LOVE STORIES

LOVE STORIES:Watu wenye tabia hii husababisha mapenzi kuwa magumu
Mapenzi yamekuwa magumu. Ni mzigo mzito kuubeba. Yanaendelea kujeruhi wengi, bado ni mateso kwa wengine. Sasa hivi, asilimia kubwa ya watu inaamini kwamba kupata mwenzi sahihi wa maisha ni ndoto za alinacha. Ni kamari, ni bahati nasibu.
Maendeleo yamekuja na mambo leo. Kile kinachoonekana ni Uzungu, kimeathiri kwa kiasi kikubwa ustaarabu wetu. Mila na desturi zetu vimepokwa na utandawazi uliotujia. Hii inamaanisha kwamba uhusiano wa kimapenzi wa sasa, hauendani na sura ya utamaduni wetu.
Vijijini kuna unafuu japo na kwenyewe fujo zimeshaingia na mambo yameshabadilika. Mijini ndiyo matatizo yenyewe. Ulimwengu wa digitali na fursa za mitandao zinatutia wazimu. Tunataka kuiga mitindo ya maisha ya wenzetu, matokeo yake tunageuka watumwa wa mapenzi.
Hayakuletwa mapenzi ili yawaumize watu, yapo kwa ajili ya kutoa faraja ndani ya jamii. Yalivyo ni kwamba baada ya misukosuko ya kimaisha, vurugu mechi za kusaka riziki na mihangaiko mingine ya kimaisha, angalau unaweza kusahau yote unaporejea kwa mwenzi wako.
Hata hivyo, mapenzi hugeuka matatizo pale ambapo kazini umeondoka pakiwa moto, unarudi nyumbani nako pia unakuta moto. Unakosa sehemu ya kwenda kujishikiza. Faraja inaota mbawa. Hapa ndipo tafsiri ya mapenzi inapokosa mashiko. Jitazame, muangalie na mwenzako!
Japo ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi siku zote hayapo tambarare hata kwa wenza waliostaarabika, ila katika kundi la mabrazameni na masistaduu ni mtihani. Kuna usemi kwamba glasi hugongana kabatini, nakubaliana nao lakini kwa makundi hayo ni pasua kichwa.
Mabrazameni na masistaduu ni zao la mapenzi ya Kichina, yaani uhusiano bandia. Inawezekana akiwa kwako akajilegeza kama amefika, kumbe anao wengine wengi. Hili ni janga zito kwa maisha ya sasa. Uaminifu haupo, uzinzi na usaliti vimekuwa fasheni ya kutukuzwa.
Wengine siyo masistaduu wala mabrazameni, wapo kawaida au pengine wana muonekano wa heshima mno. Hata hivyo, ukichimbua hulka zao ndiyo utachoka. Ni wakali wa kuwapanga foleni, akitoka kwa huyu anakwenda kwa yule. Mapenzi yametawaliwa na rangi ya Shetani.
Wapo wanaobadili wapenzi kwa sababu za tamaa, lipo kundi linaloamini miili yao ni mtaji wa kupata fedha, wengine shida za maisha zikasababisha uamuzi huo wa kujidhalilisha, wapo ambao ni tabia. Bila kugusa huku na huko hatosheki. Makundi yote hayo yamezingirwa na Ibilisi.
Mume wa mtu, anapewa sifa ya ‘uchapaji’ wa vidosho. Kwamba anajua kuwapanga kila kona. Nyumba za kulala wageni, anaingia kama nyumbani kwake. Yaani wanamjua, ni mteja wao hodari. Akifika, wanampeleka kwenye chumba anachokipenda.
Wapo wanaopiga simu, yaani namba za nyumba za kulala wageni zimejaa kwenye simu yake. Akijibiwa kwamba Sinza Kumekucha hakuna vyumba, anapiga Vatican, nako akikosa anajaribu Mori. Inahitaji sala na dua kuishi na mtu wa aina hiyo. Kuna mawili, kama hatakupa maradhi, omba usijue tabia yake, atakuua kwa presha.

