msichana ndotoni mwangu.....ep.81












msichana ndotoni mwangu.....ep.81

Mariya! Merina! ” Victor Fedorov aliita akizidi kuwatingisha watoto wake lakini bado hakuwepo hata mmoja aliyeweza kujibu neno lolote.

“Mlinzi hebu niletee maji haraka,” aliamuru, na bila kujibu kitu chochote, mlinzi alitoka mbio na sekunde tatu tu baadaye alirejea na maji kwenye bakuli kubwa.

Haraka akalipokea na kuanza kuwamwagia akiamini kwamba kufanya hivyo kungeweza kuwarejesha katika hali zao za kawaida lakini hilo halikutokea, akiwa hapo machozi yakambubujika, akaiona kabisa picha ya kubaki peke yake duniani na utajiri aliokuwa nao.

Victor Fedorov akaikataa picha hiyo na kuendelea kuwatingisha tena na tena akiwaita watoto wake kwa majina.

Watoto wake walikuwa wamebadilika kwa kiasi kikubwa, afya zao zilikuwa mbaya kupita maelezo, walikuwa wamebadilika kwa kila kitu kuanzia mavazi mpaka nywele, hali hiyo ndiyo iliyozidi kumtia wasiwasi Fedorov. Akiwa hapo ghafla akili yake ikamweleza kwamba kama alihitaji watoto wake wapone na kurejea katika hali zao za kawaida ni lazima atamfute daktari ambaye angewasaidia.
“Jambo moja linaweza kufanyika kwa sasa?”
“Jambo gani mkuu.”

”Daktari, ni lazima nipate daktari ambaye atakuja hapa kuwaangalia nitamlipa kiasi chochote kile cha fedha ilimradi tu aokoe maisha ya watoto wangu,” aliongea kwa majonzi, na taratibu akanyanyuka na kuisogelea simu lakini kabla hajaifikia alimsikia mlinzi akiguna.

Bila kujiuliza mara mbili akatoka mbio kuelekea eneo hilo, alichokishuhudia hapo kilimtoa machozi; Mariya na Merina walilala chini huku mapovu mengi yakitoka midomoni mwao pia walionekana kutupa mikono na miguu kama vile walikuwa wakikata roho. Victor Federov akalia kama mtoto mdogo.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

“Bosi hebu njoo uone mbona wanatoka mapovu!”
“Mapovu?” aliuliza akikimbia kurejea eneo hilo. Ni kweli Mariya na Merina walikuwa wakitiririkwa na mapovu kutoka midomoni mwao.

“Mungu wangu ni kitu gani hiki? watoto wangu wamepewa…”
“Wamepewa nini bosi wangu?”
“Wamepewa sumu hawa haya mapovu ni ya nini? Watoto wangu wanakufa wakati nikiwa tayari nimeshapoteza fedha nyingi, tafadhali msiniache, naomba msiniache nitabaki na nani katika dunia hii? Fedha na mali si kitu kama sina ndugu wala mtoto yeyote? Mungu nisaidie,” aliongea mfululizo.

Akiwa hapo, Victor Fedorov akionyesha kukata tamaa kabisa, mawazo yake yote yakampeleka kwa jambazi aliyemwona ndani ya msitu wa Beloomut akamshuhudia akikimbia na begi lililojaa fedha nyingi ndani yake na kutokomea.

“Kama ni fedha nilimpatia, kwa nini ameua watoto wangu? Kwa nini amewatesa viumbe wasio na hatia? Utajiri wangu umekwenda, na watoto pia wananiacha, nimekosea nini kwa Mungu? Pengine jambo hili linatokea kwangu kama adhabu kwa makosa niliyoyafanya huko nyuma? Hapana! Nashindwa kuelewa…” aliongea mfululizo akiwa pembeni mwa watoto wake ambao mpaka wakati huo walishatulia kimya, mapovu hayakutoka tena midomoni mwao na miguu na mikono yao ilikuwa imetulia kimya.

“Yametimia!” hivyo ndivyo alivyosema Victor Fedorov na kuangua kilio kikali ndani ya nyumba, mlinzi akasogea karibu yake na kumbembeleza.
“Haiko haja ya kuishi! Bora nife niuungane na familia yangu? Watoto wangu wa kwanza walikufa kifo kibaya wakati wakicheza mchezo wa kuteleza katika barafu na hawa nao …”
Kwikwi ya kulia ikamkaba ni kweli taswira za watoto wake wawili pamoja na mkewe waliokuwa wamekufa miaka mingi kabla, ilimjia kichwani mwake akajiona ni mtu mwenye mkosi duniani hata thamani ya utajiri aliokuwa nao hakuiona, akatamani kuungana na familia yake.

“Nitakufa! Si muda mrefu kuanzia sasa nitaungana na familia yangu…Mungu wangu…kwa nini yote haya…kwa nini mimi? Nimekosa nini?” alizidi kujilaumu.
Akionyesha kukata tamaa kabisa, akasogeza mkono wake wa kulia na kuupeleka moja kwa moja upande wa shingo ya Mariya ili kupima mapigo yake ya moyo ambapo yalionekana kutulia akageuka tena upande wa pili na kugusa mapigo ya Merina nayo yalionekana kuwa kimya kabisa.

Bila kusema tena neno lolote akatembea na kwenda kuketi juu ya kiti huku jasho jingi likimtoka na mwili wake ukitetemeka.
“Bosi mimi naona tuwapeleke hospitali huko tutapata mtaalamu ambaye atasema neno.”

“Lipi zaidi?”
“Mimi nashauri tufanye hivyo pengine wamezimia tu.”
“Nina hakika wamekufa, watoto wangu, wameniacha lakini naamini kabisa nyuma ya mchezo huu yupo mtu fulani sijui ni nani ila yupo, mbona nimetimiza masharti yote? Nimetoa fedha nyingi sana kuwakomboa lakini amenilipa ubaya?” aliongea muda wote huo akiwa ameketi akionyesha kukata tamaa juu ya maisha yake na mbele yake alifikiria kitu kimoja tu; kifo basi.
***
Baada tu ya kutoka ndani ya lango kuu la hoteli ya Lamada, Lina akiwa amejifunika shuka alikimbia na kuvuka upande wa pili wa barabara, watu wachache waliokuwepo eneo hilo wakimshangaa, lakini hakujali alidhamiria kuondoka hapo na kutokomea, huku akilia akasogelea moja ya teksi.

“Wewe ni mtu au mzimu?” aliuliza dereva teksi aliyekuwa ndani ya gari, haraka akaufungua mlango na kutoka nje tayari kukimbia kwani mara kadhaa historia katika eneo hilo ilionyesha kwamba mizimu ilikuja hapo kutoka makaburi ya jirani hivyo kutokea kwa mtu huyo tena akiwa katika shuka nyeupe kulimwogopesha.
“Kaka usikimbie tafadhali naomba msaada wako mimi ni mwanadamu wa kawaida.”

“Mh! Hapana usinidanganye tena ona unaongea sauti ya mwanamke, kwa jina la Yesu toka mbele ya macho yangu!”
“Mimi si mzi…” aliongea Lina lakini kijana huyo hakuwa tayari kumsikiliza bado aliendelea kurudi kinyumenyume akijiandaa kukimbia ili kuondoka eneo hilo.

“Ona! Mimi ni mwanadamu!” aliongea akijaribu kufunua shuka alilojifunika.
“Mungu wangu! Nakufa jamani, jini hili tena yuko…” alipaza sauti na kufanya teksi nyingine zote zilizokuwa jirani madereva wake wawashe magari yao na kuondoka eneo hilo kwa kasi.

Kwa uwezo wake wote alijaribu kujitetea kuwafanya watu waliokuwepo eneo hilo wamwone kwamba alikuwa ni mwanamke wa kawaida lakini ilionekana kushindikana, teksi zote zikaondoka eneo hilo na kubaki moja tu ambayo dereva wake aliondoka na kuacha gari peke yake eneo hilo.

“Nitafanya nini sasa?” alijiuliza huku akilia, alitaka kufanya kila kilichowezekana kuondoka eneo hilo kurejea nyumbani kwake, ndani ya moyo wake kulijaa hasira kali juu ya Phillip, hakika hakumpenda tena na aliapa kumchukia maisha yake yote yaliyobaki.

“Phillip amenidhalilisha kupita maelezo, sipo tayari tena kuendelea kuwa naye! Yaani hivi? Mimi kabisa? Mh! Siyo Lina nadhani ni mzimu wake?” alijiuliza akizidi kusonga mbele, kichwani mwake hakuwa na picha ni wapi alikuwa akielekea lakini alitaka tu kuondoka eneo hilo.

“Naamini nitapata tu njia ya kuondoka hapa kabla hakujapambazuka,” aliwaza.
***
“Ngrii! Ngrii!Ngriii!” Ulikuwa ni mlio wa simu, mlinzi wa Victor Fedorov baada ya kuona kwamba bosi wake alikuwa amekata tamaa aliamua kutumia uwezo aliokuwa nao, akasogea karibu na simu na kubonyeza namba kadhaa kitengo cha hatari akiomba gari la wagonjwa.

“Naweza kupata gari la wagonjwa haraka sana?”
Upande wa pili ulijibu.
“Ni nyumbani kwa Victor Fedorov nadhani ni mtu anayefahamika sana hapa kwetu, tafadhali fanyeni haraka kuna wagonjwa hapa…” aliongea kwa msisitizo.
“Hakuna haja tayari wamesha…” aliongea Victor Fedorov huku akilia.

“Hapana bosi sisi si madaktari ngoja tuwapeleke hospitali pengine huko tunaweza kupata ufumbuzi wa tatizo.”
“Kweli?”
“Ni kweli kabisa.”
“Mariya! Merina kweli mmeondoka na kuniacha wanangu? Maisha bila ninyi si kitu, nilijaribu kwa nguvu na uwezo wangu wote kuwapata lakini sasa mmeondoka wana…”

Wakiwa hapo haikuchukua hata muda wa dakika tano tayari king’ora kikasikika nje ya lango la kuingilia ndani ya nyumba ya Fedorov, mlinzi akakimbia haraka kwenda kufungua geti, moja kwa moja gari likazama ndani na watu wawili wakiwa wamevalia nguo za rangi ya bluu wakashuka.

“Yuko wapi huyo mgonjwa?”
“Siyo mgonjwa ni wagonjwa wako wawili?”
“Wawili?”
“Ndiyo.”
“Wako wapi?”
“Huku! Twendeni huku nikawaonyeshe,” mlinzi aliongea akitangulia mbele huku akikimbia.

Wote watatu wakazama ndani ambako mlinzi aliwaonyesha wagonjwa na kumtambulisha Victor Fedorov kwamba ndiye baba wa watoto hao na bila kusema kitu watu hao wakainama na kuanza kuwachunguza watoto hao wakishika sehemu mbalimbali za miili yao kuwaangalia na mwisho kabisa wakachukua kipimo maalum cha kusikiliza mapigo yao ya moyo.

Muda wote huo wakihangaika, Victor Fedorov alikuwa pembeni yao naye pia akionyesha wasiwasi mwingi.
“Wako hai?” aliuliza.

“Mh! Mh!” waliguna kwa pamoja huku wakinyanyua macho yao kumwangalia Fedorov, naye akayasoma vyema na kuelewa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.

“Tafadhali nielezeni ukweli msinifiche jambo kuna kitu hapa.”
“Mzee! Matumaini haya…” hawakumalizia sentensi yao wakamshuhudia Victor Fedorov akishuka chini na moja kwa moja akawainamia watoto wake na kuanza kuwabusu mfululizo huku akilia.







MSICHANA NDOTONI MWANGU .......EP.82

Lina aliendelea kutembea barabarani huku akilia akili yake haikuonekana kufanya kazi kwani kila kitu alichokifikiria kuwa msaada kwake kilionekana kukwamwa kabisa.

“Ni lazima niondoke hapa kabla hakujapambazuka.” Aliongea akizidi kusonga mbele.

Huku akijilaumu moyoni mwake kwa mambo yote yaliyomtokea, aliamini bila kukutana na Phillip na kumpenda kisha kufunga ndoa naye hayo yote yasingempata, akazitupa lawama zote kwa mwanaume huyo na kumchukia kabisa.

Jambo moja liliendelea kupita kichwani mwake ni kwamba, mara tu akifanikiwa kufika nyumbani ni kuchukua kila kilichokuwa cha kwake kisha kumwachia Phillip nyumba na yeye kwenda kutafuta sehemu nyingine ambako angeishi maisha yake.
“Nitaondoka, nitamwachia Phillip nyumba, kwa kitendo hiki siko tayari kumsamehe amenidhalilisha sana,” bado Lina aliendelea kujilaumu.
***
Phillip aliyekuwa ndani ya hoteli pamoja na walinzi wawili waliushuhudia mchezo mzima jinsi ulivyokuwa ukiendelea lakini hakuthubutu kufungua mdomo wake kueleza jambo lolote.
Kufanya kwake hivyo ingekuwa ni kujipalia makaa ya moto kwani mwanamke aliyetoka mbio ndani ya chumba akiwa na shuka tu mwilini mwake ni mkewe na kibaya zaidi mwanaume alikuwa akimfuata kwa nyuma huku akimwita ili arejee wamalizie shughuli iliyokuwa mbele yao, ilikuwa ni fedheha ya kutosha kwake.
“Sijui anakwenda wapi? Masikini mke wangu… nisamehe halikuwa kusudio langu kutenda haya,” aliwaza huku akikimbia kuelekea lango kuu la kutokea hotelini ili ashuhudie ni wapi Lina alikuwa akielekea.
Kabla hajatoka nje ya lango akalikumbuka gari lake, akaamua kurejea ili alichukue na kuondoka nalo kumfuatilia Lina, jambo hilo lilifanyika kwa haraka, alipolifikia bila kusema kitu akaingia ndani ya gart hilo na kuliwasha haraka akakanyaga mafuta na likatii amri ba kutoka nje ya hoteli hiyo.
Aliwashuhudia walinzi wawili aliokuwanao wakiwa na mtu mwingine wa tatu na alipotupa macho yake kumwangalia mtu yule alimtambua kuwa ni mwanaume aliyekuwa na Lina ndani ya hoteli, alikuwa akiangua kilio huku akiongea maneno ambayo Phillip hakuyasikia vyema.
“Nitamtafuta Lina mpaka nimpate nimwombe msamaha mke wangu najua ananipenda na atanisamehe,” aliongea akikunja usukuni na kutokeza barabarani.
Moyo wake ulijawa hofu na kujitupia lawama nyingine lakini alijipa moyo baada ya kuamini kwamba jambo lililokuwa limetokea siku hiyo lilikuwa ni kati ya makubaliano yake na mkewe Lina.
Hakuwa na ufahamu kabisa wa kile kilichotokea ndani ya chumba cha hoteli ile mpaka mfarakano ukatokea, hakufahamu kabisa kwamba Lina hakuwa tayari kufanya tendo la ndoa na mwanaume mwingine, kwake yeye aliamini kwamba kufanya hivyo kungeidhalilisha ndoa yake kama si kuisaliti.
Phillip akaliendesha gari taratibu huku akitupa macho yake huku na kule kuangalia kama angeweza kumwona Lina eneo hilo lakini hakufanikiwa.
Baada ya mwendo mrefu alitupa macho upande wa pili wa barabara na kufanikiwa kulishuhudia kundi kubwa la watu walioonekana kubishana kitu fulani, wazo la kuwafuata watu wale kujaribu kuwauliza likamwingia kichwani mwake.
Philip akaliendesha gari na kuelekea upande wa pili wa barabara na kupaki pembeni kisha kulizima kabisa, akashukua ndani na kuwasogelea watu wale waliokuwa wamekusanyika kila mmoja akiongea lake.
“Habari za saa hizi jamani?” Aliuliza kwa sauti ya kiume.
“Salama!”
“Naomba kuuliza.”
“Uliza tu tunakusikiliza.”
“Sijui mmefanikiwa kumwona mwanamke mmoja akipita hapa?”
“Mwanamke?”
“Ndiyo”
“Mh! Yule si mwanamke ni mzimu.”
“Mzimu?”
“Ndiyo, tena umevaa shuka nyeupe, umekimbilia kuleeee,” alisema mtu mmoja huku akinyosha kidole kuelekeza upande alipoelekea Lina.
“Wapi?”
“Wee kaka huo mzimu unaoulizia umekwenda kule.”
Maumivu makali yakauchomoa moyo wake, yalikuwa kama vile mshale wa moto, Phillip akaonekana kama mtu aliyenyeshewa na mvua, bila kujibu chochote taratibu akaingia tena ndani ya gari lake na kuanza kuondoka eneo lile bila kuuliza tena swali kwa mtu yeyote.
Watu waliokuwepo katika kundi lili wakazidi kumshangaa.
***
“Mzee hakuna haja ya kulia nashauri tuwapeleke watoto hospitalini.”
“Kufanya nini wakati wameshakufa?” Victor Fedorov aliuliza huku machozi yakimbubujika.
“Hakuna aliyesema wamekufa hawa ila…”
“Ila nini? Mbona mnazidi kunichanganya ninyi?”
“Bosi tufuate ushauri wa watalaam,” mlinzi wa Victor aliongea akimpigapiga bosi wake sehemu za mabegani.
“Sawa lakini matumaini hayapo, watoto wangu wameniacha mkiwa, Mariya na Merina wameondok…” Victor Fedorov aliangua kilio huku kwikwi ikimkaba.
Kwa Victor Fedorov tajiri ambaye alivuma kupita maelezo ilionekana kama ndoto, hakuwa tayari kuamini kwamba alibaki peke yake duniani huku akiwa ametoa karibu nusu ya utajiri wake wote kuwakomboa watoto wake Mariya na Merina lakini sasa nao walikuwa wamemwacha mkiwa katika dunia ambayo hakika hakufahamu nini ingekuwa hatima yake.
Utajiri wake wote aliokuwa nao sasa ulikuwa hauna maana tena.
“Ngoja twende hospitali nitajua kila kitu huko,” aliwaza kichwani mwake huku akishuhudia watoto wake wakibebwa mmoja baada ya mwingine na kuingizwa ndani ya gari la wagonjwa.
“Mzee kwa sababu nafasi yetu ni finyu tungeomba uendeshe gari lako ukitufuata kwa nyuma”
“Hakuna shida”
Victor Fedorov akafanya hivyo lakini akamwomba mlinzi wake waongozane wote kwani hakuwa katika hali nzuri. Baada ya kuhakikisha kwamba kila kitu kilikuwa sawa nyumbani hapo wakafunga milango na wote kutoka.
Gari la wagonjwa lilikuwa mbele yao huku likipiga king’ora cha kuashiria hatari na wao wakiwa nyuma huku Fedorov akionekana kuzama katika lindi la mawazo.
Victor Fedorov aliendesha gari sambamba kabisa na gari la wagonjwa hakutaka kuliacha hata hatua moja, hamu yake kubwa ilikuwa ni kufika hospitalini na kuona watoto wake wakifanyiwa uchunguzi maalum ambao aliamini ungerejesha majibu yakatayomfanya arejee tena katika dunia, kwani tayari alishajihesabu kwamba alikuwa ni marehemu mtarajiwa kama tu angeelezwa kwamba watoto wake Mariya na Merina hawakuwa na maisha tena.
“Hapana! Sitaki wafe, nataka waishi, Mungu naomba unisaidie jambo hili, nawapenda mno watoto wangu kama kweli watakuwa wamefariki basi na mimi nitakufa, hakika watazikwa siku moja na mimi,” aliongea kwa sauti iliyomshtua mlinzi wake ambaye muda wote huo naye alikjuwa akiwafikiria watoto hao.
“Hawatakufa,” mlinzi alijibu akimwangalia Fedorov.
“Vruuu! Vruuu!” Sauti ilisikika






MSICHANA NDOTONI MWANGU .......EP.83

“Vruuu! Vruuu!” sauti ilisikika.
Kelele za matairi ya gari yakisugua barabara zilisikika, dereva wa gari alikuwa akijitahidi kadiri ya uwezo wake kukanyaga breki ili kunusuru maisha ya mtu aliyekuwa akikatiza barabarani asubuhi hiyo.
“Mungu wangu! ” Victor Fedorov aliongea macho yake yote yakimwangalia mtu huyo, hasira ya ajabu ilikuwa imemshika lakini alipokumbuka kwamba alitakiwa kuondoka eneo hilo haraka kuliwahi gari la wagonjwa lililobeba watoto wake hakuongea neno jingine zaidi, akaliwasha gari na kuondoka eneo hilo haraka.

“Pole sana bosi,” mlinzi aliongea.
“Ni balaa hilo limeshapita zake.”
“Dah! Sijui alikuwa haoni?”
“Siyo kuona tu hata king’ora hakukisikia?”
“Msamehe, pengine mawazo ya maisha yamemchanganya.”

“Ni kweli kabisa nimeshamsamehe, ndiyo maana sikufanya chochote zaidi ya kumwangalia tu,” aliongea Fedorov akikanyaga mafuta kulifuata gari lililobeba watoto wake ambalo halikuwa umbali mrefu sana na gari lake.

Kwa mwendo wa dakika kumi nzima aliendelea kulifuata gari la wagonjwa kwa nyuma, hofu yake ikizidi kuongezeka juu ya hali ya watoto wake, na mawazo mengi yaliufunika mtima wake. Ni mlinzi ndiye aliyekuwa pembeni yake kumfariji na kumweleza kwamba kila kitu kingekwenda sawa na hakusita kumweleza wazi kwamba watoto hao hawakufa bali walikuwa katika hali ya kuzimia na muda si mrefu baada tu ya kuonana na madaktari wangepata nafuu na wote kurejea nyumbani.“Ahsante ndugu yangu, sipendi kushuhudia vifo vya watoto wangu kwani hao ndiyo ndugu pekee niliobakiza duniani, kama ikitokea wakaniacha basi na mimi sitaweza tena kuendelea kuishi dunia ya peke yangu, nitawafuata.”

Maneno hayo yalipita moja kwa moja masikioni mwa mlinzi na akili yake ikauona utajiri wa Victor Fedorov mikononi mwake kwani kama ingetokea watoto wale wakawa wamefariki dunia na Victor Fedorov kujiua kama alivyokuwa akisema basi utajiri wote ungekuwa wake, aliliamini jambo hilo kwa asilimia mia moja.
“Akijiua kweli basi nitakuwa mrithi wake, kwani hana ndugu huyu na kama mwenyewe alivyokiri kwa kinywa chake, utajiri huo utakuwa mikononi mwangu, ” aliongea.

Ni sauti ya Fedorov iliyomshtua na kumtoa katika dimbwi hilo la mawazo.
“Je,uko wapi mbona umenyamaza ghafla, umepatwa na nini?”
“Ah! Bosi unajua ninakuonea huruma sana…lakini zaidi afya ya watoto…”
“Watakufa?” alidakia tena Fedorov.

“Mh! Kwa kweli sijui chochote mpaka sasa ngoja tufike hospitali kwanza,” aliongea mlinzi huyo akimwangalia bosi wake kwa jicho la tamaa ya utajiri.
“Ongea neno wewe sasa si mlinzi tu bali ndugu yangu.”
“Unasema?”
“Wewe ni ndugu yangu bwana,” kauli hiyo ikazidi kumchanganya zaidi ubongo wake.

“Mh! Au amenigudua? Kwa nini ameniambia kitu ninachokifikiria?” alijiuliza kimoyomoyo na haikuchukua muda mrefu sana, tayari wakawa wameshafika hospitalini ambapo haraka wote wawili baada ya kuegesha gari sehemu ya maegesho wakashuka na kuanza kukimbilia eneo la mapokezi ambako gari la wagonjwa lilionekana.
“Wakikaribia eneo hilo wakashuhudia machela mbili zikisukumwa kutoka ndani na kusogezwa karibu kabisa na mlango wa gari kisha kufunguliwa na watoto wawili wakatolewa na kuweka juu yake.

“Tafadhali fanyeni haraka sana tujitahidi kuokoa maisha ya wagonjwa hawa,” ilikuwa ni sauti ya daktari aliyekuwepo ndani ya gari la wagonjwa.
Wakati zoezi hilo likiendelea Victor Fedorov alishafika eneo hilo na kushuhudia machela zikisukumwa kwa kasi ya ajabu kuingizwa ndani ambako naye alizifuata kwa nyuma akiwa na mlinzi wake.

“Na ninyi mnakwenda wapi huku?” ilikuwa ni sauti ya mwanaume aliyesimama eneo hilo akionekana kuwa mlinzi.
“Watoto wangu, hawa ni watoto wangu.”
“Watoto wako?”
“Ndiyo,” alijibu akikimbia kuelekea mbele.

“Na wewe ni nani?”
“Huyo hapo ni bosi wangu mimi ni mlinzi wake.”
“Wewe unaweza kubaki hapa acha mhusika afuate nyuma, sawa?” aliuliza akimzuia mlinzi aliyekuwa ameongozana na Fedorov.
Akashuhudia Fedorov na wauguzi waliokuwa wakisukuma machela wakitokomea na kumwacha hapo peke yake akiwa hajui nini cha kufanya.

***
“Lina! Lina! Linaaaa!” ilikuwa ni sauti ya Phillip akiita jina la mke wake.
Ni sauti hiyo ndiyo iliyopenya moja kwa kwa moja masikioni mwa Lina na kumfanya ageuke kuangalia ilitokea wapi, taratibu huku akibubujikwa na machozi akageuza shingo yake na kuangalia nyuma pamoja na kwamba kulikuwa na giza lakini aliweza kuona taa za gari zikija nyuma yake kwa kasi kubwa, akasimama. ”Tafadhali simama, simama tuongee mke wangu.”

“Mh! Sauti ya Phillip hiyo,” aliongea.
Akiwa hapo akashuhudia gari likisimama mbele yake na mwanaume akachomoka ndani yake akikimbia kumfuata.
“Nisamehe mke wangu ishara ya magoti kwako ni kuonyesha kwamba nimekukosea,” aliongea Phillip akipiga magoti mbele ya Lina.
Machozi yakambubujika Lina, hasira ilikuwa imemkaba zaidi alipomshuhudia mwanaume aliyempenda kupita kiasi akiwa mbele yake kumwomba msamaha na ni huyu ndiye aliyekuwa amesababisha kutokea kwa sakata lote hilo ndani ya hoteli ya Lamada.
“Umenidhalilisha Phillip.”

“Nisamehe ndiyo maana niko chini ya miguu yako.”
“Phillip! Phillip nyanyuka uondoke sita…” aliongea Lina akijitoa mikononi mwa Phillip ambaye muda wote huo bado alikuwa chini amepiga magoti.
Kwa nguvu zake zote Lina alijaribu kujitoa kwa Phillip lakini haikuwezekana, wote wawili wakajikuta wakigalagala chini.
Phillip bado aliendelea kumwomba Lina msamaha akimsihi akubaliane na ombi lake pia akubali kuingia ndani ya gari waondoke kwenda nyumbani, huko wangemaliza tofauti zao zote.

“Sitaki! Sitaki nasema sitaki mbona hutaki kunielewa, kwa kitendo hiki kilichotokea leo siko tayari kukusamehe.”
“Nisamehe mke wangu mimi mwenyewe ninaumia moyo.”
“Phillip uumie wewe? Nakuambia umenidhalilisha na si mimi tu hata Daniel, sidhani kama atakuwa tayari kunisamehe kwa ninavyomfahamu, huko aliko anapanga jinsi ya kulipa kisasi kwangu, masikini wa Mungu haikuwa dhamira yangu kufanya yaliyotokea ni wewe ndiye umeni…” aliongea Lina na kushindwa kumalizia sentensi yake kwani kwikwi ya kulia ikamkaba zaidi.

Phillip akautumia udhaifu huo wa Lina na kumbeba juujuu kama mtoto kisha kumwingiza ndani ya gari yeye pia kukimbilia upande wa pili na kuingia kisha kuliwasha na kuondoka eneo hilo kwa kasi ya ajabu, watu wote waliokuwepo eneo hilo wakishangaa kwa kitendo hicho.
***
“Kazi uliyonituma mzee nimemaliza na mzigo ni huu hapa,” ilisikika sauti ndani ya chumba kidogo ndani yake, mwanga hafifu wa taa ulionekana na mzee mfupi akiwa ameketi pembezoni kabisa mwa chumba hicho akaonekana.





MSICHANA NDOTONI MWANGU .......EP.84

“Haraka wapelekeni chumba cha wagonjwa mahututi,” ilikuwa ni sauti ya mwanaume aliyekuwa kwenye korido ambaye kwa kumwangalia tu ilitosha kugundua kwamba ni daktari.

Bila kusema kitu chochote, machela zote mbili zikaanza kusukumwa kupelekwa chumba cha wagonjwa mahututi huku Victor Fedorov naye akifuata kwa nyuma. Akili yake haikuonekana kufanya kazi kwa mateso aliyokuwa akiyashuhudia mbele yake, aliiona dunia haina maana kwake.

“Nisaidie jamani watoto wangu wasife, hawa ndiyo ndugu pekee niliobakiza duniani, bila hawa hata utajiri wote nilionao mimi si kitu, niko tayari kutoa kiasi chochote cha fedha lakini ilimradi watoto wangu waokolewe…” alisema mfululizo.
Hakuwepo mtu hata mmoja aliyeweza kuongea kwa wakati huo, si wauguzi wala madaktari, wote walikuwa na hofu kubwa juu ya maisha ya watoto hao. Hatimaye dakika tatu tu baadaye machela mbili ziliwasili nje ya wodi kubwa, Victor Fedorov akashuhudia maneno ICU juu ya mlango wa wodi hiyo.

”Oh! My God!”(Oh! Mungu wangu!) alisema.
“Shaka ondoa mzee, wanaingia kwenye chumba cha usalama, kila kitu kitakuwa sawa,” alisema muuguzi mmoja huku akimwangalia Fedorov kwa macho ya huruma.
“Watapona kweli?”
“Mh! Watapona.”

“Mbona umeonesha kusita dada?”
“Tuombe Mungu kwani mpaka sasa hatufahamu vyema tatizo linalowasumbua.”
Wakiwa hapo, mlango ukafunguliwa na machela zote mbili zikaingizwa ndani na kumwacha Fedorov peke yake nje akiwa haelewi nini cha kufanya, akawa analia huku akizungusha macho yake huku na kule. Pembeni kabisa ya wodi aliuona msingi, pamoja na kwamba juu yake paliandikwa kuwa si ruhusa kukaa yeye alinyoosha moja kwa moja na kwenda kuketi juu yake.

“Nitakaa hapahapa nikisubiri matokeo, siwezi kwenda mbali, moyo wangu umegubikwa na hofu kupindukia… masikini Mariya na Merina! Nimejitahidi kuokoa maisha yenu wanangu lakini naona Mungu hakupanga jambo hili, hakupanga muendelee kubaki na mimi baba yenu! Bora ningewaacha tu Tanzania pengine yote haya yasingetokea… lakini hapana ninyi ni sehemu ya damu yangu, isingekuwa rahisi kufanya hivyo,” Fedorov alikuwa akijisemea huku picha ya jinsi alivyotoa mbegu zake za kiume na kuziuza kwa familia ya Phillip na Genevieve ikijirudia kichwani mwake. Alikumbuka pia fedha nyingi alizotoa kwa ajili ya malipo kwa Ditrov ya kuwateka watoto hao kutoka mikononi mwa Phillip na kuwaleta nchini Urusi, hakutaka kuamini kuwa sasa walikuwa katika hali mbaya kiasi kile.

Akiwa katika dimbwi hilo la mawazo, ghafla akasikia mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi ukifunguliwa na wauguzi wawili wakatoka mbio wakikimbia. Alipojaribu kuwafuata ili aongee nao na kufahamu hali za watoto wake, walimzuia na kumweleza kwamba walikuwa na haraka sana hivyo aendelee kusubiri eneo hilo mpaka watakaporejea.
“Hatuwezi kukusikiliza, kuna jambo muhimu sana linatakiwa kufanyika sasa hivi.”
“Nataka kujua hali za wanangu… nisaidieni jamani… akili yangu haifanyi kazi vizuri,” alisema mfululizo lakini tayari wauguzi hao walishaondoka na kumwacha hapo.

Haikuchukua hata dakika tano, kwa mbali akawashuhudia tena wauguzi wale wakirejea, lakini safari hii wakisukuma vitu viwili kama mitungi mikubwa. Akili yake ikafanya kazi haraka na kugundua kwamba ilikuwa ni mitungi yenye hewa safi ya Oksijeni.
“Hii si mitungi ya gesi kweli?”alijiuliza huku akikodoa macho kuangalia.
Hakukosea, ilikuwa ni mitungi ya hewa ya oksijeni ikisukumwa kuingizwa ndani ya wodi ya wagonjwa mahututi, Fedorov akalia kwa uchungu.

“Hali imekuwa mbaya mpaka wanawekewa hii?” aliuliza huku machozi yakibubujika mashavuni mwake. Kwa hali aliyoiona alizidi kukata tamaa ya kuwaona tena watoto wake wakiwa hai kwani mara kadhaa wagonjwa wengi waliowekewa hewa hivyo hawakuishi muda mrefu.
“Ni kweli lakini yakupasa uwe mvumilivu, utaelezwa kila kitu kinachoendelea baadaye…” walisema wauguzi wale na kusukuma mitungi hiyo kuingia ndani ya wodi.

Fedorov akalisikia jasho jembamba likitiririka mwilini mwake taratibu huku akiwa hajui nini cha kufanya, akajikongoja na kusogea pembeni huku moyoni mwake akiwaza jambo moja tu, kubaki hapo mpaka mwisho.
“Sitaondoka, nitakaa hapa kusubiri,” alisema.
***
“Puuuh!”
Ulikuwa ni mlio wa kitu kikirushwa juu ya meza.
Mzee mfupi mwenye mwili uliojazia kisawasawa, huku akitabasamu alinyanyuka kwenye kiti na kusogea karibu na meza ambayo juu yake ilikuwa na mzigo.
“Umeifanya vyema kazi hii,” alisema huku akipadisha suruali yake vizuri.
“Bila shaka mzee, hakuna tatizo juu ya hilo?”

“Una uhakika na maelezo yako kijana?” Sauti nzito ya mzee huyo ikasikika tena, safari hii akimzunguka kijana huyo kila upande na kukagua mifuko yote ya suruali yake akimtaka kusalimisha silaha yoyote aliyokuwa nayo juu ya meza.
Bila kusema kitu chochote, kijana yule, huku akionesha kujiamini aliweka silaha zote mezani na alipomaliza aliachia kicheko.
“Kwa nini unacheka?” aliuliza.
“Bosi, inavyoonekana huniamini hata kidogo.”

“Uaminifu wangu umesafiri mbali sana na sidhani kama utarejea leo kwa mchezo mbaya niliofanyiwa huko nyuma, sipo tayari kumwamini mtu yeyote tena maishani mwangu, labda roho yangu tu. Teh!Teh! Teh!” alimaliza mzee huyo kwa kicheko cha kejeli.
“Hata mimi kijana wako?”
“Nilichosema ndiyo hicho,”alisema huku akiendelea kuzungukazunguka ndani ya chumba hicho.

