Somewhere Blog: BARNABA ANASWA NA DEMU GESTI

BARNABA ANASWA NA DEMU GESTISiku chache baada ya mwanamuziki Barnaba Elias kutangaza kujaaliwa mtoto wa kiume aliyezaa na mwanamke anayeishi naye, msanii huyo hivi karibuni alinaswa akiwa na demu mwingine kwenye nyumba ya kulala wageni mjini hapa.
Barnaba alifika Zanzibar kwa ajili ya kufanya shoo kwenye Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar (ZIFF) linaloendelea Kisiwani Unguja ambapo paparazi wetu akiwa kwenye gesti ya Malindi alimuona binti mmoja akiingia na kumtaka mhudumu ampe funguo za chumba alicholala msanii huyo.
“Mimi naomba unipe funguo za chumba atakacholala Barnaba kwani ndicho nitakacholala,” alisema binti huyo ambaye inadaiwa alitokea Dar.
Kauli hiyo ilimshangaza mhudumu wa mapokezi ambaye alimtaka demu huyo kurudia alichokisema na jibu likawa:
“Nimekwambia hivii, chumba anacholala Barnaba ndo’ changu, wewe nipe funguo mwenyewe atakuja muda si mrefu.”
Kufuatia maelezo hayo, mhudumu huyo aliamua kutoa funguo ambapo demu huyo alikwenda kuingia kwenye chumba namba 5.
Mwandishi wetu aliendelea kufuatilia mkanda mzima ambapo baada ya Barnaba kumaliza shoo yake kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe, alirudi kwenye gesti hiyo akiwa ameongozana na demu huyo kisha kuingia ndani.
Kesho yake mishale ya saa 4:30 asubuhi, mhudumu wa gesti hiyo alimtaka Barnaba kuachia chumba ili waweze kufanya usafi ambapo kauli hiyo ilimtibua msanii huyo ambaye alitaka aruhusiwe kuendelea kuwepo pale hadi saa 10 jioni.
Kutokana na mazingira hayo, ulitokea msuguano kati ya wahudumu na Barnaba lakini baadaye msanii huyo alilazimika kuondoka katika gesti hiyo akiwa ameongozana na demu huyo.
Jitihada za kumpata Barnaba kuzungumzia uhusiano uliopo kati yake na demu huyo hazikuweza kuzaa matunda mpaka tunakwenda mtamboni.

No comments:

Post a Comment