelenga zaidi kuzungumza na vijana ambao wana mitazamo mikubwa kabla hawajaingia ndani ya ndoa.
Pamoja na changamoto nyingine, wapo ambao wanaishi kwa kuigiza tabia ambazo si za asili yao. Hapo sasa ndipo kwenye tatizo na umuhimu wa mada hii unapopatikana.
Kuna mambo mengi ya msingi ya kuzingatia kabla ya kuingia kwenye ndoa ili mwenzako awe sahihi na ndoa yako isiwe mateso.
Wiki iliyopita tulianza kuona baadhi ya mambo muhimu ya kuzingatia, leo tunaendelea. Jambo kubwa kwako ni kusoma kwa umakini na kuweka ubongo wako tayari kupokea kitu kipya. Karibu darasani.
MVUTO NI ZAIDI YA UPENDO?
Kuna baadhi ya watu utawasikia wakisema: “Mpenzi wangu ananivutia sana, yaani ni mzuri sana. Najua hata nikitoka naye, marafiki zangu watanisifia kwa kuchagua vizuri.”
Hizi ni fikra potofu ndugu zangu. Mapenzi ya kweli hayapo kwenye sura wala umbile la mtu. Vipo vigezo vya muhimu kabisa vya kuzingatia tofauti na uzuri wa sura.
Sura hubadilika ndugu zangu, binadamu wanazeeka, kuna kuugua na matatizo mengine ambayo yanaweza kubadilisha mwonekano ambao ulikuvutia awali. Je, yakitokea hayo ndiyo utakuwa mwisho wa kumpenda?
Kama leo hii unamuoa kwa sababu umevutiwa na matiti yake madogo, akishazaa na kunyonyesha kisha yakaanguka, ndiyo mwisho wa kumpenda? Umempendea ngozi yake nyororo, akipata ‘aleji’ ya mafuta, ngozi ikaharibika na kuwa na mabakamabaka utakuwa mwisho wenu?
Wewe mwenye mpango wa kuolewa na mwanaume mwenye kigezo cha kifua cha kimapenzi, kesho akifutuka na kuwa na kitambi utamuacha? Ndugu zangu, kiukweli ni kwamba kigezo cha uzuri wa sura na umbile si sahihi kabisa katika kuchagua mwenzi wa maisha.
Vipo vitu vingine muhimu zaidi vya kuangalia. Uzuri ni sifa ya ziada. Kwangu mimi naweza kusema ni sifa tangulizi kabla ya mambo mengine ya msingi ambayo nitayafafanua katika mada hii.
Kama ulikuwa unaishi katika dunia ya fikra hizo, hama ndugu yangu. Uko gizani, njoo kwenye nuru.
ANAJUA MAPENZI?
Ndugu zangu, msinielewe vibaya katika kipengele hiki, msije mkadhani nahamasisha ngono kabla ya ndoa. Hapa namaanisha mapenzi kwa maana ya upendo.
Je, mwenzi wako mtarajiwa ni faraja kwako? Anakusaidia unapokuwa na matatizo makubwa ya kiafya? Yupo nawe bega kwa bega katika maswaibu yanayokukuta? Lazima awe na mapenzi ya dhati na wewe.
Lazima mwezi wa maisha yako awe anakupenda kweli kweli. Ambaye anaweza kuifanya siku yako kuwa bora. Ndugu zangu, unaweza usione umuhimu wa jambo hili, lakini nataka kuwaambia kwamba, mwenzi ambaye hata kutumia neno baby, sweetie, mumy, dear, d na mengineyo ni shida, ni tatizo.
Unatakiwa kuwa na mtu ambaye ukiwa na matatizo kazini, anakuambia: “Usijali baby, yataisha. Nipo kwa ajili yako. Mimi ndiyo faraja yako.”
Dalili za mwenzi wa aina hii utaziona mapema sana. Anza kumfuatilia kuanzia sasa hivi utagundua. Lazima awe na maneno matamu ambayo yatakutuliza jazba zako wakati ukiwa na mambo binafsi yanayokukwaza.
Nawe ambaye unatarajia kuingia kwenye ndoa na mwenzako, jifunze kuwa na maneno matamu. Kuwa mtu wa karibu na mwenzako muda wote, sikiliza shida zake, kuwa mshauri wake mkuu. Hapa nasisitiza, sizungumzi na jinsi moja. Wote wanahusika.
Wapo baadhi ya watu wanalalamika: “Mwanaume gani nikimuomba fedha za matumizi hanipi. Mbona wenzangu wanatunzwa na wanaume zao?” Hiyo siyo sahihi marafiki.
Maisha ya siku hizi ni kusaidiana. Kuwa mpenzi wake haimaanishi atamaliza shida zako zote, wakati mwingine hata wewe unapaswa kumsaidia. Hayo ndiyo mapenzi ya kweli. Marafiki, natamani kuendelea lakini nafasi yangu ni ndogo sana. Wiki ijayo tutamalizia.

No comments:

Post a Comment