“Sawa nimekuelewa bosi wangu, ni vyema ukanipatia mgao wangu na mimi niondoke kuendelea na masuala mengine.”
“Naweza kuuliza tena?”
“Bila shaka?”
“Hukuua wala kujeruhi?”
“La hasha!”

“Watoto wote wawili wapo salama?” aliuliza mzee huyo akikodoa macho kumwangalia kijana aliyesimama mbele yake.
“Mh!”
“Unaguna nini?”
“Nauliza tena wako salama?”
“Baada ya kupata mzigo huu niliwarusha kutoka ndani ya gari langu mpaka chini, mmoja baada ya mwingine na mimi kuondoka eneo hilo haraka bila kuangalia nyuma... lakini pia…” kigugumizi cha ghafla kikamshika kijana huyo na kushindwa kumalizia sentensi yake.

“Lakini nini? Umewaua?”aliuliza mzee huyo, safari hii kwa ukali.
“Hawajafa ila hali zao ni mba…ya sijui kama wataiona ke…sho?”
“Kwa nini?”
“Niliwa…” alisema kijana huyo huku akitetemeka.

“Unasema?” lilikuwa ni swali kutoka kwa mzee aliyekuwepo ndani ya chumba, bila huruma akaikamata vyema bastola iliyokuwa juu ya meza, akainyoosha na kulielekea paji la uso wa kijana aliyesimama mbele yake.





MSICHANA NDOTONI MWANGU .......EP.85

KWA muda wa saa tatu mfululizo bado aliendelea kusimama nje ya chumba cha wagonjwa mahututi, macho yake yote yakielekezwa kwenye mlango huo ili kuona mtu ambaye angetoka na yeye kuweza kumuuliza nini kiliendelea kwa watoto wake Mariya na Merina.
Victor Fedorov alikuwa ni mwanaume wa shoka lakini sasa alianza kuonyesha udhaifu wake kwani mpaka wakati huo tayari alishakata tamaa, moyo wake ulimuuma kupita kiasi, akasikiliza sauti ndani yake ikimlaumu kwa kitendo chake cha kuwateka watoto hao kutoka Tanzania na kuwaleta nchini Urusi na sasa walikuwa wakifa bila hatia.

Saa nne ilipogonga akaushuhudia mlango wa chumba hicho ukifunguliwa na kushuhudia machela ikisukumwa kutoka ndani ya wodi kwenda nje, juu yake ikionekana kulazwa mtu aliyefunikwa na shuka la kijani kuanzia kichwani mpaka miguuni, hofu kwamba tayari kulikuwa na tatizo ikaugubika moyo wake.
“Mh!” aliguna akikimbia kuisogelea.
“Unakwenda wapi?” sauti ya muuguzi ilisikika ikimuuliza.

“Nataka nione hapo,” aliongea akinyoosha kidole chake cha shahada kuelekea ilipokuwa machela.
“Kaka samahani sana sheria yetu ya kazi hairuhusu kufanya hivyo,” muuguzi huyo alijibu na tayari walishaanza kusukuma tena machela kuondoka eneo hilo, Victor Fedorov naye akifuata nyuma huku akilia.
“Dada tafadhali niruhusu nimwone huyo aliyelala hapo nataka nijue tu pengine ni mwanangu.”
“Mwanao?”
“Ndiyo!”

“Lakini hatuna ruhusa ya kufanya hivyo, kaka yangu, utanifanya nifukuzwe kazi.”
“Nionee huruma.”
“Hapana,” alijibu muuguzi huyo na kwa kasi ya ajabu akaisukuma machela kuondoka eneo hilo kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti, Victor Fedorov akaangua kilio na kushuhudia machela hiyo ikizama ndani.
Akaamini kwamba hakika mmoja wa watoto wake tayari alikuwa ameaga dunia.

***
“Nataka kuondoka na nitakuachia kila kitu ndani ya nyumba hii.”
“Uende wapi mke wangu wewe ndiye wangu wa maisha.”
“Nimeshachoka huwezi kunidhalilisha kiasi hicho halafu ukadai kwamba unanipenda.”
“Chukua maneno yangu na uyafanyie kazi, wewe mwenyewe unafahamu ni jinsi gani ninavyokupenda.”
“Mh! Unaniona mimi mjinga? Hivi unafikiri mimi mtoto, unanichapa halafu unanibembeleza kwa pipi?” aliuliza Lina akizidi kukusanya nguo zake na kuzitupia ndani ya sanduku.

“Haiko haja ya wewe kuondoka, hapa ni kwako acha mimi niondoke.”
Tayari Lina alishanyanyua sanduku akatembea na kuusogelea mlango wa chumba chao na kuufungua ili atoke nje.
“Hapana mpenzi, tafadhali nisemehe hamu ya kuitwa baba ndiyo ilinifikisha hapo.”
“Basi mtafute mwanamke mwingine ambaye atakubali kufanya unayotaka.”

Ukimya wa ajabu ukatokea kati yao Phillip aliyekuwa amepiga magoti chini akakimbia na kulikamata sanduku la Lina huku akimsihi asifanye maamuzi kama hayo, lakini zoezi hilo lilionekana kushindikana na kujikuta akiambulia teke kutoka kwa mwanamke huyo.
Hasira ya Lina ilionekana wazi, si kwamba kweli hakumpenda Phillip bali alimpenda kwa dhati lakini hakuwa tayari kukutana kimwili na mwanaume mwingine ili kupata ujauzito hivyo kitendo cha Phillip kulazimisha jambo hilo ndicho kilisababisha machafuko hayo kutokea ndani ya nyumba yao.

“Umenidhalilisha sana ni wapi nitaficha uso wangu pale nitakapokutana na Daniel? Hivi huoni umenijengea uadui mkubwa sana? Kwa hilo siko tayari kukusamehe Phillip, mimi naondoka tutaonana tena kama si hapa duniani basi akhera,” aliongea Lina kwa sauti ya upole huku akifungua mlango wa sebuleni na kutoka nje.
“Nakupenda mke wangu, ni shetani aliingilia kati penzi letu na kunipa akili isiyofaa.”
“Eti shetani, usimsingizie bure huyo shetani ni wewe mwenyewe.”
“Basi nakubali mke wangu nisamehe, tafadhali rudisha penzi lako kwangu tuanze upya, tukipanga ni namna gani tufanye ili tupate angalau mtoto mmoja.”

“Phillip sahau jambo hilo halipo tena,” aliongea Lina akiingia ndani ya gari tayari kuondoka eneo hilo.
“Hatanii, nikimwacha akaondoka nitamkosa nami sipo tayari,” aliongea Phillip na haraka akili ikamjia kichwani mwake, ili kumzuia Lina ni lazima aende na kulala mbele ya lango la kutokea.
Haraka akatoka mbio na kwenda kujitupa katikati ya lango kuu la nyumba hiyo na kutulia kimya.

Wakati yote hayo yakitokea Lina akiwa ndani ya gari lake akaliwasha na kuanza kurudi nyuma kwa kasi ya ajabu bila kuangalia. Kilichofuatia ni sauti ya mayowe iliyopigwa na mlinzi wa nyumba yao.
“Mungu wangu utauaaa! Utauaaa!” ni sauti hiyo ndiyo iliyomfanya Lina afunge breki za gari kwa nguvu na kushuka kuangalia ni kitu gani kilikuwa kimetokea.
“Phillip unafanya nini? Unataka nikugonge halafu nipate kesi?”

“ Bora iwe hivyo kuliko kuondoka.”
“Sikia wewe ni mtu mzima sasa tafadhali ondoka ili mimi nipite.”
“Sitaondoka hapa mpaka utakaponipa msamaha wako.”
“Unasema?”

“Lina umesikia nini, nasema sina haja ya kurudia.”
“Unacheza na mimi, wewe hufahamu kwamba siku zote ulikuwa ukiishi na mwanamke Mafia? Leo utanifahamu mimi ni nani? Naapa nitaondoka kwa nguvu wala sitanii...sasa kaa hapo ushuhudie ninavyoondoka. Pumbavu mkubwa wewe.”
***
“Kwa nini?”
“Niliwa…” alisema kijana huyo huku akitetemeka.
“Unasema?” lilikuwa ni swali kutoka kwa mzee aliyekuwepo ndani ya chumba, bila huruma akaikamata vyema bastola iliyokuwa juu ya meza, akainyosha na kulielekea paji la uso wa kijana aliyesimama mbele yake. Kwa alivyomfahamu mzee huyo hakika alikuwa hatanii alimaanisha alichokifanya, hofu ikaugubika moyo wake, akiwa haelewi nini cha kufanya akasikia kitu kama mkojo kikipenya kutoka ndani ya suruali yake.

“Nisemehe mzee wangu.”
“Nataka kufahamu ni kitu gani kiliendelea kwa watoto.”
“Hawajafa, nina hakika watakuwa hai japo hali zao sielewi zinaendeleaje?”
“Uliwapa nini?”
“Mh!” kijana aliguna.
“Husemi? Sasa nitakuonyesha mimi ni nani.”

“Hapana! Nipe muda nitakueleza.”
Mzee aliyekuwa ameiweka bastola kwenye paji la kijana aliyesimama mbele yake, taratibu huku akitabasamu akaishusha bastola hiyo chini.
“Fyuuuu!” kijana alishusha pumzi.
“Ninakupa dakika mbili tu kuanzia sasa uwe tayari kueleza kilichowapata watoto vinginevyo leo utani…” aliongea mzee huyo akiiweka vyema bastola yake.

Dakika mbili zikakatika bila kijana huyo kufungua mdomo kusema neno lolote, jambo hilo ndilo lililomtia hasira mzee aliyekuwa amesimama ndani ya chumba hicho kidogo, akasogea karibu kabisa na kuiweka tena bastola juu ya paji la kijana huyo na haikuchukua hata sekunde mbili mlio wa bastola ukasika.
“Paa! Paaa!” kicheko kikafuatia nyuma yake.

Je, nini kitaendelea?
N:B JITAHIDINI KUINGIA BLOG INAINGILIKA HATA KWA SIMU ZA KAWAIDA JAMANI, KWANI KUNA MASTORY YA KUFA MTU NA MIMI MUDA WANGU MDOGO HAUTOSHI NINGEPOST HUKU NA HUKU, NAWAPENDA SAAANA!!
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.86.

MAMBO yanazidi kwenda mrama kwa Phillip ambaye kwa nguvu zake zote amejitahidi kumwomba mkewe Lina msamaha ili amsamehe na kuendelea na maisha lakini inaonekana kushindikana. Lina ameingia ndani ya chumba na kukusanya nguo zake kisha kuziweka ndani ya sanduku, anamwambia Phillip kwamba anaondoka mahali hapo na kumwachia kila kitu.

Jambo hilo linaonekana kuwa gumu kwa mwanaume huyo, akiwa hapo anamshuhudia Lina akitoka kuelekea nje, naye anamfuata kwa nyuma huku akiendelea kumsihi na kumwomba radhi kwa yote yaliyotokea. Anaingia ndani ya gari na kuliwasha kisha kuliendesha kuelekea langoni bila kufahamu kwamba tayari Phillip amefika eneo hilo na kulala usawa wa lango hilo, lengo kubwa likiwa ni kumzuia asiondoke.

Upande wa pili wa hadithi hii, tunamwona mwanaume mmoja ndani ya chumba akiwa na kijana, baada ya maongezi ya muda mrefu mtafaruku unatokea na mzee huyo anataka kufahamu ni kitu gani kiliwapata watoto wawili pacha ambao walitekwa na kijana huyo kwa lengo la kujipatia fedha kutoka kwa baba yao tajiri, Victor Fedorov.
“Ninakupa dakika mbili tu kuanzia sasa uwe tayari kueleza kilichowapata watoto, vinginevyo leo utani…” alisema mzee huyo huku akiiweka vyema bastola yake.

Dakika mbili zikakatika bila kijana huyo kufungua mdomo wake kusema neno lolote. Ni jambo hilo ndilo lililomtia hasira mzee aliyekuwa amesimama ndani ya chumba hicho kidogo, akasogea karibu kabisa na kuiweka tena bastola juu ya paji la uso la kijana huyo, haikupita hata sekunde mbili, mlio wa bastola ukasika ndani ya chumba.
“Paa! Paaa!” kicheko kikafuatia nyuma yake.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…


“Unacheza na mimi wewe, hivi hufahamu kwamba siku zote ulikuwa ukiishi na mwanamke Mafia? Leo utanifahamu mimi ni nani? Naapa nitaondoka kwa nguvu zangu, wala sitanii! Kaa hapohapo ushuhudie ninavyoondoka. Pumbavu mkubwa wewe,” alisema Lina huku akitembea kwa kasi kulielekea gari na kuingia ndani yake.
“Bora unikanyage nife lakini sipo tayari kukuacha uondoke, nakupenda sana Lina, mambo yote haya yaliyotokea ni Shetani tu.

“Eti Shetani? Shetani ni wewe mwenyewe, hebu ondoka mimi nipite.”
Phillip aliendelea kulala chini huku akilia, hakuwa tayari kushuhudia mwanamke aliyempenda akiondoka mbele ya macho yake. Ghafla akiwa hapo, taswira ya Genevieve mkewe ikamjia, watoto wake wawili, Dorice na Dorica nao pia wakapita kichwani mwake kama sinema kali, machozi yakazidi kumbubujika.

“Bora nife niwafuate …” alisema Phillip, safari hii kwa sauti.
“Bosi kuna kitu gani kimetokea? Mbona mnanichanganya?” mlinzi aliuliza.
“Haya mambo hayakuhusu, ni vyema ukaachana nayo na wewe kuendelea na shughuli zako.”
“Lakini mimi ni mmoja wa watu wa familia hii?”

“Ondoka kafanye kazi, husikii?” aliuliza Phillip safari hii kwa ukali.
Taratibu bila kusema kitu, alianza kutembea kuondoka eneo hilo na kusogea pembeni ambako aliendelea kutupa macho yake na kumwona Phillip akiwa bado hajabadilisha uamuzi wake wa kuendelea kulala eneo lilelile.
“Akifanya mchezo huyu mwanamke atamkanyaga kweli, kwa inavyoonekana wana ugomvi mkubwa sana hawa, lakini ni wa nini?

Mbona walitoka wote? Lakini mwanamke amerudi akiwa amejifunika shuka mwilini mwake? Mh! Hakyanani vile, kuna kitu kikubwa hapa kimetokea…” mlinzi aliendelea kuwaza kichwani mwake, yeye pia alishaanza kuhofia kibarua chake, alifahamu wazi kuwa kama kweli Lina aongeondoka, basi ajira yake ingekuwa matatani.
Akalishuhudia gari likija kwa kasi ya ajabu kuelekea eneo hilo, alipoangalia vizuri kuona kama bosi wake Phillip alikuwa ameondoka, alishangaa kumuona akiwa bado amelala eneo lilelile bila kusogea.
***
Machela iliyokuwa ikisukumwa na kuingizwa chumba cha maiti ilimtia hofu sana Victor Fedorov, kichwani mwake hakuwa na picha kamili ya nini kingefuata baada ya hapo, mawazo mengi yakaufunika ubongo wake.
“Sijui itakuwa nini? Lakini ngoja nirudi kule wodini, najua nitapata jibu kamili,” alisema mzee huyo na kuanza kutoka mbio kuondoka eneo hilo.

Kwa dakika tatu nzima, aliendelea kukimbia hatimaye akakifikia chumba cha wagonjwa mahututi, akaweka kambi hapo kusubiri mtu ambaye angetoka eneo hilo na kumweleza ukweli juu ya afya za watoto wake na nini kilitokea.
Kwa takribani dakika tano nzima, aliendelea kuketi eneo hilo, ghafla macho yake yakaushuhudia mlango wa chumba hicho ukifunguliwa na mtu aliyevalia koti jeupe akatokeza nje.
“Ni daktari,”alisema.
Mwanaume huyo akatembea kuelekea eneo alilokuwa ameketi Victor Fedorov na kumsabahi kisha kuanza kumuuliza maswali machache.

“Kama sijakosea nadhani wewe ndiye baba wa watoto wale wawili?’
“Eh! Ndiyo kabisa.”
“Naweza kufahamu umekuja na nani?”
“Mimi?”
“Ndiyo mzee.”
“Mh! Mh! Kwani kuna kitu gani daktari?”

“Ni vyema nikafahamu, umekuja hapa na nani?”
Swali hilo likaingia moja kwa moja masikioni mwa Fedorov na kwenda kugonga sehemu fulani ya ubongo wake. Akiwa hapo akanyanyua macho na kumwangalia daktari ambaye bado aliendelea kusimama pembeni akimwangalia.
“Daktari?” aliita.
“Ndiyo mzee.”

“Nieleze ukweli, nini kimetokea ndani ya chumba hicho kwani muda mfupi uliopita nikiwa hapa nimeshuhudia machela ikipitishwa hapa kuelekea chumba cha kuhifadhia maiti na juu yake kwa nilivyoona kuna mtu…”
“Si kazi yako hiyo mzee, hebu nijibu swali langu.”
Victor Fedorov hakujibu tena kitu, akainamisha kichwa chake chini, hakuwa tayari kusikia kwamba mmoja kati ya watoto wake alikuwa ameaga dunia.
“Tafadhali naomba kufahamu kuna ujumbe muhimu nataka kuutoa kwenu.”

“Ninaye mlinzi wangu kule mapokezi.”
“Tunaweza kuongozana?”
“Hakuna shida,” alijibu Fedorov akitetemeka.
Bila kuongea tena kitu chochote na daktari huyo, taratibu akaanza kutembea akimfuata nyuma. Hofu yake ikazidi kuongezeka kwani kitendo cha kuulizwa kwamba alikuja na nani hospitalini hapo kilizidi kumtia hofu, mambo mengi yakazunguka kichwani mwake bila kujua cha kufanya.

“Nitapokea majibu yoyote nitakayopewa lakini si ya vifo vya watoto wangu.”
Akiwa katika mawazo hayo ni sauti ya daktari ndiyo iliyomshtua, alikuwa akimuuliza yu wapi mtu aliyeambatana naye.
“He! Kumbe tumefika mapokezi?”aliuliza.
“Mzee akili yako iko wapi?” Daktari alimuuliza huku akimpigapiga mgongoni.
“Yule paleee!”alinyoosha kidole chake cha shahada kuelekeza eneo alilokuwa ameketi kijana mmoja, haraka wote wawili wakatembea na kufika eneo hilo.

“Habari yako?”
“Nzuri tu.”
“Nadhani wewe ni mmoja kati ya watu waliokuja na mzee huyu hapa kwetu.”
“Ndiyo, ni bosi wangu huyu.”

“Ni vyema tukaongozana wote mpaka ofisini kwangu, ningependa kuongea na ninyi kuhusu watoto waliofikishwa hapa asubuhi hii.”
“Nini kimetokea? Hali zao zikoje? Wame…” Victor Fedorov aliuliza maswali mfululizo na alipotupa macho yake kumwangalia daktari aliyesimama mbele yake, aligundua kitu fulani katika macho yake.
***
“Piiii!Piiiii!Piiiii!” ilikuwa ni honi ya gari ikipiga kuomba kupishwa eneo hilo lakini mtu aliyeonekana kulala chini bado hakushtuka wala kujitingisha.
“Mungu wangu! Mama yangu weee! Ayaaaa! Tayari ameua...” ilikuwa ni sauti ya mlinzi wa Lina akiwa pembezoni kabisa mwa kibanda kidogo karibu kabisa na lango la kutokea.
“Nakufaaaaa!” Ndiyo sauti pekee iliyosikika.
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.87

UNAUA! Unaua! Mama yangu weee! Dah!”
Ni sauti hiyo ndiyo iliyopenya moja kwa moja masikioni mwa Lina akiwa ndani ya gari lake huku akionekana kuwa mwenye hasira nyingi, hakuwa na habari kabisa kwamba wakati anamweleza Phillip kuhusu kuondoka eneo hilo hakufanya hivyo, aliendelea kubaki palepale.
“Whaat?”(Nini?) alijiuliza baada ya kugeuka na kumwona mlinzi wake akishika mikono kichwani huku akikimbia kuelekea langoni.

Akiwa ndani ya gari huku akiwa haelewi nini cha kufanya, alimshuhudia mlinzi akiruka kutoka kwenye kibanda chake na kuruka kuelekea mbele ya gari lake.
Bila kujiuliza akashuka haraka na kuugana na mlinzi wake, akamshuhudia Phillip akiwa chini ya gari. Alipomwangalia vizuri aligundua alikuwa akilia.
“Niue! Nasema niue siko tayari kukuruhusu uondoke hapa na kuniacha peke yangu.”

Maneno yale yakapenya tena moja kwa moja masikioni mwa Lina, naye akaangua kilio kama mtoto mdogo, akainama na kupiga magoti huku akimbembeleza Phillip atoke chini ya uvungu wa gari ili waongee.
“Unasema kweli?”
“Hakika nakuambia.”
“Huwezi kunidanganya?”
“Mimi? Nakupenda sana Phillip,” aliongea Lina akimshika Phillip mkono kumsaidia kutoka chini ya uvungu wa gari.

Kwa takribani dakika tano nzima Phillip aliendelea kulala chini ya gari hata Lina alipombembeleza bado hakuwa tayari kuamini maneno yake, alichukulia kama yalikuwa ni gia ya kumtoa yeye ili apate nafasi ya kuondoka na kumwacha salama bila majeraha.
Baada ya Lina kuona ameshindwa kumtoa Phillip, aliamua kumtumia mlinzi ambaye alikuwepo eneo hilo akatumia ushawishi wake wote ili kumtoa Phillip lakini naye hakufanikiwa.
“Lina!” Phillip aliita.
“Ukitaka nitoke hapa nipatie funguo za gari.”

“Hicho tu?”
“Ukifanya hivyo naweza kutoka.”
“Basi chukua huu hapa,” Lina alijibu akinyoosha mkono uliokuwa na funguo kumwelekea Phillip ambaye aliunyakua kwa nguvu kama vile mwewe anyakuavyo kifaranga cha kuku akiwa haamini kinachotokea, akachomoza na kuketi kitako pembeni kidogo tu mwa Lina.
“Nisamehe mke wangu.”
“Nimekusamehe toka zamani sana twende ndani,” aliongea Lina akimshika Phillip mkono na kumnyanyua kutoka chini na wote wakaongozana kwenda chumbani kwao.

Walipoingia tu, Lina hakuwa na mazungumzo mengine zaidi akamkamata Phillip kwa nguvu zake zote na kuanza kumvua nguo moja baada ya nyingine huku akimmiminia mabusu motomoto na alipomaliza akazikamata pia nguo zake na kuzitupa pembeni wote wawili wakabaki kama walivyozaliwa na kazi ikawa ni moja tu.
Ndani ya chumba ni sauti pekee ya miguno na mihemo ya mahaba iliyosikika kila mmoja akionyesha ufundi wake kwa mwenzake, mara kadhaa Phillip akiendelea kumwomba mkewe msamaha kwa mambo yote yaliyotokea na kumweleza wazi kwamba alimpenda kwa dhati.

“Je, ulifanikiwa kufanya tendo la ndoa na yule mwanaume?”
“Mh!” Lina aliguna.
“Nieleze mpenzi wangu ili nitoe dukuduku lililoko ndani ya moyo wangu.”
“Kwa nini unauliza hivyo? Na kama je ilitokea nikafanya hivyo utaniacha?”
Lilikuwa ni swali gumu kutoka kwa Lina kwenda kwa Phillip ambaye alikuwa kimya juu ya kitanda mikono yake ikiendelea kuupapasa mwili wa Lina.

Kwa muda wa saa nne mfululizo bado walikuwa juu ya kitanda wakibadilisha staili kutoka moja kwenda nyingine ili mradi kila mmoja wao alikuwa akisikia raha.
“Mpenzi hebu tupumzike kidogo mwili hauna nguvu kabisa.”
“Unasema?” Phillip aliuliza.

“Nimecho…kaaa,” aliongea Lina akitetemeka.
“Bado nataka leo nikuonyesha ufundi wangu wote, nadhani utaamini maneno yangu kwamba ninakupenda.”
“Ashhhhh! Ashhhhh! Hapa…na,” Lina alizidi kulalama kitandani.
Kwa jinsi zoezi lilivyokuwa kwa Lina ilionekana ni pata shika nguo kuchanika, Phillip hakuwa tayari kumwachia Lina kwani alipania kumuonesha ufundi wake wote.

***
Victor Fedorov alisimama ndani ya chumba cha daktari akitetemeka mwili mzima, hakuelewa mpaka wakati huo ni ujumbe gani ambao daktari alikuwa akienda kuutoa kwao, hofu ya kwamba mmoja kati ya watoto wake alikuwa ameaga dunia hakuwa tayari kuupokea.
“Daktari hebu nenda moja kwa moja kwenye ujumbe wako.”
“Tafadhali naomba mketi kwanza.”
“Haipo haja, tueleze tu tukiwa wima.”

“Mh! Unajua ninyi sasa ni watu wazima yawapasa kukubali na kuelewa nini kinaendelea mpaka sasa,” Daktari aliongea na kutulia kidogo kisha kuendelea.
“Kikubwa kilichonifanya niwaite ndani ya chumba hiki ni juu ya hali za watoto wenu ambao mpaka saa wako chumba cha wagonjwa mahututi wakipatiwa matibabu lakini…”
“Fyuuuuu!” Victor Fedorov alishusha pumzi.

“Kutokana na hali zao kuwa mbaya na sisi kama madaktari tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu wote kuokoa maisha yao lakini hali inaonekana kuwa tete hivyo basi, ni vyema nikawashauri kuwahamisha kwenda katika hospitali kubwa zaidi pengine huko mnaweza kufanikiwa.”
“Daktari kwani wanawasumbuliwa na kitu gani?”
“Kwa inavyoonekana kama siyo njaa basi watakuwa wamepewa sumu.”
“Sumu?”

“Inavyoonekana.”
“Mungu wangu walitenda ubaya gani watoto hawa mpaka kustahili adhabu hiyo?” Mlinzi wa Victor Fedorov aliuliza.
“Nadhani sasa si wakati wa kuuliza hayo ni vyema mkafanya utaratibu na kuwahamisha haraka iwezekanavyo,” alimaliza daktari huyo huku macho yake yakimwangalia Victor Fedorov ambaye muda wote alinyamaza kimya akionekana mwenye mawazo mengi kichwani.

***
Central Clinical Hospital ndiyo ilikuwa hospitali iliyokuwa na sifa kila kona ya nchi ya Urusi na ilisifika zaidi kwa watendaji wake wa kazi, kuanzia madaktari, wauguzi na watu wengine wote waliofanya kazi ndani ya hospitali hiyo. Huko ndiko daktari aliyekuwa akiwahudumia watoto wa Victor Fedorov alishauri wapelekwe kwani aliamini kwamba kufika katika hospitali hiyo kungeweza kunusuru maisha ya watoto hao.
“Huko mtapata kila kilicho kizuri, madaktari, wauguzi na hata huduma ili mradi tu uwe na fedha.”

“Ahsante,” alijibu Victor Fedorov akimfuata daktari kwa nyuma mawazo yake yote yakahama kutoka eneo hilo na kwenda moja kwa moja kwa watoto wake, hao ndiyo walikuwa ni kila kitu kwake.
Maandalizi yakafanyika haraka, gari maalumu la wagonjwa likaandaliwa na watoto wakatolewa chumba cha wagonjwa mahututi huku mashine ya hewa ya oksijeni ikiwa imefungwa kwa kila mmoja wao, hakika kwa kuwaangalia iliumiza sana, walilala kimya kitandani bila kujitambua.
Victor Fedorov akashindwa kuvumilia, akamwaga machozi mfululizo.

Je, watoto hao watapona au watakufa? Nini kinaendelea kwa Phillip na Lina?
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.88

“Haraka wapelekeni chumba cha daktari,” muuguzi aliyekuwa ameongozana na watoto wa tajiri Victor Fedorov kutoka katika hospitali ya awali kwenda Central Clinical Hospital alisema baada tu ya machela mbili zilizowabeba watoto wake kuteremshwa kutoka garini.
Kwa jinsi hali ilivyokuwa, watoto hao walihitajika kuingia moja kwa moja kwenye chumba cha daktari bila kusubiri utaratibu mwingine. Haikuchukua hata sekunde tano wakawa tayari wamewasili ndani ya chumba cha daktari.


“Nini tatizo?”
“Wagonjwa sana.”
“Naweza kufahamu nini kinawasumbua?”
Ukimya wa ajabu ukatokea, hakuna mtu aliyeweza kueleza kilichokuwa kikiwasumbua watoto hao wawili.
“Mzazi wao yupo wapi?” daktari aliuliza.
“Mimi hapa,” alijibu Fedorov kwa sauti kubwa.
“Sogea karibu.”


Huku akionesha uso uliojawa na mashaka, Fedorov alisogea karibu kabisa na daktari.
“Ndiyo, hali hii imeanza lini?”
“Ni muda wa wiki sasa daktari lakini leo hali imebadilika zaidi.”
Daktari aliyekuwepo ndani ya chumba kile alianza kumpima mtoto mmoja baada ya mwingine, mara kadhaa alitingisha kichwa chake na zoezi hilo lilipokamilika akawa anaandika maelezo fulani ndani ya mafaili ya wagonjwa. Alipomaliza alimwita muuguzi akimtaka awapeleke watoto hao kwenye wodi ya wagonjwa mahututi, zoezi hilo likafanyika mara moja.


“Daktari, watoto wangu watapona?” Fedorov aliuliza huku macho yake yote yakimwangalia daktari huyo.
“Mh!”
“Tafadhali nijibu.”
“Ah! Unajua? Lakini watapona.”
“Umeonesha hofu sana, nini kinaendelea?” Fedorov aliuliza safari hii kwa sauti ya upole. Akili yake haikufanya kazi vizuri, alihisi kama anakaribia kuwa mwendawazimu.
“Usijali, wapo katika mikono salama, watapona tu hawa,” daktari alijaribu kumpa moyo Fedorov ambaye kwa kumwangalia tu ungeweza kugundua ni kwa kiasi gani yupo kwenye mateso na maumivu makali.

Machela mbili zilisukumwa moja kwa moja mpaka chumba cha wagonjwa mahututi, daktari akawa anafuata kwa nyuma.
“Watoeni juu ya mechela na kuwalaza kwenye vitanda,” ilikuwa ni sauti ya daktari akiwapa maelekezo manesi.
Haraka zoezi hilo likafanyika, watoto wote wawili wakalazwa juu ya vitanda vyao na daktari akaanza kufanya uchunguzi kwa kila mmoja akitafuta tatizo.


Kwa muda wa takribani saa tatu na nusu, bado alikuwa akiendelea kuchunguza afya za watoto hao, vipimo kadhaa vikachukuliwa na kupelekwa maabara.
Nje ya wodi, Fedorov aliendelea kusimama, hamu yake kubwa ikiwa ni kupata taarifa kutoka ndani ya wodi, jasho jembamba lilikuwa likitiririka mwilini mwake.
“Mh! Mungu wasaidie wanangu, naamini hapa ndipo mahali ambapo watarejewa na fahamu zao na maisha yao kuendelea tena hata kama itanigharimu kia…” alisema lakini kabla hajamalizia sentensi yake, macho yake yalishuhudia mlango wa wodi ya wagonjwa mahututi ukifunguliwa, yule daktari aliyewapokea wale watoto akatokeza.


Kwa mbali akanyoosha mkono wake kwa ishara na kumwita Fedorov.
“Niambie daktari, umegundua tatizo gani?”
“Mh, baada ya kufanya uchunguzi wa kina tumegundua tatizo.
“Ahsante, ahsante sana daktari na Mungu akubariki. Je, mmegundua nini tatizo?”
“Uchunguzi tuliofanya umebaini kuwa watoto wako walipigwa na kitu kizito kichwani au walianguka kutoka umbali mrefu kwani kuna baadhi ya mishipa imepasuka na kufanya damu kuvilia kwa ndani. Hilo ndiyo hasa tatizo kubwa linalowasumbua.”


Sentensi hiyo ilipenya moja kwa moja masikioni mwa Fedorov, kumbukumbu ya namna watoto wake walivyorushwa kutoka garini na kudondoka chini kama mizigo ikamjia kichwani mwake kama sinema.
“Mzee! Mzee tafadhali ongea na mimi.”
“Mh! Inawezekana kabisa daktari lakini hilo si la muhimu sana kwangu, ninachotaka ni kuokoa maisha ya wanangu, basi.”
“Hivi ninavyoongea na wewe tayari wanaandaliwa ili kuingizwa chumba cha upasuaji tukajaribu kutoa hiyo damu iliyovilia.”


“Daktari watapona?” lilikuwa ni swali jingine kutoka kwa Fedorov, tayari daktari alishaanza kuondoka eneo hilo kurejea ndani ya chumba cha upasuaji.
“Tuombe Mungu lakini pia tutahitaji utie saini sehemu fulani ya fomu zetu ili kukubaliana na suala la wanao kufanyiwa upasuaji.”
“Nipo tayari daktari,” alijibu Fedorov huku mapigo yake ya moyo yakibadilika kwa kasi.


***
Mapumziko ndani ya chumba yalifanyika kwa dakika tano tu baada ya Lina kulia na kumbembeleza sana Phillip akidai kuwa amechoka. Baada ya dakika tano kuisha kazi ilianza upya. Phillip alitaka kuonesha kwamba alikuwa ni mwanaume wa kuotea mbali, hakika hakutaka kumpa Lina nafasi hata kidogo, jambo lililozidi kummaliza nguvu.
“Mpenzi kwa leo inatosha, tafadhali nisikilize mimi ni wako tutafanya…”
“Mwaaa!Mwaaa!” Phillip alimmwagia Lina mabusu mfululizo.

Shughuli ilikuwa pevu kwani wawili hao walicheza ‘rigwaride’ kwa saa tano, Lina akionekana kuwa taabani. Hata sauti nayo ilishakatika kwa kulalama. “Nakupenda Lina ndiyo maana nafanya yote haya.”
“Mi…mi…pi..a” alijibu Lina.
“Nataka kuona nini mwisho wake.”
“Uta..niu.a…utani..ua.”

“Nataka kukupa raha ambayo nina hakika hukuwahi kuipata, leo ndiyo leo…” Phillip alizidi kujitapa huku akimpa Lina mambo, aliendelea kufanya hivyo mpaka saa saba zilipokatika, akakubali kushuka na kumwacha Lina huru baada ya kuridhika kabisa. Lina alilala kimya kitandani, macho na miguno ndiyo vitu pekee vilivyomfanya Phillip aamini kuwa bado alikuwa hai.
“Ahhhhh!” Phillip alishusha pumzi ndefu, akasogea pembeni mwa Lina na kuketi kitako huku akimwangalia kwa jicho la husuda.


“Nakupenda sana Phillip.”
“Nakupenda pia Lina.”
“Ahsante kwa mapenzi matamu, kweli leo nimekuaminia.”
“Ha!Ha!Haaa!” Phillip alicheka huku akijifuta jasho kwa taulo lililokuwa pembeni.
“Kweli sikutanii, hapa nilipo nipo hoi bin taaban sijiwezi kabisa.”
“Ahsante mke wangu.”


“Phillip,” Lina aliita kwa sauti ya upole.
“Yes baby,” Phillip akajibu.
“Ninalo wazo kichwani mwangu.”
“Unataka kuniacha tena?”
 