 

Siri nzito za kumpagawisha mpenzi wako!

Ili uweze kuwa na furaha maishani, lazima uwe katika uhusiano imara usiotetereka. Kama unaishi na mke au mume ambaye moyo wako umemchagua lazima furaha itatawala katika nyumba yenu. Lakini rafiki zangu, huwezi kuwa katika ndoa yenye furaha kama hukuwa na mchumba bora. Kwa maneno mengine, lazima uanze kuboresha uchumba wako kwanza, uwe na uhakika kwamba mwenzi uliyenaye ni sahihi ili ukiingia kwenye ndoa usijute.

Mapenzi ni sawa na bustani nzuri ya maua rafiki zangu, wakati mwingine inahitaji mbolea, kumwagiliwa maji na hata kupaliliwa.

Kwa kufanya hivyo utazidisha ladha ya mapenzi na kuyafanya yazidi kuwa na nguvu zaidi ya awali. Lakini kama hutamwagilia, hutaweka mbolea, hutapalilia, hesabu kwamba mapenzi yako yanaweza kuanza kupoteza nguvu taratibu na hatimaye kufa kabisa.

Kikubwa ambacho nimepanga kuzungumza nanyi leo ni jinsi ya kumpagawisha mwenzi wako ili awe wako peke yako. Umeshawahi kufikiria kwamba, kama ukishindwa kutimiza mambo fulani katika penzi au ndoa yako, mwenzi wako anaweza kuwa wa kushea?

Kama bado, inakubidi ufahamu hilo kuanzia leo. Mpenzi anahitaji mambo mengi ili aendelee kuwa mwaminifu kwenye penzi lenu. Ni kweli kwamba uaminifu upo kwa mtu mwenyewe, kama mtu ni mwaminifu basi atadumisha uaminifu uliopo ndani yake, lakini kama kuna mambo unakosea, lazima utasalitiwa!

Tena basi, kama mwenzi wako anakupenda, atakusaliti huku analia! Kwanini? Kwasababu analizwa ba kitendo ambacho hajapenda kukifanya ila wewe mwenyewe ndiyo umemlazimisha afanye hivyo.

Kuna nini zaidi katika dhana ya usaliti?
Tukiachana na tamaa, hulka na ushawishi, wakati mwingine mpenzi anaweza kusaliti kwa kukosa yale ya muhimu zaidi katika penzi au ndoa yake.

Kwa bahati mbaya sana, watu wa aina hii huwa hawasemi moja kwa moja kuwa wanakosa vitu fulani au wanapenda vitu fulani, badala yake hutumia lugha za ishara zaidi na kama hutaelewa basi huona suluhisho ni kutafuta pumziko lingine.

Hapa sasa mwenzi wako anakuwa si wako peke yako tena! Lakini lazima uhakikishe mpenzi wako anaendelea kuwa wako bila kushea na mtu yeyote na jambo hili linawezekana kabisa ikiwa wewe mwenyewe utataka iwe hivyo.

Zipo hatua au mambo mengi ya kumfanyia mpenzi wako ili awe wako peke yako, lakini hapa nitakupa yale ya msingi zaidi yatakayokusaidia katika penzi lako.

Njia hizi za siri nimezifananisha na shamba au bustani, ambayo ina mahitaji yake. Sasa katika uchambuzi huu, nitaainisha jinsi ya kuitunza bustani hii ya mapenzi ili kuifanya bora zaidi kila siku.

Kitu cha kwanza kabisa ni mbelea. Hapa nazungumzia penzi ambalo tayari limeshakuwa penzi! Kama ni bustani basi tayari mboga zako zimemea vizuri.

Lakini ukumbuke kwamba, bustani yako haitaweza kuendelea kuwa bora kama haitakuwa na matunzo. Hapa penzi linahitaji mbolea.
Mbolea ninayoizungumzia hapa ni maneno matamu yaliyojaa huba. Fikisha hisia zako kwa mwenzi wako kwa namna ya kipekee iliyojaa penzi la dhati.

