Somewhere Blog: AUNT EZEKIEL ANA MIMBA MIEZI SITA

AUNT EZEKIEL ANA MIMBA MIEZI SITA


SIKU chache baada ya staa wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel kuripotiwa kufunga ndoa mjini Dubai, mchumba wa staa huyo aliyetambulika kwa jina moja tu la Jeff amesema kuwa, anashangazwa na Aunt kuolewa huku akiwa na ujauzito wake, Amani linashuka na mistari ya habari hii.
Akizungumza na Amani jijini Dar hivi karibuni, Jeff amesema kuwa taarifa za kuolewa kwa Aunt alizipata akiwa nchini China na kushtuka sana.
“Kinachonishangza ni huyo jamaa anafungaje ndoa na mwanamke ambaye ana ujauzito wangu wa miezi sita ambao aliondoka nao kwenda Dubai?” alihoji Jeff.
Jeff aliendelea kutiririka kama mtu alikuwa akiimba mashairi ya Muziki wa Injili kuwa, kingine kinachomuumiza ni tabia ya Aunt kumuomba fedha za matumizi akiwa Dubai huku akijua kwamba amefunga ndoa na mtu mwingine.
“Wanawake ni mama zetu lakini ni wauaji wakubwa, inakuwaje anagawa mimba ya mtu kwa mwanaume mwingine halafu mbaya zaidi nilipokuwa China kila wiki alikuwa akiniomba fedha za matumizi nami nikawa namuagiza aende sehemu kuchukua kumbe ni mke wa mtu!” alishangaa Jeff.
Juhudi za kumpata Aunt ili kuthibitisha madai hayo ya ujauzito hazikuweza kufua dafu baada ya simu yake anayoitumia huko Umangani kutokuwa hewani.
Jambo lingine lililomshtua Jeff ni kusikia kuwa aliyemuoa Aunt huko Dubai anaitwa Sunday Dimonte kwani msanii huyo ‘alisevu’ namba yake kwa kutumia jina hilo.
“Nilipomuuliza kwa nini ananisevu kwa jina la Dimonte, Aunt aliniambia kuwa jina hilo lilimaanisha mpenzi kwa Lugha ya Kifaransa,” alisema kwa masikitiko Jeff.

No comments:

Post a Comment