 
 
 
 
 

MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.89


NDANI ya chumba cha upasuaji kulikuwa na hekaheka, madaktari wasiopungua watano wakiambatana na wauguzi waliingia na walionekana kuwa na hamu kubwa ya kutaka kuokoa maisha ya watoto wawili pacha waliolala kitandani bila kujitambua pamoja na kwamba walikuwa wagonjwa, uzuri wao ulionekana wazi. Si madaktari wala wauguzi waliokuwa na tumaini juu ya watoto hao, lakini walitaka kujaribu.
“Watoto waandaliwe kwa ajili ya upasuaji.”

“Tayari daktari.”
“Basi hakikisheni kabla ya yote mashine za hewa ya oksijeni zifungwe ili kuwapatia hewa safi haraka sana,” ilikuwa ni sauti ya daktari mmoja aliyekuwa karibu na kitanda cha mtoto mmoja.
“Sawa daktari tunafanya hivyo.”
“Wengine wagawanyike waende kwenye mashine nyingine haraka.”
“Hakuna shida.”

Haikuchukua hata sekunde mbili tayari watoto hao midomoni mwao zilishafungwa mashine hizo ili kuwasaidia kupata hewa safi.
Mambo yote hayo yalifanyika chini ya uangalizi maalum wa madaktari wao ambao ndiyo walioshika usukani wa kuendesha kila kitu ndani ya wodi na baada ya kuhakikisha kwamba maandalizi yalitosha nao pia walijiweka sawa kwa kazi.
Vifaa vyote muhimu vilisogezwa karibu, hakika kwa kuviangalia vifaa hivyo, kwa mtu mwenye akili timamu lazima ungeingia woga.
“Ni vyema tukaanza kazi sasa, ni lazima tufanye kila kinachowezekana kuokoa maisha ya watoto hawa, ni wazuri mno kufa…sawa jamani?”

“Hakuna shida daktari lakini pia bila kumshirikisha Mungu hakuna kitakachokwenda sawa,” aliongea muuguzi mmoja aliyekuwa pembeni, naye pia alionekana kuwaonea huruma watoto hao.
Zoezi likaanza, visu na mikasi ikipita huku na kule ni jambo hilo pekee ndilo lililoonyesha kwamba watu ndani ya chumba hicho walikuwa bize kupindukia. Saa ya kwanza ikapita hatimaye ya tatu bado madaktari wakihangaikia kutoa damu iliyokuwa imevujia ndani ya ubongo wa watoto hao.

***
Nje ya wodi mambo kwa Victor Fedorov yalikuwa magumu, muda wote alikuwa akizungukazunguka huku na kule bila kutulia sehemu moja, alitaka kufahamu ni kitu gani kiliendelea ndani ya chumba, hivyo muda wote macho yake hayakubanduka kwenye mlango wa chumba cha upasuaji.
Kwa saa tano aliendelea kubaki hapo, mwisho akaanza kukata tamaa kwani hakuwepo muuguzi wala daktari aliyetoka wodini.
“Kinaendelea nini humo?” aliuliza na sauti hiyo ikapenya moja kwa moja masikioni mwa mlinzi wake, huyo ndiye aliyekuwa hapo kumfariji.

“Bosi tuwe wavumilivu nahisi kazi ni kubwa.”
“Mh! Hapana moyo wangu unahisi hatari.”
“Kama ipi?”
“Sidhani kama watoto wangu watapona tena, hakika hawataamka.”
“Hapana lakini wewe siyo Mungu, hebu tumwachie yeye kila kitu anaweza,” mlinzi wake alizidi kumtia moyo na kumfariji wakati wote.

“Uwii! Mamaaa! Wananguuuu jamani…” Fedorov aliangua kilio, uvumilivu ulionekana kumshinda kabisa.
Saa saba baadaye bado hawakuona mtu, hofu ikawafunika mioyoni mwao nao pia wakashindwa kuelewa ni kitu kilikuwa kimetokea ndani ya chumba kwani isingekuwa rahisi mpaka wakati huo asitokee mtu yeyote.
“Pengine wamepitia mlango mwingine,” aliongea Fedorov.
“Hapana mlango ni huu mmoja na kama kuna tatizo ni lazima watupe taarifa sisi wahusika.”
“Pengine wanaogopa au hawajui wataanzia wapi.”

“Bosi si rahisi, ni lazima watueleze tena bila kificho.”
“Basi tusubiri tuone,” aliongea Fedorov, tayari alishanyamaza kulia kwani maneno aliyopewa na kushauriwa na mlinzi wake yalionekana kuingia kichwani mwake.
Wakiwa katika hali ya kupigwa butwaa, wakashuhudia mlango wa chumba cha upasuaji ukifunguliwa na machela ikitolewa na nyingine ikifuata kwa nyuma, Victor Fedorov akaamini kwamba hao walikuwa ni watoto wake.

“Hao hapo,” alisema kwa sauti huku akisogea karibu kuhakikisha kama alichokuwa akikiona kilikuwa sawa au ni ndoto za mchana.
Akionekana mwenye mawazo mengi na wasiwasi, akatembea kwa unyonge na kusogea karibu lakini muuguzi aliyesukuma machela hiyo alionyesha wazi kupingana na kitendo cha Fedorov kusogea karibu huku akimweleza wazi kwamba awe mvumilivu na muda si mrefu atapewa ruhusa ya kuwaona watoto wake.
“Wanaendeleaje?” aliuliza tena.

“Majibu yote kaka utayapata kwa madaktari.”
“Wako wapi sasa?”
“Subiri kidogo utawaona,” aliongea muuguzi akizidi kusonga mbele.
Ni kweli alichokuwa ameelezwa na muuguzi, alipogeuza shingo yake kuangalia nyuma alishuhudia jopo kubwa la madaktari na wauguzi wakitoka, alipowaangalia vyema aligundua simanzi lililokuwa mioyoni mwao, naye bila kusita alisimama na kuwasubiri wafike karibu na mahali alipokuwa ili awaulize.

“Daktari, hebu nielezeni juu ya hali za watoto wangu.”
“Mh! Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuondoa damu iliyokuwa imeganda ndani ya kichwa na kazi imekuwa ngumu sana ndiyo maana tumechukua muda wa saa saba, tunatumaini zoezi letu litafanikiwa kwa asilimia kubwa.”
“Watapona?” aliuliza Fedorov.
“Kazi yetu sisi ilikuwa ni kuondoa tatizo ambalo tumefanikiwa, mengine tumwachie Mungu…ah! Sijui unaweza kuja ofisi mara moja?” daktari alisema.

“Bila shaka,” alijibu Fedorov akiungana na madaktari kuelekea ofisini kwa ajili ya kupata maelezo zaidi.
Taratibu wakatembea na kuufikia mlango ambao ndiyo ulikuwa chumba cha daktari, akakaribishwa na kuingia huko na akaonyeshwa kiti ili aketi kwa mazungumzo zaidi.
“Kwanza pole sana mzee wetu.””Ahsanteni poleni na ninyi.”

“Ah! Sisi ni kazi yetu kuhakikisha tunafanya kila kinachowezekana kuokoa maisha ya wagonjwa,” daktari mmoja alijibu akimwangalia Fedorov ambaye aliketi pembeni, macho yake yakionesha wasiwasi mkubwa.
“Hawa mbele yako ni madaktari waliohusika na upasuaji wa watoto wako.”
“Ndiyo.”

“Kazi tumemaliza tunachosubiri sasa ni kuona kama tutakuwa tumefanikiwa.”
“Nahitaji kufahamu kama tu wataamka,” Fedorov aliuliza.
“Kuamka wataamka lakini ni baada ya saa ishirini na nne kuanzia sasa, yakupasa uwe mvulivu,” aliongea daktari mwingine.
“Saa ishirini na nne?” aliuliza kwa sauti.

Je, nini kitaendelea? Watoto wataamka au watakufa? Ni jambo gani Lina anataka kumweleza Phillip?
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.90

“SAA ishirini na nne?” Aliuliza kwa sauti.
Muda wa saa ishirini na nne ulionekana kama miaka mitatu au minne kwa Fedorov, asingeweza kuvumilia kukaa mbali na watoto wake ambao kwake ndiyo walikuwa ndugu pekee duniani.
“Daktari tafadhali naomba kwa ruhusa yako niwaone japo kidogo.”
“Mh! Kwa sheria za kidaktari haturuhusu mtu kufanya hivyo, yakupasa uwe mvumilivu mpaka baada ya saa hizo.”

“Lakini sitaweza, natamani kuwaona watoto wangu,”aliongea tena huku akibubujikwa machozi.
“Dk. Nyoshi mpatie ruhusa awaone japo kidogo tu pengine ataridhika.”
“Lakini daktari wewe mwenyewe unafahamu utaratibu wetu.”
“Najua ila nimemwonea sana huruma mzee huyu.”
“Sawa,”alijibu daktari huyo akinyanyuka kwenye kiti.

Taratibu mlango ukafunguliwa na daktari akaanza kumwongoza Fedorov kuelekea chumba cha wagonjwa mahututi.
“Daktari naweza kukuuliza tena?”
“Uliza tu hakuna shaka.”
“Nataka kujua kama watoto wangu watapona.”
“Kama nilivyokueleza mwanzo, kazi yetu sisi kama madaktari tumeifanya vizuri hiyo sehemu nyingine tumemwachia Mungu atende.”
“Fyuuu!” Fedorov akashusha pumzi kwa nguvu.

Wakaufikia mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi, mapigo ya moyo wa Fedorov yakaenda mbio mithili ya mtu aliyekimbia mita ndefu, walipomaliza kufanya taratibu zote wakaingia ndani.
Baada tu ya kuingia, macho ya Fedorov yakapiga moja kwa moja juu ya vitanda viwili vikiwa vimezungukwa na mashine ya hewa ya oksijeni, machozi yakambubujika.
“Mungu wangu!”Ndiyo sauti pekee iliyosikika.

“Kuna nini?” Daktari akauliza.
“Mariya! Merina,” alitamka majina ya watoto wake akisogea taratibu kuelekea kwenye vitanda hivyo huku macho yake yakishuhudia vichwa vya watoto hao vikiwa vimefungwa bandeji na kuachwa sehemu ndogo sana upande wa macho.
“Daktari mbona kama wamevimba vichwa?”
“Ni kweli kabisa lakini vitarejea katika hali yake ya kawaida kadiri muda unavyozidi kusonga.”
“Mh!” Fedorov akaguna kuonyesha kuumizwa na hali hiyo.

Kwa takribani dakika tano waliendelea kubaki ndani ya chumba hicho, Fedorov akizunguka kitanda kimoja na kurudi kingine na mara kadhaa akitamka;
“Mungu, wasaidie watoto wangu napenda kuona wanapona…sitaki wafe nataka waishi…naomba unisaidie…”aliongea kwa sauti ya chini.

***
“Phillip,” Lina aliita kwa sauti ya upole.
“Yes baby,” Phillip akajibu.
“Ninalo wazo kichwani mwangu.”
Phillip akageuka na kuketi vizuri macho yake yote yakimwangalia mwanamke aliyekuwa amelala kitandani, hofu ikaonekana kuufunika moyo wake akitaka kufahamu ni kitu gani hasa Lina alitaka kumweleza.
“Unataka kuniacha?” Akauliza.

“Haa!Haaa!Haaa!” Lina akacheka.
“Ninakuomba usije ukanieleza kitu cha kuumiza mtima wangu.”
“Phillip hivi unadhani ni rahisi hivyo?”
“Nini?”
“Kukuacha, nikuhakikishe siwezi si kwa sababu ya penzi ulilonipa leo la hasha lakini toka ndani ya moyo wangu ninakupenda na siko tayari kukukosa katika maisha yangu.”

“Mh! Nieleze basi,” aliongea Phillip, tayari macho yake yalishabadilika na kuwa mekundu.
Lina akajivuta kutoka kitandani na kuketi karibu, akamuangalia na kuachia kuachia tabasamu.
“Kwanza naomba nikutoe wasiwasi mume wangu, ukweli ninachokueleza hapa ndiyo ukichukue na kukifanya kuwa ukweli, sikuwahi na wala sikufanya mapenzi na Daniel si kwamba sikuweza ila nakuheshimu sana…”
“Ukweli?”

“Hakika.”
“Tukiwa katika harakati hizo nilikurupuka kutoka juu ya kitanda na kukimbia ndiyo maana nilitoka na shuka tu.”
“Mwaa! Nakupenda Lina.”
“Natumai nitakuwa nimekutoa wasiwasi juu ya hilo.”
“Ni kweli kabisa lakini umeniambia unalo wazo.”
“Mh! Unajua…nitapenda uuangane na mimi katika hilo.”

“Lina niondoe jakamoyo nililonalo.”
“Nataka tukubaliane ili tushirikiane kulifanya pamoja.”
“Nimeshakueleza niko tayari kwa lolote,”aliongea Phillip kwa kujiamini.
“Phillip nimefikiria sana juu ya mtoto, wazo pekee nililonalo nimeona tutafute mtoto wa kuasili.”
“Mh!”

“Kwa sababu ya tatizo ulilonalo ili mimi na wewe tuendelee kuishi na kupendana mpaka mwisho wa uhai wetu ni bora tuasili mtoto mmoja tu.”
“Unamaanisha unachokisema.”
“Hakika nimefikia hapo ili kulinda penzi letu.”
“Lina!” Phillip aliita.
“Na iwe hivyo.”

“Jinsia gani?” Phillip aliuliza.
“Chagua wewe.”
“Hapana.”
“Mimi binafsi napenda mtoto wa kike sijui wewe?”
“Hata mimi,” Lina alijibu na kumpiga Phillip mabusu mfululizo.

Takribani sekunde tano, Phillip alibaki kimya akizungusha akili yake, hakuwa tayari kukubaliana na maneno aliyoyasikia kutoka kwa mkewe Lina.
“Lina nimeamini kwamba kweli unanipenda, ahsante mke wangu ninaungana na wewe asilimia zote na ninakuahidi kulitunza penzi letu hadi mwisho Mungu akiwa mlinzi wetu, sipendi na wala sitaki kukuudhi tena...” alimaliza Phillip akiachia mabusu mfululizo.
Ghafla kama mshale uliofyatuliwa, akamkamata Lina na kumlaza tena kitandani na wote kujifunika shuka gubigubi, kilichofuata baada ya hapo kilikuwa hakielezeki wala hakiandikiki gazetini.

Zoezi hilo lilipokamilika Phillip akamshukuru Lina akimweleza wazi kwamba angeshirikiana naye bega kwa bega kukamilisha mkakati wao wa kupata mtoto wa kumuasili.
“Kesho tutaanza taratibu zote, nataka ndani ya mwezi huu tupate mtoto wetu ambaye tutamlea vyema nasi tuingie katika ulimwengu wa kuitwa baba na mama.”
“Ahsante mke wangu, ahsante kwa kunipenda.”
“Nakupenda pia.”

Je, nini kitaendelea? Watoto Mariya na Merina watapona? Phillip na Lina je, watafanikiwa kupata mtoto wa kuasili? tukutane keshooo!!
USIKU MWEMA NAWAPENDA NYOOOOTEEEE MWAAAAA!!!
 
 
 
 
 
 
 MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.92

“KWANZA naomba nikutoe wasiwasi mume wangu, ninachokueleza hapa ndicho ukichukue na kukifanya kuwa ukweli.
Sikuwahi na wala sitafanya mapenzi na Daniel, si kwamba sikuweza ila ni kwa sababu nakuheshimu sana…”
“Lina nimeamini kwamba kweli unanipenda, ahsante sana mke wangu. Naungana na wewe kwa asilimia zote, nakuahidi kulitunza penzi letu hadi mwisho wa maisha yetu, ninaomba Mungu awe mlinzi wetu, sipendi na wala sitaki kukuudhi tena,” alimaliza Phillip huku akimuachia mabusu mfululizo.

Ghafla, kama mshale uliofyatuliwa, Phillip anamkamata Lina na kumnyanyua juu, anamlaza tena kitandani na wote wanajifunika shuka gubigubi, kinachofuata baada ya hapo hakielezeki.
Wanakubaliana kuwa siku inayofuata wafanye taratibu zote na kuzikamilisha ili wampate mtoto wa kuasili. Walikuwa na hamu kubwa ya kuitwa baba na mama.

Baada ya kufikia muafaka wa kuasili mtoto ambaye wangemlea vyema na kumtunza katika maadili ya Kitanzania.
Wanaendelea kucheza kitandani mpaka usingizi unawapitia.
Upande wa pili, watoto wa tajiri mkubwa nchini Urusi, Victor Fedorov wapo hospitali na bado hali zao ni tete.
Wanakaa kwa zaidi ya saa sabini na mbili bila kuzinduka. Hali hiyo inamtia shaka baba yao, Fedorov na haamini kama wanaweza kutoka ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi wakiwa hai.
Je,nini kitaendelea? SONGA NAYO…

“HA! ” Ilisikika sauti ya mtu akiguna ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi ambako watoto wawili mapacha, Mariya na Merina walikuwa wamelazwa.
“Kuna nini tena?” mwingine aliuliza.
“Ameamka huyu! Ameamka.”
“Mungu wangu! Kweli jamani.”

Jopo lote la madaktari pamoja na wauguzi waliokuwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi walisogea karibu na kitanda.
“Chafya!”
“Mh! Kweli, hakyanani vile pacha mmoja ameamka na kupiga chafya.”
“Kweli Mungu mkubwa,” alisema mmoja wa madaktari.
“Kwa jinsi hali inavyoendelea, hata huyu mwingine ataamka muda si mrefu.”
“Ona! Amefumbua na macho.”

“Kweli,” daktari mwingine alijibu na wote wakatabasamu.
Dalili iliyokuwa imeoneshwa na pacha mmoja ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi, ilimfurahisha kila mtu. Hofu iliyokuwa imeanza kutanda katika mioyo yao ikaondoka na matumaini mapya yakafufuka.
Hakuwepo hata mtu mmoja aliyetaka historia mbaya juu ya upasuaji huo wa watoto iandikwe.


“Hebu tuendelee kusubiri, tukiangalia nini kitaendelea kwa huyu pacha mwingine, naye ataamka muda si mrefu.”
Maongezi yaliendelea ndani ya chumba hicho kila mmoja akisema lake juu ya upasuaji huo. Saa ya kwanza ikapita, matumaini ya pacha mwingine kuzinduka yakawa yanazidi kuongezeka, waliamini kwamba muda si mrefu naye angeamka.

“Daktari ni vyema tukatoa taarifa kwa mzazi wake juu ya nini kinaendelea humu ndani,” alisema muuguzi mmoja.
“Hakuna shida anaweza kupata kibali cha kuingia na kujionea mwenyewe.”
Muuguzi mwingine akatembea na kufungua mlango wa kutokea ndani ya chumba hicho, akatokeza nje na kwa ishara akamwita mzee aliyekuwa ameketi chini pembeni ya mlango wa kutokea ndani ya chumba hicho kwa ishara.
“Samahani kidogo tunakuomba,” sauti ya muuguzi ilipenya katika masikio ya mzee yule ambaye alikua ametawaliwa na uso wa huruma.

“Mh! Nini tena watoto wangu wameamka?” alihoji huku akinyanyuka.
“Tafadhali tunakuomba mara moja.”
Taratibu bila kusema kitu tena mzee yule akatembea na kuufikia mlango kisha kuuliza tena swali kama alilouliza mwanzo.
“Muuguzi nini kimetokea?”
“Hakuna matatizo kuna habari njema kwako.”

“Oh! Habari njema? Watoto wameamka?” Aliuliza.
“Mh! Ni mmoja lakini mwingine bado.”
“Hapana, kwa nini iwe hivyo?”
“Utapata maelezo yote ndani ya chumba hiki, tafadhali ingia ndani na ufuate taratibu zetu,” muuguzi alisema na kuanza kumwongoza Fedorov kwenye chumba maalum.

Mbele kidogo Fedorov akapewa maelezo kisha kuvishwa nguo maalum ambazo ilizivaa na kuingia ndani ya chumba hicho.
Baada ya zoezi hilo kukamilika alianza kumfuata muuguzi ambaye alimwongoza moja kwa moja mpaka kwenye wodi ambayo alishuhudia umati wa wauguzi na madaktari ukiwa pembeni ya vitanda kila mmoja akionesha furaha.
“Pole sana mzee wetu,”
“Mh!” badala ya kujibu Fedorov aliguna tu na taratibu akasogea katika moja ya vitanda ambavyo juu yake ndipo walipolala watoto wake Mariya na Merina.

“Mmoja wa pacha amepata fahamu zake japo bado hajaweza kusema kitu.”
“Yupi?”
“Huyo hapo.”
“Mariya!” Fedorov akamwita kwa sauti na kusogea karibu zaidi akiwa hapo akashuhudia mtoto huyo akifumbua macho kwa tabu kisha kuyafumba, machozi ya furaha yakamtoka akainama na kumbusu kwenye paji lake la uso huku akiongea.


“Nakupenda sana mwanangu nataka wote mtoke turejee nyumbani kuendelea na maisha, sipendi mniache, wewe umeamka lakini Merina bado…ahsante Mungu kwa kujibu sala zangu, sijui ningekuwa mgeni wa nani katika dunia hii, ahsanteni pia madaktari kwa kazi nzuri.”

“Usijali kikubwa tunachoomba ni huyu mwenzake naye aamke,”
“Tii! Tiii!” mlio ndani ya chumba ukasikika na kuwafanya watu wote wageuke kuangalia upande ulipotokea mlio huo.
Ilikuwa ni mashine ya hewa ya oksijeni iliyokuwa imefungwa kwa mtoto Merina ikionekana kusimama.
“Mungu wangu mashine inataka kusimama...”

***
“Ahsante mke wangu, ahsante kwa kunipenda.”
“Ahsante nawe pia.”
Safari ya kuelekea ofisini ikaanza furaha ya Phillip ikionekana wazi na mara kadhaa alikuwa akimgeukia Lina na kumweleza wazi kwamba alimpenda kupita maelezo.
Nusu saa tu baadaye waliingia ofisini na kila mmoja kuingia mzigoni lakini vichwa vyao vilionekana kufikiria juu ya kesho yake, kwani walitaka kumaliza mambo hayo haraka sana.

“Rafiki leo unaonekana una furaha sana, hebu niambie unafurahia kitu gani?” Rafiki mmoja wa Lina aliuliza.
“Maisha, hakuna kitu kingine, pia nimempata mume anayenipenda kwa dhati.”
“Mh! Mshukuru Mungu wako, mimi natamani kupata mume kama wako.”
“Wee huko unakoelekea siko, usije ukaja…” aliongea Lina lakini kabla ya kumalizia sentensi yake rafiki yake akaingilia kati.

“Ahaa! Rafiki siwezi bwana, Phillip ni shemeji yangu na atabaki kuwa hivyo maisha.”
“Unanitia mashaka, unamsifia mno…haa!Haaa,” Lina aliongea na kuachia tabasamu lililoambatana na kicheko.
Aliyekuwa ndani ya ofisi ya Lina alikuwa ni rafiki yake wa siku nyingi waliyesoma naye chuo Kikuu na hatimaye walijikuta pamoja tena katika ofisi moja lakini kila mmoja akiwa kwenye kitengo chake.
Walipendana na kuheshimiana kwa kila kitu na huyo ndiye aliyekuwa msiri wake mkubwa, halikuwepo jambo lililoendelea kati yake na Phillip na rafiki huyo asilifahamu.

“Mimi natoka nilikuja kukusalimu tu kwani ni muda sijakutia machoni.”
“Ahsante,” alijibu Lina kwa kutabasamu.
Saa zikazidi kusogea na hatimaye muda wa kutoka ukawadia, Lina akakusanya kila kilichokuwa chake, kabla ya kutoka ndani ya ofisi akanyanyua simu yake na kubonyeza namba kadhaa, baada ya muda akaonekana akizungumza na mtu upande wa pili.

“Darling muda wa kuondoka umefika, nakuja kukupitia hapo sasa hivi, twende nyumbani tukampumzike,” alisema na kukata simu kisha akaanza kutembea kutoka ndani ya ofisi yake.
Baada ya sekunde tatu tu alishafika nje ya mlango wa ofisi ya mumewe, akaugonga mlango.
“Karibu,” sauti iliskika wakati alipokamata kitasa cha mlango na kufungua mlango, macho yake yakatua kwa Phillip aliyekuwa ameketi ofisini kwake akionesha tabasamu.

“Twende nyumbani tukampumzike kesho tunatakiwa kuwahi mapema sana kituo cha Msimbazi kukamilisha kazi.., sawa?” alisema Lina akionesha kumsisitiza Phillip ambaye hakuwa na hiyana, akakusanya vitu vyake kisha akanyanyuka na kutoka nje kuelekea nyumbani.
Kwao usiku ulionekana kwenda taratibu mno, saa zikisonga pole pole lakini hatimaye asubuhi ikafika na wote wakajiandaa kwa safari, Phillip akiwa ndiye dereva.

Saa moja na nusu walifika katika kituo cha Msimbazi na kuelekea kwenye ofisi ya sista mkuu aliyewapokea na kuwakaribisha ndani ya ofisi ambako walikuta taratibu zote zimeshaandaliwa na mwanasheria aliyekuwa akiwasubiri.
Baada tu ya utambulisho mfupi sista mkuu akawaomba waanze utaratibu ili kwenda na wakati, wakapewa fomu maalum Phillip na mkewe wakaisoma vyema na kuielewa kisha wakatakiwa kuijaza kwa ufasaha.
Kwa takribani dakika kumi nzima walifanya zoezi hilo na walipolikamilisha wakairejesha tena kwa sista mkuu ambaye akawauliza kama wameyakubali masharti yote yaliyoandikwa ndani ya fomu hiyo.

“Tunakubaliana na yote yaliyoandikwa humo na tuko tayari kumtunza na kumlea mtoto tutakayemchukua hapa kwa nguvu na juhudi zetu zote, tunahakikisha atapata maisha anayostahili.”
“Basi ni wakati wa ninyi kula kiapo mbele ya mwanasheria wetu.”
“Sawa sista,” walijibu kwa pamoja na baada ya muda wakala kiapo na zoezi hilo lilipokamilika sista mkuu akauliza walihitaji mtoto wa jinsia gani na umri wake.

“Kuanzia miezi mitatu na awe wa jinsia ya kike.”
Sista hakuongeza tena neno lingine, akawataka wamfuate, akawaongoza mpaka kwenye chumba kimoja kilichokuwa karibu kabisa na ofisi yake.
Akawakaribisha na kuwaingiza ndani ambako kulikuwa na watoto wadogo wakiwa wamelala kwenye vitanda na wafanyakazi wachache wakiwa hapo kuwaangalia.

Hapo walitakiwa kuchagua mtoto mmoja tu ambaye ndiye wangemchukua na kwenda kumtunza mpaka mwisho wa uhai wake, wakafumbua macho yao yote kuwaangalia watoto hao ambao kwa kweli walikuwa wazuri mno.
“Mnachagua mmoja tu,” sista mkuu aliongea akitabasamu.
“Mh! Watoto wote wazuri sijui tuchukue yupi kati yao,” Lina alimuuliza Phillip.

“Huyu hapa anafanana na sisi,” alisema Lina.
“Sawa…sista huyu ndiye tuliyemchagua,”
aliongeza Phillip akimnyanyua mtoto mzuri aliyekuwa amelala kitandani, alikuwa ni mdogo lakini uzuri wake ulionekana wazi
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.93

MAMBO hayakuwa kama walivyotarajia kwamba baada ya saa kadhaa mtoto huyo angeamka na kuungana na mwenzake, saa ya kwanza ikapita na sasa ilikuwa ikielekea ya pili, Victor Fedorov uvumilivu ukaanza kumshinda akajikuta akimwaga machozi kama mtoto mdogo, kazi ya wauguzi ndani ya chumba ikawa ni kumtuliza wakimtaka awe mvumilivu.
“Lakini ni muda mrefu sana mbona mwenzake amesharejewa na fahamu?” aliuliza akisogea karibu kabisa na kitanda cha pacha ambaye hakuonyesha dalili yoyote ya kuamka.
“Ataamka, kuwa mvumilivu.”

“Mbona kama ni upasuaji umefanyika kwa saa sawa iweje yule aamke na huyu bado?” bado aliendelea kuuliza maswali mfululizo.
“Tafadhali tunaomba sasa mzee utupishe tuendelee na matibabu yetu tutakuwa tukikujulisha kila kitu kadiri muda unavyokwenda tunaomba uende nje,” aliongea daktari mmoja, muuguzi aliyekuwa karibu na Fedorov akamshika mkono na kumwongoza kutoka nje naye pia akijaribu kuongea maneno ya kumpa faraja.

Mzee huyo akatoka akilia, mawazo na akili zake zote zilikuwa juu ya mtoto wake huyo ambaye hakuonyesha matumaini, akatembea hatua ya kwanza na ya pili kisha akageuka nyuma kuangalia mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi.
“Sitakwenda popote nitakaa hapahapa mpaka mwisho nataka kujua nini kinaendelea,” aliongea Fedorov akiketi chini, akiwa hapo haikupita hata sekunde tatu mlinzi wake naye akaungana naye, pia akijaribu kumfariji mzee huyo lakini zoezi hilo lilionekana kuwa gumu.

“Naumia, moyo wangu una wasiwasi mkubwa sana juu ya mtoto wangu…sijui kama ataamka…lakini kama kuna kitu kibaya kwa nini wanifiche? Nataka wanieleze ukweli ili nijiandae kwa tatizo linalokuja,” aliongea akibubujikwa machozi.
“Hapana bosi hawezi kufa, Mungu mkubwa anatenda.”
“Najua hilo lakini kwa sasa nimekata…….”
“Hutakiwi kukata tamaa unachotakiwa kufanya hivi sasa ni kuamini kwamba naye pia ataamka, mimi ninaamini kwamba yuko katika mikono ya madaktari bingwa atapona tu.”
“Mh! Labda hebu tuone,”aliongea Fedorov akijifuta machozi.

***
“Mnachagua mmoja tu,” sista mkuu aliongea akitabasamu.
“Mh! Watoto wote wazuri sijui tuchukue yupi kati yao,” Lina alimuuliza Phillip.
“Huyu hapa anafanana na sisi.”
“Sawa…sista huyu ndiye tuliyemchagua.”

Mabusu mfululizo yakatua kwenye paji la mtoto waliyemchukua, alikuwa ni mtoto wa jinsi ya kike, pamoja na kuwa mtoto mdogo uzuri wake ulionekana wazi, rangi ya ngozi yake ilifanana kabisa na ya Phillip, furaha ya ajabu ikatawala, hakuwepo hata mtu mmoja kati yao aliyeamini kwamba sasa wangekuwa wakiitwa baba na mama wa mtoto waliyemuasili kutoka katika Kituo cha Msimbazi.
“Tutamlea na kumtunza mpaka mwisho wa uhai wetu tukimpatia kila aina ya mahitaji,” Phillip aliongea akimwangalia sista mkuu.
“Ombi letu kwenu ninyi ni hili hapa,” sista aliongea.
“Ndiyo sista tunakusiliza.”

“Tutakuwa tukihitaji kumtembelea mtoto huyu kila baada ya mwezi mmoja kujua na kufahamu anaendeleaje, hiyo ni moja ya sheria zetu mpaka atakapofikisha umri wa miaka kumi na nane ambapo tutakuwa huru kumwacha aendelee na maisha yake kwani atakuwa ni mtu mzima.”
“Hilo halina shaka sista na kama inawezekana tunaweza tu kuongozana mpaka nyumbani.”
“Nitawapa mtu ambaye mtaongozana naye mpaka huko kwa ajili ya kupafahamu na kama kutatokea mabadiliko yoyote yawe ya kuhama nyumba au kwenda nje ya nchi ni vyema mkatujulisha mapema, sawa?” sista mkuu aliuliza.

“Tumesikia,” Phillip na Lina walijibu kwa pamoja na kuanza kutoka nje ya chumba kuelekea ofisini kwa sista mkuu ambako wangekamilisha taratibu zote kisha kuondoka na mtoto waliyekuwa naye.
Taratibu maalum zikafanyika ikiwa ni pamoja na kupigwa picha na kutia saini kwenye makubaliano yote yaliyofanyika ofisini kisha wakakabidhiwa mtoto na sista mmoja ambaye wangeongozana naye mpaka mahali wanapoishi. Wakatoka na kumshukuru sista kisha kutembea kuelekea sehemu waliyokuwa wameegesha gari, Phillip ndiye alikuwa dereva na Lina aliketi kiti cha nyuma akiwa amempakata mtoto.

Gari liliendeshwa na kwa muda wa saa moja tu walifika nyumbani kwa Phillip na Lina wakamkaribisha sista waliyeongozana naye wakimweleza wazi kwamba hapo ndipo palikuwa nyumbani kwao ambako mtoto waliyekuwa wamemwasili angeishi maisha yake yote akitunzwa na kulelewa vyema.
“Karibu sana sista hapa ndipo nyumbani kwetu ambako mtoto huyu atalelewa na kuishi, akitunzwa kwa hali na mali.”
“Mh! Ahsanteni sana nafurahi kupafahamu tutakuwa tukija kila mwezi kumtembelea ili kujua maendeleo yake.”
“Karibuni sana.”

Dakika kumi na tano baadaye sista aliyeongozana na Phillip na Lina aliaga na kuondoka akiahidi kurejea tena baada ya mwezi mmoja kujua hali ya mtoto huyo. Wakamsindikiza kisha akaondoka.
Kwa siku nzima walishinda ndani ya nyumba wakipanga mipango yote na jinsi ya kumlea na kumtunza mtoto huyo. Lina akatoa wazo kwamba ni vyema wangemtafuta mfanyakazi wa ndani ambaye angekuwa tayari kumlea mtoto huyo na wao wangemlipa mshahara ambao angeutaka.

“Ni lazima atafutwe mtu wa kumlea mtoto huyu kwa upendo wote,” Lina aliongea.
“Kabisa, lakini nashauri awe mtu mzima kidogo.”
“Jinsi ya kumpata sasa ndiyo tatizo, sijui tuanzie wapi?”
“Hebu subiri kidogo,” Phillip aliongea akinyanyuka kitini kuelekea chumbani.
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.94

PHILLIP alitembea moja kwa moja na kuelekea mlango wa chumba chao akaingia na haikumchukua hata sekunde tatu tayari akawa amerejea akamsogelea Lina aliyekuwa ameketi bado sebuleni akimsubiri.
“Soma hapa,” shika hiki kipande cha gazeti halafu nitakuonyesha kitu.
Lina bila kusema kitu akionyesha kushangazwa na mumewe akanyoosha mkono wake na kupokea kipande hicho kisha kutulia akisikiliza maelekezo.

“Ndani ya kipande hicho kuna tangazo la kampuni inayowatafutia watu wafanyakazi wa majumbani.”
“Mh! Wewe ulikitoa wapi na ulijuaje kama tunaweza kutafuta mfanyakazi siku moja?” Lina aliuliza akiachia tabasamu.
“Si unajua tena sisi watu wenye upako huwa tunaona vitu mapema sana kabla…,” aliongea Phillip akimwangalia Lina na kuachia tabasamu.
Lina akakodoa macho yake na kuanza kusoma kipande hicho cha gazeti, ghafla akakutana na tangazo hilo akalisoma kwa umakini wa hali ya juu mpaka mwisho na kukutana na namba za simu kwa ajili ya mawasiliano kama tu mtu angehitaji mfanyakazi.