Mweleze jinsi unavyompenda na jinsi maisha yako ambavyo hayawezi kukamilika bila yeye. Huu ni wakati wako wa kumsumbua kwa meseji zilizojaa tungo za mahaba, kadi, maua na zawadi ndogo ndogo.

Baadhi ya wanandoa wakishaoana, huacha utaratibu huu. Kuna wanaosema: “Ah! Hayo mambo ya kizamani bwana, kipindi akiwa demu wangu, sasa hivi yupo ndani, kwanini nihangaike?”
Haya ni makosa makubwa ndugu yangu. Shamba bila mbolea kuna mavuno kweli? Huwezi kuvuna.

Kitu kingine muhimu katika bustani, kama ujuavyo mpenzi msomaji wangu ni maji. Bustani yako itahitaji maji kwa ajili ya kuzidisha ustawi wa mazao yako. Hapa unatakiwa kuwa mbunifu zaidi katika mambo yanayohusu mapenzi moja kwa moja.
Unatakiwa kubadilisha aina ya ufanywaji wa mapenzi, mahali pa kukutana na hata sehemu za mitoko. Inashauriwa ili kuboresha penzi ni vizuri kutoka sehemu mbalimbali na mwenzi wako. Inapendeza zaidi angalau mara tatu kwa miezi sita, kulala na mwenzako hotelini.

Hapa utakuwa unanakshi zaidi penzi lako. Outing yako ni vyema ikawa ya kimahaba zaidi, kuanzia mavazi, sehemu mnazotembelea n.k

Mfanyie mwenzi wako mambo ya kimahaba sana mnapokuwa wawili. Mbusu, mkumbatie, mwambie jinsi unavyojisikia wa pekee kuwa wake. Utundu wako wote umalizie hapa, ukifanya hivyo utakuwa umemwagilia bustani yako vyema.

Baada ya muda bustani huota majani mengine ambayo si mboga! Yawezekana kabisa, kwa bahati mbaya uchafu ukaingia bustanini. Wakati wa palizi ni muda sahihi wa kuondoa vyote hivyo.

Hata katika mapenzi pia hutakiwa kufanya jambo hili. Kugombana au kupishana kiswahili kwa wapenzi ni jambo la kawaida sana, hivyo ni vyema kuweka sawa tofauti hizo mapema, kabla tatizo halijawa kubwa zaidi. Hii ndiyo palizi ninayoizungumzia.

Usikae na kinyongo moyoni mwako, kuwa mjanja, hata kama ni yeye ndiye aliyekosea, zungumza naye ukimweleza jinsi ambavyo hupendi mgombane, mkimweleza hisia zako kwamba unatamani sana muelewane katika siku zote za maisha yenu. Weka mambo sawa.

 

 

UKITAKA KUUA PENZI LAKO FANYA HAYA HAPA,FASTA TU

Ukitaka kufa mwakani unatakiwa kufanya mambo flani ya hovyo hovyo mwaka huu,utakufa tu..

Ukimeza dawa ya sumu usitegemee itageuka kuwa ARV,itakuua tu

Kuna aina flani ya watu wanapenda sana kujitafutia matatizo,wakiwa In love huwa wanajaribu kuwa too much,kwa vitu ambavyo sio vya msingi hata na havimuongezei lolote zaidi ya matatizo.

Kuna vitu ukifanya unajua kabisa kwamba vitakusaidia kupalilia penzi lako,kuliwekea mbolea ili likue zaidi...Concentrate kufanya hivyo

Ila kuna watu huwa wana-opt kufanya mambo ambayo yanawaua wao wenyewe na mwisho wa siku huishia kujuta tu.