“Mh! Hili liko safi tena wako wa aina mbili kike na kiume sijui yupi mume wangu?” Aliuliza Lina.
“Wewe acha utani wako mwanaume wa nini hapa ndani ataweza kulea kweli?”
“Anaweza kwani si sheria na masharti tu.”
“Hapana tutafute wa kike,” aliongea Phillip akijilaza kwenye sofa.

Lina akanyoosha mkono wake na kuchukua simu yake ya mkononi kisha kuanza kubonyeza namba kadhaa na kuweka simu sikioni, haikumchukua hata sekunde mbili tayari upande wa pili ukasikika.
“Ndiyo naitwa Lina napiga simu kutoka hapa hapa Dar es Salaam, nimesoma tangazo lenu na nahitaji kupata mfanyakazi wa ndani ambaye umri wake ni mkubwa kidogo atakayeweza kulea vyema mtoto mdogo,” alimaliza Lina.
“Hakuna shida dada yupo anapatikana sijui unamhitaji kwa lini?”

“Hata leo ikiwezekana.”
“Basi ni vyema ukatueleza wewe unapatikana wapi nasi tutakuja moja kwa moja nyumbani kwako na watu wawili kisha wewe utamchagua mmoja,”
“Sawa.”
Zoezi hili likawa limekamilika Lina akatoa maelekezo ya jinsi ya kufika nyumbani kwao na watu hao wakakubaliana naye na kumweleza wazi kwamba baada tu ya nusu saa wangefika nyumbani hapo.

“Unajua nini mke wangu?”
“Mh!”
“Ubongo wangu unazunguka kuhusu majibu ambayo tutawapa watu wakitaka kufahamu juu ya huyu mtoto wetu tuliyemwasili?”
“Mume wangu siku zote huwa watu hawakosi cha kusema wataongea na kujiuliza maswali mengi sana juu ya mtoto wetu lakini mwisho watanyamaza, hili litabaki kuwa jambo la familia na si vinginevyo.”

“Mwaa! Mwaa! Mwanamke una akili sana wewe,” Phillip aliachia mabusu mfululizo kwenda kwa Lina ambaye naye aliyapokea kwa bashasha huku akinyanyuka na kutembea kwa madaha kuelekea sebuleni kumwangalia mtoto mchanga aliyekuwa amelala.
“Bado amelala huyu,” sauti ya Lina ilisikika kutoka chumbani.
“Basi njoo tuendelee kuongea hapa tukisubiri wageni.”
“Sawa nakuja lakini mume wangu jambo moja hatujalifanya bado.”

“Lipi hilo?” Phillip aliuliza kwa kutahamaki.
“Hatujampa jina mtoto wetu.”
“Hebu anza wewe kutoa la kwako,” Phillip alimwambia Lina.
“Wewe kama baba wa familia unatakiwa useme na mimi nitafuata.”

“Kutoka ndani ya moyo wangu mimi napenda sana mtoto huyu aitwe Genevieve.”
“Saaaafi!” Lina aliongea kwa sauti.
Hiyo pekee ilitosha kabisa kuonyesha kwamba jina hilo lilikuwa limepita moja kwa moja bila kipingamizi kwa pamoja wakanyanyuka na kukimbilia chumbani alikolazwa mtoto.

***
“Nashauri huyu mtoto afanyiwe CT-Scan kuangalia tena upya mfumo mzima wa kichwa chake huenda kuna tatizo ambalo halikuonekana wakati wa upasuaji wa mwanzo,” aliongea daktari mmoja ndani ya chumba baada ya kuona kwamba hali ilikuwa si nzuri kwani saa nyingi zilishapita na tumaini la kurejewa na fahamu kwa mtoto mwingine halikuwepo.
“Huo ni uamuzi mzuri.”
Haraka akapandishwa katika machela na kuanza kusukumwa kuelekea kwenye chumba ambacho kipimo hicho kingefanyika na kutoa picha kamili ya tatizo ambalo lingeonekana.

Mchakato mzima ukafanyika haraka picha ikachukuliwa na majibu hayakuchukua muda mrefu sana yakarejeshwa tena kwa madaktari ambao waliisoma vyema ripoti hiyo.
“Mungu wangu!”
“Nini tena?”
“Mh! Haya majibu nakosea au nasoma sawa?”
“Ni sawa kabisa daktari hivyo ndivyo yalivyo.”

“Kwa hiyo?”
“Hatuna jinsi ni lazima tufanye tena upasuaji ili kumsaidia huyu mtoto vinginevyo atakufa.”
“Kwani kilitokea nini mpaka kuacha bonge hili la damu?”
“Huu si wakati wa kulaumiana ni wakati wa kuokoa maisha ya mtoto huyu jamani mimi nashauri maandalizi yafanyike haraka sana na kazi ianze mara moja.”
“Mzazi wake je?”

“Ni lazima apewe taarifa na akubali jambo hili vinginevyo atampoteza mtoto wake.”
“Sawa aitwe na kuelezwa kila kitu.”
Muuguzi mmoja akatoka mbio na kumwita Fedorov akimtaka aingie ndani ya chumba ili kuongea na madaktari dakika moja tu baadaye watu wawili wakaingia ndani alikuwa ni muuguzi na Fedorov bila kupoteza muda daktari mmoja akamweleza wazi kwamba ililazimu mtoto wake arejeshwe tena chumba cha upasuaji haraka ili kuokoa maisha yake kwani picha iliyochukuliwa ilionyesha wazi kwamba kulikuwepo tatizo na kama tu wangezidi kumchelewesha basi asingeamka milele.

“Mungu wa…ngu…sa…fari hii..hatapo…” Fedorov aliongea kwa sauti ya kukatikatika huku machozi yakumbubujika, macho yake yakashuhudia machela ikisukumwa haraka kutoka nje ya wodi hiyo kuelekea chumba cha upasuaji.
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.95



MTOTO aliyeingia katika maisha ya Phillip na Lina na kupewa jina la Genevieve alikuwa ameleta furaha kubwa sana katika ndoa hiyo, kwani walimpenda kupita kawaida wakihakikisha wanampatia kila kilichohitajika katika maisha yake.
“Genevieve, hatimaye jina hili limerudi tena katika maisha yangu,” alitamka Phillip kwa sauti ya juu.
“Naam, hilo ndilo litakuwa jina lake.”

“Ahsante Lina hii itakuwa kumbukumbu kwa mpenzi mke wangu ambaye aliondoka duniani nikiwa bado nampenda, mtoto huyu ameziba kabisa pengo lake.”
“Ninafurahi pamoja na wewe mume wangu, siku zote haja ya moyo wangu ni kukuona unayo furaha kama hii,” Lina aliongea akitabasamu.
“Nitampenda mtoto huyu mpaka kufa.”
“Naungana na wewe lakini ninalo swali moja kwako Phillip.”

“Endelea.”
“Nataka kujua kama utanipenda kwa dhati kama ilivyokuwa mwanzo.”
“Lina! Hakika nakuhakishia kutoka moyoni mwangu kwamba ninakupenda mno.”
“Ahsante kwa penzi lako Phillip, hebu twende chumbani mara moja,” aliongea Lina huku akimwangalia mumewe na kuachia tabasamu. Ni Lina aliyekuwa wa kwanza kusimama na kumsogelea mumewe kisha kumshika mkono na kumnyanyua kutoka kitini wote wakaanza kutembea kuelekea chumbani.

Kilichoendelea ndani ya chumba hakika kilikuwa hakielezeki wala kuandikika gazetini, kwani miguno na mihemo ya kila aina iliendelea kwa muda wa saa nne mfululizo, kilichowashtua hapo ilikuwa ni sauti ya honi ya gari nje ya lango lao, kwa sababu walifahamu kwamba mlinzi alikuwepo kwa kazi hiyo wao waliendelea na shughuli zao.
“Lina sasa inatosha bwana.”

“Hapana, mimi bado sijachoka.”
“Wewe mtoto ataa…” aliongea Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake wakasikia sauti ya mlango ukigongwa.
“Bosi! Bosi kuna wageni hapa,” sauti ya mlinzi ilisikika.
“Nenda wewe mimi mpaka nikaoge.”

“Sawa hakuna shida mke wangu,” Phillip aliongea huku akisogelea bukta yake iliyokuwa pembeni kisha akaiweka mwilini na taratibu akafungua mlango na kutembea kuelekea sebuleni ambako alifungua mlango na kukutana na sura ngeni za watu watatu na mtu wa nne akiwa mlinzi.
“Karibuni,” aliongea.
“Ahsante sana, nadhani hatujakosea, hapa ndiyo nyumbani kwa Phillip.”
“Ni kweli kabisa karibuni sana.”

“Oke, sisi ni wale watu mliotupigia simu muda mchache uliopita mkihitaji mfanyakazi tuko hapa.”
Wakaingia ndani na mlinzi kurejea sehemu yake ya kazi, haikuchukua hata sekunde tatu Lina naye akaungana nao sebuleni, mazumgumzo maalum yakaanza na hatimaye wakatakiwa kuchagua mtu mmoja kati ya wawili waliokuwepo hapo.
“Sisi tunamchagua huyu hapa,” waliongea karibu kwa pamoja.

“Hakuna shida hata sisi tulipendekeza huyuhuyu.”
“Karibu sana mama sijui unaitwa nani?”
“Naitwa Magdalena Simon, mwenyeji wa Rukwa na nimezaliwa miaka arobaini na saba iliyopita.”
“Mh !” Phillip na Lina wakaguna, mwanamke huyo alikuwa ni mtu mzima si kwa mtoto mdogo tu bali hata kwao.
“Mama utaweza kazi ya kulea mtoto kweli? Na je wewe katika maisha yako ulibahatika kupata mtoto?” Lina aliuliza akikodoa macho kumwangalia mwanamke huyo.

“Mh! Mh! Hapana !” mwanamke huyo alijibu na walipomwangalia vyema usoni mwake waligundua alikuwa akibubujikwa machozi.
“Basi mama sisi tunakupokea kwa mikono miwili ukae nasi na ulee mtoto wetu umpe mapenzi yote.”
“Ahsante.”

Makubaliano yakafanyika wakatakiwa kulipa kiasi cha fedha ambacho ndicho mwanamke huyo alitolewa kwao na wakamshukuru mtu aliyemleta mfanyakazi huyo huku akiwaeleza wazi kwamba angekuwa karibu nao kwa kila kitu kuhakikisha hapatokei tatizo lolote. Wakaaga na kuondoka.

Wakampokea bibi Magdalena na kumwonyesha mambo yote yaliyomstahili ndani ya nyumba hiyo ikiwa ni pamoja na chumba ambacho angekitumia muda wote ambao angeishi hapo. Baada ya zoezi hilo wakamtaka aingie jikoni kuandaa chakula cha jioni hiyo ikiwa ni kama jaribio la kwanza kisha wao wakarejea chumbani.
***
Upasuaji wa pili ulikuwa umefanyika kwa ufanisi wa hali ya juu na madaktari wakihakikisha halijirudii tena tatizo kama lililotokea mwanzo wakiomba Mungu mtoto huyo mzuri anyanyuke na kuendelea na maisha.
“Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa, sasa atolewe humu na kurudishwa chumba cha wagonjwa mahututi.”

“Sawa daktari,” wauguzi waliitikia, na bila kuchelewa machela ikaanza kusukumwa kutoka nje ya chumba ambako walimkuta Fedorov akiwa amesimama.
“Oh! My God !” aliongea mzee huyo kwa sauti ya juu baada ya kuona bandeji iliyotapakaa damu ikiwa imefungwa kuzunguka kichwa cha mtoto wake.
Machela ikapitishwa na wauguzi ambao hawakuongea kitu chochote zaidi ya neno moja tu.

“Pole sana mzee.”
“Ataamka baada ya saa ngapi?”
“Saa kumi na mbili kuanzia sasa.”
“Mh!” Fedorov aliguna hakika kwa kumwangalia tu mzee huyo ungegundua tu kwamba tayari alishachoka moyoni na tumaini lote lilishapotea katika maisha yake, mpaka kufikia hapo kwa umri aliokuwa nao hakuwahi kukutana na changamoto kubwa kama hiyo.

Machela ikasukumwa na kuingizwa chumba cha wagonjwa mahututi pembeni tu ya pacha mwenzake ambaye kwa wakati huo tayari alishaanza kufungua macho na kuuliza maswali kadhaa japo kwa taabu akitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.
Victor Fedorov akatakiwa kusubiri nje ya chumba hicho kwa muda mwingine wa saa kumi na mbili.je nini kitaendelea? tukutane kesho kama kawa mwaaaaaaast gudnite all
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.96

UPASUAJI wa pili ulikuwa umefanyika kwa ufanisi wa hali ya juu na madaktari wakihakikisha halijirudi tena tatizo kama lililotokea mwanzo, wakiomba Mungu mtoto huyo mzuri anyanyuke na kuendelea na maisha.
“Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sasa atolewe humu na kurudishwa chumba cha wagonjwa mahututi.”
“Sawa daktari,” wauguzi waliongea na bila kuchelewa machela ikaanza kusukumwa kutoka nje ya chumba ambako walimkuta Fedorov akiwa amesimama.

“Oh! My God,” aliongea mzee huyo kwa sauti ya juu baada ya kuona bandeji iliyotapakaa damu ikiwa imefungwa kuzungukwa kichwa cha mtoto wake.
Machela ikapitishwa na wauguzi ambao hawakuongea kitu chochote zaidi ya neno moja tu.
“Pole sana mzee.”
“Ataamka baada ya saa ngapi?”

“Saa kumi na mbili kuanza sasa.”
“Mh!” Fedorov aliguna hakika kwa kumwangalia tu mzee huyo ungegundua kwamba tayari alishachoka moyo na tumaini lote lilishapotea katika maisha yake mpaka kufikia hapo kwa umri aliokuwa nao hakuwahi kukutana na changamoto kubwa kama hiyo.

Machela ikasukumwa na kuingizwa chumba cha wagonjwa mahututi pembeni tu ya pacha mwenzake ambaye yeye kwa wakati huo tayari alishaanza kufungua macho na kuuliza maswali kadhaa japo kwa taabu akitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.
Victor Fedorov akatakiwa kusubiri nje ya chumba hicho kwa muda mwingine wa saa kumi na mbili.
Je, nini kinaendelea hapa? Mtoto atapona na kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya tatizo kuondolewa? SONGA NAYO…

“Paa! Paa! Paaa!” Ulikuwa ni mlio wa bastola ndani ya chumba kidogo chenye mwanga hafifu na mzee mfupi aliyejazia misuli akiwa amesimama mbele ya kijana mmoja akionekana mwenye hasira kali.
“Usiniu…naomba uni…”
“Unasema?”
“Tafadhali mzee wangu kama ni huo mgawo wangu basi mimi nakuachia zote lakini wewe pia ufikirie maisha yangu.”

“Ha! Haaaa!” Sauti ya kicheko kikali ikasikika tena mzee aliyesimama mbele ya kijana huyo huku akiwa amenyoosha bastola akashuka mkono wake na kuanza kutembea kumfuata mahali alipokuwa.
“Simama,” alitamka kwa sauti ya ukali.
“Mh!”
“Ina manaa hujaelewa, nasema simama upesi.”

Kijana yule bila kusema tena kitu akaanza kujivuta kutoka sakafuni na aliposimama tu wima vitu kama maji maji vilionekana kuchuruzika kutoka ndani ya suruali yake kwenda chini.
“Hee! Umejikojolea?”
“Nisamehe mzee wangu si kusudio langu ni bahati mbaya.”
“Unaumwa?”
“Hapana ni woga tu.”

“Lakini wewe ni mtoto wa kiume unatakiwa kuwa shupavu.”
“Mh!” Kijana huyo alibaki akiguna tu huku akiwa amekodoa macho yote kumwangalia mzee huyo.
Kwa ishara akaongozwa ili kusogelea meza ambayo juu yake ilikuwa na begi.
“Fungua,” mzee huyo aliamuru.

Taratibu kijana akalisogelea begi na kuanza kulifungua huku akionyesha hofu nyingi machoni mwake. Kwa sekunde tatu tu tayari alishamaliza kulifungua na idadi kubwa ya noti ikaonekana ndani yake.
“Tayari mzee,” aliongea kwa sauti ya upole.
“Sawa kabisa, sasa nisikilize vyema tena kwa umakini mkubwa,”
“Ndiyo mzee.”

“Kwa kuwa umeonyesha kufanya kazi vyema na mimi tena kwa ujasiri wa hali ya juu nikiamini kabisa kwamba hakukuwa na madhara yoyote yaliyotokea juu ya watoto, basi nakupa mgawo huu, uende ukaanze maisha na kumbuka mtu aliyesimama mbele yako si mtu mzuri hata kidogo, upande wake wa pili unatisha sitasita kutoa uhai wako pale utakapokuwa umenisaliti au kufanya jambo tofauti na kiapo chetu, mambo yote yaliyotokea ndani ya chumba hiki ilikuwa ni kukupima imani, nilitaka kujua jinsi unavyoweza kuhimili vishindo.”
“Ndiyo mzee.”

“Una hakika watoto wako salama? Nisingependa kusikia watoto wamekufa kwani hawana hatia hata kidogo, mwenye hatia ni baba yao ambaye nitashughulika naye mwenyewe.”
“Mh! Mzee sina uhakika ila watakuwa wazima.”
“Haya kamata hii halafu utokomee nisikuone mbele ya macho yangu,”aliongea mzee huyo akimkabidhi kijana maburungutu ya noti yasiyopungua kumi. Akazungusha macho yake huku na kule ndani ya chumba hicho na kufanikiwa kuona mfuko mmoja mchafumchafu, huo ndiyo aliutumia kuweka fedha zake zote alizokabidhiwa muda mfupi uliopita akamshukuru mzee huyo na kuanza kutembea kuelekea nje.

“Kumbuka hutakiwi kusema kitu chochote juu ya maisha yangu, sawa?”
“Sawa mzee hakuna shida.”
“Tumia fedha hizo kuendeleza maisha yako, hivi sasa wewe ni mtu mzima.”
“Ahsante mzee wangu nami pia nakutakia maisha mema, utakapokuwa na shida usisite kunitafuta...,” aliongea kijana huyo akitokomea.

Hivyo ndivyo Ditrov alivyoagana na kijana huyo kisha kwa kujiamini kabisa akatembea kulisogelea begi lililokuwa juu ya meza akalinyanyua na kumwaga fedha zote juu ya meza.
“Yap! Federov alikuwa hajui anacheza na mtu wa aina gani, hajui kwamba sisi tulishatangulia zamani, sasa asubiri kisasi changu ni lazima nitamtenda ubaya…,” aliongea Ditrov kwa kujiamini.

***
Upasuaji ndani ya chumba ulifanyika kwa umakini mkubwa na hatimaye wakafanikiwa kulitoa bonge la damu lililokuwa limengandamiza ubongo wa mtoto Merina, wakarudisha kila kitu katika sehemu yake na wakamtoa kumpeleka chumba cha wagonjwa mahututi huku akiwa amefungiwa mashine ya hewa ya oksijeni ili kumsaidia kuvuta hewa safi.
Muda wote huo Fedorov bado alikuwa nje ya mlango wa chumba hicho akizunguka huku na kule.

“Ametoka!” alitamka baada tu ya kuona machela ikisukumwa kutoka ndani ya chumba cha upasuaji kutolewa nje.
“Mzee tumefanikiwa kuondoa damu iliyoonekana na tunaamini sasa mtoto ataendelea vizuri lakini yahitaji saa kumi na mbili tena kupata fahamu zake,” aliongea daktari na machela ikasukumwa moja kwa moja chumba cha wagonjwa mahututi Fedovor akitakiwa kusubiri mpaka muda huo ufike na angepewa taarifa zote.

Nje ya chumba hakutulia kabisa, alitaka kufahamu kila kitu kilichoendelea ndani ya wodi mara kadhaa akitupa macho kwenye saa yake ya mkononi kuangalia wakati hatimaye mpaka wakati huo saa kumi na mbili zilishapita hivyo mbele yake alikuwa na saa mbili tu muda alioelezwa na madaktari ufike na mtoto wake Merina kurejewa na fahamu. Macho yake yaliendelea kushuhudia wauguzi na madaktari wakitoka na kuingia kama vile walipeana zamu ndani ya chumba huku naye hofu ikimgubika likiwa limebaki saa moja tu mbele yake.

***
“Baba! Baba!” Aliita kwa sauti iliyosikika ndani ya chumba.
“Mh!” muuguzi ndani ya wodi aliguna kuonyesha mshangao wa ajabu kwani kitendo alichokishuhudia hakikuwa cha kawaida mtoto Mariya alikuwa amenyanyuka na kuketi kitako kitandani.
“Amemwita baba yake,” waliongea wakisogea karibu na kitanda alichokuwa mtoto huyo.”
“Unajisikiaje?” walimuuliza.

“Merina! Merina”
“Unaitwa nani?”
“Namtaka baba yangu…Merina uko wapi?” aliongea mtoto huyo huku akinyanyua mikono yake na kushika kichwa chake akakutana na bendeji kubwa, hiyo ndiyo ilimfanya azidi kulia.
“Baaaaba!” akapaza sauti.
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.97

“Namtaka baba yangu…Merina uko wapi?” aliongea mtoto huyo huku akinyanyua mikono yake na kushika kichwa chake akakutana na bendeji kubwa, hiyo ndiyo iliyomfanya azidi kulia zaidi.
“Baaaaba!” akapaza sauti.
“Hebu mwiteni baba yake aje hapa haraka, hatakiwi kuongea muda mrefu kutokana na hali yake,” daktari aliongea kwa msisitizo na muuguzi akaonekana akitoka nje huku akikimbia.

“Mzee tafadhali tunakuomba ndani ya chumba.”
“Mh! Tatizo jingine tena,” aliongea tajiri Federov akinyanyuka kutoka chini alipokuwa ameketi, taratibu akatembea na kuingia ndani ya chumba ambako aliongozwa moja kwa moja mpaka mahali watoto wake pacha walipokuwa wamelala juu ya vitanda.
Kwa macho yake akamshuhudia Mariya akiwa ameketi juu ya kitanda na alipotokeza tu mtoto huyo akaita tena kwa sauti ya juu.
“Babaaa!”

“Mwanangu, umeamka?”
“Sogea karibu yangu baba.”
Fedorov akasogea kisha akainamisha kichwa chake karibu kabisa na mwanaye, hapo akaachia mabusu mfululizo huku naye akilia.
“Nini kimetokea baba? Kwa nini niko hapa? Merina, je, yuko wapi?”
“Mh!” Watu wote ndani ya chumba waliguna. Hakukuwa na jibu kamili la kumpa Mariya kwamba pacha mwenzake alikuwa mgonjwa taabani muda mfupi uliopita.

“Nataka kumwona Merina,” Mariya alizidi kusisitiza huku akizungusha kichwa chake huku na kule ndani ya chumba kama vile alikuwa akitafuta kitu fulani.
Kwa nusu saa nzima walikuwa wamejaribu kumnyamazisha Mariya lakini ilionekana kushindikana, ni hapo ndipo daktari aliposhauri mtoto huyo aelezwe ukweli kwani kutokana na afya yake hakutakiwa kupata msongo wa mawazo ili kunusuru matatizo mengine yasitokee kwenye upasuaji wake wa kichwa.
“Merina,” Fedorov aliita.

“Mh!”
“Merina yule pale, yeye bado hajaamka.”
“Hajaamka? Kwa nini kalala mpaka sasa?”
“La hasha si usingizi wa kawaida bali anaumwa.”
“Anaumwa nini?” Aliuliza huku akizungusha mikono yake kushika sehemu ya kichwa.
“Mwanangu hata wewe ni mgonjwa na hapa tulipo tupo hospitalini kwa muda sasa.”

“Ina maana tunaumwa wote?”
“Huo ndiyo ukweli.”
“Basi nataka niende kumwona, si mmesema ndiye yule pale,” aliongea Mariya akielekeza kidole upande aliokuwa ameonyeshwa.
Daktari aliyekuwa ndani ya chumba cha wagonjwa mahututi akatakiwa kutoa ushauri kwani ili mtoto huyo anyamaze, ilikuwa ni lazima asogezwe mpaka karibu na kitanda cha pacha wake.
“Kwa sababu kitanda kina magudurumu kisogezwe taratibu kwa uangalifu mkubwa mpaka pale ili akamwone mwenzake, nadhani baada ya jambo hilo ataacha kulia.”

Ushauri uliotolewa na daktari ukafuatwa, taratibu kitanda kikaanza kusukumwa kuelekea eneo ambako kulikuwa na kitanda kingine ambacho juu yake alilala Merina akiwa hajitambui kabisa.
“Huyu hapa Merina.”
“Maskini wa Mungu kilitokea nini baba?”
“Mlipata ajali mbaya, hiyo ndiyo iliyosababisha ninyi nyote kuwa hapa mkiwa mmeumia vibaya.”

“Ajali! Baba!” Aliongea Mariya lakini kabla hajaenda mbali zaidi tukio zima la jinsi walivyotekwa na mwanaume wasiyemfahamu kisha kuwafungia mahali ambako walipata mateso wakiwa hawana chakula wala maji liliingia kichwani mwa Mariya kama sinema.
“Baba na yule aliyetufunga vitambaa na kutupakiza ndani ya gari kisha kuturusha kama…” kwikwi ya kulia ikamkaba, alikumbuka kila kitu kilichotokea siku nyingi nyuma.
“Nyamaza kulia mwanangu hayo yote yalishapita cha muhimu ni afya zenu.”

“Lakini baba mbona mimi nimeamka na Merina bado, kwa nini?”
“Huyu alipatwa na tatizo ambalo ilibidi afanyiwe tena upasuaji kwa mara ya pili lakini ataamka muda si mrefu.”
“Napenda iwe hivyo, sipendi kumkosa nampenda mno,” aliongea Mariya akionyesha msisitizo.
Baada ya mazungumzo hayo walimsihi arejeshwe sehemu alikokuwa lakini alionekana kugoma akisisitiza kubaki eneo hilohilo mpaka mwenzake aamke ili aongee naye.

“Nitakaa hapahapa mpaka aamke, nataka kuongea naye, najua anasikia ila kujibu tu ndiyo tatizo…Merina! Merina tafadhali amka mimi Mariya nakuita… nakupenda sana, pia baba yuko hapa naye anataka kuona umeamka ili uongee nasi tunakumi…,” aliongea mtoto huyo kwa uchungu jambo lililowafanya wauguzi na madaktari waliokuwepo ndani ya chumba nao walengwe na machozi.
Wakiwa katika mawazo hayo ghafla jambo lisilokuwa la kawaida likatokea.
“Mh! Mh!” Ilikuwa ni sauti ya mguno kutoka kwa Merina, tayari zilishatimia saa kumi na mbili tangu atoke chumba cha upasuaji, watu wote wakaonekana kupigwa butwaa.
 
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.98

MIAKA mitatu baadaye furaha ikiendelea kutawala ndani ya familia ya Phillip na mkewe Lina, mtoto Genevieve akiendelea kukua vyema mara kadhaa wawakilishi kutoka kituo cha Msimbazi cha kulelea watoto walikwenda nyumbani kwa Phillip kufuatilia maisha aliyoishi mtoto huyo, walionyesha furaha na kumshukuru Mungu kwani alipata mapenzi yote ya baba na mama.
“Hakika Genevieve amekuwa binti mkubwa sasa.”

“Sisi pia tunamshukuru Mungu kwa afya na baraka anazompa mtoto huyu.”
“Amina,” aliongea Sista Maryjoyce.
“Lakini pia anasoma shule nzuri sana mtoto wetu.”
“Ah! Inaitwaje?”

“Inaitwa FEZA huko ndiko tumeona inafaa na tunashukuru hata walimu pia wanatupa ushirikiano mzuri sana.”
“Hakika mtoto huyu alikuwa anasubiri ujio wenu katika kituo chetu, hebu mwone nadhani anajua jinsi mnavyompenda.”
“Hata sisi tunaona hivyo, tunaomba tu tuendelee kumwona akikua vyema.”
“Hizo ni baraka za kila mzazi mwenye watoto.”

Waliongea mengi huku wakiburudika kwa vinywaji, masista hawakusita kutoa sifa zao kwa familia ya Phillip wakimwombea kwa Mungu azidi kuwa na moyo huo mpaka mwisho. Baada ya mazungumzo hayo kwa sababu saa zilikuwa zimesonga sana wakaomba ruhusa ya kuondoka kurejea kwenye makazi yao, wakakubaliwa na kuondoka.
Genevieve hakuwa mbali na mahali walipokuwa wameketi hivyo alipoona tu watu wakinyanyuka vitini alifahamu wazi kwamba walikuwa wakiondoka kitendo ambacho hakukipenda hivyo kuangua kilio.
“Usilie mtoto mzuri tunakupenda tutakuja tena kukutembelea siku nyingine, sawa?” Sista MaryJoyce aliongea akimbembeleza Genevieve.

***
Mapenzi yote ya Phillip yakatoka kwa Lina na kuhamia kwa Genevieve, alitumia muda mwingi kukaa na mtoto huyo kuliko ilivyokuwa kwa mkewe jambo ambalo lilianza kuleta matatizo kwani Lina pia akitaka apate nafasi kwa mumewe.
“Mume nami pia nahitaji mapenzi yako unanishangaza sana kutwa kucha wewe na mtoto tu… huna tena muda wa kuwa nami,” Lina aliongea siku moja wakiwa wameketi bustanini nje ya nyumba yao.

“Lina yaani unasikia wivu hata kwa mtoto wetu? Mke wangu jamani si hivyo kumbuka ni mtoto huyu huyu aliyekuwa akitugombanisha mimi na wewe, tafadhali mpatie naye nafasi mbona mimi silalamiki pale unapomchukua na kutoka naye?”
“Ah! Unajua nini?”
“Mh!”
“Naona kama umenisahau sana, maana kila ukitoka na kurudi mkononi umebeba zawadi zake tu mimi ah!”

“Haa!Haa!Haaa! Lina huo ni wivu tu mke wangu achana nao hebu tushirikiane kumlea mtoto wetu bwana, Mungu ametubariki ametupa mtoto mzuri kweli kweli huyu akikua atakuwa tishio, nitashikia watu bastola.”
“Mh! Haya ngoja tuone itakuwaje, mwaa!mwaa!” Lina aliongea akisogea karibu na Phillip kisha kumwachia mabusu kwenye paji lake la uso.
“Ahsante! Mwaaa, hebu twende ndani kwanza mara moja” Phillip naye akajibu kwa busu huku akimtaka Lina waingie ndani.
“Kufanya nini?”

“Nasema hivi twende ndani.”
“Mtoto je?”
“Atabaki na Magdalena hana shida.”
“Na wewe,” Lina aliyemfahamu Phillip kupita maelezo aliongea kwani mara kadhaa alipomtaka kwenda ndani basi lazima kulikuwa na jambo.
“Hivi wewe umenielewa nakuhitaji ndani haraka sana,” Phillip aliongea akionyesha msisitizo na tayari alishaanza kupiga hatua kuondoka eneo hilo.

Lina bila ubishi naye akaanza kufuata nyuma akiwa na mtoto alipoingia tu sebuleni akamkabidhi mtoto kwa Magdalena kisha naye kufuata nyayo kuingia chumbani.
“Funga mlango kwa funguo,” alitamka Phillip.
“Unataka kunipiga?”
“La hasha mwanamke huwa hapigwi kwa ngumi na mateka, anapigwa kwa kipande cha khanga lakini wewe sitakupiga hivyo nita…” Phillip aliongea huku akimvuta Lina na kumtupia juu ya kitanda.

***
Miezi mitatu baadaye tayari afya za watoto wawili pacha Mariya na Merina zilikuwa zikindelea vizuri hatimaye wakawa wameruhusiwa kurejea nyumbani wakitakiwa kuhudhuria kliniki zao kila baada ya mwezi mmoja ili kuwaangalia kwa ukaribu.
“Ahsanteni madaktari na Mungu awabariki sana kwa kuokoa maisha ya watoto wangu, sijui ningekuwa mgeni wa nani hapa duniani bila ya kuwa na watoto, utajiri wangu wote usingekuwa na maana, hakika ninawapenda sana wanangu,” aliongea Fedorov akichomoa burungutu la fedha na kuwapa madaktari pamoja na wauguzi kama ahsante kwa jinsi walivyojitoa kwake.

“Ah! Mzee hakuna haja sisi ndiyo kazi yetu bwana.”
“Najua ndiyo kazi yenu lakini hii si rushwa nawapa soda tu jamani ndugu zangu, tafadhali pokeeni vinginevyo nitajisikia vibaya sana.”
Mabishano yakawa yametokea kwa muda wa dakika tano nzima, wakipiga hatua hiyo ya Federov kutoa fedha mfukoni mwake na kuwapatia lakini aliposihi na kubembeleza sana hatimaye walizipokea na kumshukuru.

Utaratibu maalum ukafanyika na watoto wakachukuliwa kupelekwa nyumbani ambako furaha iliendelea, akawapokea tena na kuwakaribisha wao pia walikuwa na furaha lakini zaidi ya yote walitaka kufahamu ni kitu gani kilisababisha mpaka wakawa katika hali ile.
“Wanangu ni historia ndefu sana sioni kama kuna haja ya kuwasimulia…nadhani mtaumia na nisingependa jambo hilo litokee tena, kwa ushauri wa madaktari hamtakiwi kupata kitu kitakachowafanya mfikirie sana.”
“Basi baba hakuna shida lakini tunalo ombi moja kwako.”

“Ombi gani tena?”
“Tunataka kuendelea na shule ikiwezekana hata kesho.”
“Hakuna shida mpumzike kwa muda wa wiki moja hivi halafu wiki inayofuata mtaanza tena shule.”
“Ahsante baba tunakupenda sana,” waliongea Mariya na Merina kisha kunyanyuka vitini na kumsogelea baba yao, wakamkumbatia na kuanza kububujikwa machozi.
 
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.99


MIAKA kumi na tano baadaye.
Maisha nyumbani kwa tajiri Victor Fedorov yaliendelea, Mariya na Merina walisahau kabisa mambo yote yaliyotokea maishani mwao.
Kilichotawala katika familia hiyo kilikuwa ni upendo, furaha na amani. Fedorov alihakikisha anafanya kila kitu kuwapa furaha watoto wake.
Akiwa ameketi na Mariya na Merina, aliwaeleza kwamba maisha hayakuwa rahisi kama walivyofikiria hivyo kuwataka wasome kwa bidii ili nao wapate kitu ambacho kitaongoza maisha yao.

“Nataka msome tena kwa bidii nami nitawaunga mkono kwa kila jambo, sawa wanangu?”
“Ndiyo baba nasi hatutakuangusha.”
Watoto hao kwa sababu walimpenda sana baba yao walijitahidi kufanya kila kilichokuwa kizuri ili wasimtie aibu, kwani walipata kila kitu walichohitaji.
Hakika walijivunia kuwa na baba kama Fedorov bila kufahamu kwamba nyuma yake hakuwa mtu mzuri, alikuwa mtu hatari aliyeogopwa na kila mtu.