Baadhi ya Mambo ambayo yameua mahusiano mengi sana na yanaendela kuua hata leo,na hata kesho yataua ni haya yafuatayo,Chonde chonde usifanye haya maana huwezi jua Damage ambayo yanafanya kwenye uhusiano wako:

1.MISTRUST

Sifa moja ya Penzi imara ni lile ambalo mnaaminiana...Mtu anaweza kuaga kwenda home na ukajua anaenda home kweli bila kuwa na chembe ya shaka kwamba atachepuka na kufanya Call Diversion.Ukiona penzi ambalo halina Trust,hilo penzi liko ICU na litakata Roho muda wowote.Hamtafika popote. Mistrust huwa haiji hivihivi,huwa ni zao la mambo mengi yaliyotokea ambayo yamemfanya mmoja kati ya wapenzi kupunguza imani na mwingine.Dawa ni kuhakikisha mnamaintain highest level of Trust at all time.Na moja ya njia rahisi sana ya kurudisha trust iliyopotea ni kuwa wawazi...Wawazi kwenye ratiba zenu za kila siku..Thats through Communication..Hakikisheni mna communication  muda wote,ifanyeni kuwa ratiba na sio utumwa,itawasaidia kuwa in touch na kila mmoja atajua ratiba ya mwenzie na kuwa at peace

2.EPUKA U-SPY

Kwenye Mapenzi hakutakiwi kuwa na mtu yeyote aliyesomea CCP Moshi...Hiki ni chuo cha mapolisi na maspy wa usalama wa taifa....Mapenzi ni eneo huru ambalo kila mmoja anapaswa kuwa huru....Sio mpenzi kaacha simu tayari umekwapua...Kuna vitu haviko kwenye Katiba ya Muungano...Simu ya Mtu ni personal property yake..Dont sneek,dont Spy...Ukimuomba simu kuitumia kupiga au kutext usijifanye spy na kuchungulia Inbox..Akigundua atakumind na itakuwa big issue...uhuru wa mtu binafsi uheshimiwe,haikusaidii lolote sanasana utakumbana na vitu ambavyo hutapenda utaishia kununa na kumbe hujavielewa..We are so different,mahusiano yangu na watu wangu niliozoeana nao ni tofauti na wewe...U can see messages na ukadhani ni za cheating kumbe ni kawaida...Stay safe...Dont be a police...Dont Spy,hata uwe tempted namna gani..hii imewacost wengi sana,BEWARE

3.EPUKA UBIZE

Ubize ni msala.Ukikubali kuwa mpenzi wa mtu jua kuna uhuru unapoteza...Japo uhuru kidogo...Mpenzi wako anakuwa priority na ni jukumu lako kuhakikisha anapata Attention....

Ndio unasoma lakini una mpenzi,dont replace him/her with books

Ndio unafanya kazi,una vikao,na assignments,na presentations,na warsha,na kila kitu ILA,una Mpenzi...Dont replace him/her with ur job...Kama huwezi kumanage Shule na Mpenzi....Kazi na Mpenzi....Chonde nakusihi,BE SINGLE,lasivyo utazingua tu mtu wa watu,atafeel hapendwi...hajaliwi..Atacheat,...na wala usimlaumu maana wakati ukiwa bize na mshule wako na mkazi wako,kuna mtu alikuwa na kazi na alimjali...Swali kwake ni Je,kwann huyu ameweza and my Boy ameshindwa???USIMLAUMU LIKITOKEA HILO,kosa ni lako 100%

4.EPUKA EXPECTATIONS

Kuna watu hawana simile...Dakika 2 tu nyingi wamewaza Mbinguni...

Mapenzi yanataka Patience....Anzeni mapenzi vizuri...Know him/her.....Jadili mustakabali wenu pamoja,akupe views zake....Then kama kuna kitu cha kuwasongesha mbele kila mmoja aseme/....Kama kuna vikwazo vya kusonga mbele kwenye hatua kubwa zaidi kama Ndoa mathalani,viwekwe wazi

Ni jambo liko wazi,kuna watu ni wazuri kuwa wapenzi tu lakini sio waume....Kuna watu wanafit kuwa Girlfriends tu lakini sio Wife material....Thats the naked truth

Mtu huyu ukimforce awe mume au mke inakula kwako....