“Nitahakikisha watoto hawa hawagundui jambo lolote linalohusu maisha yao na yangu,” aliongea Fedorov akisogelea kabati kubwa lililokuwa ndani ya chumba na kulifungua, taratibu akionekana mwenye wasiwasi mwingi akachomoa kitu kama faili na kuketi kitako juu ya kitanda.
Kwa umakini wa hali ya juu akaanza kusoma karatasi moja baada ya nyingine. Lilikuwa ni faili lenye siri kubwa ambayo aliamini kabisa kwamba hakuwepo mtu yeyote aliyefahamu siri hiyo.
“Maskini wa Mungu,” aliongea akigeuza shingo yake huku na kule na alipohakikisha kwamba hapakuwa na mtu aliyemwona akasogea tena mpaka kabatini na kulirejesha faili na kufunga mlango.

“Nitahakikisha hakuna mtu hata mmoja atakayefahamu umafia nilioucheza, itabaki kuwa siri yangu tu.”
Maneno aliyokuwa ameapa Fedorov yalimaanisha alichokisema lakini yeye kama mwanadamu hakufahamu kabisa kwamba maisha yake yalikuwa mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Alikuwa amefanikiwa kuficha siri kwa kuua watu wote waliofahamu umafia alioutenda.
Ndani ya faili alilolihifadhi kabatini, kuliandikwa kila kitu jinsi alivyofanikiwa kuteka watoto wawili yaani Mariya na Merina kutoka Tanzania na kuwafikisha nchini Urusi huku akihakikisha wanafutwa kumbukumbu zote na kuwafanya wamtambue yeye kama baba yao, jambo ambalo lilifanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini pia mauaji ya Ditrov na wenzake ili kuficha mpango mzima wa utekaji nyara.

Pia kulikuwa na wosia mzito juu ya mali na fedha zote alizokuwa nazo akiagiza kama litatokea lolote basi huo ndiyo urithi kwa watoto wake hao. Alipohakikisha kila kitu kimekwenda sawa, akapanda kitandani na kujilaza.
***
Kilichokuwa kinasikika ndani ya chumba kwa wakati huo ni kelele za kitanda tu, kwa zaidi ya saa tatu mfululizo Phillip na mkewe Lina walikuwa wakiwajibika ipasavyo.
“Leo ndiyo leo asemaye kesho ni mwongo, Lina ukweli nakupenda kutoka ndani ya moyo wangu na furaha hiyo imeongezeka zaidi baada ya mtoto wetu Genevieve kuingia ndani ya familia yetu…mwaaa”.

“Ahsante Phillip nami pia ninakupenda kuliko maelezo ndiyo maana sikuwaza kukusaliti hata mara moja, ingawa nilikuwa na uwezo huo.”
“Mh! Usiseme hivyo mke wangu ni shetani tu, nilitamani kuitwa baba.”
“Nami nililifahamu jambo hilo mapema ndiyo maana nikapata wazo la kuasili mtoto na kweli umekubali na sasa tunaye Genevieve.”
“Nitampenda mtoto huyu mpaka mwisho, sipo tayari kuona akiteseka wakati nikiwa hai, sasa ni wakati wa mimi na wewe kufanya kazi kwa bidii ili mtoto aishi maisha ya kifalme baadaye au?”

“Umesema kweli mu…” Lina alishindwa kumalizi sentensi yake, kigugumizi kikaonekana kumkamata.
Waliendelea kubaki ndani ya chumba kwa muda mwingine wa saa mbili na kutimiza saa tano kamili.
“Mume wangu sasa inatosha ni vyema tukatoka kwenda kumwangalia mtoto wetu ametumisi sana jamani.”
“Umesema kweli kabisa lakini ni lazima nasi tupate nafasi kama hii.”
“Ahsante nimeamini kwamba kweli unanipenda.”

“Saaana!” Phillip aliongea akinyanyuka kitandani kuelekea bafuni kuoga.
Hayo ndiyo yakawa maisha yao wakifurahia mtoto aliyeingia ndani ya familia yao, wote wakiamini kwamba ameleta upya furaha katika nyumba yao, kila mmoja akiahidi kumpenda na kumtunza kwa hali na mali lakini mapenzi ya Phillip yalionekana wazi kwa sababu mtoto huyo alipewa jina la marehemu mke wake.
“Hatimaye Genevieve amerudi tena katika maisha yangu…,” aliwaza kichwani mwake akitoka ndani ya chumba kuelekea sebuleni.
“Phillip nimekumbuka jambo moja.”

“Lipi tena hilo?”
“Kesho ni siku ya kutembelea makaburi ya ndugu zetu kuangalia na kuyaweka safi, sijui unakumbuka?”
“Mh! Ahsante sana kwa kunikumbusha, ndiyo maana Mungu amenipa mwanamke kama wewe, hakika unajali.”
Ilikuwa ni kama desturi kwa Phillip kutembelea makaburi ya mke na watoto wake kufanya ibada kisha kufanya usafi ikiwa ni ishara mojawapo ya kuwaenzi.

***
Tayari Mariya na Merina walishatimiza umri wa miaka kumi na nane na walihitimu elimu yao ya chuo kikuu, walitamani sana kufanya kazi lakini msimamo wa baba yao ulihitaji waendelee kusoma zaidi ili waje kuongoza makampuni aliyokuwa nayo, hivyo walitakiwa kupumzika kidogo kisha kuendelea na masomo ya juu zaidi.
“Nataka muendelee kusoma zaidi ninyi ndiyo warithi wangu, mtapumzika kidogo halafu mtaendelea na masomo sijui mnataka kwenda nchi gani kwa mapumziko?”

“Mh! Baba tunataka tukae hapahapa na wewe, hatuwezi kwenda mbali na upeo wa macho yako.”
“Basi sawa na ni zawadi gani mnapenda?”
“Mh! Gari aina ya Ferrari.”

“Wow! Wazo hilo ndilo lilikuwa akilini mwangu, nilitaka kuwafanya miongoni mwa mastaa mjulikane ulimwengu mzima kama mimi ninavyojulikana.”
“Ahsante baba kwa mapenzi unayotuonyesha, hakika unatupenda.
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP.100


TAYARI ilikuwa imeshatimia miaka kumi huku mtoto Geneveive akikua vyema na akiendelea na masomo yake katika shule ya Feza, mapenzi mema aliyopewa na wazazi wake wawili yalimfanya ajisikie mwenye furaha sana.
Phillip na Lina walimtunza na kumfanyia kila lililo jema wakihakikisha hapungukiwi na kitu chochote maishani mwake.
“Phillip ni vyema sasa tukamweleza mtoto huyu siri ambayo tumeiweka ndani ya mioyo yetu kwa muda mrefu.”
“Lina!” Phillip alimwita mkewe kwa mshangao.

“Ni lazima siku moja aje kuufahamu ukweli mume wangu.”
“Najua hilo lakini si sasa, bado umri wake ni mdogo, anahitaji kukua zaidi.”
“Mh! Haya kumbuka lakini sisi ni binadamu lolote linaweza kutokea.”
“Lina tafadhali achana na fikra potofu,” aliongea Phillip huku akimwita Genevieve asogee karibu yake.
Alihakikisha mtoto huyo anapata mapenzi ya dhati kutoka kwake na mkewe, hakuwa tayari kuona mtoto huyo akiumia wala kuumizwa na mtu mwingine.

“Nakupenda sana mwanangu.”
“Ahsante baba yangu nakupenda pia.”
“Genevieve mimi pia ninakupenda,” aliongea Lina akiachia tabasamu mdomoni mwake.
Hayo ndiyo yakawa maisha yao ndani ya nyumba, kuonesha mapenzi ya dhati kwa vitendo na maneno kwa Genevieve huku wakiitunza siri ya kwamba hawakuwa wazazi wake wa kumzaa bali walimuasili kutoka katika kituo cha watoto Yatima cha Msimbazi.

Waliendelea kubaki sebuleni kwa mazungumzo wakiongea na kufurahi pamoja, mara kadhaa wakimsisitiza mtoto Genevieve umuhimu wa shule, wakimtaka asome kwa bidii kwani elimu ndiyo ulikuwa urithi wake mkubwa katika maisha yake ya baadaye.
“Chakula tayari karibuni mezani,” ilikuwa ni sauti ya mfanyakazi wa ndani, Magdalena akiwakaribisha mezani kwa ajili ya chakula, wakamshukuru na kusogea mezani.

Saa mbili baadaye walishapumzika vya kutosha na mmoja baada ya mwingine wakaaga na kuingia ndani ya vyumba vyao kupumzika kwa ajili ya siku iliyofuata, Lina na Phillip nao wakiingia ndani ya chumba chao.
“Mke wangu kusema ukweli ninakupenda sana.”
“Mimi pia nakupenda Phillip sikuwahi kumpenda mwanaume mwingine maishani mwangu kama ilivyokuwa kwako.”
“Ahsante kwa kunipenda lakini ninataka kukueleza kitu kimoja.”

“Kitu gani?”
“Ninapokuwa na wewe hivi huwa sichoki kufanya tendo la ndoa na wewe, nakuhitaji kila wakati mke wangu…mh! Unajua nini?...hebu sogea hapa…” aliongea Phillip kwa sauti ya kutetemeka huku akimvuta Lina upande aliokuwa ameketi yeye.
“Mh! Mh! Bwa…na” aliongea Lina kwa sauti ya chini chini huku akisogea kumfuata mumewe.

***
Mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwa watoto wake alihakikisha wanayafaidi maisha yote mazuri, akiwapa kila kitu muhimu maishani, hivyo, baada ya maongezi yao kukamilika na watoto kuhitaji zawadi ya gari kama ambavyo baba yao alivyowauliza aliahidi kuwatafuta gari hilo ndani ya saa ishirini na nne tu.

Saa sita zikakatika watoto Mariya na Merina wakimsubiri baba yao kwa hamu kubwa, ghafla wakasikia sauti ya honi nje ya lango la kuingia ndani ya nyumba yao, haraka wakanyanyuka kwenye viti kuelekea langoni ambako mlinzi alishafungua kuruhusu gari kuingia.
“Gosh!” walijikuta wakitamka maneno hayo.
Mbele ya macho yao yalishuhudia gari aina ya Ferrari ambalo walilihitaji ndani yake kukiwa na mwanaume mmoja aliyejazia misuli, akaliendesha na kuliingia ndani kisha kuliegesha sehemu maalum na kushuka.

“Naitwa Ford niko hapa kwa maelezo ya bosi Fedorov,” aliongea mwanaume huyo.
Mariya na Merina hawakujibu kitu chochote macho yao yalikuwa bize yakishangaa huku na kule kuangalia gari hilo, wakiongea wenyewe katika mioyo yao na kujijibu.
“Hallow” aliita mwanaume huyo.

“Subiri kwanza kaka tutaongea baadaye.
Kwa muda wa nusu saa nzima waliendelea kulishangaa gari lililokuwa ndani ya ngome yao, wakijiuliza maswali mbalimbali na waliporidhika walimsogelea mwanaume aliyekuwa pembeni na kuongea naye akajitambulisha tena kwa mara ya pili kwao.
“Ahaa! Karibu sana.

“Mimi naitwa Mariya na huyu anaitwa Merina ni watoto wa Victor Fedorov.”
“Vizuri nimetumwa na bosi wangu kuja hapa nyumbani si kuleta tu gari hili bali pia mimi ndiye nitakuwa dereva wenu kwa muda.”
“Oh! Ahsante baba yuko wapi?”
“Atakuja muda si mrefu mimi nimetangulia.

Wakiwa katika maongezi hayo haikuchukua hata dakika tano, honi nyingine ikasikika nje ya lango la kuingilia ndani ya nyumba, mlinzi akaongekana akifungua lango na gari ya Fedorov kuingia ndani huku akipiga honi nyingi kuashiria furaha, akaliendesha gari mpaka sehemu ya maegesho akaliegesha na kushuka na watoto wake wote wawili wakamkimbilia na kumkumbatia huku wakimbusu kwa wingi katika mashavu yake.

“I love you daddy,”(tunakupenda baba) walitamka maneno hayo wakimwangalia baba yao kwa macho ya upole.
“I love you too,”(Nawapenda pia) Fedorov alijibu huku machozi yakimtiririka mashavuni mwake.
“Baba kwa nini unalia?”
“Mh! Hapana”

“Tafadhali tueleze nini kimekupata huko ulikotoka?”
“Hakuna kitu wanangu ila…”
“Bosi! Bosi! Nini kimetokea nini huko utokako?”
Victor Fedorov hakuwa na jibu la kutoa kwa wakati huo akasogea taratibu na kuketi pembeni ya msingi uliokuwepo hapo kwikwi za kulia zikamkamata.

Je, nini kitaendelea? Ni kwa nini analia? Tukutane kesho km kawa nite nite!!!
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP. 101.

“NAITWA Ford niko hapa kwa maelezo ya bosi Fedorov,” aliongea mwanaume huyo.
Mariya na Merina wakati hawakujibu kitu chochote macho yao yalikuwa bize yakishangaa huku na kule kuangalia gari hilo wakiongea wenyewe na kujijibu.
“Hallow!” aliita mwanaume huyo.
“Subiri kwanza kaka tutaongea baadaye,” alijibu Merina.

Kwa muda wa nusu saa nzima waliendelea kushangaa gari lililokuwa ndani ya ngome yao wakijiuliza maswali mbalimbali na waliporidhika walimsogelea mwanaume aliyekuwa pembeni na kuongea naye akajitambulisha tena kwa mara ya pili.
“Ahaa! Karibu sana. Mimi naitwa Mariya na huyu anaitwa Merina ni watoto wa Victor Fedorov.”
“Vizuri nimetumwa na bosi wangu kuja hapa nyumbani si kuleta tu gari hili bali pia mimi ndiye nitakuwa dereva wenu kwa muda..”
“Oh! Ahsante, baba yuko wapi?”

“Atakuja muda si mrefu mimi nimetangulia.”
Wakiwa katika maongezi hayo haikuchukua hata dakika tano honi nyingine ikasikika nje ya lango la kuingikua ndani ya nyumba mlinzi akaonekana akifungua lango na gari la Fedorov kuingia ndani huku akipiga honi nyingi na kuashiria furaha, akaliendesha mpaka sehemu ya maegesho, akaegesha na kushuka na watoto wake wote wawili wakamkimbilia na kumkumbatia huku wakimpiga mabusu mengi.
“We love you daddy!” (Tunakupenda baba) walitamka maneno hayo wakimwangalia baba yao kwa macho ya upole.
“I love you too!” (Nawapenda pia) Fedorov alijibu huku machozi yakitiririka mashavuni mwake.

“Baba kwa nini unalia?”
“Mh! Hapana.”
“Tafadhali tueleze nini kimekupata huko ulikotoka?”
“Hakuna kitu wanangu ila…”

“Bosi! Bosi! Nini kimetokea huko utokako?”
Victor Fedorov hakuwa na jibu la kutoa kwa wakati huo, akasogea taratibu na kuketi pembeni mwa msingi uliokuwepo hapo, kwikwi ya kulia ikamkamata.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

“TAFADHALI tueleze nini tatizo?”
“Mh!”
“Baba kwa nini unatuweka roho juu?”
“Naomba nitamke wazi leo…” kwikwi ya kulia ikamkamata tena Fedorov na kuangua kilio kama mtoto mdogo.
Kwa takribani dakika tano nzima waliendelea kubaki eneo hilo wakiwa wameshikwa na butwaa wakiwa hawaelewi ni kitu gani kilikuwa kimetokea huko alikokuwa kabla ya kufika nyumbani.

Walipohakikisha ametulia hawakuchoka kuendelea kumuuliza tena.
“Mnajua nini?”
“Eh!”
“Ninawapenda sana wanangu historia yenu inanikumbusha maisha ya nyuma ambayo yanaumiza kupita maelezo.”
“Baba lakini ya kale yamepita na tazama yamekuwa mapya. Unamkumbuka mama yetu?”
“Mh!”

“Unakumbuka nini?”
“Jinsi nilivyowalea mpaka kufikia hapa nikiwa sina msaada wowote.”
“Lakini baba hata sisi tunakupenda kupita maelezo.”
“Najua wanangu nami nawapenda pia.”
“Ahsante kwa zawadi nzuri ya gari.”

“Ni wajibu wangu kufanya hivyo kwenu kama wanangu na huyu hapa mbele yetu ndiye atakuwa dereva wenu mpaka mtakapokuwa mmefuzu vyema udereva, atawapeleka kokote mtakapotaka na kuhakikisha anawapa ulinzi wa kutosha.”
“Ahsante baba,” walijibu Mariya na Merina wakitabasamu.
“Leo nitaomba tujumuike wote kwa chakula cha jioni ili kukamilisha furaha yetu wanangu na kesho ninafikiria kufanya matembezi kidogo kwenye mchezo wa kuteleza kwenye barafu.”
“Babaaa!”

“Ni kweli kabisa kwa sasa ni msimu mzuri wa kwenda huko nitaondoka na nitarejea baada ya wiki tatu.”
“Twende wote.”
“Hapana acha mimi niende kwanza nikirudi mara nyingine nitawachukua wote.”
“Sawa baba tutashukuru.”
Wakaingia ndani na kujiandaa kwa ajili ya kutoka kwenda kula chakula cha jioni kama familia wakifurahia maisha na mapenzi makubwa waliyoyapata kutoka kwa baba yao. Kwa muda wa saa nzima walikuwa chumbani wakijiandaa na waliporidhika walitoka.
“Wow!” sauti ya Fedorov ilisikika baada tu ya kuwaona watoto wake wakitoka chumbani.

“Heheee!” walicheka.
“Mmempendeza sana wanangu hakika ninyi ni mabinti wazuri sana.”
“Ahsante baba.”
Wakatembea kwa mwendo wa madaha na kulielekea gari lao aina ya Ferarri na kuingia ndani ambapo Fedorov naye akaingia kwenye gari lake, yeye ndiye akawa mtu wa kwanza kutoka ndani, gari walilopanda watoto wake likifuata kwa nyuma.
Kwa mwendo wa nusu saa hivi walikuwa barabarani hatimaye wakafika kwenye mgahawa maarufu wa Kalinin. Fedorov akawa wa kwanza kushuka ndani ya gari na kubaki kusubiri watoto pamoja na dereva washuke ili waingie wote kwa pamoja.

Akionekana wenye furaha, akawakumbatia watoto wake na kuanza kutembea kuingia ndani ya mgahawa, wote wakionekana wenye furaha kupita maelezo. Kwa umaarufu na utajiri aliokuwa nao mzee huyo nchini Urusi alipewa heshima kubwa sana, alipokelewa kwa furaha na wafanyakazi karibu wote katika mgahawa huo na akaongozwa kupelekwa sehemu maalum kabisa akikaribishwa mara nyingi.
“Leo nimekuja na watoto wangu, huyu hapa anaitwa Mariya na huyu ni Merina, huyu mwingine ni dereva wao anaitwa Ford,” aliongea Fedorov kwa kujiamini kabisa.

“Karibuni sana ndugu zetu.”
Menu yenye orodha ya chakula na vinywaji ikawekwa mezani na mhudumu akiwataka wachague kitu ambacho wangependa kula na kunywa siku hiyo na wakionekana wenye furaha, kila mmoja aliagiza alichotamani kula.
Wakala na kunywa wakifurahi pamoja na baada ya hapo walilipa na kuondoka na kuingia maduka mbalimbali kununua vitu walivyohitaji na kurejea nyumbani.

“Usiku mwema wanangu!”
“Kwako pia baba!”
Wakaingia ndani ya vyumba vyao na kulala na siku iliyofuata Fedorov ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kuamka ili ajiandae kwa safari ambayo ingemchukua muda wa wiki mbili mfululizo akiwaacha watoto wake peke yao nyumbani, akatoka chumbani akiwa tayari na mizigo yake kisha kugonga mlango wa chumba cha watoto wake huku akiwaita majina akiwaaga na akiwatakia kila lililo jema na kutoa maelekezo ya mahali ambako wangechukua fedha za matumizi kwa muda wote ambao hangekuwepo.

Kwa pamoja wakamrukia baba yao na kumkumbatia wakimtakia safari njema na kumtaka awahi kurejea nyumbani kwani kwa muda ambao hatakuwepo watakuwa wapweke sana.
“Nitarejea muda si mrefu, mwaa ninawapenda sana,” aliongea lakini watoto wake walipomwangalia vyema usoni mwake waligundua alikuwa akibubujikwa na machozi na walipomuuliza ni kwa nini alipatwa na hali hiyo Fedorov hakujibu kitu zaidi ya kuanza kutembea kuelekea nje ya nyumba yake akiwa na begi kubwa mgongoni mwake.

***
“Phillip! Phillip!” Lina aliita mfululizo
“Naam!”
“Ah! Najisikia vibaya.”
“Kidogo tu mke wangu sita…”
“Mh! Siyo hivyo mwenzio najisikia kizunguzungu.”

“Kizunguzungu?” aliuliza kwa mshangao.
“Ndiyo, nipe…”
“Lina acha basi utani wako unanicha…”
“Hapana Phillip naumwa mbona naona giza!”
“Eh!”

“Nipe maji ya kunywa fanya haraka kabla sija…” aliongea Lina lakini kabla hajamalizia sentensi yake ukimya wa ajabu ukatokea na Phillip alipojaribu kumwita na kumtingisha hakupata ushirikiano wowote zaidi ya yote alimshuhudia Lina akilegea kama mlenda.
“Mungu wangu! Kimetokea nini?” alijiuliza akimlaza Lina vyema kitandani na yeye kushuka kitandani.
Phillip akalisogelea taulo lililokuwa pembeni na kujifunga kiunoni, jasho jingi likimtiririka.
 
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP. 102

Nipe maji ya kunywa fanya haraka kabla sija…,” aliongea Lina lakini kabla hajamalizia sentensi yake ukimya wa ajabu ukatokea na Phillip alipojaribu kumwita na kumtingisha hakupata ushirikiano wowote, zaidi ya yote alimshuhudia Lina akilegea kama mlenda.
“Mungu wangu! Kimetokea nini?” alijiuliza akimlaza Lina vyema kitandani na yeye kushuka haraka kitandani, haraka akachukua taulo lililokuwa pembeni na kufunga kiunoni jasho jingi likimtiririka. Kitu kilichokuwa kikitokea mbele yake kilionekana kuwa ni ndoto kama siyo muujiza, akakizunguka chumba huku na kule akifikiria cha kufanya.

“Lina! Lina mke wangu kimetokea nini?” aliita Phillip lakini hakupata jibu lolote kutoka kwa mkewe aliyekuwa kitandani akiwa ametulia kimya.
“Hapa ni hospitali tu, hakuna kingine cha kufanya,” aliongea Phillip.
Akiwa amechanganyikiwa alivaa shati kisha kumvalisha Lina, akausogelea mlango na kuufungua huku akiita jina la Bibi Magdalena ili aje kumsaidia.

“Njoo haraka! Tafadhali njoo upesi,” alisisitiza Phillip.
Haraka bila kuchelewa, Bibi Magdalena aliingia chumbani kwa Phillip na kumkuta Lina akiwa amelala kimya kitandani huku mumewe akizunguka huku na kule.
“Nini kimetokea bosi wangu?”
“Lina amenyamaza ghafla,” Phillip alimjibu Bibi Magdalena.
“Umempiga?”

“Huu si muda muafaka wa kuuliza hivyo tusaidieni nimpeleke hospitali,” Phillip alimwambia Bibi Magdalena.
“Sawa bosi.”
Haraka Phillip akamnyanyua Lina, Bibi Magdalena akitangulia mbele kufungua mlango, walipofika kwenye gari lililofunguliwa mlango, walimuingiza Lina na kumlaza siti ya nyuma kisha Phillip akazunguka upande wa pili na kuingia.
Kabla hajaondoka, alimuaga Bibi Magdalena na kumwambia akifika hospitali atamfahamisha kilichomsibu mkewe.

“Haya kila la kheri,” alijibu Bibi Magdalena akitembea kurejea ndani, furaha yote iliyokuwepo muda mchache uliopita ilikuwa imetoweka.
“Sijui kapatwa na nini?” alijiuliza bibi huyo akiingia ndani.
Kwa muda wa saa tatu na nusu Phillip bado alikuwa hajarejea, wasiwasi ukaugubika moyo wa Bibi Magdalana akitaka kufahamu ni kitu gani kilitokea huko alikokuwa Phillip na mkewe Lina ambaye alikuwa mgonjwa taaban.

Saa zilipozidi kusonga mtoto Geneveve alianza kumsumbua Bibi Magdalena akitaka kujua wazazi wake walikuwa wapi.
Bila kujibu kitu chochote yeye mwenyewe akiwa na wasiwasi mwingi moyoni mwake alimtuliza mtoto Theresia na kumtaka atulie kwani wazazi wake wangerejea muda si mrefu, akatoka nje na kuelekea kwa mlinzi na kumweleza wazi wasiwasi aliokuwa nao.
“Hebu tusubiri kidogo pengine wako njiani.”
“Mh! Ni muda sana mtoto naye ananisumbua sijui wamepatwa na kitu gani, eh haya ni matatizo mengine tena!” aliongea bibi huyo akionyesha kulengwalengwa na machozi.

Ghafla wakiwa katika maongezi hayo, honi ikasikika nje ya lango la kuingilia ndani ya nyumba yao.
“Si hao!” aliongea mlinzi akilisogelea lango na kufungua, hakuwa amekosea gari la bosi wake lilikuwa limesimama nje ya lango hilo.
Taratibu bila kusema kitu akionekana mwenye mawazo mengi kichwani mwake, Phillip akaendesha gari mpaka sehemu ya maegesho. Alipoangalia kwenye kibaraza cha nyumba yake, akamshuhudia mtoto wake Genevieve akikimbia kumfuata.

“Dady why are you crying?”(Baba kwa nini unalia?)
“It’s too painful,”(Inauma sana)
“What?”(Nini?)
Kwikwi ya kulia ikamkaba Phillip, akajikuta akilia mbele ya mtoto wake kitu kilichozidi kumchanganya zaidi Genevieve, naye bila kutegemea akaanza kuangulia kilio.

***
Fedorov alitembea hatua mbili na kugeuka nyuma kuwaangalia watoto wake, hakuonekana kuwa na furaha kama ilivyokuwa siku zote aliposafiri kwenda mbali.
Alipolifikia gari lake, akafungua sehemu ya kuweka mizigo akaweka begi na vifaa alivyokuwa navyo ndani kisha akawaita tena watoto wake;
“Mariya, Merina.”

“Bee,” waliitika wakikimbia kumfuata na walipomfikia karibu waligundua baba yao alikuwa tofauti kabisa.
“Lakini unaonekana hauko sawa?” Merina aliuliza.
“Unajua nini?”
“Mh!”
“Ninasikia sauti ndani ya moyo wake ikiniambia kwamba nisiwaache.”
“Basi twende wote baba!”

“Hapana nataka mbaki nyumbani nami niende kwenye mchezo huo nitarejea tu niombeeni wanangu,” aliongea Fedorov huku akiwakumbatia watoto wake.
“Lakini umesema moyo wako hautaki kwenda huko?”
“Hivyo ndivyo ninavyosikia ila acheni niende.”
“Mh!” Mariya aliguna yeye pia alihisi kitu fulani ndani ya moyo wake lakini akajaribu kupingana na hisia hizo ili kumfanya baba yake arejee katika hali yake ya kawaida.

“Nawapenda sana wanangu mbaki salama, nitarejea baada ya wiki mbili, mnapenda niwaletee nini nikirudi?”
“Mh! Mh!”
“Semeni basi!” aliongea Fedorov akifungua mlango ili aingie garini.
“Tuletee zawadi ya saa.”
“Hilo tu?”
“Mh!” Waliitikia kwa kuguna huku wakitingisha vichwa vyao kuonyesha ishara ya kukubali.

Fedorov akaingia ndani ya gari na kuliwasha kisha taratibu huku akiwaangalia watoto wake akaliendesha gari hadi langoni ambako mlinzi alifungua kisha akatoka ndani.
“See you then,”(Tutaonana) ndiyo maneno pekee aliyoongea akitokomea.
Wiki ya kwanza ikakatika hatimaye ikaja ya pili Mariya na Merina wakiwa tayari kumsubiri baba yao bila matarajio, walipojaribu kufanya mawasiliano naye kwa njia ya simu ya upepo bado Fedorov hakupatikana wakaanza kuingiwa na wasiwasi kwani halikuwa jambo la kawaida na kibaya zaidi safari hiyo aliondoka peke yake bila ya mlinzi.
“Hivi unafikiri baba atakuwa wapi mpaka sasa?”

“Kwa kweli sijui ila tusubiri tuone pengine yuko njiani.”
“Mh! Nahisi hatari fulani ndani ya moyo wangu…,” aliongea Merina kwa sauti ya upole.
Hatimaye wakiwa katika kusubiri wiki ya tatu ikaanza kuyoyoma bila baba yao kutokea, wakaingiwa na hofu na kuamua kutoa taarifa za kupotea kwa baba yao katika vituo mbalimbali vya televisheni na redio lakini hata baada ya matangazo kutolewa mzee huyo hakuonekana.

Je, nini kitaendelea? Fedorov yuko wapi? Nini kimempata Lina?
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP. 103.

MWEZI mmoja ulikuwa umekatika tayari watoto Mariya na Merina wakiwa katika kusubiri, mioyo yao ikiwa na huzuni kubwa kupita maelezo, ni mlinzi wa nyumbani kwao na dereva aliyewaendesha ndiyo waliotoa faraja kwa watoto hao wakiwapa moyo kwamba ipo siku Fedorov angerejea na huko alikokuwa hakukuwa na tatizo lolote kwani kama lingekuwepo mpaka wakati huo wangeshapewa taarifa.
“Msiwe na hofu atarejea tu, huyu mtu ni mfanyabishara pengine ameshatoka huko na kuelekea nchi nyingine.”
“Lakini bila kusema kitu chochote?” Merina alihoji.

“Inawezekana anajua hakuna kitu kibaya.”
“Hapana mimi ninawaeleza wazi kabisa ipo sauti ndani ya moyo wangu inanieleza jambo fulani la hatari, lazima kuna tatizo,” Mariya aliongea akibubujikwa na machozi.
“Usilie nyamaza baba atarejea tu tena si muda mrefu.”
“Mimi nashauri tutoe taarifa polisi.”

”Juu ya nini?”
“Upoteaji wa baba yetu, mimi ninawaambia lazima atakuwa kwenye matatizo makubwa sana kama siyo kifo.”
“Mh!” Wote wakaguna kwa mshangao.
Baada ya maongezi hayo kwisha kila mmoja akionekana kuwa na msongo wa mawazo kichwani mwake, Mariya na Merina walinyanyuka na kuingia ndani ya chumba ambamo kwa takribani nusu saa nzima waliendelea kubaki huku wakiwaacha mlinzi na dereva waliokuwa wameketi bustanini wakiendelea kujiuliza maswali na ghafla wakiwa hapo wakawashuhudia tena watoto hao wakirejea.

“Dereva tafadhali tupeleke.”
“Wapi?”
“Kituo cha polisi.”
“Lakini tumepatana tuvute subira kidogo pengine yuko njiani anarejea.”
“Hapana tumeamua twende tu polisi.”
“Mh! Haya twendeni niwapeleke.”

“Naweza kuongozana nanyi?” mlinzi aliuliza.
“Hapana wewe baki tu hapa nyumbani tutarejea muda si mrefu.”
“Sawa.”
Wakatoka wakiongozana na dereva mpaka kwenye maegesho ya gari kisha wote wakafungua milango na kuingia ndani, Mariya na Merina wakiwa wameketi kiti cha nyuma na mara kadhaa wakiongea jambo fulani kwa kunong’ona.

Gari likaendeshwa mpaka sehemu kulikokuwa na kituo cha polisi, hapo wakashuka na kuingia moja kwa moja ndani wakimtaka dereva aendelee kusubiri eneo lilelile.
Wote wawili wakatembea na kuingia ndani ya kituo na kupokelewa na askari waliokuwa eneo hilo, kwa sababu ya umaarufu wao moja kwa moja wakaongozwa kuingia kwenye chumba maalum ambako walimkuta polisi akiwa ameketi akawakaribisha na kuwataka waeleze shida yao.
“Ahsante sana,” aliongea Merina ambaye kwa kumwangalia tu machoni mwake ungegundua alikuwa akilia.
“Kuna tatizo gani?” Polisi aliuliza.

“Ni mwezi sasa umepita hatujui baba yetu yuko wapi?”
“Tajiri Fedorov?”
“Hujakosea,” Mariya alijibu.
“Mh!” Polisi naye akaguna kuonyesha mshtuko, kwani historia ya mzee huyo ilifahamika nchini kote na kwa umafia wake aliogopwa na kila mtu.
“Tunahitaji kutoa taarifa hii kwenu ili msako ufanyike haraka sana na kufahamu ni wapi alipo baba yetu, juu ya malipo hakuna shida ilimradi tu apatikane.”

“Hata akiwa amekufa?”
“Tunahitaji maiti yake.”
“Basi hakuna shida tutafungua faili ambalo tutaandika malalamiko yenu kisha tutaanza msako na mnachotakiwa kufanya ni ninyi kutangaza kwenye vyombo vya habari vyote.”
“Hakuna shida tutaifanya kazi hiyo, tunachotaka sisi ni kumpata baba yetu basi!” walijibu watoto hao kwa kujiamini.

Baada ya kuhakikisha kwamba taarifa hiyo ilikuwa imefika jeshi la polisi, waliaga na kutoka nje wakitembea kuelekea lilipokuwa gari lao, wakapanda na dereva bila kusema kitu chochote akaliendesha moja kwa moja kuelekea nyumbani.
Jambo moja lilitawala vichwa vyao: ni wapi baba yao alikuwa na kama alikuwa amekufa maisha yao yangekuwaje baada ya hapo?
“Merina tunatakiwa tuanze kutangaza mara moja kwenye vyombo vya habari bila kuchelewa.”
“Kazi hii tutampatia huyu dereva azunguke kwenye vyombo vyote vya habari hata kama watahitaji fedha lakini watoe tangazo hili.”
“Hakuna shida.”

Nusu saa tu baadaye gari lilishafika nyumbani kwa tajiri Fedorov, lango likafunguliwa na dereva kuingiza gari ndani wakashuka na kumsabahi mlinzi wao na hawakusema tena kitu chochote wakatokomea na kuingia ndani.
Watoto hao waliendelea kubaki ndani ya chumba kwa zaidi ya saa tatu wakiongea mambo mbalimbali, hata mlango wa chumba chao ulipogongwa wakitakiwa kwenda kula waliendelea kugoma wakitoa agizo kwamba watu wengine waendelee nao wangejumuika baadaye.
Hata walipoitwa tena baada ya saa sita waliendelea kubaki chumbani na safari hii hawakusikika wakijibu kitu chochote zaidi ya ukimya tu.
“Mh! Wanafanya nini hawa?”

“Sijui hata wakiitwa hawaitiki.”
“Wasije kuwa wamechukua maamuzi mabaya.”
“Haiwezekani hebu tuchungulie dirishani.”
Mlinzi na dereva wakazunguka nyuma ya nyumba na kuelekea sehemu dirisha la chumba cha watoto hao lilipokuwa na walipojaribu kutupa macho yao ndani yalikutana na pazia zito likiwa limefunikwa kwenye dirisha hilo.
***
“Genevieve?” Phillip aliita kwa sauti ya upole.
“Bee baba!”
“Si kwamba napenda kulia mwanangu lakini…” kwikwi ya kulia ikamkaba tena Phillip akaangua kilio mbele ya mtoto wake.
“Tafadhali nyamaza na utueleze tatizo, nini kimetokea huko?” Magdalena aliyekuwa mfanyakazi wa ndani nyumbani kwa Phillip aliongea.


“Hali ya Lina ni mbaya sijui kama…” aliongea Phillip na kabla hajamalizia sentensi yake mlio wa simu ikiita ukasikika, taratibu akaingiza mkono wake mfukoni na kuichomoa haraka kisha akatupa macho kwenye kioo cha simu ili asome jina.
“Hospitali!” Alitamka Phillip kwa sauti ya juu.

Je, nini kinaendelea hapo? Simu iliyoingia ina ujumbe gani kwa Phillip? Fedorov, je, yuko wapi?
 
 
 
 
 
 
 
 MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP. 104


MSAKO nchini Urusi ulikuwa mkali kweli kweli polisi wakifanya kazi usiku na mchana kumsaka tajiri mkubwa nchini humo, Victor `Fedorov ambaye alitoweka katika mazingira ya kutatanisha, makundi kwa makundi yalikuwa yakigawanyika ambapo watu wengine walielekea sehemu ambako tajiri huyo alikwenda kwenye mchezo wa kuteleza katika barafu.

“Mkuu tumefika mpaka hapa lakini hakuna mtu wala hakuna taarifa yoyote ile inayoonyesha kwamba kuna uhai wa mtu na kwa mujibu wa mazingira hatukushudia kitu chochote kinachoonyesha uwepo wa mwanadamu,” ilikuwa ni sauti ya polisi mmoja katika kundi la polisi wasiopungua kumi waliotumwa kwenda kufanya uchunguzi eneo ambalo ndilo hasa Fedorov aliaga kwenda huko.
“Kitu gani kingine kimefanyika?”

“Tumejaribu kwa uwezo wetu wote kuangalia pengine hata nyayo na nguo ili kuridhika na upelelezi wetu lakini hatujafanikiwa kuona kitu.”
“Basi ni vyema mkarejea na kufanya mkakati mwingine.”
“Sawa mkuu.”
Simu ya upepo ikakatika na polisi wakajiandaa na kupanda ndani ya helikopta kisha kurejea jijini kwa mkakati mwingine.

***
Ndani ya chumba Mariya na Merina walikuwa wakipanga mkakati wa jinsi ya kumpata baba yao ambaye mpaka wakati huo hawakufahamu ni wapi alipokuwa na kama alikuwa mzima au la! Machozi na vilio vilitawala kila mmoja akionekana kumfariji mwenzake.
“Baba atakuwa amekufa.”
“Hapana usiseme hivyo.”

“Nahisi hivyo si kawaida yake hata simu tu?”
“Mh! Unasema kweli kwa jinsi anavyotupenda haiwezekani hata kidogo.”
“Ngoja tuone uchunguzi wa polisi utasema nini?”
“Hapana Merina ni muda mrefu sana…yapata miezi mitatu sasa lazina kuna tatizo mimi ninakuambia...”

Mariya aliyekuwa ameketi kimya kitandani bila kujibu kitu machozi yakaonekana yakimbubujika, kichwani mwake hakupata picha kama kweli baba yao mpendwa angekuwa amekufa maisha bila yeye yangekuwaje? Ilikuwa ni picha ya kuumiza sana hakumfahamu mtu mwingine zaidi ya mlinzi na dereva waliyekuwa naye wakati huo.
“Kama ikitokea mzee asionekane nini kitatokea katika maisha yetu?”
“Kwa kweli sijui na hatukuwahi kumfahamu ndugu mwingine yeyote na kama sijakosea baba alitueleza kwamba mama yetu alifariki miaka mingi sana hivyo yeye ndiye alikuwa kila kitu.”

“Sawa kabisa, kitu alichokuwa amekiongea Mariya kilikuwa ni ukweli, hawakufahamu ni kitu gani kingeendelea kwao, maisha yangekuwaje na ndugu wengine wangewafahamu vipi kwani Fedorov hakutaka kuwaeleza ukweli.
“Lakini lazima kuna sehemu baba atakuwa ameandika kitu fulani hivi kweli hana ndugu?”
“Wewe hivi unamjua vizuri baba?”
“Namjua hebu…,” aliongea Merina akinyanyuka kitandani na kuanza kutembea kuelekea mlangoni akitoa ishara ya kumwita Mariya.
“Twende huku.”

“Wapi?”
“Wewe twende tu utaona ninachotaka kwenda kufanya.”
Baada tu ya kutoka ndani ya chumba chao wote wawili wakapiga hatua tatu kusonga mbele ambako macho yao yalikutana na mlango wa kioo hicho ndicho kilikuwa chumba cha baba yao.
“Tuingie huku chumbani.”
“Kufanya nini wakati ni chumba cha baba?”

‘Wewe nifuate mimi acha ubishi wako.”Haraka bila kujiuliza mara mbili wakaufungua mlango na kuzama ndani Mariya akionyesha hofu kubwa.
Kwa saa tatu mfululizo waliendelea kubaki ndani ya chumba cha mzee wao wakifanya upekuzi kila kona kusoma na kutafuta mahali ambako wangegundua kuwepo kwa nyaraka zozote za siri ambazo zingewazesha kupata angalau ndugu mmoja upande wa baba au mama yao. Lakini bado hawakufanikiwa mwisho nao wakaanza kukata tamaa kabisa lakini ghafla wakiwa hapo wakakumbuka kwamba walifanya upekuzi kila mahali na walikuwa wamesahau sehemu moja tu ndani ya chumba hicho kabati kubwa lililokuwa pembeni kabisa mwa chumba.

“Bado hili kabati hapa.”
“Ehhe kweli tulisahau.”
Wote wakakimbia kulielekea kabati hilo na kufungua mlango mmoja baada ya mwingine kupekua ndani wakitoa nyaraka moja baada ya nyingine na kuzisoma lakini bado hawakuona sehemu yoyote ambayo iliandikwa kuonyesha kama Federov alikuwa nani na alitokea wapi akiwa na ndugu wangapi.

“Mh! Mimi mwenzako nimechoka.”
“Basi pumzika mimi niendelee lazima tupate kitu humu ndani ya hili kabati vinginevyo sitatoka hapa,” aliongea Merina akiangusha vitu kutoka ndani ya kabati bila kujali.
“Mh!” Merina aliguna.

“Nini?”
“Hili kabrasha ni la nini?”
“Hebu? Tena la rangi nyekundu?”
“Fungua ndani tuone,” Mariya aliongea na taratibu akasogea karibu kushuhudia ni kitu gani kingeonekana ndani yake.

Je, watoto hao watakutana na kitu gani ndani ya kabrasha hilo?
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.....EP. 105

Walikuwa wawili tu ndani ya chumba lakini kila mmoja alionekana kuwa na hofu, walitaka kufahamu ni kitu gani kilikuwa ndani ya kabrasha hilo na kibaya zaidi lilikuwa la rangi nyekundu na juu yake maneno “Nyaraka muhimu” yalisomeka.
“Mh! Kwa nini maneno hayo?”
“Hata mimi sijui ila ngoja tufungue tuone.”
“Mimi naogopa sana.”
“Acha woga tunachotaka kufahamu sisi ni ndugu wa baba au upande wa mama yetu ambaye hatukuwahi kumfahamu.”
“Haya fungua,” Mariya alizidi kusisitiza.
Wakatembea na kuketi juu ya kitanda hapo wakiwa tayari kufungua kabrasha hilo na kwa ujasiri wa hali ya juu walilifungua na kuliacha wazi, kitu cha kwanza walichokishuhudia kilikuwa ni vyeti vilivyofungwa vizuri na vilivyoonyesha majina yao.
“Majina yetu haya.”
“Mh!” pacha mmoja aliguna na kuonyesha mshangao.
Wakaendelea mbele zaidi kufunua katarasi nyingine, hapo walikutana na wosia mzito wa Victor Federov ukieleza kwamba yeye alikuwa nani na alitokea wapi, alizaliwa miaka mingapi iliyopita, haukuishia hapo ukaendelea mbele zaidi akitaja mali zote alizokuwa nazo na kiasi chote cha fedha alizokuwa nazo katika benki mbalimbali nchini Urusi, majengo makubwamakubwa na miradi mbalimbali na alitaka vitu hivyo vyote chini ya mwanasheria aliyekuwepo ndani ya wosia huo kama siku ikitokea akafa basi utajiri wote huo uende kwa watoto wake.
Maneno yale yalichoma mioyo ya watoto hao, machozi mfululizo yakawabubujika wakilia na kuomboleza kwani mpaka wakati huo pamoja na kwamba walishatoa taarifa katika vyombo vya habari na taarifa nyingine kuzipeleka kwenye vyombo vya habari wakimtafuta baba yao kwa udi na uvumba, alikuwa bado hajapatikana.
“Nahisi hatari fulani.”
“Mimi pia naungana na wewe.”
“Ni kwa nini baba aliamua kuandika kitu kama hiki? Je, alifahamu kwamba atakufa muda si mrefu? Na huyu mwanasheria ni nani?” walijiuliza maswali mfululizo.
Huzuni ilikuwa imewagubika lakini pamoja na yote hayo bado hawakutaka kuacha kusoma nyaraka zote zilizokuwa ndani ya kabrasha hilo wakitaka kufahamu zaidi siri zilizokuwa ndani.
“Historia kamili ya watoto Mariya na Merina ilipoanzia mpaka hapa walipo leo, jinsi walivyopatikana na nani hasa alikuwa ni mama yao mzazi” maneno hayo yalisomeka kwenye moja ya karatasi ndani ya kabrasha.
“Mh!” wakaguna.
Wakaendelea mbele zaidi na kukutana na jina Genevieve huyo ndiye alikuwa mama yao wa kuwazaa lakini mwanamke huyo aliolewa na mwanaume aliyeitwa Phillip na waliishi nchini Tanzania.
Maswali mengi yaliendelea kuzunguka ndani ya vichwa vyao wakitaka kufahamu ukweli wa historia yao lakini kwa wakati huo hakuwepo mtu ambaye angewaeleza ukweli, mtu pekee waliyemtengemea alikuwa ni Victor Fedorov.
“Baba anajua ukweli wote na sasa hayupo, hebu tuendelee mbele zaidi tutajua tu,” aliongea Merina akionyesha msisitizo.
Kadiri walivyozidi kusonga mbele ndivyo mambo mengi makubwa yalivyoibuka na kuzidi kuwaacha midomo wazi bila kupata ufafanuzi wowote.
“Mama yetu aliitwa Genevieve?”
“Historia inaonyesha tulipatikana kwa kupandikizwa katika chupa?”
Bado watoto hao waliendelea kujiuliza maswali mengi kichwani mwao huku huzuni ikigubika ndani ya mioyo yao, hakika walikuwa wamesoma kitu ambacho mpaka wanafikisha umri wa miaka kumi na nane hawakufahamu ukweli wa jambo lolote zaidi sana Fedorov ndiye alikuwa kila kitu.
“Ni lazima tuzungumze na huyu mwanasheria pengine anaweza kutusaidia zaidi.”
“Umeongea jambo la maana sana.”
“Lakini kabla ya yote tusubiri kwanza tuone taarifa za polisi zitasemaje kuhusu baba yetu.”
Hivyo ndivyo walivyokubaliana na waliamua kusubiri kwa muda mpaka miezi sita baadaye lakini bado Fedorov alikuwa hajapatikana nao pia wakaamini kabisa kwamba huenda baba yao alikufa katika mchezo wa barafu na maiti yake kufukiwa na theluji.
Wakiwa wenye majonzi mioyoni mwao, walipanga kukutana na mwanasheria ambaye alikuwa kwenye nyaraka za Fedorov ili kuongea na kufahamu ukweli wa mambo yote.
Waliamini huyo angeweza kuwasaidia kwa mambo yote muhimu na kufahamu zaidi utajiri wa baba yao, ni kweli wakafanikiwa kuonana naye na kuongea naye akawaambia alikuwa ameshtushwa na habari za kupotea kwa Fedorov lakini akawaahidi kwamba angefuatilia kwa karibu majibu ya polisi na angekuwa nao bega kwa bega.
“Tunakushukuru kwa kila kitu lakini jambo moja tunaomba kutoka kwako.”
“Hakuna shida.”
“Pamoja na kwamba hivi sasa sisi ni watu wazima lakini tunahitaji uendelee kuwa mshauri na msimamizi wa mali za baba yetu.”
“Niko tayari,” mwanasheria huyo aliongea kwa kujiamini.
Wote kwa pamoja wakasimama na kumshika mkono huku wakimtaka kuwa karibu yao na kushirikiana naye kwa kila jambo, wakamshukuru na kuondoka kurejea nyumbani.
“Wiki ijayo lazima tufunge safari kuelekea Tanzania tukamwone huyo anayedaiwa kuwa mama yetu,” Mariya aliongea na Merina akamuunga mkono.
Maandalizi maalum yakafanyika na utaratibu ulipokamilika Mariya na Merina wakasafiri kuja Afrika ya Mashariki nchini Tanzania, hamu yote ikiwa ni kuwafahamu watu wawili Phillip na mkewe Genevieve, pamoja na kugundua ukweli wote wa jinsi walivyopatikana, walitamani kuwaona watu hao wakiamini kabisa kwamba walikuwa ni watu muhimu mno katika maisha yao.
***
“Haraka mpelekeni chumba cha wagonjwa mahututi na afungiwe mashine ya hewa ya oksijeni imsadie kupumua,” ilikuwa ni sauti ya daktari mmoja ndani ya wodi aliyekuwa akimhudumia Lina.
“Kimetokea nini?”
“Hali yake imebadilika ghafla, kwa inavyoonekana ana tatizo kubwa ndani ya kichwa chake ambalo linamsumbua.”
“Mungu wangu na mume wake ameondoka sasa hivi kwenda nyumbani,” muuguzi aliongea.
“Kama ana simu apigiwe haraka sana arudi hapa mara moja,” daktari alizidi kusisitiza.
Muuguzi akachukua faili lililokuwa na kumbukumbu za Lina, hapo akakutana na namba ya mumewe Phillip, haraka bila kuchelewa akakimbia mpaka mapokezi ambako aliomba msaada wa kupigiwa namba hiyo.
Haikuchukua hata dakika mbili tayari namba hiyo ikawa imeita.
“Hallow, ndiyo hapa ni hospitali tunahitaji urejee haraka sana, hali ya mke wako ni mbaya na hivi sasa ninavyoongea na wewe tunajiandaa kumpeleka chumba cha wagonjwa mahututi…,” aliongea muuguzi huyo na simu ikakatika.

Je, nini kitaendelea?mzigo unaendelea kesho km kawa! love u all mwaaa!!gudnite!!!

 
 
 
 
 
 

MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 106

“Haraka mpelekeni chumba cha wagonjwa mahututi na afungiwe mashine ya hewa ya oksijeni imsaidie kupumua,” ilikuwa ni sauti ya daktari mmoja ndani ya wodi aliyekuwa akimhudumia Lina.
“Kimetokea nini?”
“Hali yake imebadilika ghafla kwa inavyoonekana ana tatizo kubwa ndani ya kichwa chake ambalo linamsumbua.”
“Mungu wangu na mume wake ameondoka sasa hivi kwenda nyumbani,” muuguzi aliongea.
“Kama ana simu apigiwe haraka sana arudi hapa mara moja,” daktari alizidi kusisitiza.
Muuguzi akachukua faili lililokuwa na kumbukumbu za Lina hapo akakutana na namba ya mumewe Phillip, haraka bila kuchelewa akakimbia mpaka mapokezi ambako aliomba msaada wa kupigiwa namba hiyo.
Haikuchukua hata dakika mbili tayari namba hiyo ikawa imeita.
“Hallow, ndiyo hapa ni hospitali tunahitaji urejee haraka sana hali ya mke wako ni mbaya na hivi sasa ninavyoongea na wewe tunajiandaa kumpeleka chumba cha wagonjwa mahututi…,” aliongea muuguzi huyo na simu ikakatika.
“Wiki ijayo safari kuelekea Tanzania ni lazima, tukamwone huyo anayedaiwa kuwa mama yetu,” Mariya aliongea na Merina akamuunga mkono.
Maandalizi maalum yakafanyika na utaratibu ulipokamilika Mariya na Merina wakasafiri kuja Afrika ya Mashariki nchini Tanzania, hamu yote ikiwa ni kuwafahamu watu wawili, Phillip na mkewe Genevieve pamoja na kugungua ukweli wote wa jinsi walivyopatikana, walitamani kuwaona watu hao wakiamini kabisa kwamba walikuwa ni muhimu mno katika maisha yao.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO...

Taarifa walizokuwa wamezisoma Mariya na Merina kwenye kabrasha la siri la baba yao, hakika lilikuwa limewatia simanzi kubwa ndani ya mioyo yao, pamoja na kwamba waliufahamu ukweli wote lakini watoto hao walihitaji kumwona mama yao na mtu mwingine aliyekuwa ametajwa ndani ya nyaraka hizo aliyejulikana kama Phillip, walitamani kufika nchini Tanzania kwa gharama yoyote ile ilimradi tu wakutane na watu hao.


Maandalizi yakafanyika haraka chini ya Mwanasheria wao wa familia ambaye ndiye alisimamia kila kitu na safari nzima ya watoto hao akihakikisha kwa fedha zilizokuwepo wangeweza kusafiri salama na kurejea salama bila matatizo yoyote yale.
“Mariya lakini huyu ndiye baba yetu mzazi,”
“Ni kweli kabisa hilo sina shaka nalo tatizo moja tu linakuja ni kwa nini baba hakuwa mkweli kwetu?”


“Pengine alifahamu tukipata habari hizo tutaumia kwani kwa maelezo yaliyotolewa ni kwamba baba aliuza mbegu zake za kiume kwa familia ya Phillip ambazo zilipandikizwa kwa mwanamke aliyeitwa Genevieve huyo ndiye mama yetu lakini pia Phillip ni mtu muhimu kwetu ni kama baba ni lazima twende haraka, nakumbuka kuna wakati baba aliwahi kutueleza kwamba mama yetu alikufa, hivi inawezekana kweli?”
“Inawezekana hawezi kusema uongo kama huo,”


“Twende mambo mengine yote tutayajua huko huko?”
“Tutafanya nini ili kuwafahamu watu hao?” Mariya alimuuliza Merina.
“Tutatumia vyombo vya habari kutangaza na ikiwezekana kuzungumza kabisa na vyombo hivyo,” Merina alijibu.
“Kivipi?”Mariya alihoji.


“Fedha ni kila kitu kwetu,” Merina aliongea kwa kujiamini.
Hivyo ndivyo walivyomaliza mazungumzo yao na kuanza kujitayarisha kwenda Afrika wakiwa hawaelewi kabisa ni wapi baba yao alipokuwa na alipatwa na kitu gani lakini walilazimika kufanya hivyo kwa sababu ya nyaraka za siri walizozisoma. Mioyo yao iliuma mara kadhaa walipomkumbuka baba yao, ucheshi,utani na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo kwao hakika kwa wakati huo vilikuwa vimekosekana.


“Mimi naona ni bora tukaondoka na huyu mwanasheria wetu ili akasaidie mchakato huu.”
“Mh! Wazo zuri sana hebu tumpigie simu naye afanye maandalizi ili kesho jioni tuweze kuondoka.”

Wakafanya kama walivyokubaliana simu ikapigwa na mwanasheria kupewa taarifa kwamba safari iliyokuwepo mbele yao ililazimu kuongozana nao kwa gharama yoyote.
Hivyo ndivyo walivyofanya siku iliyofuata safari ikaanza, hamu yao kubwa ikiwa ni kuwafahamu watu hao wawili, Phillip na Genevieve, walitamani kuongea nao ili kufahamu ukweli juu ya nini kilichotokea.


Safari yao ilisadikiwa kuchukua saa nane mpaka kufika nchini Tanzania ambako wangefanya utaratibu maalum wa kuwapata walengwa ambao walikuwa ni Phillip na Genevieve.
***
Simu iliyokuwa imeingia kwa Phillip ikimtaarifu kwamba alitakiwa kufika hospitalini mara moja ilikuwa imemchanganya kupita maelezo, akiwa hapo alihisi hatari na kuiona taa nyekundu ikiwaka ndani ya kichwa chake.


“Lina! Lina atakuwa amezidiwa,” hivyo ndivyo alivyoongea huku akitweta na bila kuchelewa aliwaaga bibi Magdalena na mtoto wake Genevieve waliokuwa pembeni yake akiwaambia wazi kwamba alitakiwa kurejea hospitalini haraka sana.
“Twende wote baba,” Genevieve aliongea.
“Hapa…,” alijibu Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake bibi Magdalena aliingilia.
“Ni lazima tuongozane nasi tufahamu nini kimetokea huko, hatuko tayari kubaki hapa nyumbani, sawa?”
“Mh! Unajua.”


“Phillip hakuna haja ya mabishano hapo Genevieve hebu twende…,” bibi Magdalena aliongea akimvuta Genevieve kuelekea kwenye gari.
Wote wakaingia ndani na Phillip akiwa ndiye dereva alionekana kuwa mtu mwenye msongo mwingi wa mawazo lakini hayo ndiyo yalikuwa maisha hakuwa na mtu mwingine wa kumsaidia tatizo lililokuwa mbele yake, kwa kasi ya ajabu akaliendesha gari hatimaye akafanikiwa kufika hospitali ndani ya dakika kumi na tano tu.


Haraka akaegesha gari sehemu maalum na kushuka mbio bila kusema chochote kuelekea chumba ambacho ndicho hasa Lina alilazwa, Genevieve na Magdalena wakimfuata kwa nyuma nao pia wakionekana wenye wasiwasi mwingi.


Dakika tano tu baadaye alifanikiwa kufika kwenye wodi hiyo lakini alishangazwa na ukimya uliokuwepo eneo hilo, bila kuuliza wala kusubiri akausukuma mlango na kuzama ndani, kitanda kilikuwa kitupu.
“Nini kimetokea?” alijiuliza na ghafla akiwa katika kujiuliza muuguzi aliingia ndani ya wodi hiyo.
“Dada! Dada!” aliita mfululizo.
“Ndiyo kaka yangu nakusikiliza.”
“Nauliza mgonjwa aliyekuwa amelazwa hapa muda mchache tu, anaitwa Lina.”


“Lina?”
“Ndiyo.”
“Mh!” badala ya kujibu muuguzi aliguna.
“Kwa nini unaguna dada?” aliuliza Phillip akimwangalia muuguzi machoni na kugundua kitu tofauti.
“Ah! Hebu subiri kidogo.”
“Dada mbona sikuelewi tafadhali nieleze nini kimetokea hapa?” Phillip aliuliza akionyesha msisitizo.


“Kaka hali ya mgonjwa imebadilika ghafla kwa ujumla ni mbaya…,” aliongea muuguzi huyo lakini hakumaliza sentensi yake mlango ukafunguliwa kwa nguvu.
“Monica!” ilikuwa ni sauti ya kiume ikiita ndani ya wodi.
“Bee!” aliitika muuguzi huyo.
“Unagonja nini tunasubiri hilo faili haraka?”


“Sawa daktari lakini kuna huyu kaka hapa anauliza kuhusu mgonjwa Lina.”
“Hebu nifuateni nyuma haraka,” daktari huyo aliongea na wote wakaanza kutoka mbio kumfuata kwa nyuma.
Hawakupiga hata hatua kumi mbele ya mlango uliokuwa umeandikwa ICU walishuhudia machela ikitolewa kwa mwendo wa kasi kupelekwa sehemu ambayo hawakuielewa, Phillip alikuwa wa kwanza kutupa macho juu yake na kumwonga Lina akiwa amelala kimya mdomoni mwake akiwa amefungwa mashine ya oksijeni.
“Mke wangu!” aliongea kwa sauti ya juu.


“Hali yake ni mbaya tunajaribu kuokoa maisha yake imetulazimu kumpeleka chumba cha upasuaji haraka sana…” aliongea daktari huku machela ikisukumwa kuingizwa ndani ya chumba cha upasuaji, Phillip, Genevieve pamoja na Magdalena wakitakiwa kubaki hapo kusubiri.
 
 
 
 
 
 
 
 
SICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 107

Baada ya Lina kuingizwa chumba cha wagonjwa mahututi, uchunguzi maalum uliendelea na Phillip ndiye aliyetakiwa kutoa historia ya mkewe kwani kwa wakati huo hakuwa akijitambua. Akawa tayari kueleza kila kitu kilichomtokea mkewe ikiwepo ajali ya moto aliyoipata baada ya gari lake kuwaka moto.
Katika kufanya uchunguzi kuwa rahisi, jopo la madaktari likaanza kazi, na ni hapo ndipo walipogundua kwamba jeraha la moto alilolipata Lina lilileta madhara makubwa sana kwa ndani, madhara ambayo hayakufahamika mapema hivyo walitaka kujaribu kumsaidia kwa kumfanyia upasuaji ili kuondoa tatizo lililoonekana ndani ya kichwa.
Wakiwa katika hali ya kusubiri kuona kama angerejewa na fahamu zake ili kukamilisha vyema uchunguzi wao, hali ya Lina ilibadilika ghafla, ni hapo ndipo walipolazimika kumkimbiza chumba cha upasuaji ili kuokoa maisha yake.
“Hali yake ni mbaya tunajaribu kuokoa maisha yake imetulazimu kumpeleka chumba cha upasuaji haraka sana…,” aliongea daktari huku machela ikisukumwa kuingizwa ndani ya chumba cha upasuaji, Phillip, Genevieve pamoja na Magdalena wakitakiwa kubaki hapo kusubiri. Hayo yalikuwa maneno pekee aliyotamka daktari na kuingia ndani ya chumba.
Walibaki nje ya chumba wakionyesha hofu kubwa, Phillip yeye alishindwa kujizuia akajikuta akitokwa na machozi.
“Baba usilie mama atapona tu,” Genevieve aliongea akimpigapiga baba yake.
“Najua atapona lakini…” kwikwi ya kulia ikamkamata Phillip binafsi ndani ya moyo wake kwani aliufahamu ukweli kwamba Lina alikuwa katika hali ya kufa kwani ripoti ya uchunguzi iliyokuwa imefanyika ilionyesha wazi kwamba alikuwa na tatizo kubwa ndani ya kichwa chake na tayari lilikuwa limechelewa kupata ufumbuzi.
Kwa muda wa saa nne mfululizo waliendelea kusubiri, hamu yao kubwa ikiwa ni kufahamu ni kitu gani kiliendelea ndani ya chumba cha upasuaji, macho na masikio yao yote yalielekea kwenye mlango wa chumba kuangalia na kusikiliza.
“Mbona wamechukua muda mrefu sana,” aliuliza Phillip.
“Inawezekana bado wanafanya upasuaji.”
“Mh!”
“Hebu tuvute subira kidogo tuangalie,” Magdalena aliongea akijaribu kumpa Phillip moyo wa matumaini.Waliendelea kusubiri saa nyingine mbili na kufanya idadi ya saa kutimia sita lakini bado hawakuona muuguzi wala daktari akitoka ndani ya chumba hicho, wakaanza kukata tamaa na mioyo yao kuhisi kuna jambo la hatari lilikuwa limetokea na taa nyekundu iliyoashiria hatari ikawa kichwani mwa Phillip.
“Lazima kuna tatizo siyo rahisi,” aliongea Phillip akitembea kusogelea mlango wa chumba cha upasuaji, akapiga hatua tatu mbele lakini kabla hajanyanyua hatua ya nne mlango wa chumba hicho ukaonekana ukifunguliwa na mwanaume aliyevalia koti jeupe akatokeza, Phillip alipomwangalia alimgundua kwamba alikuwa ni daktari hivyo wakajikuta wakigonganisha macho na daktari akainama chini.
Taratibu akionekana mwenye huzuni akamsogelea Phillip kisha akamsabahi na kumtaka kuongozana naye mpaka ofisini kwa maongezi zaidi.
Ndani ya ofisi tu baada ya kuingia daktari hakutaka kupoteza muda zaidi alimtaka Phillip aketi kwenye kiti naye akaketi, ni hapo ndipo alipomweleza ukweli ambao alitakiwa kuufahamu.
“Pole sana ndugu yetu, sisi kama madaktari pamoja na wauguzi tumejitahidi kadiri ya uwezo wetu wote kuokoa maisha ya mke wako lakini imeshindi…”
“Lina wangu amefariki?” Phillip alitamka kwa sauti akinyanyuka kitini.
“Wewe ni mwanaume hebu jikaze kidogo kwani hayo ndiyo maisha yetu.”
“Daktari! Daktari unamaanisha unachosema?”
“Ni kweli tupu mkeo amefariki dunia akiwa juu ya kitanda cha upasuaji muda mfupi tu baada ya kupasua kichwa chake.”
“Uwiii!Uwiiii!” Phillip alipiga mayowe akiwa hataki kuamini maneno aliyoyasikia kutoka kwa daktari kwamba mkewe mpendwa alikuwa ameaga dunia.
“Huo ndiyo ukweli wote, tunasikitika sana lakini pia tunakupa pole.”
Phillip hakujibu kitu tena akanyanyuka kwenye kiti akaufungua mlango na kutoka mbio kuelekea chumba cha upasuaji huku akilia kwa sauti ambayo ndiyo iliyowashtua Genevieve na Magdalana waliokuwa wameketi nje ya wodi wakimsubiri.
“Lina hayupo nasi tena, ameondoka ametuacha” aliongea Phillip huku akilia.
“Lina amefariki?”
“Huo ndiyo ukweli hatutamwona tena,” wakiwa hapo wakashuhudia mlango ukifunguliwa na machela iliyoonekana kubeba mtu juu yake akiwa amefunikwa kwa shuka la rangi ya kijani kuanzia kichwani hadi miguu ikapitishwa mbele yao.
“Mke wangu! Huyu ni mke wangu nataka nimwone, Lina wangu kweli umeniacha kama alivyoniacha Genevieve?” Phillip alilia kwa uchungu akitamka maneno ya kuumiza moyo. Wakiwa hapo huku wote wakilia wakashuhudia machela ikisukumwa na kupelekwa chumba cha maiti.
Huku wakiwa na uchungu mioyoni mwao wakaondoka kurejea nyumbani ili kufanya taratibu nyingine, taarifa mbalimbali zikatolewa juu ya tukio hilo, simu nyingi zilipigwa na watu wengi walifika nyumbani kwa Phillip kumpa pole na kuomboleza, wengi wao wakiwa wafanyakazi waliofanya kazi na Lina ofisi moja.
Siku tatu zikatolewa kwa maombolezo, watu wakilia wengi wakisikitikia kifo kilichomkuta Lina. Familia za Phillip na Lina zikajumuika pamoja hatimaye mazishi yakafanyika Phillip akitaka mkewe huyo azikwe pembeni tu mwa kaburi la mkewe wa kwanza na watoto wake. Jambo hilo likafanikiwa na Lina akazikwa akiwaacha watu wengi katika majonzi, kwa Phillip ikionekana kuwa kama ndoto lakini huo ndiyo ulikuwa ukweli.
Ni wiki moja tu baada ya Phillip kumzika mkewe mambo yalianza kubadilika, mara kadhaa akionekana kama mtu aliyekuwa na tatizo la akili na alipoulizwa hakuwa na jibu la kutoa zaidi ya kububujikwa na machozi, kazini nako mambo hayakwenda sawa hivyo wakalazimika kumpa likizo ya muda akae nyumbani pengine akili yake ingetulia.
Ni kama vile uamuzi huo walikuwa wameukosea, kwani Phillip badala ya kubadilika hali ndiyo ikazidi kuwa mbaya, akawa mlevi kupindukia na kuongea peke yake, jambo lililozidi kuishangaza familia yake.
“Baba kwa nini umekuwa hivyo?” Genevieve aliuliza. Alikuwa ni mtoto mdogo lakini alikuwa na upeo wa kufahamu mazuri na mabaya.
“Dunia hainitendei haki, ilichukua mke na watoto wangu wawili na sasa imegeuka na kumchukua Lina… ni bora na mimi niwafuate na kuungana nao, bora nife…nasem…” aliongea huku kwikwi ya kulia ikimkaba, haraka akanyanyuka kutoka kitini na kukimbia kuelekea chumbani.
“Baba!Baba!” mtoto Genevieve alikimbia kumfuata baba yake lakini tayari alishachelewa aliposhika mlango ili ausukume kuingia ndani ulionekana kufungwa.
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 108