Ndoa ni Institution maalum kwa watu maalum kwa sababu maalum

Kama wewe sio Mtu Maalum usiingie kwenye hiyo Institution Maalum maana hutakuwa na sababu maalum

The point is,usiexpect makubwa katika muda mfupi...give yourselves time to see ile sababu maalum ya kuwaingiza kwenye jukumu maalum..mkiona maono yenu hayaoani kufika kule usiforce...
Hakuna sababu ya kuwa fancy wa Ndoa halafu mkae Mwaka 1 muachane,utakuwa umejichafulia CV bure wakati ungeweza kutulia ukapata the right guy or right woman

Dont be over-ambitious....Stay in ur lane and choose the best out of the rest
 
 

AINA ZA WANAWAKE AMBAO WANAUME WANAPENDA

Sometimes Wanawake huwa wanajiuliza Maswali mengi,wafanyeje ili wapendwe,wanahisi wana bahati mbaya,kila wanapojitoa mioyo yao inaumizwa.Jamaa hawakai,wanatupia kitu,wanakula mzigo wanatembea na Bwana..Mioyo yao imejaa matundu na hawaamini kabisa kama Wanaume huwa wanapenda,imefikia point wanadhani Wanaume hutamani tu kumbe SI KWELI!


Wanaume nao wana taste zao,hawaendi tu kama Mbwa koko,jalala moja baada ya jingine,HAPANA...Know their taste and you will enjoy theirs.

Sifa za Mwanamke ambae Mwanaume atavutiwa na kukaa ni hizi zifuatazo,JITAZAME,kama huna any of these,you better try to learn to have them,its not too late:

1.MWANAMKE MWENYE MSIMAMO
Jambo moja muhimu,the number 1 thing ambacho Mwanaume anaangalia kwa Mwanamke ni Msimamo wako...Sio Mwanamke uko kama Feni,kila sehemu unapulizia upepo,Mashariki,Magharibi kote wewe...Hapo sahau,tena sahau sana.Mwanaume anahitaji kuwa na uhakika,Mwanamke aliyemkabidhi moyo hana mishemishe na hayumbishwi na lolote,na chochote na penzi lake liko safe

Unaweza kuwa na kila kitu,Mzuri wa Sura na kila kituuuu,na bado usimpate Mwanaume wa Maana kama huna sifa hii,hakuna muujiza kwenye hili,ndo wanaume walivyoumbwa,if you lack this hamna Mwanaume wa Maana utapata,utapata vimeo kama ulivyo!

2.MWANAMKE MUELEWA

Men are simple creatures,they love to live simple,and take them simple as they are...

Ukiwa aina ya Mwanamke unamind vitu...kitu kidogo ugomvi...Unaongea na nani...Uko wapi..Na nani,Kwanini,hee,jamani kama Mahaakama kuu??Hapa unapoteza Credits

Kuwa aina ya Mwanamke muelewa ambae utamfanya Mwanaume ajisikie vibaya kufanya kitu flani ambacho ulishamwambia asifanye before...Lakini sio kukaripia na kununa kwa sababu amerudia..let him realize that amefanya kitu cha kukuudhi na hujareact,and if hes a man enough,he will know and apologize

Ila kama ni gumegume basi tena,litakausha na ndo inakuwa issue hapo...Are u patient enough to handle it??kazi kwako,ila kuna wanawake wana uwezo huu,learn from them wamewezaje..No matter how complicated the man is,they know how to handle him

Jua Lugha ya kutumia ambayo utafikisha ujumbe and yet you dont show him kwamba umemind na unamkaripia...kumkaripia Mwanaume ni msala mpya,hata kama ana kosa atakumind na itakula kwako...Una ulimi mzuri kufikisha ujumbe??