Genevieve aliendelea kugonga mlango kwa muda bila baba yake kuitikia, naye pia akaanza kulia akimwita bibi Magdalena aje ili waungane kusaidia kumfanya Phillip afungue mlango. Kwa muda wa nusu saa nzima bado walisimama nje ya mlango wakimsihi Phillip afungue lakini hakufanya hivyo zaidi sauti ilisikika kutoka ndani ya chumba ikiwaeleza wazi kwamba alitaka kufanya uamuzi mgumu hivyo alihitaji nafasi.
“Phillip lakini ni vyema ukatambua kwamba maisha baada ya kifo cha mkeo ni lazima yaendelee.”
“Najua hilo tangu mwanzo lakini inauma, ni bora nikaungana nao.”
“Usimkufuru Mungu na huyu mtoto?”
“Mtoto? Ah! Atapata wasamaria wema wengine wa kumtunza.”
“Baba! Baba!” Genevieve aliita na kwikwi ya kulia ikamkaba, hakuongea tena kitu akatoka mbio eneo hilo na kukimbilia ndani ya chumba kisha naye kujifungia.
Ukawa ni mtihani kwa bibi Magdalena hakufahamu nini afanye kwani kila kitu kilionekana kwenda kombo, kwa muda aliendelea kusimama eneo hilo akitafakari nini cha kufanya hatimaye wazo likamjia ndani ya kichwa chake kwamba ni lazima Phillip akubali kushuka kwani hali ya Genevieve ilikuwa mbaya kutokana na sentensi aliyokuwa ameitamka muda mfupi uliopita.
“Genevieve ameumizwa na kauli yako, hivyo amekimbia kuelekea chumbani, kwa ujumla ameumia.”
“Unasema?”
“Hivyo ndivyo, tafadhali nakusihi utoke na kumwendea ili kumbembeleza.”
Ukimya wa ajabu ukatokea na sekunde tatu tu mlango wa chumba ukaonekana ukifunguliwa na Phillip kutokeza huku jasho jingi likitiririka mwilini mwake, hakusema kitu zaidi ya kukimbia kuelekea upande ambako ndiko chumba cha Genevieve kilikuwepo. Akausukuma mlango na kuingia ndani ya chumba na kilichosikika muda mfupi tu ndani ya chumba hicho ni kilio, wote wawili walikuwa wakilia.
***
Ndani ya hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam ndimo Mariya, Merina na Mwanasheria wao walipokuwa wamefikia hapo ndipo pangekuwa nyumbani kwao kwa muda wote ambao wangekuwa Afrika, nchini Tanzania kusaka ukweli wa maisha ya baba yao Victor Federov kwa gharama yoyote ile.
“Tutapumzika leo na kesho tutaanza mchakato, lazima kwanza tuitishe mkutano na waandishi wa habari lakini kabla ya hayo tunahitaji kukutana na mtu mmoja ambaye tutamfanya rafiki huyo ndiye atatusaidia.”
“Mh! Naona kama ni zoezi gumu kidogo,” Mariya.
“La hasha! Ni kitu rahisi nitampata mtu hapa hapa hotelini,” mwanasheria aliwaambia.
“Haya ngoja tuone lakini pia uwe makini kwani hapa tupo ugenini,” Mariya alishauri.
“Usiwe na shaka Mariya kila kitu kitakwenda sawia.”
Baada ya mazungumzo hayo kukamilika pamoja na kwamba alikuwa ni mgeni kabisa, Morgan alitoka ndani ya hoteli hiyo kuangalia mazingira akitafuta ni namna gani angepata msaada ambao ungemsaidia kufanya kazi yake kwa urahisi, kwa kutumia lifti akashuka mpaka mapokezi hapo akawasabahi watu aliowakuta na ghafla kabla hajapiga hatua kutoka nje ya hoteli hiyo macho yake yakagongana na mtu aliyekuwa ameketi pembeni kabisa mwa hoteli hiyo mkononi akiwa na gazeti lililosomeka Uwazi, akapata hamu ya kusogea karibu yake ili aongee naye mambo kadhaa kwake hiyo akaiona kama bahati.
“Habari?” alisabahi kwa lugha ya Kiingereza.
“Nzuri tu,”
“Ah! Naitwa Morgan natokea Urusi.”
“Oh! Karibu mimi naitwa Erick Evarist naishi hapa hapa Tanzania,” Erick alijitambulisha.
“Naweza kuungana na wewe hapa?”
“Bila shaka karibu.”
“Napenda kukufahamu zaidi.”
“Ni mwandishi wa habari nafanya kazi zangu kwenye Kampuni ya Global Publishers.”
“Oh! My God!” Morgan alipaza sauti na kuwafanya watu wote waliokuwa eneo hilo kuacha shughuli zao wakabaki kumshangaa. Erick naye akashindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kinatokea eneo hilo.
Kabla hajaendelea kusema chochote, Morgan akamwomba Erick wasogee pembeni ili waweze kuongea zaidi.
“Hakuna shida,” Erick aliongea akimfuata mwanaume huyo na wote wakaketi kwenye viti vilivyokuwa hapo na mazungumzo maalum yakaanza, Morgan akimweleza wazi kwamba alifurahi kukutana naye na kazi iliyokuwa imemleta nchini Tanzania ni kutaka amsaidie kwa kila kitu na kama angehitaji kiasi chochote cha fedha angekuwa tayari kumpatia lakini tu amsaidie.
Hakuficha kitu akaweka kila kitu wazi kwamba walikuja nchini hapo kutafuta ukweli wa mwanaume aliyeitwa Phillip na mkewe Genevieve na hawakuwa na msaada wowote.
“Niko tayari kukusaidia.”
“Kivipi?”
“Nitakusaidia ufanye kitu kinachoitwa Press Conference, utakutana na waandishi wa habari ambao nitaongea nao kuwaeleza shida yako halafu utatakiwa kufanya kikao cha pamoja kisha kupiga picha ili kuandika habari hizo kwenye magazeti yetu, watu wakisoma naamini utapata ufumbuzi wa tatizo lako.”
“Inaweza ikachukua muda gani kuanzia sasa?”
“Kazi hiyo nitaifanya leo na kesho nitakupa majibu,”
“Tutakutana wapi?”
“Nitakuja hapa hapa hotelini lakini ni vyema ukanipatia namba yako ya simu ili iwe rahisi kuwasiliana na wewe.”
“Ahsante rafiki, wewe kwangu ni kama malaika, chukua hii,” aliongea Morgan akichomoa kadi yake yenye namba za simu na kumkabidhi Erick ambaye aliipokea, wakaagana wakiahidiana kukutana tena kesho yake.
Baada tu ya Erick kuondoka eneo hilo, Morgan alipandisha lifti haraka kwenda chumbani kwa akina Marina kuwaeleza kila kitu. Mariya na Marina walifurahi sana kupewa habari hizo njema.
“Mungu yupo pamoja nasi, naona mwanzo umekuwa mzuri,” Mariya aliwaambia.
“Tena tutakapofanikisha jambo hili itabidi tukamtolee shukurani ya pekee,” Marina aliunga mkono.
Wakiwa pale hotelini, waliona saa zinachelewa ili kuifikia siku iliyofuata ambayo mwanasheria wao angekutana na Erick na kumpa utaratibu wa mkutano wao na waandishi wa habari ambao ungemaliza kazi iliyowaleta Tanzania.
Kama walivyokuwa wamepanga kesho ikawadia, Morgan akiwa tayari kumsubiri Erick afike ili waendelee na mazungumzo yao na kuona walikuwa wamefanikiwa kwa kiasi gani kuhusu shughuli iliyokuwa mbele yao.
Ilipotimu saa tatu kamili asuhubi, Erick aliwasilia hotelini hapo na mazungumzo yakafanyika na mwisho ukaonekana kuwa mzuri akimweleza wazi kwamba alishafanikiwa kukutana na baadhi ya waandishi na kuwaeleza habari hiyo na walipanga kukutana siku iliyofuata pale hotelini.
Morgan akashukuru na kupeana ahadi ya kukutana na Erick siku iliyofuata kisha wakaagana.
Muda huo huo alifanya utaratibu wa kupata kibali cha kufanya mkutano ndani ya hoteli hiyo, ambapo alipewa chumba kikubwa kilichotumika kwa shughuli hiyo.
***
Hali ya Phillip ilikuwa imebadilika kabisa utanashati wote aliokuwa nao kipindi akiwa na mke wake ukawa umepotea, mahudhurio ya kazi nayo yalionekana kusuasua kitendo kilichofanya mpaka mabosi wake waaanze kuingiwa na wasiwasi.
Nyumbani nako hali ilikuwa tofauti kwani muda mwingi aliutumia kulala na alipochoka alitoka bila kuaga na kuingia mtaani kunywa pombe ili kupoteza msongo wa mawazo.
Phillip akawa ni mtu wa kukitamani kifo kuliko kitu kingine, haikuishia hapo akaanza tabia ya kutoka nyumbani na kwenda makaburini na alipofika huko alitafuta kaburi la mkewe Lina na kulala juu yake.
Ni hali hiyo ndiyo iliyozidi kuichanganya zaidi familia yake nao pia wakaingiwa na wasiwasi na kuamini kwamba si muda mrefu Phillip angekuwa mwendawazimu, ndugu na jamaa wakakaa kikao kuangalia ni jinsi gani wanaweza kumsaidia na walipomuuliza, jibu lilikuwa moja tu.
“Nataka kufa, basi.”
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 109

MAISHA yalikuwa yamebadilika kabisa kwa Phillip ni kama vile dunia yake ilikuwa imegeuka na kuwa nje ndani, akapoteza kabisa mwelekeo wa maisha yake na kusahau kwamba alikuwa ana jukumu la kumlea mtoto mdogo Genevieve ambaye bado alihitaji ushauri wa wazazi wake japo tayari mmoja alishaaga dunia.
Ushauri na ushawishi mkubwa wa ndugu, jamaa na marafiki haukusaidia kitu na hata walipoamua kutumia ofisi yake kumshauri bado hakubadilika ndiyo kwanza alizidisha ulevi na kutembea barabarani kutwa nzima akiongea na kutukana watu bila sababu.

Phillip akawa ameharibikiwa kabisa, ofisi ikaamua kumwachisha kazi kwa nguvu lakini wakiahidi kumsaidia kama tu msaada wowote ungehitajika, nyumbani nako hali kwa mtoto ikawa mbaya hata shule akawa haendi tena kwa sababu hapakuwa na ada ili aweze kuendelea na masomo, hakika maisha yakawa magumu kupindukia.
Lakini bado watu mbalimbali waliomfahamu Phillip hawakumwacha peke yake waliendelea kumshauri na kumpa moyo kwamba maisha yaliendelea na kamwe yasingesimama. Phillip akapokea ushauri wao ambao uliingia sikio la kulia na kutokea sikio la kushoto kwani hakuweza kubadilika, zaidi sana vituko viliongezeka nao pia wakaanza kuchoka na kumwacha afanye alivyopenda.

***
Ndani ya hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam chumba maalum kilikuwa kimeandaliwa tayari kwa mkutano mfupi ambao ungefanyika siku hiyo. Mariya na Merina ambao ndiyo waongeaji wakubwa, pembeni yao akiwepo mwanasheria aliyesimamia mambo yote zikiwemo mali za baba yao Victor Fedorov ambaye mpaka wakati huo hakufahamika kama alikuwa amekufa au la!
Waandishi walikuwa ni wengi mno mikononi mwao wakiwa na kalamu zao na kamera ili kuchukua habari ambayo ingepelekwa katika vyombo vyote vya habari yaani magazeti, redio na televisheni.

Mkutano ukawa umeanza, Mariya na Merina wakijitambulisha kwamba walikuwa akina nani na walitokea wapi na nini lilikuwa lengo lililowaleta nchini Tanzania, waliongea katika lugha ya Kirusi na Morgan akaitohoa katika lugha ya Kiingereza na baadaye Erick Evarist akatafsiri katika lugha ya Kiswahili.
Wakisisitiza kwamba walihitaji kufahamu mahali ambako Phillip na mkewe Genevieve wangepatikana na kwa gharama yoyote ile wangekuwa tayari kutimiza hilo lakini tu wapate ushirikiano.

Hivyo ndivyo mambo yalivyoendelea ndani ya hoteli hiyo kwenye chumba maalum, kwa muda wa saa nzima watoto hao waliendelea kuongea na waandishi wa habari wakiwaomba na kuwasihi kusaidia kuandika habari hizo ili hatimaye mtu anayetafutwa aweze kupatikana kwa urahisi.
“Wanamtafuta nani?”
“Wanasema wanatafuta familia ya Phillip na mkewe Genevieve.”
“Mh!”

“Kwa nini?”
“Hata sisi hatujui ila wanasema kwamba Genevieve ndiye mama yao mzazi.”
“Hawa watoto mbona siyo Watanzania?”
“Unalosema ni kweli lakini hatuwezi kujua, sisi tufanye tu kazi yetu,” yalikuwa ni maongezi kati ya waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo wakijiuliza maswali mengi juu ya mkutano huo na watu waliouitisha.

Baada ya habari kukamilika Mariya na Merina wakawashukuru waandishi huku wakiwashika mkono na kuwapatia bahasha ambayo ndani yake haikufahamika ilikuwa na nini na kuwatakia kila la kheri katika utendaji wa kazi zao na kuwaeleza wazi kwamba ili waweze kuwapata watu waliowahitaji, waliwategemea sana wao.
Waandishi nao wakashukuru wakiahidi kufanya kila kilichowezekana habari hiyo ichapishwe katika magazeti na ikiwezekana kutangazwa katika vyombo vyote vya habari zikiwemo redio na televisheni.

Baada ya waandishi kuondoka, wakarejea ndani ya vyumba vyao hamu yao kubwa ikabaki kusubiri nini magazeti yangeandika, ambapo macho na masikio yao yote yakaelekezwa huko.
“Nafikiria kila kitu kitakwenda sawa, tusubiri kesho tuone,” Morgan aliongea.
“Hata mimi nahisi hivyo ngoja tuone,” waliendelea kuongea wakijipa matumaini kwamba kila kitu kingekwenda sawa.
Saa zikazidi kusonga mbele hatimaye kiza kikaingia, hapo wakaamua kula chakula cha usiku na kuingia kwenye vitanda vyao wakiwa na hamu ya kujua kesho yake kitatokea nini.

***
Asubuhi ya siku iliyofuata Morgan alikuwa wa kwanza kutoka ndani ya chumba na bila kufanya kitu chochote akashuka kwa lifti mpaka mapokezi hapo akasabahi watu aliowakuta kisha kutoka nje ya hoteli kuelekea barabarani akitafuta mahali ambako angekutana na wauza magazeti na kununua ili kusoma kama habari yao ingekuwa imeandikwa siku hiyo.
Ni kweli kabisa alichokuwa amekifikiria kichwani mwake hakikuwa uongo, mtu wa kwanza tu aliyekutana naye akiwa na magazeti mkononi akamwita na kuchukua moja ya magazeti aliyokuwa nayo, macho yake yakakutana na picha ya Mariya na Merina mbele yao kukiwa na vipaza sauti vingi, hakuelewa lugha ya Kiswahili lakini aliweza kuisoma picha.

Akamwomba tena muuza magazeti ampatie magazeti mengine zaidi, nayo habari iliyosomeka ukurasa wa kwanza tu wa magazeti hayo ilikuwa ileile ya kwao, furaha ikamjaa moyoni mwake akajiona mshindi kati ya washindi na akalazimika kununua magazeti zaidi ya sita akalipa na kurejea ndani ya hoteli huku jasho likimtoka.
Haraka akapandisha lifti na moja kwa moja akauendea mlango ambao ndani yake walilala Mariya na Merina akagonga kwa nguvu na kusubiri mlango ufunguliwe na akiwa hapo akashuhudia Mariya akichungulia baada ya kufungua mlango.

“Magazeti haya hapa,” aliongea akinyoosha mkono kumpatia Mariya magazeti yote aliyokuwa nayo.
Kwa macho yake yote mawili akashuhudia kurasa za mbele za magazeti hayo zikiwa na picha yao kubwa akacheka na kutabasamu na bila kusema neno akarejea ndani ya chumba chao huku akimwita Merina.
“Merina! Merina, amka uone mwenyewe magazeti karibu yote yameandika habari yetu, kazi imekuwa rahisi sana kuliko tulivyotarajia…,” aliongea Mariya bila kuweka kituo.

Furaha ilikuwa imetawala ndani ya chumba wakiamini kwamba muda si mrefu kila kitu kingekwenda sawa kama walivyofikiria, kwa pamoja wakakumbatiana na kupigana mabusu lakini ghafla wakiwa katika furaha yao hiyo taswira ya baba yao Victor Fedorov mwanaume aliyewapenda kupindukia ikawajia, ni kweli walikuwa na furaha ya kuufahamu ukweli mwingine uliokuwa umejificha lakini pia Fedorov alikuwa ndiye mzazi wao halisi pamoja na mambo yote mabaya aliyoyatenda bado walimpenda.
“Sijui atakuwa wapi? Amepatwa na kitu gani? Inauma sana,” aliongea Merina huku akilia.

***
Asubuhi ya siku iliyofuata baada tu ya Merina na Mariya kufanya mkutano jana yake na waandishi wa habari, Phillip alikuwa katika mitaa ya Posta akikatisha huku na kule bila kuelewa anakwenda wapi.
Ghafla mbele yake akaiona meza ya magazeti na kuamua kutupa macho juu yake ili angalau asome kilichokuwa kimeandikwa siku hiyo, akasogea karibu kabisa na muuza magazeti kisha kumsabahi.
“Habari za leo?”
“Nzuri tu kaka karibu.”

“Ahsante, naweza kupitishapitisha macho kidogo?”
“Bila shaka lakini usiguse kama hutalinunua.”
Akaitika kwa ishara ya kutingisha kichwa kisha akasogea karibu na meza hiyo na kutupa macho juu ya magazeti, ni habari ya kwanza tu katika gazeti la Uwazi ikamshtua.
“Mh!”

“Mbona umeguna kaka?”
“Hii habari, inanihusu mimi kabisa na hao ni watoto wangu lakini walikufa.”
“Wewe mzee chizi nini utakuwa hamnazo watoto wako? Wewe? Hebu ondoka hapa haraka kabla sijakuitia mgambo wa jiji.”
“Dorice na Dorica,” alitamka kwa sauti ya juu.
Nimekuambia ondoka haraka,” aliongea muuza magazeti huyo akimvuta Phillip kumwondoa eneo hilo.

“Usinifanyie hivyo ndugu yangu nakuambia ukweli tafadhali nipe gazeti nione vizuri.”
“Wazee wengine bwana sijui wachawi au wanatumwa kuwangia biashara za watu! Asubuhi hii, kama unataka gazeti si ununue lakini siyo ujipendekeze kwa watoto wa watu.”
“Usinivu…,” aliongea Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake tayari akashuhudia vibao mfululizo vikipita mashavuni mwake.
 
 
 
 
 

MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 110


VIBAO mfululizo vilikuwa vimetua kwenye mashavu ya Phillip na kumpeleka chini akajikuta ameketi kitako bila kutarajia huku akilia na kujaribu kumweleza kijana yule ukweli kwamba habari iliyoandikwa ilimhusu yeye na watoto wake ambao hakika kwa wakati huo walikuwa ni marehemu.
Ni kilio cha Phillip ndicho kilichokusanya watu eneo la tukio, wengi wakijaribu kudadisi ni kitu gani kilikuwa kimetokea asubuhi hiyo. Kijana wa magazeti akaanza kusimulia tukio zima, muda wote huo Phillip akiendelea kulia.

Bahati nzuri asubuhi hiyo watu wengi walikuwa wakielekea makazini kwao, ni mfanyakazi mmoja aliyefanya kazi na Phillip alipita eneo hilo naye akitaka kuangalia nini lilikuwa tatizo. Akiwa hapo akatupa macho yake katikati ya umati wa watu akamwona mwanaume akiwa chini tena akilia.
“Mh!” akaguna akisogea karibu ili kuhakikisha kitu alichokiona.
“Phillip!” alitamka kwa sauti ya juu na kufanya watu wote kumwangalia yeye.

“Namjua huyu ni shemeji yangu pia ni mfanyakazi mwenzangu, jamani amefanya nini tena? Halafu ana tatizo la akili kidogo toka amefiwa na mkewe amekuwa hivyo, hebu njoo,” msichana huyo aliongea.
“Blandina sitaondoka hapa mpaka nipate gazeti.”
“Gazeti?”
“Ndiyo.”

“Lina nini?”
“Nimesoma kwa macho yangu habari kwamba Dorice na Dorica wako hapa Tanzania tena wananitafuta mimi na mama yao.”
“Phillip!”
“Hutaamini lakini huo ndiyo ukweli, wewe nunua usome kisha utanipatia na mimi.”

Msichana huyo bila ubishi akafungua mkoba wake na kutoa noti ya shilingi mia tano kisha kununua gazeti la Nipashe haraka akatupa macho yake ukurasa wa mbele, yeye pia akashuhudia picha kubwa iliyoonyesha wasichana wawili na chini yake kulionekana habari iliyowahusu lakini pia ikimtaja Phillip kwa majina yote matatu na Genevieve ambaye kwa historia aliyokuwa ameipata alikuwa ni mke wa Phillip aliyefariki dunia miaka kadhaa iliyopita.
“Naota au?”

“Huoti unachokiona hapo ni kweli tupu, tafadhali nisaidie nahitaji kujua wako wapi niwafuate nikaongee nao niujue ukweli,” aliongea Phillip akinyanyuka kutoka chini.
Watu wote waliokuwa eneo la tukio pamoja na kijana aliyekuwa akiuza magazeti wakaonekana kupigwa na butwaa kwani kwa wengi Phillip alionekana kichaa.
“Twende,” aliongea msichana huyo akimshika Phillip mkono, wakatembea mpaka kwenye mgahawa mmoja hapo wakaketi na kwa umakini wa hali ya juu wakaanza kusoma habari hiyo mwanzo mpaka mwisho na kuelewa sehemu ambayo watoto hao walikuwa wamefikia.

“Nisaidie ndugu yangu nahitaji kuonana nao leo hii.”
“Hakuna shida ila watakubali? Unayo kumbukumbu gani itakayokufanya wakuamini kwamba wewe ni baba yao?”
“Ninazo nyingi tu mojawapo ni picha zao za utotoni ziko nyumbani naweza kwenda kuzichukua.”
“Basi twende tukajaribu,” msichana huyo akaamua kushirikiana na Phillip ili kumsaidia.

Wakatembea mpaka kando kidogo na hapo akaita teksi ambayo iliwapeleka moja kwa moja nyumbani kwa Phillip ambako aliingia ndani na bila kusema kitu chochote akaingia chumbani kwake na kutoka na bahasha mkononi huku akikimbia akitoka tena nje na kuielekea teksi iliyokuwa ikimsubiri, akaingia ndani na dereva akaondoka kwa kasi ya ajabu moja kwa moja kuelekea katika hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam ambako wangejitambulisha na kuomba kuonana na Mariya na Merina.
Njia nzima Phillip alikuwa akilia, hakuamini mambo yaliyokuwa yanamtokea maishani mwake na mara kadhaa akamwomba msichana aliyekuwa naye ajaribu kumfinya pengine angeamka kutoka usingizini.

“Phillip shemeji yangu huoti hata kidogo yote yanayotokea ni kweli tupu, tatizo ni moja tu iweje watoto waliokuwa wamekufa na kuzikwa wawe hai? Hapo mimi nashindwa kabisa kuelewa na je, watakubali na kuamini kwamba wewe ndiye baba yao?”
Swali hilo lilipenya moja kwa moja masikioni mwa Phillip na kwenda ndani kabisa ya kichwa chake, akaiona picha yote jinsi walivyohangaika mpaka kufikia kununua mbegu za mwanaume mwingine ambaye aliitwa Victor Fedorov, alipofika hapo machozi yakambubujika.

Gari likaendeshwa na hatimaye nusu saa tu baadaye lilishawasili nje ya hoteli hiyo maarufu na wakalipa kisha kushuka kutembea kuelekea mapokezi ambako wangejitambulisha na kuomba kusaidiwa shida yao.
Kwao zoezi halikuwa gumu walifanya kama walivyopanga na kufanikiwa kuonana na watoto hao wawili. Mapokezi simu ikapigwa moja kwa moja kwenye chumba alicholala Morgan na simu hiyo ikapokelewa.

“Naongea kutoka mapokezi hapa kuna wageni wenu wawili.”
“Wawili? Wa jinsia gani?”
“Mwanamke na mwanaume.”
“Mh! Sawa waeleze tutakuwa hapo baada ya dakika tano kuanzia sasa hivi.” Morgan alijibu na kukata simu na bila kuchelewa akatoka chumbani kwake kwenda kwa akina Marina hapo akawapa taarifa na kuwataka wajiandae kukutana na wageni waliokuwa wamefika pale kuwatafuta.

“Pengine ndiyo hao tunaowatafuta.”
“Umejuaje hebu tukawaone kwanza.”
Haraka wakajiandaa na walipokuwa tayari wakatembea kuelekea sehemu kulikokuwa na mlango wenye lifti wote watatu wakashuka kuelekea chini wakitamani kuonana na watu hao.
“Je, tutawaamini vipi kama kweli ndiyo wenyewe?” Morgan aliuliza.

“Kabla ya yote tutahitaji kuwasikiliza kwanza wao na kama kuna kitu chochote kinachoonyesha kwamba wao ndiyo haswa walengwa wa safari yetu.”
“Hilo nakubaliana na wewe,”Merina alidakia na tayari walishafika chini mlango wa lifti ukaonekana kufunguka na kutoka nje.

Huku vichwani mwao wakijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu wakatokeza mapokezi na macho yao kukutana na watu wawili, mwanamke na mwanaume, ambao hawakuwafahamu kabisa lakini ghafla kabla hawajapiga hatua nyingine kwenda mbele zaidi wakashtushwa na sauti kubwa ndani ya chumba.
“Dorice! Dorica! Si mliku…,” aliongea Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake akaanguka chini kama mzigo.

Je, nini kitaendele
 
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 111


GARI likaendeshwa na hatimaye nusu saa tu baadaye lilishawasili nje ya hoteli hiyo maarufu na wakalipa kisha kushuka kutembea kuelekea mapokezi ambako wangejitambulisha na kuomba kusaidiwa shida yao. Kwao zoezi halikuwa gumu, walifanya kama walivyopanga na kufanikiwa kuonana na watoto hao wawili. Katika eneo la mapokezi simu ikapigwa moja kwa moja kwenye chumba alicholala Morgan na simu hiyo ikapokelewa.
“Naongea kutoka mapokezi, hapa kuna wageni wenu wawili.”

“Wawili? Wa jinsi gani?”
“Mwanamke na mwanaume.”
“Mh! Sawa waeleze tutakuwa hapo baada ya dakika tano kuanzia sasa hivi.” Morgan alijibu na kukata simu na bila kuchelewa akatoka chumbani kwake kwenda kwa akina Marina hapo akawapa taarifa na kuwataka wajiandae kukutana na wageni waliokuwa wamekuja hapo kuwatafuta.

“Pengine ndiyo hao tunaowatafuta.”
“Umejuaje hebu tukawaone kwanza.”
Haraka wakajiandaa na walipokuwa tayari wakatembea kuelekea sehemu kulikokuwa na mlango wenye lifti, wote watatu wakashuka kuelekea chini wakitamani kuonana na watu hao.

“Je, tutawaamini vipi kama kweli ndiyo wenyewe?” Morgan aliuliza.
“Kabla ya yote tutahitaji kuwasikiliza kwanza wao na kama kuna kitu chochote kinachoonyesha kwamba wao ndiyo haswa walengwa wa safari yetu tutafahamu huko.”
“Hilo nakubaliana na wewe,” Merina alidakia na tayari walishafika chini mlango wa lifti ukaonekana kufunguka na kutoka nje.

Huku vichwani mwao wakijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu wakatokeza mapokezi na macho yao kukutana na watu wawili, mwanamke na mwanaume, ambao hawakuwafahamu kabisa lakini ghafla kabla hawajapiga hatua nyingine kwenda mbele zaidi wakashtushwa na sauti kubwa ndani ya chumba.
“Dorice! Dorica! Si mliku…” aliongea Phillip lakini kabla hajamalizia sentensi yake akaanguka chini kama mzigo.
Je, nini kitaendelea? SONGA NAYO…

ULIKUWA ni mshtuko mkubwa Phillip alipoanguka chini watu wote ndani ya chumba walianza kukimbizana huku na kule kutafuta msaada, Blandina aliyekuwa ameongozana na Phillip yeye pia alikuwa akilia huku akimwita Phillip.
“Tafadhali usife, huu ndiyo wakati wa kuufahamu ukweli, amka nakuomba.”
Lakini bado Phillip aliendelea kulala chini akiwa hajitambui.

Haraka daktari aliyefanya kazi ndani ya hoteli kwa dharura akaitwa na mara moja akaanza kumpatia Phillip huduma ya kwanza ili kumnusuru na umauti ambao ulikuwa unamnyemelea.
Kwa takribani nusu saa nzima daktari aliendelea kumpatia huduma ya kwanza Phillip mwisho naye akaanza kukata tamaa akieleza wazi kwamba ni vyema mtu huyo akapelekwa hospitali kwa uchunguzi zaidi.

“Hospitali?”
”Ndiyo kwa jinsi hali ninavyoiona ni bora iwe hivyo.”
“Mh!” Blandina akaguna lakini ghafla wakiwa katika kujadili wakashuhudia Phillip akifungua macho yake na kuangaza huku na kule ndani ya hoteli.
Haraka kama vile alikuwa akiota akakurupuka kutoka chini na kusimama akionekana kutafuta kitu ambacho hakikuonekana kwa wengi.
“Bahasha yangu! Nataka bahasha yangu nilikuwa nayo muda si mrefu.”

“Hii hapa,” Blandina aliongea akinyoosha mkono kukabidhi bahasha kwa Phillip.
“Nasema ukweli watoto hao hapo ni wa kwangu lakini sikuwahi kuwapa majina hayo ya Mariya na Merina waliitwa Dorica na Dorice!”
“Lakini hawa ni Mariya na Merina si majina hayo unayosema wewe!”
“Hakika ninawaeleza ni watoto wangu ushahidi wangu upo, ni picha nakumbuka vizuri sura zao na mama yao pia,” Phillip aliongea mfululizo.
Morgan ambaye ndiye alikuwa mwanasheria aliyeongozana na akina Merina na Mariya akasogea karibu na Phillip ili kupata ushahidi wa picha kama Phillip mwenyewe alivyosema.

“Naweza kuona picha hizo?” aliuliza.
“Hizi hapa,” Phillip aliongea akifungua mfuko wa khaki na kuchomoa picha zilizokuwa ndani yake akazikabidhi kwa Morgan ambaye alianza kupitisha macho juu yake.
“Mh!” akaguna, picha zilizokuwa mikononi mwake zilikuwa za watoto wawili waliokuwa wamesimama mbele yake yaani Merina na Mariya akashuhudia picha nyingine za watoto hao wakiwa na mama yao mzazi ambaye ndiye aliitwa Genevieve, yeye pia akapigwa na butwaa.

Mariya na Merina nao pia wakasogea karibu na Morgan ili kushuhudia kilichokuwa kikiendelea, macho yao yakatua moja kwa moja katika picha zao na mwanamke mmoja akiwa pembeni yao, huyo ndiye alikuwa mama yao.
“Anafanana na sisi kabisa kwa kila kitu,” waliongea kwa sauti.
“Ni kweli yawezekana huyo ndiye tunayemtafuta.”
“Je, yuko wapi mwanamke huyu?”

“Genevieve alikufa!”
“Unasema?”
“Amini ninachowaambia, huo ndiyo ukweli wangu kama mnaweza kusadiki maneno yangu basi sadikini,” Phillip aliongea huku kwikwi ya kulia ikimkaba.
Maswali yakawa mengi bila majibu, ni kweli walimtafuta mwanaume aliyeitwa Phillip na mkewe Genevieve lakini kilichozidi kuwashangaza zaidi ni kwamba iweje mwanaume huyo aseme kwamba walikufa na kuzikwa miaka mingi iliyopita ili hali wao walikuwa hai?

Baada ya mvutano mrefu wakaomba chumba maalum ili waweze kuongea vizuri kuupata ukweli waliokuwa wakiutafuta Morgan akiwa ndiye kiongozi wa kikao, huko waliongea mengi Phillip akijaribu kueleza ukweli na ni kwa nini aliamini watoto hao walikufa. Akasimulia ajali ya gari kulipuliwa kwa bomu na watoto wote kufahamika walikufa.
Ilikuwa ni historia chungu lakini ilibidi Merina na Mariya waikubali, wakataka kuonyeshwa makaburi ili wakashuhudie kwa macho yao, jambo ambalo halikuwa na tatizo. Historia nyingine iliyokuwa imewaumiza watoto hao ni taarifa kwamba mama yao alikufa muda mrefu lakini pia alizikwa pembeni mwa makaburi yao.

“Hatuna muda wa kupoteza tunachohitaji sisi ni kuona hayo makaburi tena kama inawezekana sasa hivi,” Morgan aliongea.
“Hakuna shida tunaweza kwenda,” Phillip aliongea kwa majonzi.
Safari kuelekea makaburini ikaanza na kwa sababu walitumia usafiri wa kukodi haikuchukua muda wakawasili katika makaburi ambako walisemekana kuzikwa, wakashuka wakiwa na hamu ya kufahamu historia ya kifo. Kwa sababu makaburi yao hayakuwa mbali sana haikuchukua muda kuyafikia ambapo wakashuhudia picha zikiwa katika fremu kwa pamoja wakaangua kilio.

“Ni kwa nini haya yote? Mbona sisi tuko hai? Kuna nini kilitokea? Lazima ipo siri ambayo hatuwezi kuifahamu, na huyu ndiye mama yetu?” wakauliza.
“Mnachokiona wanangu ndicho kilichotokea, sikuwahi kufahamu kwamba hamkufa, mimi pia nahisi ni mchezo ulichezwa naomba mnisamehe.”
“Ukweli ni historia inayosikitisha sana lakini hatuna budi kuikubali pamoja na kuugundua ukweli huu wewe utabaki kuwa ba..ba..ye…tu!” waliongea watoto hao huku wakilia.

Mioyo yao ilikuwa imeumia kupita kiasi kwa historia waliyokuwa wameipata lakini upande mwingine walionekana kufurahia kujua ukweli kwani walioufahamu kama ndiyo ukweli haukuwa sawa, Federov alikuwa ndiye baba yao halisi na mama yao alikuwa Genevieve lakini Phillip alihusishwa zaidi kwani ndiye aliyewalea wakiwa watoto wadogo baada ya kununua mbegu za kiume kutoka kwa Fedorov.
“Tunakupenda sana,” waliongea wakitembea kuondoka eneo la makaburini kurejea hotelini ndani ya vichwa vyao wakiwaza na kuwazua mambo mengi bila kupata majibu, walihitaji kupata historia zaidi ili waamini kwa asilimia zote.

“Lakini tunahitaji kupata historia ya ndani zaidi ili kukufahamu vizuri.”
“Hakuna shida niko tayari kueleza kila kitu ambacho mtahitaji.”
Wakati wakiongea hayo walishafika eneo la maegesho la hoteli ya Kempinski jijini Dar es Salaam, wakashuka na kuingia ndani ili kuendelea na maongezi zaidi wakiwa tayari kumsikiliza Phillip.

Walitaka kusikia kama Phillip angekuwa tayari kusema ukweli wake wote alioufahamu ili nao waoanishe na maelezo ambayo waliyasoma kutoka kwenye nyaraka za baba yao.
“Historia nitakayosema inaumiza kupita maelezo lakini naomba muipokee kwa mikono miwili na kuichunguza hapo ndipo mtaugundua ukweli wote.”
“Mh! Tuko tayari kukusikiliza.”

“Mimi na mama yenu ambaye ni marehemu yaani Genevieve tulifunga ndoa miaka mingi iliyopita na maisha yetu yalikuwa ya raha mustarehe, jambo moja tu lilikosekana kwa bahati mbaya mimi sikuwa na mbegu za uzazi za kuweza kuzalisha mwanamke hivyo tukatafuta daktari ambaye tulimpata kama sikosei aliitwa Dk. Koher huyu alitusaidia sana na tukafanikiwa kupata mbegu za kununua kwa mwanaume mmoja aliyekuwa maskini akiishi mtaani, huyo aliitwa Victor Fedorov.

Ukafanyika utaalam wa kitabibu na ninyi mkazaliwa, furaha ndani ya nyumba ikaongezeka huku tukiwalea vyema na kuwatunza mpaka mlipofikisha umri wa miaka mitano ndipo tukaamua kuwapeleka shule lakini siku moja asubuhi nikapata ujumbe kwamba gari iliyokuwa imewabeba ilitegeshwa bomu hivyo lingelipuka na watoto wote kufa.

Nilijitahidi sana kunusuru maisha yenu lakini nilishachelewa, gari likalipuka na watoto wote ndani ya basi kuaminika kufa, tulilia na kuomboleza baadaye tukafanya mazishi ndiyo yale makaburi niliyowapeleka yakiwa na picha zenu juu. Akili yangu inavurugika zaidi iweje leo muwe hai tena katika nchi nyingine kabisa…,” aliongea Phillip muda wote huo akibubujikwa na machozi.
“Usilie tafadhali nyamaza.”
“Inanichanganya akili iweje muwe hai wakati mlishakufa tukawazika? Hapana hii ni ndoto pengine nitaamka na kukuta kila kitu kiko sawa, hebu nifinye.”