3.MWANAMKE DIRECTOR

Baba ni kichwa cha nyumba....mimi huamini Mama ni macho yaliyo kwenye kichwa hicho

Women play a very vital role in DIRECTING THE HEAD TO THE RIGHT WAY

Kichwa bila macho si utajigonga tu????Mwanamke ni jicho...

Ukikalia kujiremba tu na kuwaza mambo mengine bila kujua kuna kichwa kinasubiri maelekezo yako,utaonekana bogus..kutwa uko kwenye Umbea,huna muda wa kujua ur man anafanya nini,ana plan gani mwaka huo,unamsaidiaje kuzifikia,sasa we faida yako nini kwenye maisha yake??

be the kind of a woman ambae Mwanaume aki-achieve jambo anasema I have a woman beside of me who engineered this...Kama hujawahi kufikia hatua ya kuwa appreciated na ur man kwa jambo hili jua kuna mahali umefeli...Na hili haliji hivihivi,linakuja pale kunapokuwa na proper communication between you and ur man...Bila good communication:
 1.Hutajua what ur man is up to
 2.Kwa sababu hujui what he is up to hutakuwa na msaada.
 3.Akifaulu,jua haupo kwenye picha ya mafanikio yake na ur simply useless
 4.Akifeli,ur part of his failure kwamba humsaidii lolote..ur simply useless and actually absent in his life kwa sababu uwepo wako haumsaidii its better he becomes alone!YOU HEARD???

Women have planning and control ability,USE IT...Usikae tu kama muuza genge unasubiri wateja,Do your job and Win him!

4.MWANAMKE MSAFI NA MZURI

Usafi huu sio wa nguo tu na kunukia,ni zaidi ya hilo...

Usafi unaanzia ndani..Msaidie Mwanaume awe msafi pia,rohoni hadi mwilini...Rohoni how???Jitu halisali,halikumbuki kuna Mungu,lipo tu,unadhani mtajenga Familia gani baadae???

Msaidie kum-remind kukumbuka hilo,Mafanikio ya nje huanzia ndani..Dirty inside,Dirty Outside...Mambo mengine anafanya nje na yanaku-affect kwa sababu umefeli ku-inspire change ya ndani...Ngumu hii lakini ndo hivyo..You can save a lot of energy kama atakuwa msafi wa ndani,everything outside will be set automatically...Whatever u see in physical started in Spiritual...Yeah right! Hata ulimwengu uliumbwa,na vyote unavyoviona baada ya Plan ya Spirit kumalizaika.Soma Kitabu cha Mwanzo kwenye Biblia,uone Uumbaji ulifanyikaje...Same applies na hapa,Uumbaji wa vitu vya nje,Mahusiano imara,Familia bora,inajengwa ndani..

Sio kazi yako ni kuuliza Baby hatuendi Club,Baby this...Unamkumbusha kusali???Utatengeneza mme freemason bila kujua...Mtu hasali we upo tu unaona sawa...CHANGE!

Huu usafi mwingine wanawake mmejaliwa,biashara za kunuka kikwapa no,Kusafisha nyumba vema saafiii...mengine si kama kawa??Mpango mzima uko hapo.

Uzuri huwa ni subjective...Unaweza kuwa mzuri kwangu lakini ni wa kawaida kabisa kwa mwingine....Ukiwa msafi unaweza ukamfanya Man wako aone potential,hata kama wewe sio mzuri sana lakini anaona Kiongozi wa Familia inside you and he will definitely opt you.

Hamna limbwata wala nini,tupa kule mbali...

Kama huna hizi sifa 4,aisee waza upya...Unaweza bahatisha ndulute ukaolewa,lakini jusitegemee muujiza,goma litapata Pancha tu...Jamaa hataweza kukaa na nunda...Atajutia Mahari aliyolipa ila atasepa kimyakimya..

To avoid that,please make sure you do your Homework well ili Mtihani ukija unafaulu tu bila shida...

Jitathmini halafu KAA HUMO! .

No comments:

Post a Comment