Je, nini kitaendelea? Historia aliyoitoa Phillip mbele ya watoto wake baada ya kutoka makaburini wataiamini?
 
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 112

PHILLIP hakuwa katika ndoto kama alivyokuwa akifikiria kwani mambo yote yaliyokuwa yakimtokea yalikuwa ya kweli japo historia iliumiza mioyo ya wengi.
Vilio na machozi kwa Merina na Mariya havikukauka, walilia na kuomboleza kwa mambo mengi lakini kubwa zaidi ni lile la kuelezwa kwamba walikufa miaka mingi iliyopita kwa ajali ya bomu ambalo lilitegwa kwenye gari lao la shule na kuzikwa sehemu ambayo waliishuhudia kwa macho yao.

“Ni nini kilitokea? Kuna nini baba alifanya? Huu lazima utakuwa ni mchezo,” Merina na Mariya walisema kwa lugha ya Kirusi.”
Muafaka ukawa umefikiwa kwamba Phillip apewe muda wa kutafuta nyaraka zote muhimu za kumtambulisha kwamba yeye ndiye haswa alikuwa baba aliyewalea watoto hao. Akapata cheti cha ndoa na nyaraka nyingine kadhaa, pia baadhi ya ndugu nao wakasimama kusema ukweli mbele ya mwanasheria Morgan aliyepewa jukumu la kuongoza mambo yote yaliyotakiwa.

Siku ya kwanza ikapita, ikaja siku ya pili na hatimaye wiki ikakatika wakiwa bado katika uchunguzi mzito. Vielelezo vingi vilipatikana na baadhi ya watu wakatoa ushahidi wao kuhusu Phillip.
Jinsi watu wengi walivyotegemea ndivyo ilivyokuwa kwani baada ya uchunguzi wa kina, ukweli ulibainika. Phillip akaonekana kuwa mwenye haki pamoja na kwamba hakuwa baba wa kuwazaa watoto Mariya na Merina.
“Nini kinaendelea kwa sasa?” Morgan aliuliza siku moja.

“Nadhani mtu pekee wa kumtafuta kwa sasa ni Eric Evarist ili atusaidie tena tupate nafasi ya kuzungumza na waandishi wa habari.
Jambo hilo likafanyika mara moja, mwandishi huyo akatafutwa na kupewa taarifa kamili. Siku mbili baadaye, kilifanyika kikao kingine ndani ya hoteli ileile waliyofikia.
Waandishi wa habari wakafurika ndani ya chumba maalum tayari kwa kuchukua taarifa muhimu, macho na masikio vikawa makini kabisa kuhakikisha hawakosei kitu chochote.

Hata waandishi wenyewe baada ya kusikia historia iliyokuwa imetolewa na mashahidi wa pande zote mbili, walishtushwa sana. Kilichowatatiza ni kwamba, iweje watu waliozikwa siku nyingi wawe hai tena?
“Ndugu zangu ninayo mambo matatu tu muhimu ya kuongea nanyi asubuhi ya leo lakini nianze kwa kuwaomba radhi kuchukua muda wenu mwingi kuja hapa kwetu,” aliongea Morgan na alipomaliza akapokelewa kwa shangwe, nderemo na makofi mengi ndani ya chumba.

Mariya na Merina ndiyo walioanza kufungua mkutano huo, wakati wakiongea, Morgan ambaye ndiye alikuwa mwanasheria wao, alikuwa akitafsiri kwa lugha ya Kiingereza ambayo waliamini kabisa itaeleweka kwa watu wote. Walipomaliza, Phillip naye alikaribishwa kuongea na waandishi, akaeleza kila kitu bila kificho. Machoni mwa watu alionekana kama mwongo aliyetaka kujipatia fedha kutoka kwa watoto hao matajiri lakini Morgan alikanusha vikali uvumi huo, akasimama kumtetea Phillip kwa kipindi chote.
“Hadanganyi, ni kweli ndiye baba halisi wa watoto hawa.”

“Mh!”
“Huo ndiyo ukweli?”
“Lakini anasema wake walishakufa miaka mingi iliyopita kwa ajali, pengine wanafanana tu.”
“Uchunguzi wa kina umefanyika na tumegundua kila kitu, kwa hilo naomba tukubaliane na tuungane na huyu ndugu yetu hapa,” Morgan alisema kwa kujiamini.

Wakiwa hapo, waliongea mambo yote lakini jambo moja likabaki kuwa siri ya familia kwamba watoto hao walikuwa si mali ya Phillip kwani hakuwa na uwezo wa kumpa ujauzito mwanamke. Jambo hilo liliendelea kubaki siri ya familia ili kulinda heshima yake.
Kwa muda wote huo, Phillip aliendelea kumwagika machoz. Si kwamba alikuwa akiliakwa majonzi bali furaha ya kukubaliwa na watoto wake wawili ambao kwa wakati huo walishabadili majina na kuitwa Merina na Mariya (Dorice na Dorica) ndiyo kitu kilichomliza.
Wote kwa pamoja wakasimama na kukumbatiana, watoto pia walikuwa wakilia kwa furaha kwani walimpata mtu waliyekuwa wakimtafuta pamoja na kwamba Genevieve ambaye ndiye mama yao alishakufa.

Kazi yote ikawa imeachwa mikononi mwa vyombo vya habari kutangaza ukweli kwa Watanzania kwamba mwanaume ambaye ndiye hasa alikuwa akitafutwa, alikuwa amepatikana na Mariya na Merina wakishirikiana na mwanasheria wao walikuwa wakiwashukuru watu wote waliofanikisha kupatikana kwa Phillip. Mariya na Merina walikuwa na hamu kubwa ya kuwafahamu ndugu wengine wa Phillip, ikabidi wasubiri vyombo vya habari vifanye kazi yao.

Baada ya waandishi kuondoka, Phillip aliwaongoza Mariya, Merina na Morgan kuelekea nyumbani kwake ambako angekutana na familia yake, yaani mtoto wake Genevieve na bibi Magdalena ili kufahamiana zaidi, jambo ambalo lilichukua muda wa nusu saa hivi. Baada ya kufika nyumbani kwa Phillip, mapokezi yakafanyika kisha wakaungana na familia kufahamiana zaidi.
Waliongea mengi huku furaha ikitawala, mara kadhaa Phillip alionesha mapenzi ya dhati kwa watoto wake kwa kuwapiga mabusu mfululizo kama ishara ya mapenzi ya dhati kwao. Baada ya kumaliza utambulisho huo, waliaga na kuondoka wakimtaka Phillip kufika hotelini asubuhi ya siku iliyofuata ili wazungumze zaidi.
***
Magazeti yote ya siku iliyofuatia yaliandika habari ya kupatikana kwa Phillip, mwanaume aliyekuwa akisakwa kwa udi na uvumba ambaye haswa ndiye alikuwa baba wa Merina na Mariya watoto wa Kirusi waliokuja nchini kuufahamu ukweli wa maisha yao.
Vichwa vingi vya habari vilisomeka tofauti, wapo walioandika: “Baba wa watoto ajitokeza.” Mengine yakataka vipimo vya vinasaba (DNA) vifanyike ili kujua ukweli wa historia. “Watoto walioaminika kufa miaka mingi iliyopita wafufuka,” liliandika gazeti lingine. Kila gazeti liliandika lilivyotaka ilimradi kufanya biashara. Lakini wote hao hawakuufahamu upande wa pili wa shilingi kwamba nyuma yake kulikuwa na historia nyingine, tena ya kusikitisha ambayo ilikuwa ndani ya mioyo ya watoto wenyewe na Phillip.
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 113

WATANZANIA wengi wakabaki midomo wazi baada ya kusoma habari hizo kwenye vyombo vya habari mbalimbali. Wengi wakijiuliza kuna kitu gani kilitokea mpaka dunia ikaamini kwamba watoto hao waliokuwa wakiuza magazeti kwa wakati huo walikuwa wamekufa kumbe walikuwa hai. Maswali hayo yote hayakuwa na majibu na yakaendelea kuwa kitendawili kwa wengi.
Wakati dunia ikishangaa kwa upande wa Mariya, Merina na Phillip, kwao ilikuwa furaha kubwa, wakifurahia kuonana wakiwa hai, masikitiko makubwa yalitokea tu pale walipomkumbuka mama yao yaani Genevieve lakini wakajipa moyo na kuamini kwamba hiyo ndiyo dunia waliyoishi ndani yake, furaha kidogo na uchungu mwingi.

Si watoto tu waliowaza siku iliyofuata hata Phillip naye hakupata hata lepe la usingizi, akifikiria kesho yake ingekuwaje, lakini alikabidhi kila kitu mikononi mwa Mungu ili yeye ndiye awe jaji wa kila jambo ambalo lingekwenda kutokea, lakini zaidi alitaka watoto hao wafahamu kwamba pamoja na kuwa hakuwa baba yao wa kuwazaa lakini aliwapenda kwa dhati kupita maelezo na shahidi pekee alikuwa ni Mungu na mama yao Genevieve ambaye kwa wakati huo alikuwa ni marehemu.

Akaamka na kujiandaa na baada ya maandalizi hayo akatoka sebuleni na kuisabahi familia yake, hapo akaaga na kuondoka kuelekea hotelini akiahidi kurejea muda mfupi baadaye na kuwapa taarifa ni kitu gani kilizungumzwa. Njia nzima aliwaza na kuwazua bila kupata majibu, hatimaye nusu saa tu baadaye akawasili kwenye hoteli waliyokuwa wamefikia watoto wake, hapo akaingia moja kwa moja mapokezi na kuomba mawasiliano nao.

“Niko hapa kuonana na watu watatu, Mariya, Merina na Morgan,” aliongea.
“Sawa, karibu sana kaka taarifa zako ninazo kitambo sana.”
“Ahsante,” alijibu Phillip akijivuta kuelekea kwenye kiti kilichokuwa maeneo hayo na kuketi kusubiri na haikuchukua muda akawaona watoto hao wakitokeza na kutembea kumwelekea huku wakionyesha uso wa tabasamu wakamsabahi na kumkaribisha kwenye chumba maalum ambacho kiliandaliwa.

Wakaingia ndani na kuanza mazungumzo ambayo hakika Phillip mwenyewe hakuwa tayari kuyaamini mara zote alibubujikwa na machozi mfululizo. Morgan aliyekuwa pembeni akiwa ndiye mkalimani akitafsiri jambo moja baada ya jingine na mwisho muafaka ukawa umefikiwa.
“Kwa muda wa wiki nzima tumesubiri kuona kama kungejitokeza mtu mwingine na kudai kwamba sisi ni watoto wake lakini historia yako uliyotueleza inaendana kabisa na vielelezo vyetu.

“Awali tulikuwa navyo hivyo tumelazimika kukuamini kwa asilimia zote ingawa ukweli wote uko wazi, hakika pamoja na mambo yote yaliyotokea maishani mwetu, wewe bado utabaki kuwa baba yetu.” “Tutakupenda mpaka mwisho na hivi tunavyoongea na wewe tayari tumeishaanza kufanya utaratibu maalum wa kuondoka na wewe, si wewe tu bali pia familia yako yote ili tukaishi wote kama ndugu.”
“Ahsante, ahsanteni kwa kunijali wanangu hakika mnanipenda lakini kuna jambo moja linalosumbua ubongo wangu…,” aliongea Phillip lakini hakuweza kumalizia sentensi yake kwikwi ya kulia ikamkaba.

“Ni kwa nini unalia?”
“Mh! Unajua…”
“Hebu nyamaza ueleze linalokusibu.”
“Nalia furaha lakini pia swali moja linazunguka kichwani mwangu ni kwamba itakuwaje tukifika huko wakati ukweli wote mmeufahamu kwamba mimi si baba yenu?”
“Wewe ndiye baba yetu hakika tunayo kila sababu ya kusimamia hilo hata ikiwezekana kwa mtutu wa bunduki.”
“Mnasema kweli?”

“Kweli kabisa!”
“Na je vipi kuhusu Victor Fedorov ambaye ndiye mhusika wa kila kitu?””Tutakwenda kujua hukohuko kwani yapata kipindi kirefu sasa tangu ametoweka katika mazingira ya kutatanisha na hivi tunavyoongea nawe tumeliachia kazi jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kujua ni wapi alipo na kama yuko hai au la!” Mariya aliongea akimpigapiga Phillip mgongoni.

Hatimaye muafaka ukafikiwa kwamba kwa kuwa Mariya , Merina na Morgan walikuwa wametoa muda wa wiki nzima kusubiri kuona kama kungetokea jambo lolote lakini halikuwepo, uamuzi pekee walioufikia ni kuondoka na Phillip na familia yake yote. Hivyo utaratibu ukaanza mara moja wakitakiwa kuwakilisha vielelezo vyao vyote muhimu ili kupata vibali vya kuondoka nchini.
Hilo ndilo likawa jambo kubwa mbele yao, kwa Phillip yote hayo yakionekana kuwa ndoto akiamini kwamba ipo siku angeamka kutoka katika usingizi mzito aliokuwa amelala na kuona kila kitu kikiwa tofauti. Siku zikazidi kusonga mbele Morgan akishughulikia vibali vyote muhimu, hatimaye baada ya muda mrefu akafanikiwa kuvipata na furaha ikaendelea kutawala kati yao.

“Nashukuru Mungu kila kitu kimekwenda sawa, kilichobaki mbele yetu ni safari tu nadhani ni bora tukafanya maandalizi haya haraka ili turejee nyumbani kuendelea na shughuli nyingine kubwa, zaidi ni ile tuliyoiacha ikiendelea kuhusu Victor Fedorov, ni lazima tufahamu nini kiliendelea baada ya sisi kuondoka, alipatikana akiwa hai au alifikwa na umauti?” aliongea Morgan akionyesha msisitizo na kuwafanya watu wote waliokuwepo hapo wakimsikiliza kumwaga machozi, kwani bado watoto Mariya na Merina walimhitaji baba yao kupita maelezo ili naye ashuhudie kilichokuwa kimetokea na kumkubali Phillip na familia yake yote kama mmoja wa familia yao.

Kila kitu kikaenda kama walivyotarajia, Phillip akapewa nafsi ya kuaga ndugu, jamaa na rafiki zake akitakiwa kuwataarifu juu ya safari ambayo ilikuwa mbele yake naye akafanya hivyo bila kusita huku furaha ikiendelea kutawala katika moyo wake, kwa walio wengi walionekana kumpongeza na kufurahia tukio hilo lakini baadhi pia wakionekana kuumizwa kwa kumkosa kwani pamoja na matatizo yote aliyokuwa nayo alikuwa ni mtu wa watu.

Siku mbili baadaye safari ilishawadia wote kwa pamoja wakiwa ndani ya gari la kukodi liliwachukua na moja kwa moja kuwapeleka uwanja wa ndege ambako wangefanya utaratibu na kuondoka kuelekea nchini Urusi kwenda kufaidi maisha.
 
 
 
 
 
 
 
 MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 114

KWA Phillip, Genevieve na bibi Magdalena jambo lililokuwa likitokea mbele yao lilionekana kama ndoto na muda si mrefu wangezinduka kutoka katika uzingizi mzito. Lakini ukweli ulikuwa umebaki pale pale kwamba walikuwa safarini kuelekea nchini Urusi wakiambatana na wenyeji wao watatu yaani Merina, Mariya na Morgan ambaye alisimama kama mwanasheria wao.

Ndege waliyokuwa wamepanda iliondoka uwanja wa ndege wa Dar es Salaam saa tisa na ilitarajiwa kutua nchini Gairo kwa mapumziko kidogo, hatimaye Moscow ilitakiwa kutua muda wa saa mbili asubuhi na hapo ndipo ingekuwa mwisho wa safari yao.
Kama walivyokuwa wametarajia waliwasili saa mbili kamili za asubuhi, ndege ilipokanyaga tu ardhi ya nchi hiyo Mariya na Merina wakawa wa kwanza kushuka huku wakiwakaribisha Phillip na familia yake, muda wote huo furaha ilikuwa ikitawala kati yao walishasahau machungu yote na kilichokuwa mbele yao ni kuyafaidi maisha.

“Karibuni sana nyumbani,” Morgan aliongea kwa lugha ya Kiingereza.
“Tunashukuru sana,” Phillip alijibu akiachia tabasamu laini usoni mwake.
Wakati Phillip akifurahia kuingia nchini urusi, kichwani mwa Mariya na Merina pamoja na kuwa na furaha walifikiria jambo moja tu, baba yao alikuwa wapi hivyo walipanga baada ya kufika tu kwenda kufuatilia taarifa za uchunguzi wa polisi ili kujua nini kilitokea baada ya wao kuikabidhi kazi ya kumsaka baba yao mikononi mwao.

Wakaondoka ndani ya uwanja wa ndege moja kwa moja kuelekea nyumbani, huko wakapokelewa na wenyeji wao kisha wakawakaribisha Phillip na familia aliyoambatana nayo.
Wakahakikisha kila kitu kinakwenda sawa na wageni walikuwa wamepata mahitaji yote muhimu wao wakaaga na kutoka kuelekea makao makuu ya polisi kufuatilia majibu ya uchunguzi, wakiongozana na Morgan.

Gari likaendeshwa kwa kasi na baada ya nusu saa tu baadaye walishawasili kituoni hapo.
Kwa umaarufu wao walikaribishwa moja kwa moja ndani na kuonana na mkuu wa polisi wakafanya mkutano mfupi wakitaka kujua nini kiliendelea na ripoti ya polisi haikufichwa ilielezwa wazi kwamba tangu kupotea kwa Victor Fedorov yapata miezi sita, walikuwa wamefanya kila walichoweza na juhudi zote zilionekana kufikia ukingoni, wakapitiliza mbele zaidi na kusema kwamba huenda alikufa na kufunikwa na barafu nzito hivyo kumpoteza kabisa.

Baada ya taarifa hiyo huzuni kubwa ikawafunika wao pia wakahisi kukata tamaa ya kumwona tena baba yao akiwa hai, lakini wakatamani kuona hata maiti yake tu waizike kwa heshima zote lakini hilo nalo lilikuwa limeshindikana, wakabaki njia panda wakisubiri muujiza. Huku wakionyesha masikitiko makubwa wakamshukuru mkuu wa polisi, wakamuaga na kurejea nyumbani.
Mioyo yao iliuma kupita kiasi, mara kadhaa kumbukumbu za baba yao ziliwajia ndani ya vichwa vyao wakikumbuka wema, ucheshi na upendo mwingi aliowaonyesha na sasa alikuwa ametoweka kama upepo mbele ya macho yao.

Ni mawazo hayo ndiyo yaliyosababisha watoto hao kububujikwa na machozi, hakika walikuwa wamepoteza mtu muhimu sana katika maisha yao na asingekuwepo wala kutokea mwingine ambaye angeweza kukidhi shida zao ni kweli alikuwa mkosaji lakini bado aliendelea kubaki kuwa ndiye baba halisi na kibaya zaidi na cha kuumiza, mama yao waliyefunga safari mpaka Afrika, nchini Tanzania kumfuata naye alishakufa miaka mingi iliyopita.

Baada ya gari kufunga breki ndani ya jengo lao, haraka bila kuongea kitu watoto hao wakashuka mbio huku wakikimbia na kuingia ndani ambako nako walipita mbio sebuleni na kuingia chumbani kwao, jambo hilo liliwashangaza wengi na hata Phillip aliyewashuhudia alipojaribu kufuatilia hakupata jibu la kueleweka zaidi sana alisikia sauti ya vilio ikiambatana na kwikwi.

“Morgan kimetokea nini huko mlikokwenda?”
“Hali ni mbaya mpaka sasa hakuna taarifa yoyote muhimu juu ya Victor Fedorov na uchunguzi wa polisi umefikia kikomo jambo moja tu naweza kusema huenda alikufa na kufunikwa na barafu nzito, basi”
“Mungu wangu!” Philllip aliongea kwa sauti ya juu.
“Huo ndiyo ukweli japo unauma hatuna budi kuukubali,” Morgan aliongea naye machozi yalionekana kububujika kwenye mashavu yake.

“Inauma,” Phillip alijibu.
Morgan na Phillip waliendelea kubaki sebuleni kwa muda mrefu wakiongea mambo mengi kama kubadilishana mawazo hatimaye ushauri ukatoka kwamba Mariya na Merina waitwe ili waweze kuongea nao mambo fulani.

“Hata mimi naunga mkono jambo hilo ni lazima tuwape maneno ya faraja, walikubali tukio hilo na kusubiri kama pengine atakuwa hakufa basi ipo siku atajitokeza na kuugana nao,” Phillip aliongea na sekunde tatu tu baadaye Mariya na Merina walishafika sebuleni na kuungana nao, hapo wakafanya mkutano mfupi wa majonzi wakijaribu kuwaeleza wazi kwamba hapakuwa na sababu ya kuhuzunika kwani kila jambo linalotokea katika maisha ya mwanadamu waamini kwamba lilikuwa na sababu.

Wakionyesha majonzi makubwa, wakakubaliana na kilichotokea, zaidi sana Morgan aliwataka kufahamu haki zote za baba yao na yeye angekuwa nao bega kwa bega kuhakikisha hakuna kinachopotea.
Maneno hayo yakawa yamerejesha furaha kwa watoto hao, wakageuka upande aliokuwa ameketi Phillip na kwa pamoja wakatamka maneno haya;

“Umekuja kuchukua nafasi ya baba yetu, hakika wewe ndiye, kuanzia leo utachukua majukumu yote na kuifanya familia kuwa yenye furaha siku zote, tafadhali tunakuomba ukubali na kwa pamoja tunasema tunakupenda,” aliongea Merina kisha walisimama na kutembea kumwelekea Phillip.

Walipomkaribia wakapiga magoti na kuanza kulia huku wakimweleza kwamba walimpenda sana.
“Ninawepanda pia wanangu Mungu alikuwa nayo sababu niwashukuru pia nanyi kwa kunikubali kunipokea na kunilea, Mungu awabariki sana,” Phillip aliwaambia Merina na Mariya.
Kwa pamoja wakakumbatiana na kuanza kulia, yalikuwa ni machozi ya furaha pamoja na kwamba walikuwa katika masikitiko makubwa ya kupotelewa na baba yao kipenzi.

Baada ya muungano huo wote kwa pamoja walidhamiria kushikamana kama ndugu wakiapa kutimiza wajibu na kulinda heshima ya baba yao ambaye alikuwa ndiye muasisi wa utajiri wote waliokuwa nao.
“Jambo la muhimu hivi sasa pamoja na yote tuliyoongea ni muhimu tukatangaza habari za kifo cha Victor Fedorov kwenye vyombo vya habari kwa muda usiopungua mwezi mmoja tuone nini matokeo yake,” Phillip alitoa wazo na wote wakalipokea kwa mikono miwili.

Je, nini kitaendelea baada ya kutangaza kifo kwa mtu ambaye hakujulikana alikufa au yu hai?
 
 
 
 
 
 
MSICHANA NDOTONI MWANGU.......EP. 115

Ilionekana kuwa safari nyingine ngumu lakini ilikuwa ni lazima waizoee na kuikubali ili maisha yaendelee kwani hivyo ndivyo dunia ilivyokuwa. Kwa pamoja wakakubaliana na kusimama, tegemeo lao kubwa kwa wakati huo akiwa ni Phillip, ndiye alikuwa baba wa familia kipindi chote wakisubiri kuona nini kingetokea baada ya kutangaza kwenye vyombo vya habari.
“Tutakupenda mpaka mwisho na jambo pekee kwa hivi sasa ni vyema Genevieve akaanza shule haraka iwezekanavyo ili naye apate elimu kama sisi,” Mariya aliongea siku moja wakiwa sebuleni.
“Ni kweli kabisa ni lazima aanze shule mara moja, kesho nitakwenda kuongea na mwalimu wa shule tuliyosoma.”
“Ada je?”
“Tutalipa hakuna shida huyu ni mdogo wetu ni lazima tutimize wajibu kwake.”
“Ahsanteni wanangu Mungu awabariki sana,” Phillip aliongea huku akibubujikwa na machozi.
Furaha ilikuwa imeizunguka nyumba ya Victor Fedorov, kazi zote zikiwa chini ya usimamizi wa Phillip kama baba na Morgan ambaye alikuwa ndiye haswa mwanasheria wa miradi yote iliyomilikiwa na tajiri huyo.
Siku nazo zikazidi kusonga mbele mambo yote yakiwa sawa kama walivyopanga, Genevieve akiwa tayari ameshaanza shule, Phillip, Mariya na Merina wakihakikisha miradi yote inakwenda sawa.
Mwezi wa kwanza ukapita bado wakiwa katika kusubiri, taarifa mbalimbali zikiendelea kutolewa na vyombo vya habari wakati mwingine hata televisheni kubwa nchini humo, lakini bado hakukuwa na majibu yoyote hatimaye nao wakaanza kukubaliana na madai ya polisi ya uchunguzi wao walioufanya kwa kina na kuamini kwamba huenda mzee huyo alikufa na kufunikwa na barafu nzito.
“Pengine inawezekana kweli baba alikufa kitambo kama uchunguzi unavyosema.”
“Hapana hebu tusubiri pengine anataka kutupima kama tumekua.”
“Mariya hakyanani amini tu kwamba baba amefariki.”
“Sijakataa, inawezekana ikawa hivyo ninachokiona mimi hebu tusubiri zaidi.”
“Sawa,” Mariya aliitikia.
Kwa muda wa miezi minne mfululizo bado waliendelea kusubiri huku wakiendelea na shughuli zao kama kawaida na ilipotimia mwezi wa tano wakaanza kuchoka na kukata tamaa kwani walikuwa wamefuatilia kwa karibu sana kila kitu kuchunguza kwa umakini wa hali ya juu na jibu walilokuwa wamelipata halikutofautiana na polisi. Huzuni na majonzi vikatawala upya wakikumbuka mema yote aliyowatendea baba yao enzi za uhai wake.
Hatimaye ikatimu miezi sita wakiwa katika kusubiri mwisho wakafikia uamuzi wa kuutangazia umma kwamba Victor Fedorov aliaminika kufa katika mchezo wa kuteleza kwenye barafu.
“Ni lazima sasa tutangaze kwamba Victor Fedorov alikufa.”
“Tunaungana na wewe.”
“Je, kama ikitokea siku moja akarudi?”
“Hiyo itakuwa habari nyingine lakini sidhani kama jambo hili litatokea.”
“Mh!”
“Huo ndiyo ukweli, hakuna haja ya kuguna wala kujiuliza mara mbilimbili.”
“Morgan kesho asubuhi mchakato huo uanze, sisi kama watoto wa marehemu tupate wasaa japo wa dakika kumi tu katika televisheni ya taifa kuuelezea umma juu ya jambo hilo.”
“Nakubaliana nanyi na kazi hiyo kesho asubuhi itafanyika.”
Saa zikazidi kusonga mbele hatimaye kesho waliyoisubiri kwa hamu kubwa ikawadia na Morgan akafanya taratibu zote na kurejesha majibu kwa Mariya na Merina kwamba alishafanikiwa kuongea na televisheni hiyo kubwa. Maandalizi maalum yakafanyika hatimaye wakaiweka habari hiyo kweupe ikiliacha taifa la Urusi katika mshangao mkubwa na maumivu kutokana na ushirikiano wa mzee huyo kwa jamii iliyomzunguka, umaarufu wa Victor Fedorov ulikuwa mkubwa hivyo kitendo cha kutangazwa kwamba aliaminika kufa kiliwaumiza wengi.
Majonzi, vilio na kuomboleza vikatawala nyumbani kwake, watu mbalimbali maarufu wakiongozwa na rais wa nchi hiyo walifika kutoa pole na rambirambi, wengi wao wakitaka kujua historia kamili ya tukio. Sehemu maalum ilitengwa na kuweka picha kubwa ya Fedorov huku chini yake kukiwa na maneno “Герой ушел” yakimaanisha “Shujaa ameondoka”.
Kutokana na umaarufu wa tajiri huyo nchini Urusi, serikali ikatoa wiki nzima ya maombolezo ishara tosha kwamba alikuwa kipenzi cha watu wengi, hakuwepo mtu hata mmoja aliyefahamu upande wake wa pili kwamba alikuwa ni mtu hatari kupindukia.
Ikiwa ni siku tatu tu tangu kufanyika kwa maombolezo ya Fedorov, kama familia waliamua kwenda kutembelea eneo ambalo ndilo haswa lililoaminika kuchukua maisha ya baba yao kipenzi ambapo mashada mengi yakawekwa eneo hilo pamoja na picha yake kama kumbukumbu pekee katika maisha yao na zoezi hilo lilipokamilika wakarejea nyumbani kuendelea na maombolezo.
Siku ya nne asubuhi jambo la ajabu likatokea na kufanya watu wengi kupigwa na butwaa, ni taarifa kwamba mwili wa mtu asiyefahamika ulikuwa umeonekana ndani ya shimo kubwa lililokuwa Mashariki ya Urusi na mtu mmoja aliyekuwa akifanya mchezo wa kuteleza katika barafu ndiye aliyegundua hilo na kuamua kutoa taarifa polisi ambao walifika mara moja eneo hilo.Gari maalum likatolewa likiwa na polisi ndani yake na likaenda moja kwa moja mpaka eneo husika ili kushuhudia tukio hilo, na ni kweli kabisa wao pia macho yao yaliona kama walivyokuwa wameelezwa.
Haraka taratibu za kuutoa mwili zikafanyika na kuufikisha katika hospitali kuu nchini humo kwa utambuzi, watu wengi walifika na kuangalia kama wangeweza kumfahamu.
***
Akiwa mafichoni aliweza kufuatilia mambo yote ya tajiri huyo mkubwa lengo lake likiwa ni kutaka kulipa kisasi kwa ubaya aliomtendea, hakuwepo mtu hata mmoja aliyefahamu kwamba Ditrov alikuwa hai sehemu fulani kama ilivyoaminika kwa wengi alishakufa muda mrefu.
“Nitakaa hapa huku nikifuatilia nijue jinsi ya kumpata huyu mpumbavu na kulipa kisasi, safari hii atanijua mimi ni nani,” aliwaza Ditrov siku moja lakini ghafla akazipata habari kwamba Victor alitoweka katika mazingira ya kutatanisha na alikuwa akitafutwa bila mafanikio na kama familia walishaamua kuliweka jambo hilo wazi kwamba alikufa.
“Mh! Atakufaje kabla sijakutana naye? Lakini acha afe ili mimi niendelee kula maisha na sasa nitarejea nyumbani,” alijisemea Ditrov. Akafanya maandalizi ya safari kurejea nyumbani nchini Urusi, huko ndiko alikofahamu ukweli kwamba hakika mwanaume huyo alikuwa amekufa na mwili wake ulikuwa umeokotwa kwenye shimo wakati wa mchezo wa kuteleza katika barafu na watoto wake walithibitisha jambo hilo.
“Maisha sasa mswano pamoja na ubaya wake Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amina!” alimaliza Ditrov huku machozi yakimlengalenga.
***
“Mimi naona tukafanye ukaguzi wa mwili huo,” Morgan aliongea ikiwa ni siku ya nne tu.
Bila ubishi wakaondoka nyumbani kuelekea hospitali kila mmoja akiwaza jambo kichwani mwake, bila kupoteza muda moja kwa moja mpaka chumba cha kuhifadhia maiti hapo wakajitambulisha na kuomba kuutambua mwili wa mwanaume aliyeonekana akiwa amekufa.
“Mh!” Merina ndiye aliyekuwa wa kwanza kukagua.
“Kwa nini umeguna?”
“Hapana siye baba, mbona amevimba kiasi hiki? Halafu amekuwa mweusi kupindukia.”
“Hebu?” Mariya akadakia naye bila kukawia akatupa macho yake kuangalia na ghafla wakashuhudia kilio kikali ndani ya chumba.
“Huyu ndiye!” ndilo neno pekee aliloweza kutamka Mariya na kufuatiwa na kwikwi kali.
“Unasema?” Phillip akauliza.
“Hakika nawaambieni aliyelala hapo ni baba yetu!”
Morgan akasogea karibu na kuangalia kwa umakini ni kweli alikuwa Victor Fedorov, mwili wake ukiwa katika hali mbaya kutokana na kukaa katika barafu kwa muda mrefu.
“Hii ni maiti ya Fedorov!”
“Mna uhakika?”
“Ulio kamilifu, hatujakosea hata kidogo, tungependa kupewa kibali cha kuuzika kwa heshima zote,” ndivyo alivyotamka huku akiukagua vyema mwili huo.

Taratibu maalum zikafanyika wakitafuta vibali husika ili kupata ruhusa ya kuuzika mwili huo kwa heshima zote na hatimaye uchunguzi ulipokamilika na kuridhika wakakabidhiwa mwili wa Fedorov ili wauzike.

Jambo hilo liliamsha vilio upya watu wakalia na kuomboleza, wengi wakionekana kuzimia kwa tukio hilo lakini hatimaye mwili wa Fedorov ukashushwa kaburini kwa heshima zote, watu mbalimbali wakahudhuria msiba huo. Lilikuwa ni tukio la kuhuzunisha sana pengine kuliko yote yaliyowahi kutokea kwa wakati huo. Tajiri mkubwa, Victor Fedorov akawa amezikwa.
Kama familia, baada ya maziko wakatoa muda wa mwezi mzima kuomboleza wakisimamisha shughuli zote kwa ajili ya maombolezo.
Mwezi mmoja ulipomalizika wakiwa katika majonzi walianza tena kazi zao na Phillip akateuliwa kushika wadhifa wa Victor Fedorov, akipewa majukumu yote kama baba wa familia hiyo mpya.
Furaha, upendo na amani vikitawala ndani na nje ya familia huku akipewa heshima zote kwa kila kitu. Maisha kwa Phillip yakanyanyuka tena baada ya kuwa ameshaumizwa moyo mara kadhaa lakini akaonekana kusahau na kufurahia maisha mapya akifuta maumivu yote aliyowahi kuyapata maishani mwake.
“Мы любим не только вас, но и Женевьевы и его жены Магдалены. Для нас вы являетесь частью нашей крови ...”
(Tunakupenda si wewe tu bali pia Genevieve na bibi Magdalena. Kwetu sisi ninyi ni sehemu ya damu yetu...) waliongea Mariya na Merina kwa lugha ya Kirusi na wote kwa pamoja wakanyanyuka na kumsogelea Phillip wakammwagia mabusu mfululizo huku wakimkumbatia, ishara tosha kwamba walikuwa wamemkubali na kumpokea kama baba yao katika maisha yote yaliyobaki baada ya Victor Fedorov kufariki.
“Морган! Женевьева! Г-жа Магдалена пожалуйста, приезжают сюда, чтобы быть счастливыми вместе.” (Morgan! Genevieve! Bibi Magdalena tafadhali njooni huku tufurahi pamoja.) Mariya alipaza sauti yake kuwaita watu hao ambao walikuja mbio na wote kwa pamoja wakakamilisha furaha kwa kukumbatiana wakiachia vicheko.
MWISHOOOOOOO!!!!!
Nachukua nafasi hii kuwashukuru wapenzi wangu wote kwa kunivumilia tangu mwanzo mpaka mwisho wa hadithi hii.

WHATS NEXT??????......nite nite!!!
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

1 comment: